SULTANA - Chanzo Ni Mapenzi

book cover og

Utangulizi

SULTANA (CHANZO NI MAPENZI).
Sultana na Sona ni ndugu wa damu na wote ni wanawake. Sultana ni mkubwa, Sona mdogo. Hawakubahatika kupata malezi ya wazazi wao. Walitangulia mbele ya haki mapema. Baada ya wazazi wao kufariki Sultani anabeba jukumu la kumlea mdogo wake akiwa na umri wa miaka 16 huku mdogo wake akiwa na miaka 10. Anajikuta anapoteza usichana wake kwaajili ya mdogo wake Sona na mwishoe anakuwa changudoa anayeogopeka sana mpaka nawanawake wenzie/wake za watu. Wanaume wanampangia foleni kumnunua na yeye habagui achagui anachotaka ni pesa tu. Hali hiyo inamuumiza mdogo wake Sona. Aliamini akiendelea kuwa karibu na dada yake hawezi kutimiza ndoto zake. Anamwambia dada yake ni namna gani anaumia kwa tabia zake na uamuzi wake wa kwenda mbali nae ili apambanie ndoto yake akiwa na amani, na zaidi anauvunja undugu wao wa damu kwa kumwambia dada yake kuwa wasijuane kwa chochote. Baada ya miaka kadhaa wanakutana tena ila Sona anaendelea kumkataa dada yake. Vita ya mapenzi inaibuka baada ya ndugu hao wa damu kuzama kwenye huba La kijana Liam. Liam ni kijana tajiri na asiyejua kujikweza. Anatokea kumpenda sana Sultana hajali kuwa ni kahaba anampenda hivyo hivyo na ukahaba wake. Hali ya Sultana kupendwa na Liam inamuumiza Sona. Anatumia kila mbinu ili kuwatenganisha na yupo tayari kumuuwa dada yake kama alivyomuuwa Marmar. Anajificha ndani ya wadhifa wake kufanya mauaji ya kikatili ili kufanikisha dhamila yake. Hataki Liam awe na mwanamke yoyote isipokuwa yeye Sona. Liam kwenyewe hana Habari nae anamchukulia kama rafiki yake wa karibu............FULL STORY IPO TAYARI.

SIMULIZI : SULTAN(CHANZO NI MAPENZI)
MTUNZI : NURU HALISI
SEHEMU 01

Mwanzo.......
Ukiyaangalia vizuri macho yake utagundua hayana tofauti na yale ya Simba jike.
Kama angezaliwa Mwanaume basi angeitwa Jemedari wa vita.
Wakati mabinti wengine wakiwatazama Wanaume kwa aibu, yeye aliwakodelea macho bila kupepesa kana kwamba anaangalia movie ya kusisimua.

Songa nayo 🌻
Jina lake anaitwa Sultana, akiwa na miaka 16 alipoteza usichana wake ili tu aokoe maisha ya mdogo wake.
Tangu hiyo siku aliisahau ndoto yake ya kuwa Rubani wa ndege aina ya Airbus A320
Aliamua kujikita katika biashara ya kutembea na Wanaume tofauti tofauti bila kujali umri wao.

Kitu pekee alichokipa kipaumbele kila alipokutana na Wanaume ilikuwa ni pesa. Jina lake lilikuwa maarufu ndani ya Kijiji cha Odes kuliko zao la tumbaku

"Sijivunii kuwa na Dada kama wewe....matukio yako yamekuwa ni ya kutisha kuliko hata ya watu wasiojulikana. Nahitaji kutimiza ndoto zangu hivyo kuanzia sasa nitakaa mbali na wewe, kama hatutaonana tena katika ulimwengu huu naomba usihuzunike sana ipokee kama hatma yetu". Mara nyingi Sultana huwa anayakumbuka maneno ya Sona (mdogo wake wa kike) hasa akiwa amelewa. Japo ni miaka kumi imepita sasa lakini anahisi ni kama jana

Siku yake huwa inaenda vibaya kuliko kawaida.....upendo alionao kwa Sona hauwezi kupimika na mizani ya Mangi

Shauku ya kumtafuta mdogo wake ilimuijia ghafla, aliamini sehemu pekee atakayoweza kumpata Sona ni Jijini Odes, hivyo alifunga virago vyake akaelekea stendi kuu kusubiria magari yanayoenda Jijini Odes.

Pumzi nzito kama mtu aliyetua mzigo zilisikika miongoni mwa Wamama na Mabinti baada ya kusikia Sultana ameonekana maeneo ya stendi.
Ni wazi kabisa alikuwa tishio kwao kuliko hata tetemeko la ardhi.
Waliiomba miungu yao isimrudishe kabisa Kijijini kwao, adhabu ya kifo au kupotea kusikojulikana ingemfaa zaidi.

Baada ya Sultana kukaa siti ya dirishani, alifumba macho yake.....hakufurahishwa na namna watu walivyokuwa wanamuangalia.

Safari ya kuelekea Jiji la Odes ilianza, watu wengi akiwemo yeye walionekana kuwa na shauku ya kufika.

🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
Ndani ya Jiji la Odes;
Katika jumba la kifahari lililojulikana kama Jumba la dhahabu, ukimya ulitawala kwa sababu ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Marmar.

Binti huyu alipoteza maisha siku moja kabla ya harusi yake.
Ripoti ya Daktari ilithibitisha kifo chake kimetokana na sumu aliyoivuta kwa njia ya hewa.
Ingawa ni miaka miwili imepita sasa lakini imekuwa ngumu kusahaulika katika Jumba la dhahabu.

"Liam yupo njiani, naomba kila kitu kiwekwe vizuri....hakikisha rangi nyeupe inatawala ukumbini na si hizo mlizoweka....msisahau kutakuwa na wageni pia" Bi. Fatma (Mama yake Liam) aliongea
Wafanyakazi walifanya kama walivyoagizwa....kila kitu kiliwekwa katika mpangilio mzuri.

Kabla ya Liam kwenda nyumbani kwao, alipita katika Casino lililojulikana kama "the night watchman"
Kuna mtu alihitaji kuonana naye kwanza kabla ya kwenda kushiriki kumbukumbu ya kifo cha Marmar, aliyesalia kidogo kuwa mke wake

"Sielewi kwanini umewekeza nguvu nyingi kuchunguza kwa mara nyingine kitu kilichokwisha kuthibitishwa na Daktari bingwa miaka miwili iliyopita, kama ningekuwa ni wewe nadhani ningefunika kombe mwana haramu apite..." Sona (mdogo wake Sultana) alishauri

"Naomba uniambie hicho ulicho fanikiwa kupata kwa kipindi chote nilichokuwa nje ya Odes..." Liam aliongea, ni wazi alitaka kusikia matokeo na si ushauri

Sona alimpatia bahasha iliyokuwa na ushahidi wa kila kitu
Liam hakuwa na subira, alichana bahasha ajionee kitu kilichopatikana.
Mapigo ya moyo wake yalizidi kwenda kasi kutokana na taarifa aliyokutana nayo

"Marmar alikufa kwa sababu alianza kufatilia kesi iliyofungwa muda mrefu...." Sona aliongea

"Nahitaji kumjua Muuaji na si chanzo cha kifo chake hilo ndilo lilikuwa lengo la Mimi kukuachia hii kazi....." Liam aliongea akionekana kutofurahishwa na taarifa alizopatiwa

"Alikuwa ni rafiki yangu, alinikaribisha Jijini Odes nikiwa sina sehemu ya kwenda...kwa pamoja tulitimiza ndoto zetu za kuwa Polisi. Kila kitu kitafahamika ni swala la muda tu naomba uniamini" Sona aliongea huku machozi yakimlenga lenga kwa kushindwa kufurahisha moyo wa Liam

"Nisamehe, umejitahidi kwa kiasi chake" Liam aliongea baada ya kuona Sona ana dalili ya kulia

Kwa pamoja waliingia kwenye gari, walihitaji kwenda kushiriki kwenye kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wao Marmar.

Watu wote walidondosha machozi baada ya kumuona Liam, tabia yao ya huruma ilimfanya ajisikie maumivu.
Fatma (Mama yake) alilitambua hili hivyo alimtuliza kwa kumkumbatia.

Muda wote Sona alimtazama Mwanaume huyu kwa matamanio....alijipa matumaini ipo siku atakuwa Mkwe katika Jumba la dhahabu.

"Iliandikwa wewe ufe ili Mimi ni bakie na Liam.... naomba usinichukie sana, hakukuwa na njia nyingine tofauti na wewe kufa kifo kile " Sona alijisemea ndani ya moyo wake huku akiitazama picha ya Marmar

"I wish urudi kwangu kama Mzimu...." Liam alijisemea akisogeza mdomo wake auzime mshumaa lakini kabla hajafanya hivyo
Watu wote waligeuka baada ya kumshuhudia mtu akija usawa wao akiwa amevalia mavazi meupe sawa na yao

Itaendelea πŸ’₯
SIMULIZI : SULTAN ( CHANZO NI MAPENZI)
MTUNZI : NURU HALISI
SEHEMU 02

Endelea 🌻
Sultana alisita kidogo baada ya kuona watu wote wanamtazama yeye.
Moyo wake ulishtuka mara elfu moja pale alipomuona Sona, mwanzo alihisi ni ndoto lakini kadri alivyozidi kumtazama alimtambua mdogo wake wa pekee ingawa ni miaka 10 imepita

"Kwanini uko hapa...." Sona alimtupia swali Dada yake akijitia hamjui

"Nilijua hili ni hekalu, na hata ni kaona inapendeza Mimi kutubu dhambi zangu kabla jua halijazama, ila nikiangalia muonekano wa mazingira napata picha kuwa haya ni makazi ya watu na si hekalu.... naomba radhi" Sultana aliongea kwa unyenyekevu

"Bila shaka wewe ni Mgeni Jijjni Odes, watu wengi hulifananisha Jumba hili na hekalu....mara ya kwanza Sona kutia miguu yake Jijjni Odes aliingia pia mahali hapa akihisi ni sehemu ya kufanya maombi....kuwa na amani" Bi. Fatma aliongea huku akionesha kufurahishwa na muonekano wa Sultana

"Kama hamtajali naomba nifanye maombi kwa dakika chache kisha nitaondoka...." Sultana aliongea baada ya kuiona sanamu ya tembo ukutani

Bi. Fatma alimpa ishara ya kukubaliwa ombi lake.
Sultana aliachia tabasamu kwa kupatiwa ruhusa, dimpozi zilizokuwa mashavuni kwake zilibonyea na kumfanya aonekane mrembo maradufu.
Liam alijikuta akiduwaa kumtazama, kitendo hiki hakikumfurahisha Sona hata kidogo

Sultana alifanya maombi yake kwa dakika kumi, baada ya kumaliza alivua bangili pamoja na hereni zake akaziweka mezani kama sadaka

"Hukuwa na haja ya kuweka sadaka, hili si hekalu...." Bi. Fatma aliongea

"mungu tembo amepoteza muda wake kusikiliza maombi yangu....ni jukumu langu kutoa sadaka kama sehemu ya shukurani" Sultana aliongea kisha akaondoka

Watu wote walibakia kumsindikiza kwa macho na hata wakasahau kama wapo kwenye kumbukumbu ya kifo cha Marmar

"Huenda akapotea njia kama ilivyokuwa kwangu mara ya kwanza kufika Jijini Odes.... nitakuwa msaada kwake" Sona aliongea kisha akaelekea nje.

Sultana akiwa anashuka ngazi alisimama baada ya kuhisi kuna mtu nyuma yake, hakuishia kusimama aligeuka nyuma pia.

"Sona....." Aliita huku machozi yakimlenga

"Jiji la Odes ni tofauti na Kijijini kwetu, kwa kuwa umeshaniona naomba urudi....sitarajii tukutane tena" Sona aliongea, hakuonesha dalili ya kumfurahia Dada yake

"Ni miaka 10 imepita bila sisi kuonana, unawezaje kuniambia hivi?" Sultana aliuliza

"Mimi ni yatima nisiyekuwa na Dada wala wazazi.....iwe mwanzo na mwisho kujitia unanifahamu undugu wetu uliisha ile siku nimeondoka, Wanaume wa huku si wajinga kama wa Kijijini kwetu hivyo kuwa makini...." Sona alimshauri kisha akaondoka

Sultana aliachia tabasamu.... kitendo cha kumuona tu mdogo wake ilikuwa ni faraja kwake. Alijifuta machozi kisha akaendelea na safari yake

Sona anarudi ukumbini kuendelea na ibaada, alishangaa sana baada ya kumuona Bi. Fatma kavaa bangili na hereni za Dada yake zilizotolewa kama sadaka. Alitamani kujua sababu ya kufanya hivyo lakini hakuwa na ujasiri wa kumuuliza kwanini ameamua kuvaa vile vitu.


Mida ya usiku Bi. Fatma akiwa chumbani kwake alijikuta akilikumbuka tabasamu la Sultana

"Huyo ni malaika aliyeletwa na mzimu wa Marmar.....uzuri wake unatosha kuipendezesha nyumba hii bila kuweka mapambo ya gharama..." Bi. Fatma aliongea

"Una maanisha nini...." Ali (dreva wake) aliuliza

"Sijamaanisha chochote, lakini kama ikitokea nimekutana naye nitakuwa wa kwanza kujipendekeza kwake kwa ajili ya Liam" Bi. Fatma aliongea

"Vipi kama ni mke wa mtu?" Ali aliuliza

"Mke wa mtu hawezi kutoa bangili na hereni zake kama sadaka, acha kuwa na maswali mengi..... ikitokea umekutana naye kabla yangu hakikisha unajipendekeza kwa ajili yangu" Bi. Fatma aliongea

Ali aliishia kujikuna kichwa chake hakuwa na neno la kusema

Upande wa Sona akiwa nyumbani kwake alikunywa pombe kali ili asahau maneno magumu aliyomueleza Dada yake lakini haikusadia kitu.
Michezo yote waliyocheza utotoni ilijirudia kichwani kwake.

"Najua kama si kupoteza usichana wako Mimi ningekufa.....lakini pamoja na yote haya ulipaswa utimize ndoto zako na si kuwa kahaba" Sona aliongea pekee huku akilia
Alitamani kujua Dada yake anaendeleaje, alitamani kusikia hadithi za Kijijini kwao.
Lakini hakuwa tayari kumpa nafasi kwa sababu kashaamua kusahau kila kitu kuhusu wao.

Kulivyo pambazuka asubuhi, Sultana alifungasha virago vyake.... alihitaji kurudi Kijiji Odes. Alifanya malipo yake dirishani kisha akaondoka
Wanaume wengi walimgeukia, wengi walitamani kummiliki lakini kwa namna macho yake yalivyokuwa makali sawa na ya Simba jike walipoteza ujasiri wa kumuongelesha

Kabla hajaenda stendi aliingia kwenye hoteli ya gharama sana kula.
Hakuwa mtu wa njaa.....kwa kipindi chote alichofanya kazi ya kuuza mwili wake alijikusanyia pesa ya kutosha.

Aliagiza chakula kisha akaanza kula bila kujivunga....dakika tano zilikuwa nyingi sahani ilikuwa nyeupe
Mhudumu alimletea chakula kingine

"Sijaomba kuongezewa chakula...." Sultana aliongea

"Boss pale kakulipia...." Mhudumu aliongea huku akionesha kwa kidole
Sultana aligeuza shingo yake amuone mtu aliyemnunulia chakula

Itaendelea πŸ’₯
SIMULIZI : SULTAN ( CHANZO NI MAPENZI)
MTUNZI : NURU HALISI
SEHEMU 03

Endelea 🌻
Sultana aliachia tabasamu baada ya kumuona Liam....hakutaka kukivungia chakula, alikula chote kwa dakika chache

"Sijui vyakula vyao wanapika kwa kutumia nini....ni kingi kwa macho lakini ni kidogo sana pale unapoanza kukitia mdomoni" Sultana aliongea baada ya kusogea kwenye meza ya Liam

"Mhudumu leta sahani nyingine...." Liam alimuagizia chakula kwa mara ya pili

Safari hii Sultana hakula badala yake alianza kukikagua
"Sasa nimeelewa kwanini tumbo langu linahitaji kula bado.... vipande vya nyama vimekatwa vidogo sana kama punje ya mchele...mboga mboga wamezifanya nyepesi sana kama karatasi, wali wao wameusambaza ili uonekane mwingi, kama ningeujua huu mchezo mapema nisinge kula" Sultana aliongea na kumfanya Liam atabasamu

"Anyway, hapa ni mjini vitu vingi vipo juu sana....kama akikata vipande vya nyama ukubwa wa ngumi yangu atapata hasara badala ya faida" Liam alikumbusha

"Na hii ndio sababu narudi Kijijini maisha ya kule ni rahisi sana tofauti na huku" Sultana aliongea

"Muonekano wako hauruhusu kuishi Kijijini unatakiwa kuwa pambo kwenye Jiji kama hili.." Liam alishauri

"Ni ngumu kuishi Jiji kama hili bila kazi.... usiniambie unataka kuwa sponsor wangu, nipo tayari kwa hilo kikubwa nisilale njaa wala kusumbuliwa na mwenye nyumba" Sultana aliongea huku akitabasamu

Liam alijikuta akimtazama na hata akasahau kama ni zamu yake kutoa jibu.

"Tutaonana kwa wakati mwingine..... nahitaji kuwahi gari" Sultana aliongea baada ya kuona mtu anayeongea naye katekewa

"Ni kitu gani kimekuleta mjini, au wewe ni mfanya biashara wa mazao napenda sana kilimo lakini sijui nianzie wapi" Liam aliongea

"Nikikueleza kazi nayofanya utapatwa na mshtuko wa moyo....uwe na siku njema" Sultana aliongea kisha akasimama asepe
Liam hakuwa tayari kumuacha binti huyu aondoke bado alikuwa na hamu ya kuongea naye

"Usihofu kuhusu usafiri nitakurejesha mwenyewe siku ya kesho na gari langu....sijui umeniroga lakini nimejikuta ni kitamani kuongea na wewe" Liam aliongea, simu yake iliita.... mpigaji alikuwa ni Sona aliirudisha mfukoni badala ya kupokea

"Kuliko tukae hapa kuwa mwenyeji wangu....natamani kuiona fahari ya Jiji la Odes nikijua siku ya kesho utanipeleka Kijijini kwetu" Sultana aliongea
Liam hakuwa na ubishi.....kwa pamoja waliingia ndani ya gari wakaanza kuzunguka huku na kule


Sona hakukata tamaa, aliendelea kupiga simu mpaka mida ya usiku lakini Liam hakupatikana.

Ukweli ni kwamba Liam na Sultana walikuwa kwenye Club moja kubwa kuliko yote Jijini Odes wakishangaa namna watu wanavyocheza mziki

"Watu wanajirusha kama kesho hawataliona jua.... hakika wanajua kuitendea haki leo yao" Sultana aliongea

Liam hakuwa na maneno ya kuongea zaidi ya kumkodolea macho.

"Kwanini unanitazama hivyo, usiniambie unafikiria ni namna gani utapata figo zangu ukauze....au unataka kuchuna ngozi yangu " Sultana aliuliza

"Una uzuri wa pekee, ni kawaida kwa Mwanaume yoyote kukuangalia bila kukoma...." Liam aliongea

"Jiji la Odes ni la kawaida sana.... itapendeza ni kipumzika" Sultana aliongea, macho yake yalionekana kuwa na usingizi kupita kiasi

Liam alikuwa mwema, alimpeleka kwenye hotel aliyoamini inatoa huduma nzuri kuliko zote ....bahati mbaya kulikuwa kumesalia chumba kimoja.

"Naomba unisamehe tutalala hapa wote...." Liam aliongea
Sultana hakuwa na muda wa kuzungumza alijitupa kitandani, dakika tano zilikuwa ni nyingi kwake kusinzia

Liam alikuwa na wakati mgumu alijikuta akimsogelea Sultana aliyekuwa hajitambui.
Kitendo cha kushika tu mgongo wake bila ruhusa alikula kofi la uso

"Huna haja ya kunivizia.....tamka kiasi cha pesa ulichonacho nitakuhudumia kulingana na kodi yako..." Sultana hakuona aibu kuzungumza kuhusu kazi yake

Liam hakutaka kujua kuhusu biashara yake, alimpatia pesa alizonazo huku akiahidi kumuongezea zingine siku ya kesho akipita ATM

Walijikuta wakifanya mapenzi baada ya kuafikiana.
Kwa mara ya kwanza Sultana alifurahia kwa namna Mwanaume huyu alivyokuwa ana mtendea kama mkewe na si Kahaba

Kulivyo pambazuka asubuhi..... walielekea ATM kutoa pesa, zilikuwa ni pesa nyingi kiasi kwamba Sultana aliogopa kuzichukua
Liam alimkabidhi zote, kwa kuwa wote walikuwa na njaa walikuwa na njaa iliwalazimu kupita hotelini kunywa chai

Ilikuwa ni hoteli ya kifahari, walisubiria dakika chache lifti ifunguke ili waingie.

Macho ya Sultana yalipatwa na mshangao baada ya lifti kufunguka.....begi lake la pesa lilidondoka chini

Itaendelea πŸ’₯
SIMULIZI : SULTAN ( CHANZO NI MAPENZI)
MTUNZI : NURU HALISI
SEHEMU 04

Endelea 🌻
Sona akiwa amevalia sare za Polisi alitoka ndani ya lifti akiwa na wenzake, kama kawaida yake alivunga hamfahamu Sultana badala yake alianza kuongea na Liam

"Kuna changamoto ilitokea hapa, hivyo sisi kama Polisi tulifika kuweka mambo sawa....sina uhakika kama mtapata huduma siku ya leo kwa sababu jengo hili linatakiwa kufungwa kwa ajili ya upelelezi" Sona aliongea

"Kitu gani kimetokea...." Liam aliuliza

"Watu wawili wamepatikana wamekufa.....bahati mbaya ni Raia wa Israeli, nadhani unaelewa balaa lilipo kama wahusika wa mauaji haya hawatapatikana. Kwa siku kadhaa hakutakuwa na huduma ya usafiri..." Sona aliongea kisha akaondoka na wenzake

"Mahali hapa hapafai tena... tuondoke" Liam alimuambia Sultana

Kwa pamoja waliingia kwenye gari, Sultana alijikuta akidondosha machozi... ndani ya moyo wake alifurahi kuona mdogo wake katimiza ndoto yake.
Mavazi ya Kipolisi yalimpendeza kupita kiasi....

"Kwanini unalia...." Liam alimuuliza
"Mimi pia ni mgeni Jijini Odes, nimejikuta tu ni kiwahurumia wageni waliopatikana wamekufa...." Sultana aliongea

"Nitakutafutia sehemu nzuri ukae mpaka pale huduma ya usafiri itakapo rejeshwa, ni sehemu salama kuliko hata nyumbani kwangu" Liam aliongea

Sultana alitikisa kichwa kuashiria ameelewa.
Haikuwa shida kwa Liam kumpangishia mrembo huyu hoteli iliyo mgharimu shilingi milioni moja kwa siku.
Huduma za Burj Al zilikuwa nzuri sana hasa kwa mtu anayeamua kufanya makazi mahali kwa siku kadhaa.

"Hapana, siwezi kukaa hapa...unakoelekea utaniomba kwa mpalange, niache nijitafutie mwenyewe sehemu ya kulala" Sultana alishtuka baada ya kuoneshwa makazi yake ya muda

Liam alijikuta akicheka kwa maneno aliyoambiwa
"Naomba ukue kiakili....ni aibu kuudhalilisha urembo wako kwa kuongea maneno bila kutumia tafsida" Liam aliongea

"Yule Polisi wa kike ni nani yako...." Sultana alijikuta akiuliza

"Ni rafiki wa familia yangu.....ni Polisi pekee anayeogopeka hapa Jijjni Odes, hivyo hata hili tukio lililotokea atalikamilisha kwa muda mfupi utaweza kurudi Kijijini kwenu, yeye pia ni mzaliwa wa Odes Kijijini" Liam aliongea

Sultana aliachia tabasamu habari hizi zilimvutia na hata akasahau kama yupo Burj Al
Liam alitaka kuondoka lakini Sultana alimzuia

"Naomba nijue unafanya kazi gani....kama nilivyokuambia Mimi ni Kahaba ninaye tegemea mwili wangu kujiingizia kipato. Naomba nijue pia kuhusu kazi yako....unatumia pesa vibaya sana niambie unazitoa wapi" Sultana aliuliza

"Ninafanya biashara nyingi sana, nikianza kukutajia moja baada ya nyingine jua litazama nikiwa naongea....." Liam aliongea

"Nitajie japo moja vinginevyo sitalala hapa...." Sultana alitishia

"Namiliki Kampuni la utengenezaji wa Meli linalojulikana kama Star ships" Liam aliongea kisha akasepa kuna mahali alionekana kuwahi

Sultana alidumu kwenye mshangao, amezoea kukutana na Wakulima lakini kwa mara ya kwanza katembea na CEO wa Star ships


Upande wa Sona akiwa kazini kwake alijikuta akipoteza focus hasa akikumbuka namna alivyomuona Dada yake akiwa na Liam.
Tabia za Sultana anazifahamu hivyo alikuwa na uhakika wawili hawa tayari wamekutana kimwili

:Niliwaona wakiingia Burj Al hotel....lakini Liam kaondoka nina uhakika yule mrembo atakuwa pale: Ujumbe uliingia kwenye simu ya Sona

Alifunga ofisi kisha akaondoka, dakika 15 zilikuwa ni nyingi alifika Burj Al
Aliulizia chumba kilicho chukuliwa na CEO wa Star ships
Baada ya kufahamishwa aliingia kwenye lifti

Sultana akiwa anahesabu pesa, mlango wake uligongwa.....sura ya Sona ilionekana kwenye TV ndogo.

Sultana alisimama akaenda kufungua mlango....kama kawaida yake aliachia tabasamu lakini Sona alimkazia

"Ulikuja Jijjni Odes kwa ajili yangu au kutafuta Wanaume!.... umewezaje kutembea na Liam, ulipaswa kuniuliza Mimi na yeye tuna uhusiano gani kabla hujamuonesha u.......chi..... wako" Sona alifoka

"Ndiyo Mimi ni Kahaba....lakini pua zangu zinajua kunusa yupi ni Mume wa Sona wangu na yupi si wake.....Liam hana uhusiano wowote na wewe ndio maana nilikubali kufanya biashara naye, nimesikia wewe ni rafiki wa familia yake ni kawaida kumlinda sababu ya tabia zangu.... usiwe na hofu pindi huduma ya usafiri itakapo rejeshwa nitaondoka..." Sultana aliongea akiachia tabasamu

Muonekano wa uzuri wake ulimkwaza Sona..... taratibu alijishika mfukoni mwake
Sultana hakuamini alichokiona

Itaendelea πŸ’₯
SIMULIZI : SULTAN( CHANZO NI MAPENZI)
MTUNZI : NURU HALISI
SEHEMU 05

Endelea 🌻
Sona alimshikia Dada yake bastola huku uso wake ukiwa umekunjamana

"Usiku wa leo nitautumia vizuri kuwatafuta wauaji wa wageni kutoka Israel.....hivyo kutakapo pambazuka asubuhi naomba uondoke na kamwe usije kurudi Jijini Odes, endapo utaenda kinyume na makubaliano yetu nitaachia risasi bila kujali ulipoteza bikira yako ukiwa na miaka 16 kisa Mimi" Sona aliongea kisha akairudisha bastola yake kwenye koti

Sultana alibakia kukodoa macho, kila kitu alichokuwa ana kiona na kusikia ilikuwa ni ndoto kwake

Sona alitaka kuondoka lakini aliijiwa na wazo jipya kichwani mwake

"Utalala nyumbani kwangu usiku wa leo....kutakapo pambazuka asubuhi nitakurejesha mwenyewe Kijijini Odes..." Aliongea kisha akaanza kukusanya virago vyote vya Sultana pamoja na pesa zake, alimshika mkono kisha wakaondoka

"Pindi CEO wa Star ships atakapouliza kuhusu huyu binti mwambie kaondoka na Mwanaume mwingine.... Mama yako ni msafirishaji mzuri wa madawa ya kulevya, endapo utazungumza tofauti na maagizo yangu itanilazimu nianze kufatilia hatua zake" Sona alimchimba mkwara Dada wa mapokezi kisha akasepa na Dada yake

Wakiwa ndani ya gari, alimfunga Dada yake kitambaa cheusi machoni

"Kwanini unanitendea hivi kama mateka?" Sultana aliuliza

"Sitaki ufahamu sehemu ninayoishi....ni hivyo tu" Sona aliongea
Sultana aliachia tabasamu, dimpozi zilizokuwa mashavuni kwake zilimfanya aonekane mrembo ingawa macho yake yalikuwa yamefungwa.....Sona alijikuta akiumia ni kama alikuwa anamuonea wivu Dada yake kwa muonekano aliojariwa, aliendesha gari kwa kasi kana kwamba ana fukuzana na majambazi

Nyumba yake ilikuwa nzuri kuliko kawaida..... Sultana alifurahia mafanikio ya mdogo wake baada ya kutolewa kitambaa

"Nisamehe lakini nitakufunga mikono na miguu ili usije kutoroka...." Sona aliongea, safari hii alimzimisha Dada yake kwa kumpulizia madawa ya usingizi.

Alimfunga mikono na miguu, baada ya kumaliza alielekea sehemu aliyoamini ataweza kuwa kamata Wauaji.

Upande wa Liam, anarejea Burj Al hotel akiwa kabeba zawadi kwa ajili ya Sultana. Anashtuka ndani ya moyo wake baada ya kukuta chumba kimepangwa vizuri kana kwamba hakukuwa na mtu.
Alirudi mapokezi kujua ni kitu gani kinaendelea

"Ooh, baada ya wewe tu kuondoka kuna Mwanaume mwenye asili ya kiarabu alikuja kumchukua....nadhani ni mpenzi wake" Dada wa mapokezi aliongea

Moyo wa Liam ulivunjika kwa namna fulani, hakuona hata maana ya kuondoka na zawadi alizokuwa kamletea Sultana, alimuachia Dada wa mapokezi


Kulivyo pambazuka asubuhi, Sona anarejea nyumbani akiwa na jeraha mkononi mwake.
Alimfungulia Dada yake mikono na miguu....

"Kabla sijaelekea kazini nitakupeleka Kijijini Odes...." Sona aliongea

Sultana alinyoosha mkono wake taratibu akalishika jeraha lililokuwa mkononi kwa mdogo wake

"Hii si kitu, huna haja ya kupata presha" Sona aliongea, hakujali kama Dada yake ana njaa au la...alichotaka yeye ni kumtoa Jijini Odes

Wakiwa ndani ya gari aliijiwa na wazo jipya
"Kama nitamrudisha Kijijini Odes nina uhakika atarudi kunitafuta....haonekani kukata tamaa kuhusu Mimi" Sona alijisemea kisha akabadilisha uelekeo wa gari

Alihitaji kuiwahi Meli iliyokuwa inaelekea China....
Hakutaka kusikia nasaha za Dada yake hivyo alimzimisha kwa kuipiga shingo yake kwa nguvu

"Kama atapatikana hana uraia au kibali maalumu cha kuishi Nchini humo hukumu yake itakuwa ni kifo....kuliko umpeleke huko ni heri umtupe baharini afe" Polisi mmoja aliyekuwa anaelekea China aliongea

"Siwezi kumuua.... nina uhakika uzuri wake utamuokoa pindi atakapokuwa China hastahili kukaa Jijini Odes wala Kijijini kwetu.... safari njema" Sona aliongea kisha akaondoka...ndani ya moyo wake hakuonesha kuumia.

Aliwahi kazini haraka kukabiliana na Waharifu aliowakamata.

Sultana anarejesha fahamu akiwa kwenye mabehewa ya mizigo.....kabla hata hajafikiria vizuri alisikia kelele za watu wakiomba msaada

"Usijiokoe pekee yako.... hakikisha unasaidia watu wawili na zaidi huo ndio Uzalendo wa watu wa Jijini Odes.... Meli inazama" Sauti ilisikika kupitia kipaza sauti

Sultana alichanganyikiwa..... alianza kufunua huku na kule akimtafuta Sona, hakuwa tayari kujiokoa pekee yake kama tangazo lililivyo sikika
Ghafla mlango wa mabehewa ya mizigo ulivunjwa.
Sultana alibakia kukodoa macho


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote