Kutana na JENSEN kijana mwenye moyo wa baridi kijana alie funga moyo wake na kujiapiza kamwe hatakaa ampe moyo kiumbe kinachoitwa mwanamke ,na hii ni baada ya kuwa na historia mbaya na swala zima la mapenzi ๐ฅบ lakini kiapo hicho kiliyeyuka mara baada ya kukutana na SIENA .
Binti ambae aliingia kwenye maisha yake na kuvunja kuta /uzio ulio uzunguka moyo na kuingia ndani ya moyo wa kijana mazima , kiasi cha kijana kutubu na kusema SIENA (UDHAIFU WANGU NI WEWE)๐ฅฐalooh hii kitu ni tamu fanya kushuka na mimi ๐
SIENA (Udhaifu wangu ni wewe)
SEHEMU YA 01
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
UTANGULIZI
Kutana na JENSEN kijana mwenye moyo wa baridi kijana alie funga moyo wake na kujiapiza kamwe hatakaa ampe moyo kiumbe kinachoitwa mwanamke ,na hii ni baada ya kuwa na historia mbaya na swala zima la mapenzi ๐ฅบ lakini kiapo hicho kiliyeyuka mara baada ya kukutana na SIENA .
Binti ambae aliingia kwenye maisha yake na kuvunja kuta /uzio ulio uzunguka moyo na kuingia ndani ya moyo wa kijana mazima , kiasi cha kijana kutubu na kusema SIENA (UDHAIFU WANGU NI WEWE)๐ฅฐalooh hii kitu ni tamu fanya kushuka na mimi ๐
SONGA NAYO...................
Ikiwa ni ijumaa mida ya jioni nilitoka na kwenda kwa mshikaji kufika nikakuta jamaa anagomba na mpenzi wake kwenye sm, bila kumsumbua nilisogea hadi kwenye sofa nikaka tulii.
Waligomba mwisho binti akamkatia sm jamaa , jamaa baada ya kuona amekatiwa sm akanigeukia na kuanza kulalamika akidai binti anamdharau sana.
Kwa upole niliinuka nikenda kwenye friji na kuchukua kinywaji kisha nikarudi kukaa na kumwambia, "sikia bro achana nae ,kwanini uumize kichwa kwasababu ya ujinga kama huo?"
"Jensen huu ni ujinga?"
"Yeah! Sasa kidume kama wewe uko hapa unagombana na kitoto cha juzi si ujinga huo, kwanza nisha kwambia achana na mapenzi kula raha ona leo uko hapa unauchosha moyo."
"Natamani kukutukana ila nisawa hujui lolote kuhusu mapenzi ndo maana unaropokwa tu "
"Sikia achana nayo vp leo tuenda wapi maana nataka kuianza weekend mapema ,na nataka leo nipate demu flani hivi mtamu"
Frank aliniangalia kwa jicho kali na kusema "Sina mood ya kutoka kama unaenda nenda mwenyewe au mcheki Marko "
"Aaaa ndo nini yaani umevurugwa kiasi hicho ,oya embu acha ufala bwana tuondoke "
"Kweli siendi kokote " aliongea na kuchukua sm akampigia Demu wake kwa mara nyingine wakaendelea kuzozana , nilimuangalia nikatikisa kichwa kumsikitia.
Na bila kuongea neno niliinuka na kuondoka zangu kwenda kutafuta sehemu za bata , ngoja nikwambie.
Moja ya kitu ninacho chukia katika dunia hii ni kiumbe kinachoitwa mwanamke , yani ninapo sema nachukia basi jua nina wachukia zaidi ya neno lenyewe๐
Na hakuna kitu chochote kwenye hii dunia kinacho weza kunifanya nikaacha kumchukia mwanamke,na kunifanya nimpende .
Kiufupi sina ndoto ya kuwa na mpenzi wala kuoa ,zaidi nina chapa na kupita wala sirudii mwanamke hata mara mbili ni moja tu inatosha.
Huyo ndo mimi sijutii kwani ndio life pekee lenye amani bila stress za kijinga ,kwanza wanawake wenyewe hawana mapenzi kitu pekee kilichopo kwenye akili yao ni pesa .
Eeh ukiwa na pesa tu unapiga yoyote unaemtaka na kwa wakati wako ,sasa kama naweza kumpata yoyote nikamchapa kisa pesa yanini niuhangaishe moyo kwa ujinga .
Haya safari yangu iliishia moja ya club kali sana hapa mjini, bila presha nikatafuta sehemu ya parking nikapark gari langu kisha nikaingia mzigoni.
Kama kawaida yangu nikaenda sehemu nikatulia na kuanza kuangalia mtoto wa kuruka nae, mida ilienda kila nikiangalia naona pisi nisizo zielewa .
Nikaona sina mda wa kupoteza nikalipia kinywaji nilicho tumia kisha nikachomoka kurudi nyumbani , sikutumia mda mrefu nikafika na kupark gari kisha nikaingia ndani.
Kufika nikakuta binti wa kazi amelala kwenye sofa huku tv iko on, macho yangu yalitua kwenye kiuno kulicho beba mzigo mzito .
Kidume nikapiga fundo ma mate na kusogea karibu nikataka kumshika nikasita na kujiambia " hii sio aina ya mwanamke ninaeweza kupita nae "
Niliongea na kutaka kuondoka kuelekea chumbani ila nikasimama na kuangalia tena ,moyoni nikasema bwanaee kwani kuna haja gani ya kuangalia status na type kwani nataka kuoa au kula .
Nilivyo waza hivyo nikarudi na kuminya mzigo kidogo binti akaruka kwa mshtuko, nikamwambia tulia na kupelekea mkono kwenye ziwa.
Binti aliniangalia kwa uoga huku akitamani kukakataa ila mdomo ukawa mzito, jambo lililonipa wepesi kidume nikaanza kutoa mipapaso binti akaanza kutoa miguno.
Nikamuangalia hapo nawaza nimpeleke chumbani ila nikaona hapana kitanda changu hakijawahi kulaliwa na Malaya yoyote yule , sebleni napo nikaona hapana.
Kiufupi upuuzi wote naufanyiaga mbali na nyumbani ,so sikutaka kuvunja hilo nilichofanya nikambeba na kutoka nje hapo karegea kama bamia ilotiwa gadi.
Basi nikamfikisha nje, na kumpeleka sehemu ambayo huwa napumzika nikamuinamisha Kinga iko wapi shwaaa nikala vitu baada ya kumaliza nikaingia ndani bila hata kuongea kitu.
Kwa aibu binti alivaa nakubaki amekaa , nikiwa juu nilimuangalia nikasema huyu hatakiwi kubaki hapa , kwakua ilikuwa usiku nikaona ngoja nimuache.
Nikaingia bafuni na kuoga kisha nikachukua pc yangu na kupiga baadhi ya kazi kisha nikalala kwa amani๐
Usiku uliisha kesho yake asubuhi kama kawaida niliamka na kuingia chumba cha mazoezi nikapiga zoezi ,nilivyo maliza nikashuka chini kuangalia nini kimeandaliwa kwaajili ya chai.
Kufika jikoni binti akangalia chini kwa aibu huku akifikinya vidole, nilimuangalia na kumuuliza " umeandaa nini kwaajili ya chai"
"Nimepika rost ya maini na chapati za maji pamoja na chai ya maziwa " aliongea kwa uoga sana huku akiwa bado anaangalia chini.
Sikushangaa maana sinaga mazoea na mfanya kazi wangu yoyote iwe nyumbani au ofisin, mara zote naonesha uso wa ukali kiufupi sicheki na wowote.
Na nahisi pia inaweza kuwa sababu ya binti huyu kushindwa kuongea jana ,ila hamana lolote boss kuwa mkali haiwezi kuwa sababu ya kukubali kutumika bila kusema hapana.
Niliwaza na kutoka nikarudi chumbani na kuoga kisha nikarudi chini na kukuta tayari meza imeandaliwa , bila kupoteza mda nilikula na baada ya kumaliza nikamuita binti na kumwambia .
"Sikia Kusanya kila kilicho chako uondoke " niliongea na kuweka pesa mezani ,pesa ambayo ilikuwa ni mshahara wa kazi mbili .
Binti alitaka kuongea ila jicho nililomuangalia lilitosha kumfanya ashindwe kuongea , kinyonge akachukua pesa na kuondoka mbele yangu.
ITAENDELEA
SIENA (UDHAIFU WANGU NI WEWE)
SEHEMU YA 02
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO.................
Aliingia chumbani na kujusanya nguo zake kisha akaondoka huku akifuta machozi, sikuumia wala kumzingitia ndo kwanza nilikaa na kuwasha TV.
Sekunde kadhaa zilipita baada ya binti kutoka ndani akaingia Frank akiwa na uso wa sinto fahamu na kuniuliza "bro vp mbona binti wawatu ametoka akiwa analia?"
"Analia kwa mapenzi yake, vp umepona ?"
"Achana na mimi tuongee kuhusu huyu binti ,nini kimetokea yani umemfanya nini maana haiwezekani aondoke akiwa analia"
"Aisee nimekujibu analia kwa mapenzi yake sasa maswali ya nini tena "
"Oh come on Jensen mtu ataliaje bila kuwa na sababu "
"Aaah si nimekwambia ni mapenzi yake au hiyo sio sababu ?"
"Hakuna kitu kama hicho, we kuna kitu umemfanya ila punguza ukali kwa wafanyakazi wako bhana we huoni shida kubadilisha watu kila siku?"
"Kama wanafanya ujinga ninyamanze ili iweje wakati natumia pesa yangu kuwalipa"
"Kuwalipa watu sio sababu na bora hata huo ubabe uufanyie kwa hao wa ofisin ila huku nyumbani wallah ipo siku utanyweshwa sumu hutaamini ."
"Achana nayo mh nambie "
"Aa fresh vp jana ulifanikiwa kwenda ulikataka kwenda"
"Yeah nilienda but sikuona cha maana nikageuza zangu"
"Hukuona cha maana au ndo uchaguzi wako we unakosaje demu club "
"Pamoja na kwamba sihitaji kuwa na mpenzi ila haimanishi nitaokota kila mwanamke anaepita mbele yangu, nahitaji mwanamke ambae nikisimama nae mbele za watu kila mtu anasema kweli hiki chombo.
Na sio uozo ukiojaa kila aina ya UTI ,ila kww mara ya kwanza jana nimeenda nje ya mipaka yangu nikamla binti wakazi"
"Nilijua tu kuna kitu umefanya ,sasa kama ulipita nae why aondoke akilia usinambie ulimbaka?๐ณ
"Sura yangu inaonekana kama kibaka eeh?"
"Aaah sio hivyo ila kwanini aondoke analia na saizi unasema ulimpitia"
"Sikumbaka bwana alikubali mwenyewe nijapiga fresh sema nimekosea sana "
"Bora umejua kuwa ulikosea ila kwanini usinge andelea nae tu maana ni binti mzuri na ana heshima kiufupi yuko poa kwenye kila idara"
"Niwe nani yule binti ?"
"Yeah"
"Hata kama ningekuwa na mpango wa kuwa na mwanamke nisinge mchagua yeye hata kwa dawa ,binti yupo yupo hana mbele wala nyuma kwanza najutia kulala nae.
Coz hakuna cha maana nilichopata zaidi ya kujidhalilisha , tena umenikumbusha"
Niliongea na kuchukua sm nikampigia kijana mtunza bustani "Naam boss" aliitikia baada ya kufika .
"Sikia kuna vile viti vilivyoko karibu na garden ,vitoe vyote "
"Sawa boss unataka niviweke wapi"
"Utajua wewe utupe au uchukue ni wewe kikubwa nisivione pale tena "
"Sawa boss" alijibu na kuondoka ,Frank akaniuliza.
"Vp tena mbona unaviondoa si umevi chukua juzi tu ?"
"Naviondoka kwasababu nilimgongea nani anaitwa Nuru yes nilimgongea pale"
"Sasa kama ulifanya hivyo kuna haja gani ya kuvitoa "
"Frank moja kati ya sheria niliyojiweka ni mwanamke yoyote nikishampitia sitaki tena kumuona machoni mwangu,sio yeye tu bali kila kitu kinacho muhusu.
Na ndio sababu nimuondoa mapema sana "
"Unahitaji kuombewa ,sasa utaharibu vingapi"
"Sina cha kuharibu na ndio maana sileti mwanamke yoyote ndani ya nyumba yangu "
Frank aliishia kuniangalia na kukosa cha kuongea ,tukabaki tunaangalia mpira mda ulienda ilipofika mchana akaondoka na kuniacha mwenyewe.
Jioni ya siku hiyo sikupanga kutoka kwenda sehemu yoyote so nilifanya mambo yangu na kuupa mwili nafasi ya kupumzika.
Siku iliisha kesho yake asubuhi niliamka nikafanya mazoezi kama kawaida baada ya hapo nikajiweka vizuri na kutoka kwenda kutafuta kifungua kinywa.
Sasa wakati nikiwa njiani nikampigia sm mama , sim iliita sana bila kupokelewa nikaamua niachane nae.
Basi nikifika sehemu niliyo kuwa nataka nikashuka na kupata chai , sasa baada ya kumaliza kupata chai niliinuka ili niondoke lakini nikajikuta nikiishia kusimama na ni baada ya kumuona ................
ITAENDELEA
SIENA (UDHAIFU WANGU NI WEWE)
SEHEMU YA 03
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO.............
Faith binti aliekuwa mwanamke wa ndoto zangu enzi hizo nikiwa hai, na naweza kusema yeye ndio mwanamke pekee ambae nimewahi kulala nae mara moja tu.
Na zaidi yake hakuna mwanamke mwingine ambae nitamuona kama nilivyo muona yeye wala kumrudia.
Nilisimama kwa mda wa dakika moja na kuamua kuondoka lakini bahati mbaya aliniona na kuja mbio kunisalimia.
"Ooh wow Jensen! Habari yako jamani sikutegemea kama nitakuona hapa ,vp unaendeleaje na naona uko vizuri sana"
Aliongea kwa kuchangamka sana huku akijichekesha chekesha, kitu ambacho kiliudhi na niseme katika watu ambao siwezi kuongea nao au kukaa nao meza moja ni aina hii ya mwanamke.
Yaani unakuta kidada kinaongea kama kimemeza flash ,anaongea bila kitu wala koma, na usi shagae kusikia nasema kuwa siwezi kukaa au kuongea na mwanamke wa hivi.
Ile hali nimetoka kusema alikuwa mwanamke wa ndoto yangu, yes alikuwa na kwa kipindi kile nilimpenda haswa ila kwasasa namuona kama chizi si chizi tahira si tahira kiufupi simkubali .
Japo ni binti flani pisi na yuko matawi ila kwa macho yangu yote hayo sioni.๐
Basi niliitikia salamu yake bila hata kuongeza neno nikataka kuondoka akanizuia kwa kunishika mkono.
Aisee nilichukia na kuwambia " Faith jiheshimu embu niachie na usije kurudia kunishika unanielewa"
"Oh please Jensen kwanini unataka kunifanya nijione sifai kwani mimi nawewe tuna ugomvi baba angu"
Sipendagi kuongea mara mbili ,nilichofanya nikutoa mkono wake na kuondoka nikamuacha amesimama huku akiniangalia ,usoni alijitahidi kuonesha tabasamu japo moyoni aliumizwa sana na kitendo kile.๐๐
Nilitoka pale na kurudi nyumbani ambapo nilifika zikapita kama dakika 20 geti lilifunguliwa ,nikainuka na kuangalia ili kujua ni nani anaekuja kwangu bila taarifa.
Nikagundua ni mama yangu ,taratibu nilirudi kukaa ,mama akapark gari na kuingia ndani.
"Shikamoo mama " nilimsalimia baada ya kufika na kukaa .
"Marahaba mh kuna nini maana umenipigia sm kama vile umetekwa na ukasahau kuwa nilikuwa kanisani"
"Ulikuwa kanisani sawa sasa mi ningejuaje bila kuambiwa"
"Uambiwe nini ina maana hujui kama leo ni siku ya ibada?"
"Okay basi "
"Basi nini muone ,kwanza yuko wapi Nuru aje aniandalie walau chai "
"Hayupo"
"Kaenda wapi sokoni au "
"Kwao "
"Mungu wangu we mtoto ina maana umesha mtimua na huyu, kwani Jensen una shida gani haswa eeh?"
"Mama sina shida yoyote ila kazi imemshinda ndo maana kaondoka"
"Kazi imemshinda wapi au umemfukuza we huku ndani kuna kazi gani ya kumshinda , hivi hujisikii vibaya kila siku unabadilisha wasichana.
Na nahisi ulinipigia ili kuniambia nikutafutie mtu kataa nisikie "
"Ni kweli nilikupigia kukuomba unitafutie mwingine "
"Nikutafutie mwingine ili akae wiki umtimue si ndio ,aaah hapana hii kazi siifanyi tena , yaani mtu mmoja umeshakaa na wasichana wasio pungua 50.
Hapo bado hujaoa hujapata watoto sasa ikifikia umepata yote hayo siutakuwa unawatimua kila baada ya nusu saa?"
"Kama wakienda tofauti na mimi wataondoka ndio , so unanitafutia au nitafute mwenyewe "
"Tafuta mwenyewe mimi habari za kuonekana kituko kila siku sitaki, we nyumba gani isokaa watu kila siku wanaingia na kutoka .
Na nikuulize unaoa lini "
"Kuhusu hilo sahau ila kama kuna lingine ungependa nifanye niambie"
"Lingine lipi, hivi nwanangu we huoni kama umri unasogea baba angu mh!! ,tafuta binti mtulivu oa then mengine yatafutaa au unataka nife bila kushuhudia ndoa yako mwanangu?"
Sikumjibu niliinuka na kumuuliza " unataka kula au kunywa nini?"
Jambo hilo lilimchukiza sana akainuka na kunambia "kijana unajua wazi sipendi dharau za kijinga ,nimekuuliza nataka ujibu na sio kuniletea habari za kupumbavu"
"Upumbavu gani nilio leta mama, kwani niseme mara ngap kwamba sitaki kuoa ? Au nilazima mimi kuoa" niliongea kwa hasira sana.
Mama alipunguza hasira na kusema " mwanangu sio kwamba tuna kulazimisha ila tunataka ufanye hivyo kwasababu ni jambo jema "
"Sijakataa kama ni jema but sitaki wala sitaki kuona mtu akinambia maswala ya kuoa na wewe unalijua "
"Najua na nakulewa lakini baba angu.....!"
"Mama tafadhali " alishusha pumzi ndefu na kani semesha kwa upole.
"Jensen niambie mwanangu ni kitu gani ambacho kimetokea na kukufanya uwe hivi mh nambie baba angu"
"Hakuna kitu mama ni maamuzi yangu "
"Hapana baba tafadhali niambie mimi ni mama yako na rafiki yako pia huenda nita kusaidia "
"Mama ondoa shaka hakuna kitu sawa " niliongea na kuondoka ambapo nilipiga hatua chache akasema .
"Una mahusiano ya jinsia moja?" Kauli ile iliyotamkwa kwa uoga na wasi wasi wajuu ilinifanya nikasimama na kumgeukia mama nikamuangalia na kuona macho yake yatoa machozi.
Kipole nilishusha pumzi nakumrudia kisha nikamwambia.
ITAENDELEA
SIENA (UDHAIFU WANGU NI WEWE)
SEHEMU YA 04
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO..............
"Mama kijana wako nimekamilika na sina hisia yoyote na mtu wa jinsia yangu"
"Sasa kwanini uko hivi mwanangu ,au uliwahi kuumizwa ?"
"Hapana ila sina mapenzi yoyote na ndoa ila kama utataka wakujuu nitajitahidi nikuletee ila ndoa hapana mama"
"Kwanini hapana Jensen, mbona mimi na baba yako tumekuwa na maisha mazuri tu maana kama tungekuwa hatukuishi vizuri ningesema huenda ndo sababu.
Lakini haiko hivyo sasa shida ni nini na me sitaki kukuona ukiharibu maisha ya binti za watu kwa kuwazalisha na kuwaacha ,bali nataka uoe uwe na mke wako.
Na ukumbuke tuna kutegemea katika kuendeleza jina la baba yako maana wewe ndie mtoto wa kiume peke yako katika familia yetu, hivyo jina la baba yako limelala kwako."
"I'm sorry mom,hii ndo itakuwa mara ya kwanza kuenda kinyume na wewe coz siwezi "
"Kwanini usiweze ,unaogopa mapenzi kwasababu ya kilicho mtokea kaka yako?"
Swali lake lilinifanya nikasimama haraka na kutaka kuondoka bila kumjibu kitu ,mama alinishika mkono kunizuia na kuniuliza.
"Ni kweli uko hivyo kwasababu ya hili "
"Ni mapenzi yangu wala hali huasiani na lolote " niliongea na kujitoa mkononi mwake nikaenda ilipo friji na kutaka kuchukua kinywaji akainuka na kusema.
"Haina haja naondoka ,ubaki salama "
Hakusubiri nijibu akaondoka na kuniacha nikimsindikiza kwa mchap.
Baada ya mama kuondoka niliingia chumbani kwangu na kuchukua picha kubwa iliyokuwa ndani ya droo ya kabati kisha nikakaa chini.
Macho yangu yaliangalia picha ile ,picha ya kaka yangu ambae alifariki miaka mitano iliyo pita huku kifo chake kikitokana na mpenzi ๐๐ฉ
Niliangalia picha ile kwa mda mrefu sana ,moyo ulijaa maumivu yasiyo elezeka ,kwani nilimkumbuka sana ndugu yangu.๐
Basi kinyonge nilifuta machozi na kuinuka nikarudisha picha nilikoitoa kisha nikapanda kitandani na kuzama kwenye tafakari nzito.
Kumbu kumbu na matukio ya nyuma ya mimi na kaka yangu yalijirudia kwa wingi kichwani na kunifanya nifunikwe na huzuni kuu๐๐ฉ.
UPANDE WA mama yangu baada ya kutoka huku alienda nyumbani na kufika anakinyonge bila hata kusalimia.
Baba alimuangalia na kumuuliza " vp mke wangu mbona uko hivyo kuna nini?"
Kitendo cha baba kuuliza hivyo mama alianza kulia na kujilaza kifuani kwa mumewe , baba alimkumbatia na kumuuliza kwa upendo sana .
Mama hakuongea alilia hadi pale alipoona inatosha ,akajitoa kwenye kumbato na kumwambia baba .
"Najisikia vibaya sana na sijui kwanini Mungu anaruhusu hili kwangu"
"Unani changanya ujue embu nambie nini kimetokea"
"Nimetoka kwa Jensen "
"Kama sijakosea umeaga unaenda kanisani sasa inakuwaje saizi unasema umetoka kwa Jensen?"
"We nae ina maana hujui kama nilienda ibada ya kwanza au unajitoa ufahamu"
"Umeanza haya nambie huko kwa Jensen kuna nini hadi urudi katika hali hii?"
"Mume wangu nahisi kuchoka mimi , sijui kwanini Mungu amekuwa akinipa adhabu ngumu hivi.
Mwanzo alinifanya nikeshe kuomba yote kwasababu ya kutaka watoto, ikampendeza nikapata watoto wawili kama macho.
Nilifurahi na kumtukuza sana ,huku nikiwalea watoto wangu kwa upendo na kumaadili ya roho na mwili.
Lakini aliikatisha furaha yangu mda ambao ulikuwa ni wamavuno yangu, mwanangu alikufa na kuondoka katika dunia hii .
Nililia lakini nikarudi kumshukuru kwa ajili ya huyu mmoja alieniachia, ila leo anaibua lingine tena"
Baba alishtuka kusikia hivyo akamuuliza kwa sauti ya juu " nini kumkuta Jensen !!?"
"Niambie kwanni huyu mtoto hataki kuoa na sio kuoa tu sijawahi kumuona au kusikia kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na binti yoyote yule.
Nimefuatilia nikitaka kujua kama ana mahusiano au hisia na vijana awenzie lakini hamna sasa shida nini?."
Baba alimuangalia na kurudi kukaa vizuri kisha akamwambia " utakuja kuniua na presha ,yaani umetoka huko kama vile kuna jambo kubwa kumbe ujinga tu."
"Ujinga !! Ina maana unataka yuko sahihi kuto kufanya maamuzi ya kuoa ?"
"Ushasema maamuzi ,sasa unataka kumfanya nini ,muache yeye ni mtu mzima akiwa tayari ataoa kwanini kumpa presha isiyo na maana "
"Aaaaah nimeelewa wewe ndo una muharibu mwanangu"
"Na mharibu kivp?"
"Kivp we hujisikii "
"Sijisikii nini kwani ni uongo? Sikia mke wangu Jensen sio mtoto anajua zuri na baya hata hivyo bado umri una ruhusu so muache ataoa kwa wakati wake"
"Wakati wake upi jitu lina miaka 32 ndo unasema ataoa kwa wakati wake ?"
"Sasa 32 mbili ni miaka mingi kwa mtoto wakiume ?"
"Aaaah nimiaka michache we siulinioa ukiwa na 39 "
"Usinifananishe mimi na watoto wa kizazi hiki ,sasaiv mambo ya mebadilika "
Mama alisonya na kutaka kumjibu ila kabla hajajibu walishtushwa na sauti ya mtu nyuma yao.
Wote waligeuka mara nyuso zao zikabadilika na kupamba na tabasamu nono.
ITAENDELEA
SIENA (UDHAIFU WANGU NI WEWE)
SEHEMU YA 05
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO..............
Kwa furaha mama aliinuka na kusema "Faith mwanangu karibu sana "
"Asante shikamoo baba shikamoo mama" alisalimia na kukaa .
Wote waliitikia salama na kuanza kupiga story, mama akainuka na kumpatia kinywaji kisha amaongezi yao yakaendelea.
Mda ulienda mchana ukapita Faith akiwa nyumbani na ilipofika jioni kaomba kuondoka , sasa kabla mama hajampa ruhusa ya kuondoka akamuuliza.
"Samahani hivi bado mnawasiliana vizuri na Jensen?"
"Ndio mama vp kuna nini?"
"No nimeuliza maana animeonana nae leo ila hakunambia kama umerudi"
"Oh kuhusu hilo sijamwambia ila nimetaka kumsurprise "
"Ooooh nimeelewa ,aam naomba samahani kwa hili nitakalo ongea ila nahitaji sana msaada wako."
"Sawa mama kuwa huru "
"Nilikuwa naomba kama itakupendeza uolewe na mwanangu Jensen " kauli hiyo ilimshtua baba na kujikuta akipaliwa juice , mama hakujali akaendelea kuongea na Faith.
"Mama kwanini unataka niwe mke wa Jensen ile hali sina mahusiano nae!" aliuliza Faith kwa mshangao sana .
Mama alitabasamu na kumajibu " nikweli hauna mahusianao nae na ndio maana nimesema naomba, aaam iko hivi Jensen hataki kabisa kuoa.
Na nimejaribu sana kumfuatilia ila sijaona historia ya mahusiano kwake zaidi yuko bize na mambo mengine , sasa kama mzazi natamani sana kumuona akianzisha familia.
Lakini imekuwa ngumu mno, na ndio maana nimewaza unisaidie katika hili maana najua nyie mko karibu kwa miaka mingi.
Hivyo inaweza kuwa rahisi kutengeza hisia bora za mapenzi na mkawa wanandoa wazuri maana mnafahamiana vizuri sana"
Faith alikaa kimya kwa mda akionesha kufikili "samahani kama nitakuwa nimekukwaza" aliongea mama baada ya kuona Faith amekaa kimya.
Faith alitabasamu na kumwambia mama" Hapana mama hujanikwaza ila nilikuwa najaribu kifikilia hili swala , aam kidogo linauzito kwasababu ili litokee hilo lazima upendo uwepo.
Na maanisha mapenzi kitu ambacho kwetu hakipo zaidi tuna urafiki tu"
"Naelewa yote mwanangu ila naomba utumie kila njia ifaayo Jensen akupende na akubali kuanzisha maisha na wewe"
Kabla Faith hajajibu baba alitaka kuongea ila mama akamkanyaga kumziua , kweli akatulia Faith akasema.
"Unafikili itawezekana?"
"Bila shaka mwanangu kinacho takiwa ni wewe kuwa tayari labda nikuulize si unampenda Jensen?"
Swali la mama likimfanya Faith akaangalia chini kwa aibu na kushindwa kujibu, mama alitabasamu na kumshika begani na kusema.
"Na kuahidi utakapo fanikisha hili swala nitakupa zawadi kubwa sana na daima nitakuwa mama mwema sana kwako "
"Haina shida mama nitafanya hivyo wala usijisumbue kwa lolote" aliongea Faith akiwa bado kaangalia chini kwa aibu.
Mama baada ya kuona binti kakubali aliinuka akaingia chumbani na kutoka na kibox kidogo ambacho ndani yake kulikuwa na mkufu wa dhahabu.
Alifika na kumkabidhi Faith huku akisema " niliandaa zawadi hii kwaajili ya mke wa mwanangu kwakua umepatikana sina haja ya kukaa nao tena "
Faith alitaka kuukataa mama akamshika mkono na kumpatia mkufu huo huku akitabasamu, Faith alipokea na kuomba kuondoka .
Hakukuwa na laziada akaruhusiwa na bila kuchelewa akainuka na kuondoka.
Baba alikaa kimya huku akimuangalia Faith namna anavyo tembea kutoka ndani na alipo fika mlangoni akamgeukia mkewe na kumuuliza.
"Ni upumbavu gani huu unataka kufanya"
"Nadhani umesikia vizuri so sioni haja ya kuuliza maswali "
"Huoni haja ya mimi kuuliza maswali, hivi umeanza kuchanganyikiwa eeh mtu kashakwambia siko tayari kuoa sasa yanini kumtafutia mtu? ,au umesahau kama zama zimebadilika ?"
"Zimebadilika kwao sio kwangu na mtoti wangu , wee kaa subiri uone namna kijana atakavyo badilika na kurudi kwenye njia nzuri"
"Jichanganye siku utakuja kulia mbele yangu sitakufuta machozi "
"Nitatumia hata tissue ๐,ila siwezi kukaa na kuona jitu lina zeeka bila ndoa"
"Haya "
Siku hii ilipita kwa upande wangu iliisha nikiwa vibaya mno , Kesho yake asubuhi niliamka na kujiandaa nikaenda kazn .
Kufika huko mida ya chai nikamuomba msaidizi wangu anilitee maana sikutaka kutoka nje , kweli zilipita dakika kadhaa binti akagonga nikaruhusu aingie.
Akafungua mlango na kutembea kwa mwendo wa madaha, akafika na kuweka cahi mezani , macho yangu yalitua kwenye kifua kilicho tuna vizuri.
Kisha nikamuangalia binti huyo usoni na kumwambia " ukiwa unakuja ofisin kwangu tafadhali vaa vizuri ,sio kunijia ukiwa umeacha maungo yako wazi ,mimi sio mwanaume wako ni boss wako.
Na hakuna namna yoyote utakayo fanya kubadilisha hilo maana naona unatumia nguvu nyingi na kuishia kujidhalilisha " niliongea kwa msisitizo huku nikiwa nimekunja sura.
"Samahani boss" aliongea huku akitengeza nguo yake vizuri kisha akaondoka.
Sekunde chache baada ya binti huyo kutoka akaingia Marko huyu ni rafiki yangu kinyama, Marko aliingia huku akishika ndevu zake na kukaa .
"Vip bro uko poa" alisalimia baada ya kukaa.
"Yeah kama unavyoniona ,mh naona ulipotea ghafla "
"Aaah mambo mengi si unajua tena , halafu nimepishana na binti flani hivi akitoka humu aisee nimkali kinyama "
Aliongea nimamuangalia jicho kali na kusema " umeanza kujisahau ee?"
"Aah bwana acha zako ,utawalindaje wafanya kazi kama dada zako ,we tulia mtu akipenda achukue chombo"
"Nadhani mtaani vyombo unavyo taka havijaisha ,so unaweza kutumia hivyo nasio wafanyakazi kazi wangu"
" kwa hiyo hata nikitaka kuoa utakataa"
"Wakuoa yuko wapi wewe au mwingine ?"
"Ona dharau zako kwamba mimi siwezi kuoa au sifai?"
"Achana na hizo mada mh nambia kuna ishu gani"
"Sina jipya nilikuwa nakatiza nikaona si mbaya nikapita kukucheki mara moja "
"Oh nashukuru sana "
"Pamoja , sasa acha niondoke basi tutaonana wakati mwingine "
Nilijibu sawa akainuka na kutaka kuondoka ila nikamuita na kusema .
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote