Follow Channel

SIERRA

book cover og

Utangulizi

SIERRA
SURA YA 1

Sierra
"Hannah, Martina, darasa langu si saluni ya urembo. Tafadhali wekeni vipodozi vyenu chini," naliita wasichana walioko nyuma ya darasa ambao wako bize sana kujipodoa hadi hawasikilizi neno hata moja ninayosema.
"Hannah! Martina!" nikawakemea tena.
Wanainua macho yao taratibu kutoka kwenye kioo walichokuwa wakikitazama.
"Ndiyo, Mwalimu," Hannah anaitika, akidhani naita mahudhurio.
"Weka vipodozi chini."
"Dakika moja tu."
"Hapana. Sasa hivi."
Ni asubuhi ya Ijumaa. Wikiendi iko karibu kiasi kwamba nahisi ladha yake mdomoni, lakini kama hiki ndicho kielelezo cha siku yangu itakavyokwenda, basi nadhani ningependa kujiondoa mapema.
Ninapenda kazi yangu...siku nyingi. Nilitamani kuwa mwalimu kwa muda mrefu sana, lakini kila mwaka huwa kuna wanafunzi wachache ambao hunisumbua kupita kiasi. Hannah ni mmoja wao.
Hapo mwanzo hakuwa kwenye kundi langu la wanafunzi, lakini baada ya kutofautiana vibaya na msichana mwingine, ilibidi ahamishwe. Na kwa kuwa mimi ni "mpole", nilijitolea kumchukua. Nilipaswa kujua ningejuta hilo.
Sasa si tu yuko kwenye darasa langu la Kiingereza la GCSE, bali pia huja hapa kila asubuhi.
Akinitazama kwa tabasamu tamu lisilo na maana yoyote, anafanya maigizo ya kuweka kila kipodozi ndani ya mkoba wake polepole.
Siwezi kujizuia kukunja macho kwa kuchukizwa, kisha najigeuzia kwenye kompyuta yangu ili kuendelea na mahudhurio.
"Mwalimu," anaita tena. "Umeona nani anafanya mkutano leo?"
"Ah...hapana."
"Yaani OMG. Mgoogloe sasa hivi."
Amekwishasimama kwenye kiti chake na kukimbilia mbele ya darasa.
"Hannah, kaa chini. Tutachelewa."
"Mwalimu, tafadhali. Haraka tu. Utaelewa mara moja ukimwona."
Ninapumua kwa nguvu nikijaribu kuzuia hasira zangu zisianze kufukuta, kisha namrudisha kwenye kiti chake. Kila mtu anajua kuhusu mafanikio ya Zade Meadows.
Pengine yeye ndiye mtu maarufu zaidi kuwahi kutoka shule hii, na shule inapenda kulitaja jina lake kila inavyopata nafasi. Huwa anakuja mara kwa mara, lakini hii ni mara yangu ya kwanza kumwona kwa macho.
Amefanikiwa sana, ana utajiri wa kutosha, na kwa mujibu wa kila mfanyakazi wa kike — na baadhi ya wanaume — ni mtanashati wa ajabu. Kwangu mimi hayo yote yanasikika kama hadithi ya kufikirika.
Ninakamilisha haraka mahudhurio na matangazo ya kila siku, kisha nawasindikiza wanafunzi kuelekea ukumbi mkuu kuona huu mkutano wa ajabu.
Nikiwa nyuma ya Hannah na marafiki zake, nawatizama wakitengeneza nywele zao na kujiviringisha sketi zao juu zaidi.
"Hamdhani kuwa yeye ni mzee sana kwa ajili yenu?"
Wakigeuka, wasichana wananitazama kwa macho makali.
"Mimi nina miaka kumi na sita tayari," Hannah ananung’unika. "kwani? Unadhani atakupenda zaidi wewe?"
Nikicheka kwa kejeli, sihangaiki hata kujibu. Haijalishi kama atanipenda mimi — si kwamba mimi nipo tayari kumpenda yeye, hata kama ana sura ya kuvutia kama mungu wa Kigiriki.
Tunaungana na kundi lote kwenye ukumbi na ninawatazama wanafunzi wangu wanapoketi nyuma. Kuna gumzo la furaha kuliko kawaida, na ninapotazama mbele, naelewa kwa nini.
Kila mwalimu, isipokuwa mimi, amesimama kwenye kikundi, wakimzingira Bwana Meadows pengine.
Nini hasa kuhusu mtu huyu kinachowafanya kila mmoja kupoteza mwelekeo?
Mkuu wa Idara hatimaye anakohoa kuashiria kuanza kwa mkutano.
Lakini mimi bado nimeshughulika kuwatazama wasichana ambao wanaendelea kuzungumza na kucheka kana kwamba hawapo kwenye hafla rasmi.
Punde tu sauti nyingine inaposikika, mwili wangu wote unasisimka.
Ni sauti nzito, ya kukwaruza, na ghafla tumbo langu limejaa vipepeo. Nikihisi ni kama najidanganya, naendelea kuwachunguza wanafunzi mbele yangu, lakini ninapoona kuwa wote wameduwaa wakimtazama mwanaume anayezungumza kwenye jukwaa, na mimi naamua kumtazama pia.
Ninavuta pumzi kwa mshangao mara tu ninapomwona.
Macho yake mepesi yananikodolea macho moja kwa moja na hata ninapojaribu, siwezi kugeuza macho yangu.
Moyo wangu unapiga kwa kasi na joto la mwili wangu linapanda haraka huku tukitazamana.
Chumba kizima kinapotea. Wazo kwamba kuna wanafunzi mia kadhaa karibu yangu linayeyuka kabisa akilini mwangu.
“Ukishajua unachokitaka, unapaswa kutumia kila njia uliyonayo kuhakikisha unakipata.”
Maneno yake yanapenya taratibu ndani ya fahamu zangu, kisha kwa kutikisa kichwa kidogo, anageuza macho yake pembeni.
Ninavuta pumzi nzito kwa nguvu, kisha najiegemeza ukutani na kujirusha kwenye kiti kilicho karibu nami.
“Mwalimu, uko sawa kweli?”
Harry, mmoja wa wanafunzi wangu, anauliza huku akinitazama kwa mshangao anapoona jinsi ninavyopumua kwa shida.
“Ah…ndiyo. Niko sawa.”
Lakini uso wake wa wasiwasi unaonyesha wazi kuwa sionekani nikiwa "sawa" hata kidogo. Hata hivyo, anarudisha macho yake kwa mwanaume aliye juu ya jukwaa.
Nikijaribu kutuliza mapigo yangu ya moyo ambayo yameanza kwenda mbio, ninalenga macho yangu kwa wanafunzi. Lakini kwa bahati nzuri, sihitaji kuwa na wasiwasi — kila mwanafunzi ametulia kabisa, macho yote yakiwa yameelekezwa mbele ya ukumbi.
Kwa jicho la pembeni, ninamchungulia yule mwanaume anayezunguka kwa utulivu juu ya jukwaa. Amevaa suti ya kijivu iliyokaa mwilini mwake kana kwamba imeshonwa juu ya ngozi yake. Mungu wangu, nani anayemudu kununua suti ya namna hiyo?
Taya lake limechorwa vyema, limefunikwa kwa ndevu ndogo zilizonyolewa kwa ustadi wa hali ya juu, na nywele zake… ni za rangi ya fedha.
Endeleaa…


SIERRA
SURA YA 2

Zade
Shule hii ni sehemu kubwa sana ya maisha yangu. Watu wanaweza wasiamini wakinitazama sasa, lakini mwanzo wangu haukuwa wa kifahari hata kidogo.
Nilikulia kwenye chumba cha kupangisha chenye vyumba viwili pamoja na wazazi wangu, na nilihudhuria shule hii ya mjini. Kwa miujiza fulani, walimu wachache waliona kitu kizuri ndani yangu, na niliweza kuhitimu nikiwa na matokeo ya wastani.
Lakini kilicho muhimu zaidi kuliko barua zile chache kwenye cheti, ni ushauri kutoka kwa walimu hao.
Sidhani kama walijua kuwa kile walichoniambia kingebaki moyoni mwangu, lakini walinipa ujasiri wa kuhatarisha, kuweka kila kitu nilichokuwa nacho mezani kwa imani kwamba kitazaa matunda.
Nawadhamini sana walimu wale waliokua na imani nami miaka hiyo. Bila wao, nisingekuwa mwanaume niliye leo.
Ndiyo maana nimesimama hapa, nikiangalia ukumbi ukijaa vijana waliokaribia kuandika historia yao wenyewe.
Kama nitaweza kumfikia hata mmoja tu kupitia maneno yangu leo, basi nitajua kuwa nimelirudishia japo kidogo sehemu hii ambayo ndiko kila kitu kilipoanzia kwangu.
Hotuba yangu naifahamu kwa moyo. Nimeitoa mara nyingi.
Lakini pindi ninapopanda jukwaani na kuwatazama wanafunzi na walimu walioketi mbele yangu, akili yangu inakuwa tupu mara tu ninapomtambua mwalimu mmoja ambaye sijawahi kumuona hapo awali, akiwa anatupia macho makali wanafunzi walioko mbele yake.
Amevaa mavazi ambayo ni ya kawaida kwa mwalimu — sweta ya rangi ya waridi iliyonakishiwa vizuri na sketi ya A-line.
Haipaswi kuonekana ya kuvutia, lakini namna nguo hizo zinavyozingira umbo lake, inabadili maana nzima.
Uume wangu unajibu haraka, na mate yananijaa mdomoni ninapoachia macho yangu yamtembelee kwa utulivu.
Kimya kikiendelea kwa sekunde moja zaidi ya kawaida, maneno yangu — ambayo nimezoea — yananza kutoka kinywani mwangu bila shida. Lakini bado macho yangu hayajamwacha.
Natarajia angalau atanitazama, lakini inaonekana hachukizwi wala havutwi na macho yangu.
Ni hali ya kupendeza, ukizingatia kuwa kila mfanyakazi mwingine ambaye ameniona leo asubuhi alikimbilia kuja kuniambia “hi”... hasa wanawake.
Naweza kuonekana najiamini kupita kiasi — na huenda ni kweli — lakini najua taswira niliyo nayo hadharani.
Na ni kweli, mara nyingi hutumika kunisaidia nipate ninachotaka.
Lakini kuna kitu ndani yangu kinaniambia kuwa jina langu na sifa yangu havitanisaidia sana kwa huyu mmoja.
“Ukishajua unachokitaka, tumia kila njia kuhakikisha unakipata.”
Maneno hayo yanamfanya ageuze kichwa na kunitazama, na laana, nahisi pumzi ikinikatika kwa muda macho yetu yanapogongana.
Sijui ni rangi gani ya macho yake kutoka hapa nilipo, lakini tayari nimeshikwa na mvuto wake.
Ananitegea jicho kwa muda mfupi zaidi ya kawaida.
Huenda yeye hajui, lakini muda huo mfupi unatosha kuniambia kuwa yuko na hamu fulani.
Nasimamia maneno yangu — ukishajua unachotaka, hakuna kitakachokuzuia.
Mwalimu huyu mwenye nywele nyekundu za kuvutia atakuwa wangu kabla siku haijaisha.
Hamasa ya kumwangalia kila baada ya sekunde chache inazidi kuongezeka kadri mkutano unavyoendelea.
Labda nimekosea na yeye hajisikii kama ninavyohisi, au labda anacheza mchezo mzuri wa kujifanya haoni.
Ningebashiri kwa uhakika kuwa ni hilo la pili.
Mara tu kengele ya kipindi cha kwanza inapolia, anafuata wanafunzi wake kutoka ukumbini kwa haraka.
Wazo la kumfuata linakandamizwa ghafla pale mwalimu mkuu anapokuja kuniambia jinsi hotuba yangu ilivyogusa wengi.
“Asante sana, Zade. Kama kawaida, hotuba zako huwa na msisimko wa kipekee. Sina shaka kuwa wanafunzi watajifunza mengi kutokana nayo.”
“Asante. Kama nimemgusa hata mmoja tu, basi imenilipa.”
Naishia kutumia saa kadhaa naye, tukijadili kuhusu upanuzi wa shule ambao ninaufadhili pamoja na mambo mengine.
Ni mtu mzuri, na japokuwa ni mkubwa kwangu kwa miaka michache tu, anaonekana kufurahia urafiki wetu wa ghafla.
Sina uhakika kama uhusiano huu utavuka mipaka ya shule, lakini sina tatizo kumpa ushirikiano.
Inatusaidia wote, na kwa upande wangu, kuna nia…
Nahitaji kumtafuta yule mwalimu mwenye nywele nyekundu.
Nitapita kila darasa kama itabidi, lakini natumaini haitafika huko.
“Naona kulikuwa na walimu wapya asubuhi ya leo. Umeajiri watu wapya?”
“Walimu wetu wakongwe kadhaa wamestaafu. Pengine wengine waliokufundisha pia,” anasema kwa kicheko.
Anapenda sana kazi yake, shule hii, na wanafunzi wake, hivyo najua kuwa kuuliza swali hilo kunanipa nafasi ya kupata ninachotafuta.
Ana shauku sana ya kuzungumzia malengo yake.
“Bwana Richardson, yule mwenye koti la mistari, ni mpya katika idara ya IT. Wanasema ni bingwa wa programu, ingawa mimi siielewi sana hiyo.
Bwana Ashcroft anafundisha sayansi, na Bi Walsh ni mwalimu mpya wa Kiingereza. Anavutia sana na ni mzuri kwa wanafunzi. Wanamkubali kweli.”
Ninasogea kidogo kitini.
Naam, si wanafunzi pekee wanaomkubali, nafikiria huku nikitafuta njia ya kujua yuko wapi bila kumfanya mwalimu mkuu ahisi nia yangu halisi.
Endelea…


SIERRA
SURA YA 3

Sierra
Baada ya kuhisi kuwa siku hii ingeendelea kuwa mbaya, nimejikuta nikishangazwa kwa namna ya kupendeza. Vipindi vyangu vinne vya leo vimeenda vizuri kiasi cha kuridhisha, na isipokuwa wanafunzi wachache ambao hawajakabidhi kazi ya nyumbani, sijakumbana na matatizo yoyote.
Lakini hiyo haimaanishi kwamba ninaweza kuelekeza akili kwenye kazi ninayojaribu kusahihisha.
Mkutano wa asubuhi huenda umepita kwa saa kadhaa sasa, lakini bado nahisi mshtuko wa umeme ulionipitia mwilini wakati alinitazama.
Bado nahisi hisia zile tumboni kila nikikumbuka jinsi macho yetu yalivyokutana — hata tukiwa na umbali mkubwa ndani ya ukumbi ule.
Mlango wa darasa unapogongwa, sichukulii kwa uzito wowote. Wanafunzi wamezoea kuweka vichwa vyao ndani kuuliza maswali au kuazima vitabu.
"Ndiyo," ninasema bila hata kuangalia juu kutoka kwenye insha ninayoihangaikia kwa bidii.
Mlango unafunguka na kuingiza mlio wa kishindo laini, na ninakaribia kuinua macho yangu, nikijiuliza kwa nini mtu huyo hajasema chochote — ndipo nasikia ile sauti.
"Bi Walsh?"
Moyo wangu unaruka na mwili wangu unatetemeka.
Shit. Kwa nini yuko kwenye darasa langu?
"Ndiyo... aa... hodi."
Kiti changu kinagonga ukuta kwa kishindo nyuma yangu ninaposimama haraka na kunyosha mkono wangu kwa ulegevu ili kumshika mkono.
Tabasamu linacheza midomoni mwake anapotazama kutoka usoni kwangu hadi kwenye mkono wangu uliojitokeza mbele.
Taratiibu, anainua mkono wake na vidole vyake vinateleza juu ya vya kwangu.
Umeme unakipita mkono wangu mzima punde tunapogusana, na macho yangu yanapaa juu kwa mshangao.
Macho yake yanapanuka kwa sekunde moja tu, lakini kama ameshangazwa na hisia hizo, haonyeshi kwa dhahiri.
Vidole vyake vya joto vinauzunguka mkono wangu mdogo na kabla sijaelewa kinachotokea, ninavutwa karibu naye ghafla.
Joto la mwili wake linaniunguza upande wa mbele wa mwili wangu.
Ninajaribu kulenga macho yangu kwenye tai yake ya fedha mbele yangu.
Kisha anainama, na pumzi yake inanisisimua kwenye sikio.
"Niambie kama huna mpenzi," ananong’ona kwa sauti ya amri.
Nikiwa nimeshtushwa kwamba alikuja hapa kwa ajili ya jambo moja tu, mwili wangu unafanya kazi kabla akili haijachakata.
Ninauvuta mkono wangu kwa nguvu, na kabla sijajua kilichotokea, kofi langu limepiga shavu lake na sasa anashika taya yake.
Macho yake yamejaa moto — na kama nilidhani kwa sekunde moja kuwa kofi hilo lingemzuia, basi nilikuwa nimekosea kabisa.
"Nitachukulia hilo kama ndiyo," anasema kwa utulivu.
"Chukulia utakavyo. Samahani, lakini niko bize."
"Hakuna shida."
Namtazama anavyopita haraka kutoka upande mmoja wa darasa hadi mwingine.
"Nina muda wote wa siku."
Mdomo wangu unabaki wazi kwa jinsi anavyojiamini kupita kiasi.
"Unataka kutazama nikisahihisha insha hizi?"
"Hapana. Nitasubiri umalize kuzisahihisha, halafu nakuchukua kwenda kupata chakula cha usiku."
"Sikumbuki kukubali hilo."
"Utakubali."
"Kweli?"
Sijui kama ninapaswa kukasirika au kuvutiwa na namna anavyojiamini.
"Nina uhakika kuna wanawake wengi huko nje wanaokubali kila neno lako, Bwana Meadows. Lakini naweza kukuambia kwa hakika, mimi si mmoja wao."
"Shukrani Mungu kwa hilo. Wanawake wa aina hiyo wananiboa sana."
Ninasimama na kumtazama, nikiwa nimechanganyikiwa kabisa na mazungumzo haya yote.
"Twende basi. Niliruka chakula cha mchana, na sipendi kula usiku sana."
"Sitakwenda kula nawe chakula cha usiku," najibu kwa msisitizo, lakini sura yake ya kujiamini inanionesha kuwa huyu ni mwanaume ambaye hupata anachotaka — na hiyo inajumuisha mimi.
Ananiangalia kila ninaposogea kuelekea mezani na kuinua kiti changu.
Ninavuta karatasi ile ile niliyokuwa naisoma kabla na kujaribu kuelekeza akili yangu humo.
Lakini maneno yananitatanisha, hayaingii kichwani.
Ninachoweza kuhisi ni harufu yake ya kiume iliyojaa hewani na mtetemo wa ajabu unaonipitia nikijua kuwa bado ananitazama.
Ninapuliza pumzi ndefu ya kufadhaika, naweka mikono yangu juu ya meza, kisha najipa ujasiri kumtazama tena.
Maneno yaliyokuwa karibu kutoka mdomoni mwangu yanayeyuka pindi macho yetu yanapogongana tena kwa nguvu ile ile ya awali.
Ninayarudisha macho yangu chini haraka na kumchunguza tena — nywele zake za fedha zinamfanya aonekane mzee zaidi kwa mbali kuliko alivyo kwa kweli, macho yake ya buluu ya barafu, mashavu yake makali na taya iliyochongwa kwa ustadi.
Sifiki mbali kabla hajasafisha koo na kunirudisha macho juu kwake.
"Tunaweza kwenda sasa?"
Uso wake umejaa tabasamu la dhihaka, ukionesha upande tofauti wa huyu mfanyabiashara mwenye jeuri.
Ninapima chaguo langu — kukaa hapa nikijifanya kusahihisha insha huku akinitazama, au kutoka tu kwenda kula.
Chaguo moja linaonekana kuvutia zaidi, hata kama si kwamba ninavutiwa naye.
"Sawa, lakini lazima unipeleke nyumbani kwanza kubadilisha nguo."
Ninaposimama tena, nachukua koti langu lililokuwa nyuma ya kiti na kuanza kuivaa.
Lakini kabla sijalivaa, tayari yuko pembeni yangu.
"Kwa nini? Mwonekano huu wa mwalimu asiye na hatia ni wa moto kupindukia."
Aibu inayopanda usoni mwangu haikomi mpaka inashuka hadi shingoni na kifuani.
"Niruhusu," anasema kwa sauti tulivu, akichukua koti langu na kulishikilia kwa ajili yangu.
Kitendo chake cha kistaarabu kinakinzana kabisa na maneno yake ya awali.
Endelea….

SIERRA
SURA YA 4

Zade
Kwa mkono wangu nyuma ya mgongo wake mdogo, namuongoza Sierra kuelekea sehemu ya maegesho ya walimu hadi kwenye gari langu.
"Naweza kupanga mtu akuchukulie gari lako na kulipeleka nyumbani," nasema kwa uhakika.
"Bila shaka unaweza," anajibu kwa kicheko — japo nahisi ni zaidi ya kuungulia.
"Gari lako ni lipi?"
"Sina gari."
"Oh."
"Kwa kawaida hupanda treni kwenda kazini. Si sisi sote tunaweza kumudu magari ya kifahari kama hilo," anasema huku akielekeza macho kwenye Porsche yangu na kuonekana kama haijamvutia kabisa.
Nilijua tangu pale macho yetu yalipokutana kuwa huyu mwanamke ni tofauti. Lakini sikutarajia kuwa itachukua juhudi kubwa kiasi hiki kumshawishi aende chakula cha usiku nami.
Sikumuomba afunge ndoa nami, kwa jina la Mungu.
Baada ya kumfungulia mlango na kumsaidia kuingia, ninazunguka hadi upande wa dereva tayari kuanza "miadi" hii.
Sikujitayarisha hata kidogo kwa harufu ya manukato yake iliyojaa ndani ya gari — vanila iliyochanganywa na harufu ya maua inayonigusa moja kwa moja kwenye mishipa.
Kuna kitu juu ya mwanamke huyu kinachonigusa kila sehemu ya nafsi yangu, na ni jambo la ajabu kwamba sijui ni nini hasa.
Najua tu kwamba sina uwezo wa kujitenga naye.
Wanawake wengi husahaulika mara tu baada ya usiku mmoja wa moto. Lakini Miss Walsh ni tofauti kabisa.
Hata jina lake la kwanza silijui bado, lakini tayari yupo chini ya ngozi yangu.
"Hii ni ya ajabu," analalamika huku gari likitembea polepole katikati ya msongamano wa jiji.
"yaani ningekua karibu kufika nyumbani sasa hivi kama ningetumia treni. Unafanya nini sasa?" anauliza ninapogeuka na kuingia barabara ya pembeni na kupaki.
"Inaonekana unapenda sana treni ya chini ya ardhi. Miaka mingi imepita tangu niitumia. Basi twende nayo."
Ninapofika upande wa abiria, bado ameketi pale mdomo wake ukiwa wazi kwa mshangao.
"Uko serious?" anauliza ninapomshika mkono na kumvuta kutoka kwenye gari.
"Nilikuambia leo, nikishatamani kitu huwa napata."
"Sikujua hilo linajumuisha usafiri wa umma."
"Mimi pia."
"Hutapigwa faini? Eneo hili linaonekana kama ni la wakazi tu."
"Litakuwa sawa. Twende."
Bado nikiwa nimeushikilia mkono wake, tunatembea bega kwa bega kuelekea kituo cha treni.
Treni ya chini ya ardhi ni kila kitu nilichokikumbuka — na haraka ninakumbuka pia kwa nini niliiacha miaka mingi iliyopita.
Tukiwa tumeketi ndani ya behewa, tukiwa tumepambwa na wanafunzi na watalii, nahisi macho yake yamenikodolea.
Ninapotazama, anacheka kimyakimya.
"Unacheka nini?" nauliza.
"Wewe huendani kabisa na mazingira haya, Bwana Armani."
Ninapotazama upande wangu, siwezi kujizuia kukubaliana naye.
Tuko kwenye dunia mbili tofauti kwa sasa.
"Ulijua vipi suti yangu ni ya Armani? Nilidhani huvutwi na vitu vya bei ghali."
"Sivutwi. Nilihisi tu."
Ananiongoza kupitia vituo vitatu vya treni hadi tunapopanda ngazi za umeme, nami nikiomba tu nipate pumzi safi tena.
Yeye anaonekana nyumbani kabisa kwenye mazingira haya — amezingirwa na watu wa kawaida wa jiji.
Ni ukumbusho mchungu wa jinsi nilivyojitenga na uhalisia.
Haijapita muda mrefu tangu haya ndiyo yalikuwa maisha yangu.
Haikuwa kila mara ofisi za juu na magari ya mamilioni pamoja na suti za wabunifu maarufu.
"Najua si kile ulichokizoea," anasema kwa huzuni tunapopita barabara chakavu hadi kufika kwenye jengo la nyumba za kupanga.
"Hujawahi kuona nilikokulia. Pale kunafanya hapa paonekane kama Kensington."
"Siamini sana hilo, lakini kama unasema..."
Sehemu kubwa ya nafsi yangu inataka kumueleza jinsi nilivyopambana mpaka nikafika nilipo, lakini sehemu nyingine — iliyo na njaa na shauku kwake — inataka zaidi.
Kuchimbua yaliyopita kutachelewesha yote mawili.
Nikifanikiwa, tutajipa nafasi ya kuongea kutoka moyoni baadaye.
"Umewahi kurudi mapema, mpenzi wangu," sauti ya kike inaita mara tu tunapoingia ndani ya nyumba.
"Oh... una mgeni."
Mwanamke aliyejitokeza sebuleni bila shaka ni mama wa Sierra.
"Mama, huyu ni Bwana Meadows. Ameshikilia sana kunipeleka chakula cha usiku," anasema kwa sauti ya haraka.
"Anasubiri kwa hamu vilevile, huoni?" nacheka nikijibu kwa kejeli.
Akininyooshea mkono wake kwa adabu, anasema,
"Nimefurahi kukutana nawe. Mimi ni Dawn. Utapenda chai?"
"Hatukai mama. Nataka kubadilisha nguo tu." Sierra anasisitiza.
"Acha dharau. Una muda wa kunywa kikombe kimoja, si ndiyo, Bwana—"
"Niite Zade. Na nitafurahia kikombe cha chai, asante sana."
"Karibu ndani, nitakuletea muda si mrefu," mama yake anasema kwa furaha.
Ninapotembea kuelekea sehemu aliyoniambia, natabasamu nikisikiliza mazungumzo mafupi na makali kati ya mama na binti yake nyuma yangu.
"Samahani sana. Ngoja niweke maji ya moto," mama anasema kwa aibu.

Endeleaa…


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote