SIKUJUA WA MTAA WA SILALI

book cover og

Utangulizi

Kwakuwa leo siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu namsamehe huyu bibi. Mtoeni nje ya kambi aende na mambo yake". Ni maneno yaliyotoka kinywani kwa Captain Isaac. Bibi yule hakutaka kutoka mpaka apate kilichompeleka. Hakutaka kuendelea kuvunga alimuomba Captain Hela ya bia huku akisema hata yeye leo ni siku yake ya kuzaliwa. Wanajeshi wote walimshangaa huyo bibi kipofu anayeomba hela ya bia. Alionekana kuchoka kimaisha sana ni muda ambao alifaa kujisogeza karibu na MUNGU ila kwake ni kama vile ndo alikuwa anazidi kujipeleka motoni. Captain alimpeleka nyumbani kwake. Walianza kunywa Bia wote. Bibi alikua kasi kunywa mpaka Mjeshi huyo alimshangaa. Bibi alijikuta anajisahau sasa na kuuachia muonekano wake. Kumbe hakuwa mbibi wala kipofu kama wanajeshi walivyodhani. Alikuwa ni binti mdogo tu anayefahamika kwa jina la SIKUJUA WA MTAA WA SILALI. Ni binti maarufu sana mitaani na yote ni kwaajili ya tabia zake mbaya mbaya za wizi , utaperi , mdomo mchafu, udangaji n.k. Anadondokea mikononi kwa Captain wa jishi Mr Isaac......mwisho wa siku wawili hao wanadondokea penzi zito kilo 250. Licha ya Sikujua kuwa na mahusiano na mtu mzito haimfanyi yeye kuacha wizi na utapeli na hatimaye anamuibia hadi mama mkwe wakeπŸ€£πŸ˜„πŸ˜„πŸ™ŒπŸ™Œ.........WADAU HII STORY TAMU MPAKA TAMU TENA. YAANI UNASOMA KITU ROHO INAPENDA. USIKOSE MKASA HUU UNAOKONGA MOYOπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ‘ŒπŸ˜‹.

SIMULIZI : SIKUJUA WA MTAA WA SILALI
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 01

MWANZO.......
Kila sehemu unayopita utasikia watu wakijadili kuhusu Sikujua! kila kitu ni Sikujua.
Yaani hili jina limekuwa maarufu sana kuliko hata vijora vya mwendokasi.
Kuitwa Sikujua badala ya jina lako ni kawaida sana ndani ya mtaa wa Silali

Sikujua mwenyewe sasa hajijui kama ni mtu maarufu mtaani kwao.
Ni binti mdogo tu lakini akili zake hazina tofauti na Nyumbu wa pori la Serengeti.

Utasikia Sikujua alikuwa hapa, Sikujua alipita pale hivyo mara nyingi watu wa Silali hukaa chonjo ili mradi tu wamtie machoni.
Ni binti choka mbaya tu kama wengine.....kudanga na kuiba vitu vya watu ni kawaida sana kwake.

Ameshazoea kulala Polisi, na mara nyingi akiona kesi inamzidia haoni tabu kutoa rushwa ya ngo....no.
Kitu pekee anachokilinda ni tigo tu....yupo radhi akae Polisi Mwezi mzima lakini si kugawa tigo yake.

Mbali na kuwa mwizi na Mdangaji, binti huyu ni tapeli na dalali mzuri kwa watu wanaohitaji vyumba, viwanja, magari n.k

Kuna muda unaweza kumfananisha na Beyonce lakini kuna wakati anaonekana kama Zuwena wa kwenye wimbo wa Diamond.

Ni kawaida yake kupanda kwenye daladala akiwa hana pesa na pale anapodaiwa huonesha kitambulisho feki cha Polisi au Mwanajeshi.

Siku ya leo alikuwa na hamu sana na kunywa bia...alijipitisha sana kwenye viwanja ilimradi tu aitwe lakini hakuwa na bahati kabisa.
Hiki kitu kilimuuma sana kwa sababu alihisi koo lake linamkauka.

Kila bar aliyoingia walimgomea kumhudumia mpaka atoea pesa kwanza.
Sikujua hakuamini kama utapeli wake una fahamima kila sehemu anayoenda.

"Tokeni hapa na hizo K zenu zilikokaa upande mfyuuu" Sikujua aliporomosha tusi baada ya kuzuiliwa kuingia kwenye bar mpya iliyofunguliwa hivi karibuni, hakutarajia kama hata wao wana taarifa zake za utapeli.

Wazo la kujifanya omba omba kipofu lilimuijia.
Hakuna omba omba hata mmoja aliyewahi kuingia kwenye Kambi ya Wanajeshi wa Silali lakini yeye aliamua kujizima data siku ya leo.
Siku zote akitaka kitu huwa ametaka bila kujali kitamuweka hatarini au la.

Alijiweka katika hali ya Bibi kizee, hakutaka kujua nini kitatokea alijikokota taratibu mpaka Kambini kwa Wanajeshi.

Ili ahurumiwe zaidi, alianza kuimba wimbo wa Taifa.

🎡 Mungu ibariki Afrika, wabariki viongozi wake
Hekima umoja na amani,
Hizi ni ngao zetu, Afrika na watu wake
Ibariki Afrika, ibariki Afrika *2
Tubariki watoto wa Afrika.

Hakuna kitu Wanajeshi wanaheshimu kama wimbo wa Taifa.
Walisimama kwa ukakamavu huku mikono yao ya kulia ikiwa kifuani kuonesha mapenzi ya dhati kwa Nchi yao.

Macho yao yalielekea sehemu alipokuwa Sikujua aliyeonekana kama Bibi kizee kipofu aliyechoka kupita maelezo.

Waliisikiliza sauti yake inayotetemeka mpaka alipomaliza kuimba beti la pili la wimbo wa Taifa.

Kufumba na kufumbua alizingirwa kwa kosa la kuimba wimbo wa Taifa kiholela.
Watu hawa hawakuwa na mzaha hata kidogo, kitu pekee wanachokipa kipaumbele ni Taifa lao na si njaa za omba omba.

Kabla hawajamhukumu, vilisikika vishindo vya viatu. Sikujua alichungulia kwa jicho dogo sana sana, alifanikiwa kuona buti kubwa na refu kwenda juu.
Alipenyeza jicho lake taratibu achungulie sura ya Mmiliki wa buti hilo lakini hakufanikiwa, kama angejilazimisha kumkodolea zaidi basi angegundulika kuwa yeye si kipofu.

"Leo ni birthday yangu, tutamsamehe huyu ms*ge, muondoeni hapa" Isaac (Captain wa kikosi cha Wanajeshi wa Silali) alizungumza akataka kuondoka.

Sikujua hakuwa tayari kuondolewa bila kunywa bia au kupatiwa pesa ya kununua bia.

"Hongera kwa kuzaliwa siku ya leo Mheshimiwa, Mimi pia ni birthday yangu leo. Nitafurahi kama utaninunulia bia au kunipa pesa ya kununua bia" Sikujua aliongea kwa kutia huruma.

Captain Isaac aliachia tabasamu baada ya kusikia Bibi kizee huyu ni shabiki wa bia.
Aliwataka Wanajeshi wengine waondoke.....
Alipo hakikisha wameondoka, alijishika mfukoni mwake akataka kumpa pesa Sikujua lakini alisita.

"Karibu nyumbani kwangu tunywe bia pindi utakaporidhika nitakurudisha nyumbani kwako" Isaac aliongea

Sikujua alifurahi ndani ya moyo wake, aliushuhudia mkono wa Isaac ukimshika eti asaidiwe kutembea.

Kwa pamoja walitembea mpaka kwenye nyumba ndogo ya Captain Isaac.

Sikujua aliweza kunusa harufu ya bia, moyo wake ulilipuka kwa furaha.
Walianza kunywa bia huku wakipiga stori, hadithi nyingi za Sikujua zilikuwa ni za enzi ya Mwl Nyerere kadiri muda ulivyozidi kwenda Captain Isaac alishangazwa na namna Bibi Kizee huyu anavyo kunywa bia kama maji.

Siku zote huwa anajiona ni mnywaji mzuri lakini siku ya leo alikubali kuzidiwa na Bibi Kizee.

Aliagiza kreti lingine likaletwa, hapa ndipo Sikujua aliharibu.... alijikuta amefumbua macho yake.
Uzuri wa Captain Isaac pamoja na kreti la bia vilimchanganya........ITAENDELEA.........

SIMULIZI : SIKUJUA WA MTAA WA SILALI
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 02

ENDELEA.......
Hakuwa akiongea sauti ya mtetemo tena wala hadithi za enzi ya Mwl Nyerere, alijiachia na sauti yake nzito iliyokaa kimcharuko zaidi.

Alianza kuropoka namna anavyowachuna pesa Wanaume wanaomshobokea bila kujua yeye ni kubwa la matapeli.

Captain Isaac alijikuta akitabasamu kimtindo, hakuamini kama huyu mbwa kamletea uhuni kambini kwake.

Sikujua hakujua kama ameshaharibu..... aliendelea kukandamiza bia huku akisimulia mara ya mwisho alivyo kojozwa na yule Mzaramo anayefanya kazi kwenye saluni ya Mr P.

Wakati anamalizia chupa ya mwisho ndio alishtuka kama kasha chafua hali ya hewa.

Alitaka kujitia kipofu lakini Captain Isaac alimzuia, taratibu alisimama akiwa kakunja uso wake.

"Sina uhakika kama vijana wangu wamet*mba siku ya leo, kila mmoja wao akifunga bao zake mbili watanishukuru sana" Captain Isaac aliongea.

Sikujua kusikia hivi alianguka chini kuomba msamaha, ni mwepesi sana wa kutoa machozi.

"Sidhani kama ulikuja hapa bila kujipanga....nina uhakika ulijiandaa kushinda au kushindwa" Captain Isaac aliongea.

Sikujua aliendelea kuomboleza, alitamani kugawa tigo yake ili asamehewe lakini akifikiria ndio kitu cha thamani alichobakiza alizidisha kulia.

Alijilaumu kwanini asingeondoka baada ya kunywa bia mbili. Alianza kujinasa vibao huku akiongea kisukuma.
Aliita Mizimu ya kwao ije kumuokoa lakini haikusikia....

Captain Isaac alijikuta akitabasamu kwa namna Sikujua alivyokuwa akiomboleza.
Kwake ilikuwa ni kama burudani kwa siku yake muhimu ya leo.
Aliamua kuzuga kuwaita Wanajeshi wote, Sikujua alikata moto kwa hofu safari ilikuwa ni kweli na si kuigiza.

"Sitaki kuamini amehatarisha maisha yake kuja hapa kunywa bia, ashukuru siku ya leo nipo kwenye hali ya furaha" Captain Isaac alijisemea.

Alifanya mpango wa kumtoa Kambini, alienda kumuacha kwenye Lodge iliyokuwa karibu na Kambi yao.
Alimuachia shilingi elfu 70 mkononi mwake akiamini atakunywa supu ataporejesha fahamu.

Kulivyo pambazuka, Sikujua ana kurupuka usingizini kwa kulia, aliomba msamaha asiingiliwe na Wanajeshi wote wa kambi ya Silali.

Baada ya kuona hajibiwi alizidisha kulia.... ukimya uliokuepo mahali hapa ulimshtua. Alifumbua macho akihisi pengine yupo kuzimu baada ya kubakwa na Mamia ya Wanajeshi.

Anazimia kwa mara ya pili baada ya kugundua yupo sehemu salama tena akiwa kawekea pesa mkononi mwake........ITAENDELEA.........

SIMULIZI : SIKUJUA WA MTAA WA SILALI
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 03

ENDELEA.........
Anakuja kushtuka muda ukiwa umeenda sana. Alijiona shujaa kwa kutoka salama mikononi mwa Captain Isaac.

"Naamini sura yangu ndio imeniokoa siku ya leo....." Sikujua alijifariji huku akijionea aibu namna ngozi yake ya uso ilivyopauka kwa kukosa mafuta.

Shilingi elfu 70 zilizokuwa mkononi mwake zilimpa jeuri, kabla ya kuondoka aliiba shuka akalichomeka tumboni kwake akawa kama mjamzito.

Hakuna hata mmoja aliyemtilia shaka.....barabara yote ilikuwa ni yake akipanga bajeti namna atakavyoitumia elfu 70.

Watu wengi walimpa hongera kwa ujauzito lakini wachache wanao mfahamu kiundani zaidi walijua kuna kitu ameficha tumboni mwake hivyo walimpongeza kwa kufanikisha zoezi lake la wizi.

Baada ya kufika ghetoni kwake alijikuta akipiga chafya mfulilizo. Chumba kilikuwa kichafu.... alichungulia uvunguni akakutana na ugali uliokauka, alitamani kuula lakini hakuwa na mboga.

Pua zake zilinusa harufu ya nyama, aliachia tabasamu pana baada ya kujua jirani yake kapika kitu roho inapenda.

Alipohakikisha hakuna mtu nje alifunua sufuria akaiba nyama pamoja na mchuzi.

Alipambana na ugali wake mpaka alipomaliza, kilichofutia ilikuwa ni kuachia ushuzi tu.
Hakupata tabu hata kidogo....alipumzika kama nusu saa hivi.

Alichukua maji akaingia bafuni, dakika 20 zilikuwa ni nyingi kwake kuonekana kama Beyonce wa Jay Z.
Mwendo wake wa maringo uliwaacha midomo wazi watu aliopishana nayo

Njia nzima aliifunga kwa wimbo wa Zuchu_ Napambana... 🀣🀣🀣🀣🀣

🎡Naamka asubuhi, sina hata buku sh'ndala
Chakukila sijui, bora hata pakulala
Chumbani matandabui, mende wamefanya utawala
Na mjomba panya haelewi, riziki yake hasara

Eeh!
Kwacha kwacha, Nakwenda nakwenda
Sijakubali kudoda, hii ngoma haisambii
Na ndoto za aliniacha, sijapenda sijapenda
Aliekupa kigoda, mi' atanipa kumbi 🎡

Kama si simu kuishiwa chaji basi barabara zima wangeisoma.

Aliingia Supermarket akaanza kuchagua vitu bila kuzingatia bei zilizoandikwa.

"Boss lipia laki mbili na nusu...." Cashier alimuambia

"K kibuyu wewe! laki mbili na nusu pesa au kokoto...kwa vitu gani nilivyochukua, sasa sikia naondoka na vitu vyote na hauna kitu cha kunifanya" Sikujua alileta ubabe.

Cashier hakuwa tayari kusumbuana naye alimpa ishara Mlinzi aje kumsaidia

Sikujua hakuwa tayari kurudisha vitu....alikuwa radhi kuanzisha vurugu na si kuondoka mikono mitupu.
Akiwa katika kujibizana na Mlinzi, alijikuta akipata kigugumizi baada ya kumuona Captain Isaac.
Mwendo wake wa kunesa kama twiga wa Mikumi ulimuacha mdomo wazi.

Macho yake na ya Captain Isaac yaligongana.....Sikujua alijikuta akibabaika hasa akikumbuka uhuni aliofanya jana.

Captain Isaac alipiga hatua akamsogelea akiwa bado kamkazia macho.
Kwa namna alivyokuwa kama Beyonce isingekuwa rahisi kumkumbuka.

"Ni kiasi gani anadaiwa...." Captain Isaac aliuliza alihitaji kumsaidia Mtoto mkali asijue kama ni Sikujua.

"Laki mbili na nusu...." Cashier aliongea huku akiachia tabasamu, alitamani aonekane lakini Captain Isaac si mtu wa kushoboka hovyo.

Pesa iliwekwa mezani kisha Sikujua akaambiwa abebe vitu vyake.
Alijikuta akijing'ata ng'ata hakuamini kama kasaidika.

Bahati mbaya simu yake iliyofungwa na kamba ilidondoka ikasambaratika.
Watu wote waliangalia chini, walishangazwa na kilema cha simu walichokiona na siyo simu tena.

Katika harakati za kupambana kuokoa simu yake, wigi lilidondoka.
Nywele yake ya mnyoosho iliyochakaa kupita kiasi ilionekana.

Hapo ndipo Captain Isaac alimkumbuka, alijikuta akiachia tabasamu kimtindo.
Aliinama chini akamuokotea vipande vyote vya simu yake pamoja na wigi lake.
Ili kumfichia aibu alimtoa nje, hakujua kama mtu huyu hanaga mshipa wa aibu hata kidogo..........ITAENDELEA....

SIMULIZI : SIKUJUA WA MTAA WA SILALI
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 04

ENDELEA......
Alimuingiza kwenye gari lake lenye rangi ya Jeshi.
Muonekano wa macho yake ulitosha kumueleza Captain Isaac kuwa hiki kichwa ni kibovu.

"Una miaka mingapi...." Captain Isaac aliuliza

"Na miaka 20..." Sikujua aliongopa, miaka yake ni 28 hakuwa tayari kuonekana Shangazi

"Kwahiyo umezaliwa 2005?" Captain Isaac aliuliza

"Hapana, nimezaliwa 1997..." Sikujua alijikoroga

"Kwahiyo una miaka 28?" Captain Isaac aliuliza

"Oyaah pu..... zako zina maji au nini, nimesema miaka yangu ni 20... huoni hata muonekano wa ngozi yangu!" Sikujua alifoka.....kabla hajajibiwa alishtuka baada ya kukumbuka kuwa kamtusi huyu jamaa.

Macho yake siku zote hayana tofauti na chemichemi, machozi yasiyo julikana yametoka wapi yalianza kububujika. Alianza kuomba msamaha huku akimshika Captain Isaac, bahati mbaya alimshika maumbile yake.

Alijikuta akiangua kilio kwa mara nyingine, alianza kuomba msamaha kwa kumshika maumbile yake. Akiwa katika harakati za kuomba msamaha kamasi zilichuruzikia kwenye gwanda la Captain.

Aliongeza kilio kwa mara nyingine tena, kila alipoomba msamaha aliongeza kosa, mwisho wa siku alichoka akaamua kuwa kauzu liwalo na liwe.

Captain Isaac alifungua dirisha akapuliza sigara kidogo kabla hajamaliza kipisi chake, Sikujua alimpokonya akavuta pia.

Captain Isaac alijikuta akitabasamu, simu yake iliita..... alimsogeza Sikujua karibu na saluni ya kike akaacha maelekezo atengenezwe vizuri.

"Msukeni nywele za laki na themanini..... hakikisha anawalipa" Captain Isaac alimpa pesa Dada wa Saluni, alihitaji kumyoosha Sikujua kwa uhuni wake.

Sikujua kuona pesa imelipwa alijua ni kwa ajili yake. Aliwahimiza wamuweke mikia mpaka mapajani.

Hakika alipendeza sana, ile anataka kuondoka alichanganyikiwa baada ya kuambiwa alipie laki na 80.....alishika glass ya maji akanywa kwanza ili apate nguvu ya kuongea.........ITAENDELEA.........

SIMULIZI : SIKUJUA WA MTAA WA SILALI
MTUNZI; NURU HALISI
SEHEMU 05

ENDELEA......
"Hata hayo maji uliyokunywa utalipia my dear," Dada wa Saluni aliongea.

"Kwa macho yangu nimeshuhudia yule Mjeda akikupatia pesa.... unawezaje kuniomba pesa tena!" Sikujua alifoka.

"Pesa aliyonipatia haihusiani na wewe, Mimi si mzuri wa kuongea naomba kusikia kutoka kwako unatoa pesa au hautoi" Dada wa Saluni aliongea

"Pesa sitoi, kama huyo Ms*.......nge hajakupatia basi kaniletea Kaka yako au Baba yako tumalizane. Halafu sikiliza wee mb.......wa inaonekana huu Mtaa wewe ni Mgeni na ndio maana unanirefushia mdomo wako!.... naondoka bila kulipa, kama wewe ni Mwanamke kweli unaye tarajia kuingia leba ni tunishie msuli ni kuoneshe kazi" Sikujua aliongea huku akimtukana Captain Isaac kimoyo moyo huko aliko.

Dada wa Saluni si mtu wa kuongea sana....alimshtua mwenzie wakamvamia Sikujua wampige.

Balaa zito lilitokea kati yao, Sikujua hajawahi kukubali kushindwa na kiumbe kinachoitwa Mwanamke..... yupo radhi apoteze macho lakini si kuhesabika amefeli.

Alijitahidi kadiri ya uwezo wake, alipopata upenyo aliondoka kwa kukimbia na Brazilian hair yake iliyokuwa usawa wa mapaja.
Dada wa Saluni aliamua kumpotezea kwa sababu pesa aliyopatiwa ilizidi hata nywele alizosuka.

Sikujua akiwa mwenye hasira kali alitukana njia nzima kwa uhuni aliofanyiwa na Captain Isaac.

"Sina uhakika kama anayasikia matusi yangu.....nitamfuata huko huko Kambini kwake" Sikujua alijisemea kisha akaongozwa na hasira zake.

Watu wengi huogopa kukisogelea kibao kilichoandikwa "Kambi ya Wanajeshi wa Silali" lakini yeye alikipiga teke.

Siku ya leo alionekana kuvurugwa kupita kiasi.
Machozi ya uchungu yalikuwa yana mtiririka kisa na maana Captain Isaac kamfanyia uhuni.

Wanajeshi wakiwa wanapiga stori za hapa na pale kuhusiana na matokeo ya mpira ya Kombe la Africa, walishangazwa na ujio wa Sikujua.
Nywele zake za Brazilian hair zilikuwa zinapeperushwa na upepo.... walijikuta wakiduwaa kwa kumtazama.

"Niitieni hapa huyo Yatima wa nguvu za kiume!" Sikujua alifoka.

"Yatima wa nguvu za kiume!" Waliuliza kipamoja.

Kabla Sikujua hajajibu, alijikuta akikodoa macho baada ya kumuona Captain Isaac akija kwa mwendo wa kihuni. Kifua chake kilikuwa wazi....Six part zilionekana vyema kabisa. Aliweza kuzihesabu bila kukokosea

Sikujua alijikuta akimeza mate, pamoja na kudanga miaka nenda rudi hajawahi kukutana na Mwanaume mwenye mwili wa kujengeka kama wa Captain Isaac..........ITAENDELEA.......


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote