Follow Channel

SALMA WA MTAA WA SABA

book cover og

Utangulizi

Salma wa mtaa wa saba ni simulizi inayozungumzia msichana wa uswahilini alichangamka anakutana na kijana Fariss lakini kukutana kwao kwa mara ya kwanza hakukuwa na heri wanatokea na maneno ya kashfa.
Salma anapanga kumkomoa Fariss anamchukulia simu yake. Fariss anarudi mtaa wa saba akiwa na hasira anauliza mpaka akafanikiwa kumpata Salma. Anaenda nyumbani kwakina Salma anamkuta akiwa kavalia kanga moja nyepesi. Ile kumuona tu hasira zake zote ziliyeyuka .Salma anamfanyia vibweka na kumfanya Fariss achanganyikiwe.
Salma anamrudishia simu yake lakini anamwambia arudi tena siku nyingine.
Fariss anaondoka akiwa mdogo . Anafika nyumbani anajikuta hana Wallet akajua ni kazi ya Salma. Kwakuwa alikuwa na shauku ya kumuona tena Fariss anarudi mtaa wa saba anamkuta Salma akiwa katikati ya ugomvi.
Badae Salma anaenda kuonana na Fariss anamostia walet , Fariss anaomba Salma amuibue moyo wake ili awe kwenda mtaa wa saba kila siku.
Fariss anachanganyikiwa na penzi la Salma anaamua kuacha kila kitu na kuituliza moyo wake kwa Salma . Anakutana na familia ya Salma ambayo mama yupo moto na kaka yake Abuu ni Kibaka na mvuta bangi, hiyo Salma kwenye shuhuri hakosi.

Je Fariss ataweza na na Salma mtoto wa kungwi wa mtaa wa saba?

SALMA WA MTAA WA SABA 1
MTUNZI SMILE SHINE.

Ukisikia mtaa wa saba ni mtaa wa saba kweli ni mtaa iliyochangamka matukio ya kila aina yanapatikana kwenye huo mtaa. Ukipita huku unakuta na wamama wanasutana au vigodoro, ulitokezea kule unakuta watoto wakicheza gololi , kuikata kushoto wavuta bangi na vibaka yani kwenye huo mtaa hakuna mtu mzembe mzembe kwanza wenyeji wote wanajuana akija mgeni anajulikana wanaanza kuulizana huyu katoka wapi? Au kaka kwa nani?

Haya sasa tuanze...

Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili jioni kijana Fariss alikuwa anatoka kazini , kwenye gari yake aina ya range Rover velar nyeusi. Kwenye gari alikuwa na rafiki yake kipenzi Meyael.
Siku hiyo barabara ilikuwa na foleni kubwa sana walisimama kwenye foleni karibia nusu saa. Meyael alichokaa kukaa pale kwa muda mrefu akamwambia Fariss.
" Fariss huku kuna foleni sana tutakaa sana hapa kwanini tusipite barabara ya chini? Fuata hiyo gari inayoingia kwenye barabara ya vumbi alisema Meyael
" Alafu ni kweli sijui kwanini sikukumbuka hili mapema.
Alisema fariss huku akijaribu kutoka kwenye foleni akaingia kwenye sheri moja na badae akafuatia barabara ya vumbi iliyokuwa inapita kwenye mitaa iliyokuwa na nyumba nyingi za watu.
Fariss aliendesha gari kwa mwendo wa kasi alijisahau kuwa yupo kwenye barabara za mtaani huku akisikiliza muziki kwa sauti ya juu kidogo.

Wakati huo huo upande wa pili wa barabara kulikuwa na msichana mmoja anavuka barabara huku mkononi kwake akiwa kashikilia kipande cha gazeti lililofungwa .
Mara Meyael akasema kwa sauti ya hofu.
" Fariss unagonga mtu. Ilikuwa bahati fariss alifunga breki na gari ikasimama.
Fariss na Meyael walishuka haraka kwenda kumuangalia mtu waliotaka kumgonga. walimkuta mwanadada mmoja akiwa kachuchumaa na gazeti lake likiwa chini vitu vyake vyote vilimwagika.
" Wewe dada kwani ulikuwa huoni kama gari inakuja unavuka barabara kwa maringo kama vile anamiliki baba yako. alisema fariss huku akimuangalia yule binti kwa hasira.
Yule binti alisimama huku akimuangalia Fariss kwa macho ya ukali , alishika kiuno na kusema
" Wewe baba naomba ufungue huo mdomo wako mchafu kama kuongea hata mimi najua sana kuongea na isiombe nikaufungua huu mdomo wangu utaomba poo ...
alafu hapa ulipo kumbuka ni mtaani kwangu na mimi ndio Salma alwatan wa huu mtaa wa saba.
" Vitoto vya uswahilini bwana sijui vipoje?
" Koma wewe mtoto unaninyonyesha ? Alafu usijitie sana kuongea umeona mboga yangu imeanguka kwenye mchanga nataka mboga yangu haraka sana kabla sijakujazia nzi hapa.
Fariss aliangalia chini kisha akamuangalia Meyael wakacheza kwa dharau.
" Utumbo, miguu ya kuku ndio mboga? Wenzio wanakula kuku nyie mnaambulia hizo takataka hata nikimpa mbwa wangu hali hizo takataka.
Salma alikunja uso wake kwa hasira kisha akanyoosha mkono wake na kuumkunja Fariss.
" Oya hebu niache...
" Sikia hivi utanifanya nini na nipo mtaani kwangu.
" Wewe mtoto wa kike acha Shobo, usishobokee watu usio wajua. Alisema Meyael.
" Wewe tena nyamaza sitaki ujichanganya kwenye hii kesi. Maana sishindwi kuwachanganya wote wawili.
Meyael alitaka kunyanyuka mkono lakini Fariss alizuia maana alijua ikiwa atampiga yanaweza kutokea mengine.

Baada ya fariss kuona Salma hatanii akauliza
" Unataka nini sasa?
" Umetaka kunigonga hili ninesamehe , lakini hili la kuniharibia mboga zangu utalipa ili iwe fundisho siku nyingine usiweze kurudia tena kuwa na dharau kwa watu usiowajua.

Fariss alimuangalia alafu akauliza
" Kwani shilingi ngapi?
" Hapa ni buku tu.
" Sikiliza nikwambie kwa hadhi yangu siwezi kutoa hela yangu nikanunue miguu , maeneo haya wapi kuna super market?
" Kule barabarani.
" Panda kwenye gari nikakuchukulie kuku mzima. Hata kama utataka kuku wa KFC nitakununulia. Aliongea fariss kwa kujiamini ili kuweka heshima.
" Afadhali neema imenishukia siku ya leo.

Salma alipanda kwenye gari bila uwoga wowote Fariss aliendesha gari kwa kufuata maelekezo ya Salma mpaka wakafika super market.
Walishuka Fariss pamoja na Salma wakaingia super market .
Fariss alitoa hela na kununua kuku mzima na kumkabidhi Salma.
" Shika leo kusheherekeae pamoja na majirani zako.
" Unanipa kwa masimango unafikiri nita susa? Mwenzio sina tabia ya kususa kwaheri.
Salma alichukua mfuko wa kuku na kuondoka huku Fariss akimsindikiza kwa macho.
" Mshamba mmoja muone vimiguu vyake.
Baada ya hapo Fariss alirudi kwenye gari.
" Mmmh ya leo kali. Alisema Meyael.
" Nimekutana na slay queen wa buza. Na njia ya huku sipiti tena tusije tukakutana na balaa lingine.
Meyael aliishia kumcheka.
Fariss aligeuza gari na kuelekea njia nyingine.
Walifika sehemu Fariss alitaka kuwasiliana na mtu alitafuta simu yake alipokuwa kaiweka lakini hakuiona. Alisimamisha gari na kuendelea kutafuta.
" Vipi unatafuta nini?
" Siioni simu yangu.
Walitafuta kila sehemu simu haukuwepo.
" Meyael naomba unipigie.
Meyael alichukua simu akajaribu kupiga simu ilikuwa inaita lakini haikusikika ikiita ndani ya gari.
Fariss na Meyael waliangaliana , Meyael akasema
" Slay queen kachukue simu yako .


SALMA WA MTAA WA SABA 2
MTUNZI SMILE SHINE

Fariss alishusha pumzi huku mikono yake ikiwa kichwani .
" Meyael yule msichana amechukua simu yangu.
" Hahahaha....
" Unacheka?
" Sicheki kwa mazuri ila Salma wa mtaa wa saba kakuweza kakugeuza mtaji.
" Hivi huyu ni mwanamke gani ? Kila tabia za ajabu anazo yeye . Sijawahi kukutana na mtu mwenye ulimi mkali kama yule, nadhani hata Kibaka wa Tandale hawezi kunizidi ujanja kiasi hiki.
" Lakini bro ukweli ni kwamba yule dada ni kichwa ana conference ya hali ya juu. Hata mimi nimemuogopa aisee.

Fariss alitulia huku akiwa anatafakari jambo Meyael akauliza.
" Sasa tunafanya je kuhusu simu yako?
"Hapa hakuna kingine cha kufanya nageuza gari naenda kumtafuta .
" Utampatia wapi kaka hiyo andika umeshalizwa .
" Hapana siwezi kukubali simu yangu ipoteze kirahisi hivyo lazima nitampata , nitatumia gharama zozote kuipata simu yangu.
Kuna vitu vingi vya muhimu kwenye ile simu.

Fariss aligeuza gari na kuanza kurudi mtaa wa saba. Alipofika karibu na walipotaka kumgonga Salma alisimamisha gari pembeni na kushuka haraka akaelekea sehemu akawakuta wanawake wamekaa wanasukana nywele.
" Habari za sauti wakina dada.
" Salama.
" Samahani naomba kuuliza kitu.
" Uliza tu kaka.
"kuna dada mmoja Mjanja Mjanja hivi , muda mfupi alikuwa maeneo haya amevalia dela la rangi ya blue ina mpasuko mrefu na masikioni alikuwa kavalia hereni kubwa za duara.
Wale wakina dada waliangaliana kisha wakamuangalia Fariss. Mmoja wao akauliza
" Unamuongezea Salma?
" Ewaaaaa huyo huyo .
" Sawa , sasa nyoosha na hii barabara ukifika nyumba ya nne ingia na kichochoro ile nyumba ya nne nyuma kuna nyumba nyingine ina rangi ya bluu basi gonga hapohapo ndio kwa kina salama.
" Bingo. Fariss alishangilia kimnyakimnya kisha akasema.
" Asanteni sana dada zangu.

Bila kuchelewa alienda alikosimamisha gari akapanda na kuanza kuendesha.
" Vipi umefanikiwa?
" Ndio sasa subiri timbwili linaloenda kutokea huko yani yule msichana simuachi salama kumuonyesha mimi ni nani namchukua naenda kumlaza ndani hata siku mbili ili ajue kuwa kuna watu wa kuchezewa na sisi wengine hatupotezi muda kwenye mambo ya kijinga.
Meyael alitulia kimnya ndio kwanza alichukua chupa yake ya maji baridi akawa anakunywa maana alimuelewa Fariss akiamua kufanya jambo huwa hacheki kwahiyo kilichokuwa kinaenda kutokea ni kisasi cha simu na yote yaliyotokea kwa siku hiyo.

Waliofika sehemu waliyokuwa wameelekezwa Fariss alisimamisha gari.
" Unaenda au vipi?
" Mimi sitaki kusikia kelele wewe nenda kamalizane nae.
Fariss alishuka kwenye gari akafunga mlango kisha akaingia kichochoro na kuiona nyumba aliyoelekezwa.
Alifuata ile nyumba akasimama kwenye mlango mkuu wa kuingilia ndani na kuanza kugonga kwa fujo.
Wakati huo Salma alikuwa akipepea jiko lake la mkaa kwaajili ya kubandika mboga.
" Ohoooo kumekucha watu wa kudai wameshafika, na wakimuona huyu kuku maneno yatawatoka ngoja kwanza nimfuche huku.
Alichukua ile sufuria iliyokuwa na kuku akiweka chini ya meza na kuifunika vizuri kisha akawa anaelekea mlangoni huku akisema
" Jamani basi tumesikia mtavunja huo mlango.

Baada ya sekunde chache Salma alifika mlangoni huku akiwa kavalia kanga yake moja akafungua mlango na kukutana na sura ya Fariss . Wakati huo fariss alikuwa kakunja uso lakini baada ya kuona muonekano wa Salma matuta ya usoni kwa fariss yalifutika.
" Una matatizo gani? Mbona unagonga mlango kwa fujo hivyo?
"Kilichinileta hapa ni kitu kimoja tu Nataka simu yangu.
Salma alimuangalia Fariss huku akionyesha tabasamu hafifu usoni kwake . Kisha akasema
" Nilijua tu utafuata simu yako. Simu yako ipo salama , sikuwa na shida nayo ila nilichukua makusudi ili ulipe kwa dharau zako na maneno yako ya kejeri kusema kuwa mboga zangu hata mbwa wako hawezi kula.
Nimeamua kukuonyesha sio kila mtu niwakubeza.
" Hivi unajua ni kiasi gani umenipotezea muda wangu?
" Wewe ni mbinafsi sana kwani hukuona jinsi ulivyoupoteza muda wangu?
" Hebu acha kunipotezea muda nipe simu yangu.
" Nitakupa lakini unatakiwa kujua kila mtu anahitaji heshima,ukiheshimu wengine na wewe utaheshimiwa.
Alisema Salma kisha akageuka kuingia ndani. Fariss macho yalimtoka kwa jinsi alivyokuwa akimuangalia Salma anavyotembea na huko nyuma kutetemeka mithili ya jenereta lililowashwa.
" Mmmmh..... Hii balaa Fariss nimekuwa mdogo kama piliton. Amejua kuituliza moyo wangu.

Baada ya muda Salma alirudi akiwa kashika simu ya Fariss mkononi. Kwa madoido Salma alimkabidhi Fariss simu yake
" Shika simu yake.
Farris alichukua simu akaiangalia mara ghafla akashitukia kakumbatia.
Fariss aliduwaza na kuganda.
Salma alivunja kumbatio na kuweka mikono yake nyuma.
" Karibu tena mtaa wa saba sisi ni wakarimu sana.
Fariss alimuangalia sana usoni kisha akageuka kuondoka bila kusema chochote.

Fariss alipiga hatua chache kutembea mara akasikia anaitwa.
" Hey.
Fariss aligeuka kumuangalia.
" Ninatumaini siku sio nyingi utakuja tena hapa.
Farris alimuangalia Salma bila kuelewa , lakini macho ya Salma yalikuwa na jambo, yalikuwa na mvuto wa kike pia sauti yake ilienda kutuliza ghadhabu za Farris.
" Usichelewe kuja tafadhali maana sitaweza kusubiri kwa muda mrefu.

Taratibu Salma alifunga mlango . Farris alirudi kwenye gari akiwa kapoa.
Meyael alipomuona alishangaa kumuona jamaa kapoa ni tofauti alivyokuwa kaenda wa moto.
" Vipi bro mbona kama umevunjika moyo ? Umepata simu yako kweli?
" Farris alivuta pumzi ndefu alafu akashusha na kusema.
"Meyael yule mtoto ni noma , ana roho ya simba, nilichokikuta huko siwezi kuhadithia ila tambua akili yangu haipo sawa na hapa nilipo kajikuta natamani kumuona tena.


SALMA WA MTAA WA SABA 3
MTUNZI SMILE SHINE

Meyael valimuangalia Fariss kisha akaguna na kutingisha kichwa.
" Farris achana na watoto wa uswahilini bwana washa gari twende zetu.
" Sawa lakini kwa nilichokiona hata ungekuwa wewe isingeweza kujizuia Meyael.
" Tamaa zitakuponza, Unajiendekeza bwana nakujua sana wewe ni mtu wa totoz sana unapenda kuonja moja sana.
" Wewe meya unasema tu sababu haujaona.

Waliondoka mitaa ya uswahilini huku taswira ya Salma ikijirudia kichwani kwa Fariss kuna wakati Meyael alikuwa akimuongelesha laki hakuwepo pale alikuwa mbali kimawazo.

Fariss alifika nyumbani akikagua kwenye mfuko wake wa nyuma ili atoe Wallet lakini hakuiona.
" Nimeacha wapi Wallet? Alijiuliza huku akiendelea kujisacho kila kona ya mfuko lakini hakuiona , alitoka nje kwenda kukagua kwenye gari pia hakuona . Alisimama na kushika kiuno alafu akashusha pumzi ndefu.
" Mmmmh kweli Fariss nimepatikana leo nimekutana na kiumbe hatari sana , Salma , Salma...
Alicheka kidogo na kutingisha kichwa .
" Salma anaonekana mtundu sana. Ok nitarudi kama alivyotaka nirudi. Kesho nitakuwa kwenye uwanja wa nyumba yao

Kesho yake Mida ya saa nne asubuhi Farris alikuwa mtaa wa saba , alipakia gari yake vizuri kisha akaingia kichochoroni alipokaribia karibu na nyumba ya kina Salma alisikia kelele na wakina dada sio chini ya wanne wakiwa wanazozana. Salma alikuwa kati yao alikuwa anaongea balaa huku mkono mmoja ukiwa umepandisha kijora chake na kujibana kwapani na kufanya paja lake lionekane.
" Hata kama mnanidai ndio mnivamie asubuhi hivi kabla hata sijanywa chai?
" Hizo sio shida zetu tunachotaka tupe hela ya kijora.
" Hiyo hela sina mnataka nini sasa.
" Tutaingia humo ndani tutachukua kitu chochote.
" Aaaaaa subutu kama wanawake kweli ingizeni mguu kwenye hicho kizingiti .
" Unafikiri tunashindwa .
Alijibu mmoja huku alitangulia ndani.
" Nenda mpaka chumbani...
Yule dada aliingia mara ghafla alitoka akiwa anakimbia , aliwapita wenzie kama mshale.
" Huyu vipi mbona katoka mbio kuna nini?
Wakiwa bado kwenye mshangao alitoka Abuu kaka yake Salma Kibaka mzoefu pele mtaani kipindi hicho alikuwa jela na jana ndio alitoka.
Wale wakina dada walipomuona waliondoka bila kuaga kila mmoja alitafuta kichochoro chake.
" Aoooooo .... Mnakumbuka nini Simameni sasa kama wanawake kweli . Ovyoooo.
" Kelele za nini hapa? Abuu alimuuliza Salma.
" Achana nao .
" Unajua nataka utulivu lakini utnaniletea wambea wanzako wanakuja kuniletea fujo.
" Makubwa safari hii jela imekifanya utake utulivu?

Abuu alimuona Fariss akiwa kasimama akamkazia macho.
" Yule nae ni nina hapa mtaani ?
Salma aligeuka kumuangalia alipomuona fariss aliachia tabasamu la mbali.
" Sasa kuna utulivu wewe nenda Kalale huko ndani.
" Unamjua?
" Kaka mengine yakupite. Alisema Salma huku akimfuata Fariss.
" Oya wewe kuwa na adabu mimi sio shoga yako nitakupasua sasa hivi.
Salma hakujali maneno ya Abuu alifika aliposimama Fariss akamshika mkono wakaenda kukaa kwenye kibaraza cha nyumba ya pili.
" Vipi umekuja tena kama nilivyokwambia?
" Sikuwa na nia ya kuja ila nimefuata kitu changu.
" Kitu gani?
Aliuliza salama huku akimuangalia Farris usoni kwa jicho lake zuri lililolegea.
Jicho la Salma lilizidi kumvuta Fariss .
Fariss alimuangalia moja kwa moja mpaka aliposhituliwa na simu yake iliyokuwa inaita.

Farris aliacha kumuangalia akatoa simu mfukoni na kupokea.
" Hallow.
" Nipo ofisini kwako sijakukuta. Upande wa pili Aliongea Meyael
" Nimetoka kidogo nitarudi muda sio mrefu.
Aliongea Fariss kisha akakata simu.
" Mmmh uliniambia umefuata kitu ni kitu gani hicho?
" Wallet yangu.
Salma alisimama akafungua kijora chake na kuingiza mkono kwenye taiti yake iliyokuwa na mfuko akatoa Wallet na kuishika mkononi.
" Ni hii si ndio?
" Ndio.
Salma alimkabidhi ile Wallet, Fariss alifungua ile Wallet na kuangalia ndani kama kuna vitu vyake vyote. Akitoa hela akahesabu ilikuwa sh elfu 80 kifupi Salma hakuchukua kitu chochote kila kitu kilikuwepo vilevile.
" Naweza kukuuliza kitu? Fariss aliuliza.
Salma alikaa alafu akasema
" Uliza.
" Kwanini ulichukua Wallet yangu.
" Niliamua tu.
" Ndio maana ukaniambia nitarudi tena?
" Ndio nilijua nilichukua kitu chako lazima urudi.
Farris alitabasamu.
" Sasa umefurahi kuniona tena mtaa wa saba?
Salma hakujibu swali la Fariss.
" Humu kulikuwa kuna hela sasa kwanini haikuchukua kuwalipa wale watu waliokuwa wanakudai?
" Sikuwa na nia ya kuiba nilikuwa nataka kukusumbua tu.
" Oooh sasa sasa hivi utaniibia nini ili nirudi tena mtaa wa saba?


SALMA WA MTAA WA SABA 4
MTUNZI SMILE SHINE

Salma alicheka cha kuombea kisha akageuza yale macho yake makubwa yaliyokuwa yamepakwa wanja na kufanya yawe na mvuto zaidi na kumfanya Fariss awe na hamu ya kumuangalia zaidi.
" Bado unatakurudi mtaa wa saba?
" Huwenda wewe ndio umenifanya nipende kuwa hapa mara kwa mara. Alijibu Fariss huku akimuangalia kwa makini
" Kwa sasa sina cha kuibia labda nikuibie huo moyo wako.
" Waooo....ukifanya hivyo itakuwa nafuu kwangu maana nitafika hapa kila siku .
" Unahisi itakuwa sehemu salama kwa moyo wako kuwa hapa?
" Kabisa naamini itakuwa salama.

Salma alinyanyuka akaondoka huku akipiga hatua ndogo ndogo sehemu zake za nyuma zikatingishika. Hapo ndipo alipokuwa anazidi kummaliza Fariss wa watu.
Akiwa bado anamsindiza kwa macho Salma alisimama na kumgeukia kisha akauliza.
" Unaitwa nani vile.
" Farris .
Salma aliachia tabasamu alafu aligeuka na kuendelea kutembea akielekea kwao na Fariss akaamua kuondoka.

Fariss alirudi kazini na kwenda kukutana na Meyael.
" Vipi ulikuwa wapi?
" Nimetoka mtaa wa saba.
Meyael alimuangalia Fariss usoni alafu akauliza.
" Usiniambie kuwa ulienda kwa Salma.
" Ndio nilienda kuonana nae.
" Bado kuna unachokihitaji kwake?
" Unajua jana aliichukulia kitu changu kingine ikabidi nikifuate.
" Alijuibia nini?
" Wallet.
" Wallet aliibaje.
" Nilipoenda kuchukua simu alinikumbatia nikaona kawaida tu kumbe alichomoa Wallet.
" Amekupa?
" Ndio hii hapa. Farris alitoa Wallet akamuonyesha.
" Farris huyo msichana sio wa kuwa nae karibu achana nae.
" Meyael hebu achana na hizo habari hujui tu moyo wangu unavyotapatapa kuhusu Salma.
" Kwahiyo unataka kujiweka pale.
" Nitajaribu maana naona mtoto nae anajileta flani.
" Mtawezana? Maana nakujua vizuri wewe na huyo Salma nati moja kama imelegea.
" Kumbe unanijua basi tulia uangalie nikishindwa mapema sana nakimbiza mbawa zangu alafu mambo yake wala hayaniumizi akili naweza kuishi na watu wa aina ile si unajua mimi ni baharia.
" Mmmmh sawa lakini kumbuka na wewe una dada na utakuja kuwa baba hayo inayofanyika watoto wa wenzio yatakukuta.
" Subutu nitamtoa mtu kiungo muhimu.
Alisema Fariss kisha akanyanyuka na kutaka kuondoka.
" Unarudi mtaa wa saba au?
" Aaaaah naenda ofisini kwangu bwana.

Siku zilienda Fariss alikuwa Bize sana na mambo ya kazi hivyo ilikuwa ngumu sana kupata muda wa kwenda kumtembelea Salma lakini kichwani kwake alikuwa akimfikiria sana .
Siku moja ilikuwa ni siku ya jumamosi na ndio siku Fariss alikuwa kupata muda akaamua kutoka na marafiki kwaajili ya kufurahi . Walitoka na kwenda club moja ya kawaida lakini ilikuwa imechangamka sana watu wengi walipenda kwenda hapo.
Fariss na wenzie walienda kujichanganya na watu wengine wakawa wanacheza muziki huku wakiangalia wadada wazuri wa kucheza nao . Kila mmoja alipata wa kucheza nae kama kawaida Fariss alikutana na dada mmoja wakawa wanacheza huku akimsifia kwa upande fulani alikuwa anatengeneza mazingira ya kutaka kuondoka nae ule usiku.
Katika cheza cheza mara alitokea Salma akamshika bega yule dada aliokuwa anacheza na Fariss.
" Tuondoke siwezi kuendelea kukaa hapa .
Salma alimnongoneza mwenzie sikuoni wakati huo Fariss alikuwa akimuangalia kwa makini alihisi kama anamfananisha.
" Vipi wewe mambo ndio kwanza yameanza kuchangamka.
" Sawa endeleeni Abuu akijua sipo nyumbani ataniletea shida.
Salma aliamua kuondoka, Fariss alishindwa kubaki pale aliachana na yule dada akaamua kumfuatilia nyuma Salma.

Salma alipofika nje alisimama sehemu kwaajili ya kutafuta usafiri kila pikipiki iliyopita ilikuwa na abilia ilibidi aendelee kusimama na hali ya hewa ilikuwa sio rafiki kulikuwa na upepo pia wingu la mvua ilitanda angani kukawa na giza.
Fariss alifika nyuma ya Salma na kumshika begani.
Salma aligeuka alipoona ni mwanaume alianza kuropoka.
'" wewe kaka jaribu kujishikiria sio kila anayekuja club anakuja kujiuza au anashinda na mwanaume ? Mimi sina hayo mambo katafute wenye uhitaji.
" Salma.
Baada ya fariss kuita jina lake ndipo Salma aligeuka kumuangalia usoni. Alipogundua yule mwanaume ni Fariss moyo wake ulipasuka.
" Fariss....
" Ndio.
" Sijategemea kukuona maeneo kama haya, hata wewe huwa unakuja huku changanyikeni kwenye disco vumbi ukitoka hapa vumbi mpaka kwenye kope za macho.
Fariss alishindwa kujizuia kucheka, alicheka kisha akasema
" Huwa nakuja mara nyingi tu si unajua mambo mengi sehemu kama hizo huwa tunakuja ku refresh mind. Napenda sana sehemu zilizochangamka kupita kiasi.
" Oooh sawa.
" Mbona upo hapa , unamsubiri mtu?
" Nasubiri usafiri nataka kurudi nyumbani.
" Mbona mapema?
" Mapema kwako lakini kwangu muda umeenda sana alafu najuta sijui kwanini nilikuja hapa siku ya leo.
" Kwanini ujute? Sasa upo na mimi twende tukafurahi .
" Hapana nataka kuondoka tu hapa.
" Basi usiwe na wasiwasi ngoja nikachukua gari nikupeleke.
" Kweli?
" Ndio, subiri hapa nakuja sasa hivi.
"Nafuu imejiingiza fanya haraka kabla hajapatikana mdhamini mwingine .


SALMA WA MTAA WA SABA 5
MTUNZI SMILE SHINE

Farris alienda kuchukua gari baada ya dakika kadhaa alifika na gari yake na kusimama mbele ya Salma.
Salma alifungua mlango wa gari na kupanda na kukaa kwenye siti ya pembeni ya dereva.
Farris aliwasha gari wakaanza safari ya kuelekea mtaa wa saba.
Wakiwa njiani kila mmoja alikuwa kimnya.
Salma aliamua kuvunja ukimnya kwa kusema.
" Umeadimika sana hautaki kurudi uswahilini kwetu .
Fariss alitabasamu kisha akasema
" Hakuna ulichoniibia ningeweza je kurudi tena?
Salma aliishia kucheka.
" Ulisema labda uniibie moyo wangu lakini nilipokaribia kuutoa na kukukabidhi uliamua kuondoka.

Waliendelea kupiga story za kuchokozana walipokaribia kufika maeneo ya kwa kina Salma Fariss alichukua simu yake na kumpa Salma.
" Weka bamba yako hapo.
Salma alipokea na kuandika namba yake ya simu , alipomaliza alimrudishia simu yake.
" Unauhakika ni namba yako na sio namba ya gari?
" Hahaha ni namba yangu na jina nime save.
" Ume save nani?
" Malkia wa mtaa wa saba.
Fariss alimuangalia kisha aliachia tabasamu.
" Natamani kuwa na wewe muda wote maana mambo yako huwa yananifanya nifurahie sana.

Wakati huo walikuwa wamefika na gari ilisimama pembeni lakini bado waliendelea kuongea na Salma alishawahi kuwa anamuwahi Abuu asije akajua hayupo nyumbani.

Wakati wanaendelea kuongea dirisha la upande wa Fariss liligongwa.
Fariss na Salma waliangalia kwa makini . Fariss alitaka kufungua lakini Salma akamuwahi.
"Acha usifungue.
" Unajua ni nani?
" Ndio. Alijibu Salma huku akifungua mlango wa gari na kushuka.
" Haaaaaa kumbe ni wewe dogo unatoka wapi saizi?
Ilikuwa ni sauti ya Abuu akiongea kwa ukali.
Salma alimuangalia Abuu bila kujibu. Abuu alimfuata aliposimama na kumsukuma pembeni akachungulia kwenye gari.
" Wewe ndio unamvuruga dogo na kumfanya asittilie nyumbani si ndio. Hebu shuka haraka.
" Abuu hebu muache.
Abuu alimgeukia Salma
" Oya kaa mbali na hili acha niongee na huyu mzinifu mwenzio.
Oya toka humo ndani kabla sijapianzisha varangati langu.
" Sikiliza bro mimi nimempa lift tu....
" Acha kujipanga kishamba hivyo shuka.
Fariss akaona isiwe tabu alishuka kwenye gari na kukutana na vijana wengine wanne wakiwa wamevaa kihuni na mmoja alikuwa kashika panga.
" Songea hapa unaogopa ogopa nini mtoto wa kiume.
Fariss alisogea karibu na Abuu.
" Na wewe songea hapa.
Abuu alimuita Salma.
" Abuu tuheshimiane na mimi sio mtoto wa kusema unifuatilie na kunichunga endapo utamdhuru huyu kaka wa watu nitakutwanga jiwe la kichwa alafu baada ya hapo nitaenda kushitakiwa polisi, alafu huyo sio wa huku ujue baba yake ni mtu mkubwa sana kwenye hili taifa kumgusa tu safari hii unaenda kunyongwa sasa endelea.
Salma alitoa vitisho kumtetea Fariss .
Abuu alimuangalia Fariss kisha akasema.
" Sawa anaonekana mtoto wa kishua sasa ndio azini watoto wa watu?
" Wala sio mzinifu, soja zini nae .
" Sasa ni nani kwako mbona kama una uchanganya?
" Ni mpenzi wangu , mwanaume wangu ninaempenda.
Abuu alimuangalia Salma alafu akasema
" Umakini nini kujifungulia hayo maneno ?
" Ni mapenzi tu kaka naomba utambue huyu ndio moyo wangu popote utakapomuona mtambue kama shemeji yako.
Abuu alimuangalia Fariss ambae alikuwa kimnya muda wote kisha akauliza.
" Wewe unampenda mdogo wangu?
Fariss alimuangalia Salma , Salma alitingisha kichwa akimaanisha Fariss akubali.
" Ndio ni mwanamke ninaempenda sana.
" Sawa nakuacha sababu dogo anakupenda ila usije ukazibgua baba sitajari mtoto wa waziri au raisi nitakufanyia mbaya.
Abuu aliwaangalia wenzie kisha akasema
" Oya twendeni.
Walianza kuondoka huku waliwaacha Salma na Fariss wakiwa wamesimama.
Walifika mbele kidogo Abuu alisimama na kugeuka nyuma.
" Oya bwana shemeji nisababishie ya fegi.
Farris aliingiza mkono mfukoni akatoa kiasi cha pesa ambacho hakuhesabu akampa.
" Asante na unakaribishwa nyumbani.

Abuu alivyoondoka Salma alimgeukia Fariss.
" Uliogopa eee...
" Niliogopa lile panga tu.
" Nisingekubali akifanyie jambo baya alafu nisamehe kwa kusema kuwa ni mpenzi wangu ilikuwa ni njia ya kumfanya aondoke bila kujidhuru.
" Usijali hilo ni swala dogo.
" Mmmmh naona unataka kuwa hapa lakini muda umeenda na mitaa ya huku sio salama sana hasa kwako wewe mgeni .
" Sawa acha niende tutawasiliana.
" Sawa.
Salma aliingia uchochoro ni akaelekea kwao na Fariss alipanda kwenye gari akaondoka huku akiwa na tabasamu na kusema.
" Yani raha tupu shemeji yangu mbabe wa mtaa, mwanamke wangu malkia wa mtaa, aaah yani mtaa wa saba unanikosha.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote