Follow Channel

SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI

book cover og

Utangulizi

SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI 1
MTUNZI SMILE SHINE

" Max fanya haraka urudi mke wako ameondoka siku ya pili leo kamtelekeza mtoto hapa nyumbani kwangu. Ilikuwa ni sauti ya Irene dada wa Max, hizo taarifa zilimshitua Max lakini hakutaka kuamini kama mke wake anaweza kumfanyia hivyo binti yao .
" Haiwezekani Hilda hawezi kumtelekeza shalon.
" Ndio nakwambia fanya haraka urudi maana kasema hana uhusiano na nyie tena yani amewaacha na maisha yenu nae kaenda kutafuta maisha yake mengine.
max kwanza hakuamini kama mke wake anaweza kufanya kitendo cha ajabu cha kumuacha binti yao mdogo na kwenda kusikojulikana tena ukiwa max hayupo alikuwa safarini nchini sweden.

Max alipokataa simu ya dada yake aliamua kumpigia simu mke wake Hilda bahati alibahatika kumpata kwa njia ya video call na Hilda alipokea .
" Hallow max.
" Hilda.....
" Niambie max.
" Hilda niliyoyasikia ni kweli?
" Yapi hayo uliyoyasikia?
" Kuhusu wewe kuondoka nyumbani na kwenda kumtelekeza mtoto kwa dada Irene?
" Sijamtelekeza nimempeleka kwa shangazi yake ile ni damu yake pia anatakiwa kumlea mtoto wa ndugu yake.
" Na wewe upo wapi?
" Nipo sehemu inayostahili kuwepo, max unatakiwa kuanza maisha mapya wewe na mtoto wako .....
" Unamaana gani kusema hivyo au nimekukosea nini mpaka uchukue hayo maamuzi?
" Hakuna ulichonikosea nimeamua tu sababu nimechoka kuishi na wewe.
Max alitulia kwa muda huku akiugulia maneno makali yaliorarua moyo wake.
" Sawa vipi kuhusu mwanao Shalon?
" Hiyo ni zawadi nimekuachia.
Aliongea Hilda bila kuwa na uchungu hata kidogo ndio kwanza alinyanyua grass ya mvinyo na kunywa.
" Hilda....... Max hakumaliza kuongea alinyamaza na kukazia macho kwenye simu yake.
Alimuona Hilda akiwa na James ex wake wa zamani.
James alimbusu Hilda kisha akamuangalia max na kumpungia mkono.
Max alishajuwa sababu ya yeye na mwanae kuachwa hakuwa na haja ya kubishana na mtu alikata simu na kujiandaa na safari ya Tanzania.

Max ni mwanaume wa miaka 35 ni baba wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa shalon, shalon ana miaka saba ana matatizo ya kuona hali hiyo ilitokea ghafla alipokuwa na miaka miwili . Max alihangaika sana kumtibia mwanae alienda hospitali mbali mbali kwani alikuwa na matumaini mwanae atakuja kuwa sawa pia madactari walimpa matumaini kuwa tatizo la shalon sio kubwa kuna uwezekano mkubwa wa kupona tena ila kuna hitaji muda kidogo hivyo uvumilivu unatakiwa.

Baada ya shalon kupata hilo tatizo mama yake Hilda aliamua kuwatoroka max na mtoto wake bila kusema sababu ya kuwaacha.
Max aliumizwa sana na maamuzi ya mke wake , aliishi kwa unyonge sana hasa pale binti yake alipokuwa akimuita mama yake.

Siku moja Shalon alikuwa alikuwa amekaa chumbani kwake akawa anamuita baba yake ambae alikuwa jikoni anaandaa kifungua kinywa.
" Baba, Baba.....
" Nakuja malaika wangu.
Max alienda chumbani kwa shalon akamkuta kakaa kitandani huku akiwa kapakata mto wake.
Max alikaa pembeni na kumbusu binti yake shavuni. Shalon alitoa tabasamu huku akimpapasa baba yake usoni.
" Baba nimeota ndoto nzuri sana.
" Eheee niambie princess wangu umeota ndoto gani?
" Nimemuota mama amekuja akanikumbatia na kunibusu nilifurahi sana .
" Mmmmmh. Max aliishia kuguna
" Baba ulisema mama atakuja hivi karibuni anakuja lini?
" Siku sio nyingi atakuja .
" Natamani awe mtu wa kwanza kumuona siku nitakayo weza kuona.
Hapo ilikuwa baada ya wiki mbili Shalon alitakiwa kufanyiwa upasuaji ili aweze kuona.

Max aliumizwa sana na maneno ya Shalon hakujua ameambiwa nini tena maana kila siku amekuwa alimdanganya kuwa mama yake atakuja .
"Ila Hiyo ni ndoto tu malaika wangu usifikie mamani.
Shalon alipoteza tabasamu lake baada ya baba yake kumwambia hivyo.
" Vipi mbona sioni tabasamu lako zuri kipenzi?
" Kwahiyo ndoto yangu haikuwa kweli mama yangu hatakuja? Lakini uliniambia mama yangu ananipenda na atakuja kwaajili yangu.
" Ndio atakuja .
Shalon aliachia tabasamu , alimpapasa baba yake na kumkumbatia kwa furaha
" Sawa unatakiwa kupiga maswaki na kuoga nimeshakuandalia chai.
Max alimchukua binti yake akaenda kumuogesha na kumvalisha vizuri baada ya hapo walikaa mezani wakawa wanakunywa chai.
Akili ya max haikuwepo pale alikuwa anawaza atapamta wapi Hilda mama yake Shalon maana tangia alivyoondoka hawakuwahi kuwasiliana na wala hajui alipo.
" Hilda sikuwahi kukifanyia kitu kibaya lakini kwanini umeamua kunikimbia na kumuacha binti yetu ambae unajua kabisa anahitaji huduma zako, ona sasa nitamwambia nini binti yangu kuhusu mama yake , itakuwa sawa nikimwambia mama yako alikutoroka na kwenda kwa mwanaume mwingine? Sijui siku akiona nitamjibu nini kuhusu mama yake na nimeshamuahidi mama yake atakuja.

Max aliwaza mengi mpaka ajisahau kama alikuwa analisha mtoto mpaka shalon alivyopapasa akishika mkono wake ndipo akashituka.
" Baba mbona hunilishi, kwani unafanya nini?
" Nipo pembeni yako mwanangu nisamehe kwa kuchelewesha kukulisha.
Aliongea max huku akiwa anaendelea kumlisha.

Upande wapili anaonekana dada mmoja mrembo Dala akiwa anakaa mbele ya kioo anajiremba uso wake huku mdogo wake Shakira akiwa amekaa kitandani anamuangalia
" Dada Dala unataka kutoka tena usiku huu?
Aliuliza Shakira mdogo wake Dala.
" Ndio mdogo wangu si unajua kazi zangu ni za usiku.
" Kwahiyo Nitakuwa nalala mwenyewe? Shakira aliuliza ,
Dala alimgeukia mdogo wake na kumwambia.
" Unatakiwa kuzoea maana hii ndio kazi yangu kwa sasa na ninafanya kwaajili ya kukidhi mahitaji yako unatakiwa kuusoma, kula na huduma nyingine zinazostahili.
" Kwani unafanya kazi gani?
Dala alisita kidogo kujibu swali la mdogo wake , lakini Shakira alimuangalia kwa makini akiwa anasubiri jibu kutoka kwa dada yake.
" Sio muhimu kuijua kazi yangu ila unatakiwa kujua dada yako nahangaika kwaajili ya maisha yetu , tunatakiwa kuishi vizuri kama watu wengine.
Aliongea Dala huku machozi yakitaka kutoka. Alimaliza kujipodoa akavaa viatu vyake .
" Acha niwahi.
" Sawa.
" Kuwa makini mdogo wangu , kumbuka kufunga mlango vizuri.
" Sawa.

Dala aliondoka akaenda kazini kwake kwenye bar moja maarufu pale mjini na siku hiyo ya weekend ilikuwa inapiga live band na watu wengi walikuwepo hapo wakipata moja moto, moja baridi huku waliburudika .
" Dala huu ndio muda wa kuja kazini?
Meneja wa ile bar alimuuliza huku akiwa anaangalia saa yake ya mkononi.
" Samahani foleni ilikuwa kubwa barabarani.
" Hii ni kawaida yako sasa leo iwe mwisho kuchelewa endapo ikitokea nitakifukuza kazi,
" Naomba unisamehe....
"Nenda kaendelee na kazi haraka
Dala alienda kubadili nguo haraka na kuanza kuhudumia wateja.

Max alikuwa kwenye hiyo bar akinywa huku akitafakari maisha yake na binti yake , pia bado alikuwa akijiuliza atapata wapi mwanamke wa kuwa mama kwa binti yake ambae atamchukulia Shalon kama mwanae.
Aliwaza sana badae akajikuta anasema
" Hakuna mwanamke anaeweza kuwa na uchungu na mtoto wa mwanamke mwenzie.
Wakati anaongea hivyo Dala alipita karibu yake na kusikia alichokiongea Max.



SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI 2
MTUNZI SMILE SHINE

Dala alisimama akamuangalia jinsi anavyokunywa kilevi chake na kuongea mwenyewe kama mtu aliechanganyikiwa.
" Huyu mtu anaonekana anamatatizo.
Huruma zilimfanya asogea karibu yake na kumsalimia.
" Habari yako kaka!
Max alinyanyua macho yake akamuangalia juu mpaka chini kwa macho ya mtu aliekuwa kalewa kisha akamwambia
" Niambie mrembo, unataka nini kutoka kwangu?
" Kuna tatizo linakusumbua?
Max alitabasamu huku alinyanyua grass yake ya pombe na kunywa kisha akaweka grass mezani.
" Ni kweli nina tatizo unaweza kunisaidia?
" Kama hilo tatizo lipo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia.
" Sikujua kama kwenye hii dunia kuna watu wanaoweza kujali matatizo ya wengine, hatimae leo imefikiwa na mimi.
" Unamaana gani kusema hivyo?
Max alitulia kidogo kisha alimuangalia Dala usoni na kusema.
" Naweza kuwa na wewe usiku wa leo?
Dala alimuangalia kisha alifikiria kwa muda kisha akasema
" Unamaanisha kuwa na mimi kivipi?
" Usijifanye mtoto ambae haelewi chochote .
" Tafadhali nipo kazini. Alijibu Dala kisha akataka kuondoka
" Hebu tulia mtoto wa kike mbona unarukaruka hivyo kama pesa mimi ninayo . Alisema Max huku akitoa pesa kiasi kama elfu 50 na kumpatia kabla hajafanya chochote.
" Hii ni kama advance tu. Shika hii baada ya hapo utafutaji zaidi, ninayo pesa ya kutosha.

Kwakuwa Dala alikuwa na majukumu mazito na pesa anayelipwa pale bar haikidhi mahitaji yake na alikuwa akidaiwa ada ya shule ya Shakira akajikuta anapata tamaa na kukubali kutoka na Max .
" Sawa utaniongeza shilingi ngapi?
" Usijali kuhusu pesa kikubwa anipe huduma nzuri .
" Sawa nakuja sasa hivi.
Dala alikubaliana na max akaenda kuongea na mwenzie akamuachia pesa kidogo kisha yeye akaondoka na max.

Walifika kwenye chumba cha hotel max aliagiza pombe akaendelea kunywa huku Dala akiwa anamsubiri afanye kazi iliyompeleka apewe chake aondoke.
" Mmmh kwa hizo pombe anazokunywa kama maji kuna jambo hapa ? Dala alianza kumtilia mashaka na kuona kama kaenda kuangalia mtu anashindana na pombe.
" Nimekuja kupoteza muda wangu bure kumbe mtu mwenyewe mlevi kupita maelezo.

Muda ulizidi kwenda hakukuwa na dalili ya kufanya chochote ikabidi Dala aulize.
" Mbona sikuelewi na muda unaenda wewe umekazana kunywa pombe tu.
" Kwani wewe shida yako nini mrembo?
" Kwani hapa nimekuja kukuangalia unavyokunywa?
" Nimekuambia tunywe umekataa sasa unataka nifanye nini?
" Mimi situmii pombe na hapa sijafuata hicho kumbuka umeniita kwa jambo lingine na sio kukuangalia....
" Kwani shida yako si nipesa nitakupatia hizo pesa wewe tulia hapo na muda wako wote wa kuwa na mimi nitaulipia mimi ndio Max bwana sina shida na pesa ndogondogo.

Max aliendelea kunywa, ile hali ilikuwa inakera sana Dala alitamani kuondoka ile sehemu lakini muda ulikuwa umeenda sana . Alizunguka ndani ya kile chumba huku alichungulia dirishani.
" Kwani huwezi kutulia sehemu moja?
Max aliuliza
" Tangia nimeanza kukutana na wanaume sijawahi kupata mwanaume kama wewe yani unaboa sana.
" Hivi unaitwa nani vile?
"Dala.
" Una miaka mingapi?
" Miaka yangu itakusaidia nini?
" Kama hutaki kujibu basi .
Dala alimuangalia kisha akamjibu.
" Nina miaka 21.
" Mbona bado mdogo sana alafu unafanya kazi hatari kama hizi? Umri kama wako sasa hivi wapo shule wanasoma lakini wewe unauza bar na kujiuza .
Hiki neno kujiuza kilimuumiza Dala kwani haikuwa tabia yake ndio kwanza siku hiyo alikuwa anaanza. Alitamani kumwambia lakini alijua hawezi kumuamini .
" Kila mtu anachagua jinsi ya kuishi na kujipatia kipato hivyo usiniingilie
" Hii ndio njia sahihi kwako kwa kujipatia kipato?
" Kaka kama unaona hii ni kazi haramu basi hata wewe umefanya kitu haramu maana mimi na wewe wote tunashiriki kwenye huo uharamu wewe unataka starehe mimi nataka pesa.

Maswali ya max yalikuwa kama yalikuwa yanaamsha machungu. Dala alienda kukaa kitandani mpaka usingizi ukampitia, alikuja kushituka majira ya saa kumi na mbili asubuhi, alimuona max Kalala pembeni yake. Alimuangalia na kutaka kuchomoa Wallet ili achukue pesa lakini akaamua kuacha
" Sijui kapatwa na nini, kunichukua kwaajili ya kunipotezea muda wangu bure, hii ni hasara.
Dala alivaa viatu vyake alipomaliza aliondoka na kumuacha max akiwa bado Kalala.

Baada ya wiki mbili kupita max akimpeleka binti yake hospitali kwaajili ya kufanyiwa upasuaji na zoezi zima lilikamilika . Shalon akiwa bado kafungwa bandeji kwenye macho yake alikuwa akiuliza kama mama yake kafika.
" Shangazi mama yangu amekuja?
Irene alimuangalia ndugu yake na Max alimuangalia bila kujibu chochote.
" Bado hajafika ila amesema kesho kutwa atakuwepo hapa.
" Nataka nikifunguliwa macho yangu nimuone yeye kwanza.
" Sawa nitamwambia awahi kufika. Utamuona akiwa kakaa pembeni yako.

Max alitoka pale wodini na Irene akamfuata nyuma.
" Unaenda wapi sasa?
" Acha nikapumzike kichwa changu hakipo sawa.
" Lakini umesikia mtoto wako anachokitaka sijui utamwambia nini ili akielewa.
" Niache kwanza.
Alisema Max alafu aliondoka akionekana hayupo sawa.
Ilipofika Jioni alienda kwenye ile bar anayofanya kazi Dala . Wakati anashuka kwenye gari alimuona Dala anarumbana na kijana mmoja .
" wewe ni malaya tu ndio maana una ng'ang'ania kufanya kazi hapa ili wanaume wakushikeshike.
" Nimekuambia kazi siachi , kwani tangia nimeanza mahusiano na wewe ilishawahi kunisaidia nini? Napitia maisha magumu , mdogo wangu ananitegemea, natakiwa kumlisha, kumvisha ,kumlipia ada ya shule na kodi ya nyumba kama mpenzi wangu ilishawahi kunisaidia hata jukumu moja ? Zaidi wewe mwenyewe unaniomba hela ndogo ndogo.
" Kwahiyo ndio unatangaza kila mtu ajue kuwa unanipa hivyo vibukubuku vyako.
" Huna msaada na mimi karisto kazi inayojua wewe ni kuoga kuvaa vizuri, kujipulizia marashi unukie vizuri, kuvaa Cheni na hereni watu wakuone wakusifie. Usharo baro ndio unaweza wewe lakini kufanya kazi aaaaaaaah.
"Basi sawa kuanzia sasa tusijuane endelea na mambo yako na mimi niendelee na yangu.
" Kila la kheri. Kwanza nashukuru kwa kutua gunia la misumari lililokuwa linaelekea mabegani kwangu.

Kalisto aliondoka kwa hasira na Dala alipiga hatua chache akielekea bar kabla hajafika mbali max alimuita.
" Dala....
Dala alisimama na kugeuka kumuangalia mtu aliekuwa anamuita.
" Ni huyu tena mwanaume asiyekuwa na hisia sijui anataka nini kwangu.
Alijisemea dala huku akiwa kasimama anamsubilia Max ambae alikuwa anamfuata pale aliposimama.



SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI 3
MTUNZI SMILE SHINE

Max alifika karibu na dala kabla hata ya salamu Dala akasema.
" Ehee unasemaje na wewe?
" Mbona unanipokea kwa ukali?
" Usinipotezee muda nina mambo mengi ya kufanya .
" Mmmm punguza jazba kwanza waungwana wakikutana wanasalimiana alafu mambo mengine yanafuata. Habari yako.
" Salama.
" Dala naomba unipe muda tuongee.
" Huoni kama huu ni muda wa kazi?
" Naweza kulipia ilimladi tuongee tu.
" Siwezi kurudia kosa.
" Najua nilikukera sana siku ile lakini nitakupa hela yako pia kuna swala lingine naomba tujadili tukikubaliana nitakulipa laki 5 kwa mwezi.
Dala alishituka na kumuangalia max usoni alipotajiwa hiyo hela.
" Kazi gani hiyo ya kulipwa laki tano kwa mwezi?
" Nipe muda tuzungumze. Ni jambo serious sana.
Dala alimuangalia huku akiwa anatafakari kitu .
"Kumbuka nipo kazini.
" Naelewa ila naomba unipe muda kidogo tuzungumze .
Dala alikubali waliondoka wakaenda kukaa sehemu iliyotulia kwaajili ya kuzungumza.
Max alitoa kiasi cha shilingi laki mbili akampatia.
" Hayo ni malipo ya kuwa na mimi ule usiku.
" Khaaaaa pesa zote hizi na hatukufanya chochote?
"Usijali. Hata hivyo sikuwa na nia ya kukufanya chochote.
Dala alizichukua zile hela na kuweka ndani ya mkoba wake.
" Asante.
" Dala naweza kukuuliza maswali mawili au matatu?
" Ndio wewe uliza tu.
" Kwanini unafanya kazi ya kujiuza?
Dala alimuangalia kisha akainamisha macho yake chini.
" Najua wengi hawapendi kufanya kazi kama unayofanya ila kuna sababu unaweza niambie sababu yako ni ipi?
" Ni ugumu wa maisha, pia nilikwambia ukweli hautaweza kuniamini.
" Unaweza kinaelezea kwa kirefu?
" Naishi na mdogo wangu, ana miaka 13 sasa, hatuna wazazi na mimi ndio tegemeo lake hivyo natakiwa kufanya kazi na kujituma kwaajili ya maisha yake nataka asome sitaki aje kuishia kama mimi . Kusema ukweli sijawahi kuuza mwili wangu siku ile ilikuwa mara ya kwanza na nilifanya vile sababu ya kutafuta ada ya shule ya mdogo wangu.
" Kwahiyo hufanyi biashara ya kujiuza?
" Ndio , kazi yangu ni kuuza bar tu.
"Pole sana.
" Unamuda gani kwenye tangia umeanza hiyo kazi ya bar?
" Huu ni mwezi wa pili.
" Nilihisi kuwa sio mzoefu kwenye hiyo kazi ya kujiuza maana wasichana wa nafanya hiyo kazi wanajulikana tu. Sasa nikikupa kazi utaweza kuifanya?
" Kama inamalipo mazuri nitafanya.
" kama nilivyosema mwanzo ni laki 5 kwa mwezi.
" Ni kazi gani ambayo unataka nifanye?
" Kuwa mama wa mtoto wangu.
Dala alishituka akawa kamkatoa macho kwa mshangao, Max aliangalia chini kwa sekunde kadhaa alafu akasema
" Yani namaanisha mke wa kukodi.
Dala bado aliendelea kushangaa.
" Hilo ni jambo geni sana kwangu inawezekana vipi? Sijawahi kusikia wala kuona.
" Haya mambo yapo sana sema kwako ndio mageni. Upo tayari kufanya hiyo kazi?
" Unamaanisha kumlea tu na kuigiza kama mama?
" Ndio ipo tayari kufanya hivyo?
" Ndio nipo tayari lakini kabla sijaamua hiyo kazi unatakiwa kunipa maelekezo ya kutosha.
" Ok, ni binti yangu anaitwa shalon nimeishi nae tangia alipokuwa na miaka miwili, alikuwa na matatizo ya kuona ila siku tatu zilizopita alifanyiwa upasuaji na hivi ninapoongea na wewe bado yupo hospitali. Tamanio lake kubwa ni kumuona mama yake baada ya kutolewa bandeji.
" Kwani mama yake yuko wapi?
Max alishindwa kujibu swali la dala. Dala alihisi huenda mama yake Shalon amefariki.
" Samahani haikuwa dhamira yangu kukukumbusha yaliyopita , naelewa ni uchungu kiasi gani kuondokewa na watu tunaowapenda kwani kuna muda hata mimi napitia hali hiyo ninapowakumbuka wazazi wangu.
" Tuachane na hayo , upo tayari kuanza kazi kesho?
" Nipo tayari kufanya hiyo kazi.

Max alitoa kadi yenye namba zake za simu na kumpatia Dala.
" Hizi ni namba zangu za simu naomba kesho Mida ya saa nne asubuhi unitafute.
" Sawa.
" Kwaheri.
Max aliaga akaondoka .
" Afadhali nimepata kazi nzuri sasa Shakira atasoma shule nzuri na kupata mahitaji mengine bila shida yoyote.

Kesho yake Mida ya saa nne Dala akimtafuta Max.
" Hallow Dala.
" Umejuwaje kama ni mimi?
" Hakuna mtu mwingine ambae nilikuwa nina miradi nae zaidi yako pia sauti yako haiwe kunipotea. Uko wapi kwa sasa?
"Nipo nyumbani.
" Unaweza kuja Tumaini hospital
" Sawa nafika hapo muda sio mrefu.
" Sawa chukua usafiri wa binafsi ili ifike haraka.
" Sawa.
Dala alichukua usafiri anaelekea Tumaini hospital.
Alipofika alimpigia simu max akatoka nje kwenda kumpokea.
" Tulikuwa tunakusubiri wewe shalon anatakiwa kufunguliwa nacho yake .
" Lakini sijachelewa sana.
" Huu ndio muda tuliopanga hivyo haujachelewa.

Walielekea kwenye wodi aliyokuwa kalazwa shalon wakamkuta Irene anamnywesha juice Shalon.
" Habari.
" Salama.
Dala na Irene walisalimiana na Shalon aliposikia sauti ya Dala akauliza.
" Huyo ni mama yangu? Shalon aliuliza.
" Ndio ni mama yako amefika. Alijibu max
Shalon aliachia tabasamu kisha akauliza
" Mama yangu anaitwa Hilda mbona sasa mnamuita Dala?
" Hilo ni jina lake lingine.
" Nimekumiss mama nataka kukuona.
Dala aliwaangalia Irene na Max. Max alimuonyesha ishala apite na kwenda kuungana nae. Dala alimpita na kwenda kukaa pembeni ya shalon alimkumbatia na kumbusu.
" Mwanangu Shalon nilikumiss pia binti yangu nakupenda.
" Nakupenda mama , doctor aliniambia nitaona nataka kukuona wewe kwanza
" Nipo hapa pembeni yako kipenzi utaniona. Hata mimi natamani kuona macho yako mazuri .
Shalon alitoa kicheko kikubwa alionekana mwenye furaha mno. Hali ya Shalon kuwa na furaha ilimfanya Max ajisikie vizuri maana hakuwahi kumsikia akicheka kwa sauti zaidi ya tabasamu tu.

Baada ya muda mchache kupita doctor alifika kwaajili ya kumfungua Shalon. Kila mmoja alikuwa makini kuangalia , Iren alikuwa na wasiwasi endapo Shalon utagundua kuwa dala sio mama yake itakuwaje.
" Max itakuwaje kama shalon akigundua kuwa huyu sio mama yake?
" Sio rahisi maana haijui sura ya mama yake.

Baada ya shalon kufunguliwa alipewa kioo ajiangalie.
Shalon alijiangalia huku akitabasamu.
" Huyo mrembo unaemuona ni wewe shalon.
Shalon aligeuka kuwaangalia wote waliokuwa wamesimama kisha akarudisha macho yake kwa Dala na kumuabgalia kwa makini . Irene alimfanya Max alijua kila kitu kinaharibika.
" Nilikwambia anaweza ahisi sio mama yake.
Mapigo ya moyo ya max yalianza kudinda kwa kasi.
" Mwanangu unaona?
Dala aliuliza na shalon akatingisha kichwa akimaanisha ndio.
" Mama....
Shalon alimkumbatia na kusema
" Niambie hautaondoka na kuniacha mimi na baba.
Dala alimkumbatia vizuri na kusema
" Naanzaje kumuacha mtoto wangu mzuri hivi.......



SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI 4
MTUNZI SMILE SHINE

"Sitaondoka nitakuwa na nyinyi siku zote na wapenda sana.
Shalon akimkumbatia Dala kwa furaha kubwa na siku hiyo alikuwa ni mtu mwenye furaha sana baba yake na Irene walikuwa watazamaji na kutabasamu .
Max alisogea karibu yao na kusema .
" Haya shalon muda wa kurudi nyumbani umefika mambo mengine utaenda kuongea na mama ukiwa nyumbani.
" Sawa baba.
Max alibeba vifaa vyao, shalon hakutaka kukaaa mbali na Dala alimshika mkono wakaongozana pamoja mpaka kwenye gari.
" Max, Dala mimi sitaongozana na nyie acha niwahi nyumbani kwangu. Irene aliwaaga
" Sawa kwakuwa Dala yupo kila kitu kitakuwa sawa.
" Dala tunakutegemea kwenye hili mpaka mambo yatakapokuwa sawa.
" Usijali dada Irene nipo pamoja na nyie kwenye hili.
Iren aliondoka na Max, Dala na Shalon wakipanda kwenye gari huku Dala akiwa kampakata shalon na kumuonyesha tabasamu pia shalon alikuwa akitabasamu huku akishika uso wa Dala.
" Masikini mtoto mdogo anaonekana alikuwa anapitia magumu kaone kalivyofurahi kanafikiri mimi ndio mama yake .
Alijisemea Dala huku akimuonea huruma akajikuta akimbusu na kumfanya shalon zaidi kufurahi na furaha ya sharon ilimpa faraja flani Max, na kuhusi alifanya chaguo sahihi .
Walifika nyumbani na kwenda moja kwa moja chumbani kwa Shalon kwaajili ya kumpumzisha.
Max alitoka chumbani kwa shalon akawaacha wanapiga story na Dala huku shalon akicheka kwa furaha.
Kwakuwa pale ndani hakukuwa na mtu wa kusaidia kazi ilibidi max aingie jikoni na kuanza kupika alipomaliza alipeleka chakula chumbani kwa Shalon.
" Shalon ni muda wa kula sasa.
Shalon alimuangalia dala alafu akamwambia
" Mama naomba unilishe.
" Shalon wewe ni mkubwa sasa kwanini ulishwe? Usimsumbie mama bwana.
" Hapana kama mtoto wangu anataka kulishwa nitafanya hivyo. Songea hapa binti yangu mzuri.
Shalon alinyanyuka na kukaa mapajani kwa Dala kisha wakaanza kulishana.
Walimaliza kulishana Dala akamuweka shalon kitandani na kumtaja alale. Alimbembeleza mpaka alipopitiwa na usingizi alitoka sebleni lakini hakuona mtu lakini alihisi kuna mtu jikoni ikabidi aende akamkuta Max anasafisha viombo.
Max alipomuona alimkaribisha.
" Dala karibu ukae.
" Shalon amelala nadhani naweza kwenda nyumbani.
" Kwanza nashukuru sana Dala sikutegemea kama ungemuonyesha mapenzi binti yangu mpaka hajashituka kuwa wewe sio mama yake mzazi. Pia nilikuwa
Naomba jambo moja kama litawezekana.
" Jambo gani?
" Naomba uhamie hapa.
" Hiyo itakuwa ngumu sana kumbuka naishi na mdogo wangu anahitaji uwepo wangu.
" Sawa tutafanya kitu kwaajili ya mdogo wako .
" Umefikiria kufanya nini? Usiniambie kuwa unataka nae aje huishi hapa.
" Lakini nilifikiria hivyo.
" Hapana sipendi mdogo wangu ashuhudie maisha inayoishi.
" Basi sawa ataenda boding alafu likizo tutajua.
Dala akafikiria akaona mbona kama hela yake itaishia kulipia ada .
" Sina uwezo wa kumlipia shule ya bweni.
" Gharama zipo juu yangu na pesa niliyokuahidi ipo palepale.
" Basi sawa acha leo niende .
"Sawa.
" Naomba kesho usichelewe kuja maana Shalon huwa anaamka Mida ya saa nne ningependa muda huo uwepo hapa.
" Nitajitahidi kufika mapema kabla ya huo muda.
Max aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali akatoa Wallet na kutoa kiasi cha pesa.
" Shika hii.
" Ya kazi gani?
" Utafanya nauli muda umeenda sana.
" Ninayo.
" Naomba upokee hii tafadhali.
Dala alipokea ile pesa alafu akaondoka.
Max alienda chumbani kwa Shalon akaenda kusimama pembeni yake , alimuangalia aliona jinsi shalon alivyokuwa Kalala usingizi mzuri wa amani na sura yake ilikuwa na tabasamu ilionekana alifurahishwa na kitendo cha kukutana na Dala akijua ndio mama yake .
Max alimfungulia vizuri kisha akatoka chumbani na kwenda sebleni kuangalia mpira.

Kwa upande wa Dala alifika nyumbani kwake alikaa na mdogo wake na kumueleza kuwa amepata kazi mpya.
" Shakira mdogo wangu nimepata kazi mpya .....
Kabla hajamaliza kuongea Shakira alidakia.
"Subiri kwanza, kazi iliyopata niya usiku?
" Hapana....
" Afadhali sikuwa napenda kazi zako za kutoka usiku unarudi asubuhi watu walikuwa wanakusema vibaya kuhusu wewe.
" Achana na mambo ya watu . Ila kazi niliyopata sitakaa hapa na wewe unatakiwa kuhama shule unaenda kusoma shule ya bweni.
" Dada unapesa ya kunipeleka huko?
" Usijali kuhusu hilo kila kitu kitaenda sawa.
Shakira alimuangalia dada yake huku akiwa na mashaka .
" Mbona unaniangalia hivyo?
" Hapana .
" Basi nenda Kalale kesho tuamke mapema nikupeleke sehemu ninayoenda kufanya kazi na ikiwezekana swala la kwenda shule lianze mara moja .
" Sawa.
Shakira alinyanyuka na kwenda kuandaa kwaajili ya kulala.

Usiku max akiwa alikuwa amepigiwa na usingizi sebleni mara alihisi kama anatingishwa. Alifumbua macho kuangalia alimuona Shalon kasimama huku akifikicha macho.
" Binti yangu kipenzi mbona upo hapa?
" Mama yuko wapi? Max alinyanyuka kwenye kochi akakaa.
" Mama.... Yupo.....
Hayupo chumbani nimeenda kuangalia hakuna mtu , dad niambie mama yangu ameondoka ameniacha tena , mama yangu hanipendi?
Aliongea shalon kwa sauti ya kutaka kulia.
Max akimvuta binti yake akamkumbatia .
" Hapana mwanangu mama yupo.
" Lakini hayupo ndani.
" Nisikilize nikwambie mama yako kaenda kuchukua vitu vyake vyote kesho mapema sana atakuwa hapa.
" Kama asipo kuja.
" Ni lazima aje sababu anakupenda sana.
Shalon aliachia tabasamu .
" Sasa twende ukalale.
" Nitaenda kama utalala na mimi.
" Sawa mrembo wangu.
Max alizima taa wakaelekea chumbani kwa Shalon, shalon alipanda kitandani max akamfunika vizuri na kuanza kumsomea kitabu cha hadithi mpaka usingizi ulipompitia.
Na alikosa usingizi alikaa huku akiwa anamfikiria mke wake jinsi alivyomua cha na kuonekana hana shida kabisa kuhusu wao na wala hajali pia alijiuliza itakuwaje kama Dalah hataweza kukaa muda mrefu na shalon.
" Sijui nimwambie nini shalon ili anielewe maana sina imani sana na Dalah mwanamke muuza bar hivi anaweza kumpa maisha gani binti yangu? Hapa natakiwa kuwa imara na ikiwezekana baada ya muda flani nimwambie shalon ukweli kuwa Dala sio mama yake na asahau kuhusu mama mimi ndio kila kitu kwake.



SINGLE DADY NA MAMA WA KUKODI 5
MTUNZI SMILE SHINE

MAX aliwaza sana mpaka akapitiwa na usingizi.
Kulipokucha aliamka mapema akachukua simu yake akasngalia saa .
" Saa mbili acha nimpigie simu Dala awahi kuja kabla shalon hajaanza kusumbua.
Alipiga simu ya Dalah ikaanza kuita. Baada ya sekunde kadhaa simu ulipokelewa.
Wakati huo ndio kwanza Dalah alikuwa anatoka usingizini.
" Hallow boss.
" Mbona kama bado upo usingizini.
" Hapana nimeamka muda kidogo.
" Naomba baada ya dakika kumi uwe umefika Shalon akiamka akuone ukiwa hapa.
" Dakika kumi?
" Ndio , jana usiku kanisumbua sana kuhusu wewe.
" Dakika kumi labda kwa ndege ila kwa usafiri wa huku kwetu wala nisikudanganye .
" Usipende daladala chukua taxi.
" Sawa lakini....
" Ni nauli au? Kama tatizo nauli nitakuja kulipa.
" Sawa boss, lakini vipi kuhusu mpango wa mdogo wangu?
" Kila kitu tuliongeza jana kwani umesahau?
" Nakumbuka kila kitu.
" Basi wahikuja na nimeshafanya mipango leo hii hii anaenda shule kuendelea na masomo.
" We Max unanitania au?
" Usipite muda njooni haraka.

Max alimaliza kuongea akakata simu. Dala kuanza kuhimiza Shakira afanye haraka wawahi kuondoka.
" Shakira fanya haraka tunatakiwa kuwahi kwa Max
" sawa dada lakini kama itakuwa salama kwako na kama sio salama naomba tuacha sitamani upate shida kwaajili yangu dada.
" Shakira niamini mimi kila kitu kipo sawa huko naenda kufanya kazi ya kulea mtoto tu na kuhusu shule tayari umeshatafutiwa
" Kwahiyo mshahara wako ndio unanilipia ada?
" Ndio.
" Kwani unapokea mshahara shilingi ngapi?
" Ohoooo naona sasa maswali yanazidi wewe jua swala moja la kusoma mambo mengine hayakuhusu.
Dalah alijibu kwa ukali baada ya shakira kuwa na maswali mengi.
Shakira alikuwa mpole alichukua kila kilichokuwa cha muhimu wakafungasha kisha wakatoka na mabegi yao.
" Nisubiri hapo napeleka funguo kwa mama happy.
" Sawa.
Dalah alipeleka funguo kwa jirani yao kisha akarudi kumchukua Shakira na safari ya kwenda kwa max ikaanza.

Walifika nyumbani kwa max wakamkuta Shalon na baba yake wamesimama nje wakiwa wanawasubiri.
Shalon alipomuona Dalah akimkimbilia na kumkumbatia.
" Mama ulienda wapi?
" Nilienda kumchukua Shakira.
" Kwani yeye ni nani?
" Mmmh ni mdogo wangu.
" Umemleta nije kucheza nae?
" Ndio leo utacheza nae .
Shalon alimuangalia ahakila huku akitabasamu ,
Shakira alikuwa anamshangaa dada yake kuitwa mama.
" Mama , dady kapika chai twende tukanywe .
Shalon alimshika mkono Dalah wakawa wanaingia ndani na kwenda kukaa kwenye meza ya dinning wakaanza kunywa chai.

Max alimaliza kunywa chai akanyanyuka na kusema.
" Dala nipo nje ukimaliza nakuhitaji kwaajili ya maongezi.
" Sawa nakuja sasa hivi.
Max alitangulia nje baada ya muda Dala alinyanyuka.
Shalon bali na Shakira nakuja sasa hivi.
" Haya mama.
Shalon alimuangalia Shakira huku akiwa anatabasamu alionekana kuwa na upendo na kuvutiwa kuwaona nyumbani kwao.

Dala alitoka nje akaangaza macho akamuona Max amekaa kwenye benchi bustanini. Alipiga hatua kumfuata.
" Niambie max.
" Ni kuhusu Shakira anatakiwa kuanza shule leo kwasababu yupo darasa la mtihani haitakuwa vizuri kumchelewesha.
" Asante sana max kwa kujali.
" Dala mahali mdogo wako na kumpatia kila anachotakiwa kupata na mimi ninatumai hivyo kwa Shalon.
" Usiwe na wasiwasi max nitamlea Shalon kama mtoto wangu wa kumzaa yani mwenyewe utafurahi mbona.
Max alimuangalia kuanzia juu mpaka chini kisha akasema.
" Nina mengi sana ya kuongea na wewe ila kwa sasa acha tumpeleke Shakira shule. Nenda kajiandaeni tuondoke.
" Sawa. Alijibu Dala kisha akawa anaondoka
Kabla hajafika mbali max alimuita.
Dala alisimama na kugeuka kumuangalia.
" Tunakwenda ni sehemu ya heshima naomba ubadili hiyo suruali yako uliyokubana ingependeza kama ungevaa gauni ya kukustiri maungo yako.
" Sawa.
Dala aliondoka lakin bado max akimsindikiza kwa macho . Dala alikuwa kabarikiwa umbo zuri sana hakika mwanaume Rijali hawezi kujizuia kumuangalia mara mbili mbili au kutokumtamani. Huenda Max nae alikuwa kwenye wakati mgumu.

Dala alienda chumbani akibadilisha nguo kisha wakachukua begi la Shakira kisha Shakira alimshika mkono Shalon wakaenda kupanda kwenye gari na safari ya kuelekea shule ilianza .
Walifika kwenye shule moja iliyokuwa nje ya mji lakini ilionekana ni shule nzuri sana na yenye mazingira ya kuvutia Shakira alivutiwa na muonekano wa ile shule.
" Shakira umeionaje hii shule? Max aliuliza.
" Inamuonekano mzuri nimepanda.
" Ok nimeshafanya malipo ya ada na kila kitu. Utapatuwa sare za shule na kila kitu kinachohitajika.
" Asante sana.
" Ukiwa na shida utanitafuta na hii ni namba yangu ya simu. Alisema max huku alimkabidhi kadi yenye namba zake.
" Asante sana .
Alishukuru Shakira huku machozi yakitaka kutoka.
" Jamani mdogo wangu umeona hii bahati iliyokushukia?
" Ndio dada .
" Unatakiwa kuwa makini pia soma kwa bidii.
" Sitakuangusha kwa hilo dada.
Baada ya kuongea waliagana na Shakira alafu waliondoka wakarudi nyumbani.

Usiku Dala na Shalon walikuwa wamekaa sebleni wakicheza na Max alikuwa akiwaangalia. Max alionekana kuwa na mengi ya kuongea na Dala lakini alishindwa sababu shalon hakumpa nafasi Dala alimganda na kumfuata kila anapoenda.
" Dala muda umeenda sana naomba ukambembeleze shalon alale.
" Sawa baba shalon. Shalon mama ni muda wa kulala twende zetu.
Shalon hakubisha aliongozana na dala huku wakiwa wameshikana mkono.
Alipanda kitandani ,dala alimbembeleza mpaka alipopitiwa na usingizi. Alipokuwa anataka kuondoka mara Max alifika.
" Shhhhhhi usije ukapiga kelele amelala.
" Ok njoo. Aliongea Max kwa sauti ndogo kisha dala alinyanyuka taratibu na kumfuata Max sebleni.
Dala alikaa kwenye kiti na kumsikiliza Max anachotaka kuongea.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote