Follow Channel

TALIA - (FORBIDDEN LOVE)💔❤️‍🩹

book cover og

Utangulizi

Baada ya kupoteza wazazi wake kwenye ajali mbaya ya gari, Talia, msichana mwenye roho safi na aliyelelewa katika upendo, anahamia nyumbani kwa mama yake wa ubatizo – Aunt Sandra, anayemchukulia kama binti wa damu. Talia anakaribishwa na kupendwa na familia nzima, hasa na watoto wa Aunt Sandra –Eli Miller pamoja na kaka yake Damian– vijana wawili wenye mvuto wa kipekee lakini tabia tofauti kabisa.
Kadri miaka inavyosonga, Talia anajikuta akimpenda sana mmoja wa vijana hao – Eli, mvulana mwenye haiba ya utulivu lakini mwenye hisia za kina anazoficha. Penzi linajengwa kimya kimya, hadi wakati Lola, binti wa mfanyakazi wa ndani, anapoingia kwenye nyumba hiyo kwa sababu za kifamilia, unahisi nini kitaendelea?.........

SONGA NAYO…….

TALIA - (FORBIDDEN LOVE)💔❤️‍🩹
SEHEMU: 1

Sauti ya mvua ilisikika ikinyesha kwa mbali huku gari la Aunt Sandra likielekea kwenye makazi yao ya kifahari yaliyopo Mbezi Beach. Nilikuwa kimya, nikiangalia matone ya mvua yakigonga kioo cha dirisha, moyo wangu ukiwa mzito kama anga la jioni ile.
Nilikuwa nimepoteza kila kitu – wazazi wangu walifariki wiki tatu zilizopita kwenye ajali ya gari walipokuwa wakitoka Morogoro. Nilikuwa pekee yangu, hadi Aunt Sandra aliponichukua kama binti wake. Hakuwa mama yangu wa damu, bali alikuwa rafiki kipenzi wa mama yangu na mama yangu wa ubatizo.
Alinipokea kwa mikono miwili.
“Talia, hapa ni nyumbani sasa. Usiogope kitu,” alisema kwa sauti ya upole niliposhuka kwenye gari lake. Nilijitahidi kutabasamu, japo moyo ulikuwa umejaa maumivu.
Ndani ya nyumba kulikuwa na harufu ya sabuni ya lavender, mapazia meupe, na sakafu iliyong’aa. Niliwaona vijana wawili waliosimama mlangoni – walikuwa ni Eli mtoto wa Aunt Sandra pamoja na Liam rafiki wa karibu wa Eli. Walisimama kwa heshima, macho yao yakinitazama kwa haya.
“Karibu,” Eli alisema, sauti yake ikitulia kama sauti ya mziki wa taratibu. “Mimi ni Eli, huyu ni rafiki yangu Liam.”
Liam alitabasamu kwa upole, “Sasa tutakuwa ndugu.” Alisema akinikazia macho kwa namna fulani ambayo moyo wangu ulijibu kimya kimya. Nikamjibu kwa kichwa.
Nilihisi joto la kupokelewa, lakini pia kuna kitu kilikuwa tofauti... japo sikuweza kukitaja.
Siku ziliendelea. Niliingia shule ileile waliyosoma kaka hao wawili, maisha yalianza kunitabasamia tena. Aunt Sandra alinijali kama mama. Niliishi nao kama dada wa damu. Lakini moyo wangu mdogo ulianza kuvutiwa – na si kwa wote wawili.
Ni Eli aliyekuwa wa kwanza kunifanya niwe na ndoto za usiku. Mvulana mtulivu, mcheshi kwa wakati, lakini mwenye macho ya kuzungumza mengi kuliko kinywa chake. Alinielewa zaidi kuliko mtu yeyote. Kila mara nilipokuwa kimya, alikuwa karibu kuuliza “uko sawa, Talia?”
Siku moja tulikuwa bustanini, wakati wa jioni. Mwangaza wa jua ulikuwa dhaifu, na hewa ilibeba harufu ya maua ya waridi.
“Talia,” Eli aliniita kwa sauti ya kujiamini, “unafahamu kwamba... sijawahi kukutana na msichana kama wewe?”
Nilikosa cha kusema. Moyo wangu ulikimbia kwa kasi ya ajabu.

Sikua na chochote cha kumjibu, niliishia kutoa macho tu…….kwani hata mimi alikua ameshaanza kuniingia moyoni kimtindo.

Itaendelea

TALIA - (FORBIDDEN LOVE)💔❤️‍🩹
SEHEMU: 2

Usiku mmoja ukiwa ni wa utulivu usio wa kawaida. Nilikuwa nimekaa kitandani, nikitazama dari la chumba changu kipya huku nikihisi harufu ya karafuu kutoka kwenye mashuka mapya. Kulikuwa na hali ya utulivu uliovaa upweke. Macho yangu yalishindwa kulala kwa sababu moyo ulikuwa unadunda—ukimuwaza Eli.
Siku ile bustanini haikuondoka akilini mwangu. Maneno yake yalibaki masikioni:
"Sijawahi kukutana na msichana kama wewe..."
Je, ilikuwa ni kweli au ilikuwa tu hisani ya kaka anayejali?
Kesho yake asubuhi, nilimkuta jikoni akiwa amevaa t-shirt ya kijivu iliyomkaa vizuri mno, na suruali fupi ya nyumbani. Alikuwa anakunywa kahawa na kutikisa miguu yake kwa utaratibu, huku akichezea simu.
“Habari ya asubuhi,” nilisalimia nikijikakamua kutokuonyesha msisimko wa ndani.
“Mzuri,” alitabasamu akiniangalia, “umependeza leo… wait, huwa unapendeza kila siku.”
Aliniangalia juu hadi chini. Nilishtuka kidogo lakini moyo ukachafuka kwa raha ya siri. Alinifanya nijisikie kama mwanamke, si msichana tena.
Niliketi karibu naye, na kwa muda mfupi tulikuwa kimya.
“Kuna kitu nataka kukuambia, Talia…” alisema kwa sauti ya kujiamini, lakini macho yake yalikuwa na ukakasi wa hofu ndogo. “Lakini si leo… leo tuwe rafiki tu.”
Akanyanyuka, akapita nyuma yangu, akaniwekea mkono begani. Alinishika laini, kwa muda mrefu kidogo kuliko kawaida. Na moyo wangu ukadunda kwa kasi.
Wiki moja baadaye
Nilimjua Eli tofauti. Tuliongea sana. Tulicheka. Tulitembea jioni. Na siku moja, alinipeleka kwenye rooftop ya nyumba yao – mahali ambapo walikuwa na sehemu ya kukaa, maua, meza na taa ndogo za rangi.
“Umepapenda hapa?” aliuliza akisimama nyuma yangu. Nilisema, “Niko salama kila mara nikiwa nawe.”
Akanishika mikono yote miwili, akanizungusha nikakutana naye uso kwa uso.
Akaniangalia, kisha akasema: “Talia... I can't lie anymore.”
Alinibusu.
Si busu la haraka. Si busu la mashaka. Lilikuwa busu la mtu aliyekuwa amezuia hisia kwa muda mrefu. Mikono yake ilipanda kiunoni mwangu, na yangu ikazunguka shingo yake.
Tulikuwa peke yetu. Mawazo yote yalinyamazishwa na mapigo ya mioyo yetu.
Eli aliniinua taratibu akanikalia kwenye meza ya mbao. Nilishtuka kwa mchecheto, lakini hofu hiyo ilizimwa na moto uliokuwa ukizidi ndani yangu. Midomo yetu iliendelea kucheza, na miili yetu ilianza kuzungumza lugha ya chumbani.
Mikono yake ilisafiri taratibu, kwa uangalifu, akiniangalia kila mara kutafuta idhini isiyo ya maneno. Nilimpa.
Nguo zilianguka moja baada ya nyingine, hatua kwa hatua, kama karatasi zinazofunua zawadi ya siku nyingi.
Mwangaza wa taa nyekundu uliangaza ngozi zetu zikiungana. Kulikuwa na harufu ya joto, pumzi za haraka, na sauti zisizo za kawaida.
Usiku huo… niliutambua upendo kwa mwili. Na Eli alitambua mimi si mtoto tena – bali mwanamke aliyempenda kwa roho na mwili.
Lakini siku chache baadaye...
Lola aliwasili.
Na kila kitu kilianza kubadilika.

Itaendelea………


TALIA - (FORBIDDEN LOVE)💔❤️‍🩹
SEHEMU: 3

Siku ya kuwasili kwa Lola haikua ya kawaida. Nilikuwa nimekaa sebule, nikisoma kitabu cha riwaya huku nikisubiri chakula cha mchana, wakati mlango wa mbele ulipofunguliwa na sauti mpya ikaingia.
“Heee! Mungu wangu, hapa ni peponi!”
Msichana mrefu, mweupe wa rangi ya maziwa, macho makubwa ya miale na nywele zilizoning’inia kwa mtindo wa asili aliingia kama staa wa sinema. Alikuwa na suruali fupi iliyoonyesha mapaja yake, na top iliyomuacha nusu kifua wazi.
“Lola!” Aunt Sandra alipiga kelele kwa furaha, akamkumbatia binti huyo kwa upendo. “Karibu nyumbani, mpenzi. Kuanzia leo, hii ni nyumba yako.”
Nilitabasamu kwa heshima. “Karibu sana.”
Akanigeukia, akanikazia macho, kisha akatabasamu kidogo—tabasamu ambalo halikufika moyoni.
“Mmmh… wewe lazima ni Talia,” alisema kwa sauti ya kuvutia sana. “Wamesema una roho ya dhahabu.”
Sikujua kwa nini niliingiwa na baridi la ghafla. Kulikuwa na kitu kwenye macho yake, kama ushindani usioeleweka.
Jioni hiyo, nilimkuta Eli na Liam wote wakiwa sebuleni wakimtazama Lola akiangusha maelezo ya maisha yake.
“Nilikuwa najifunza fashion Arusha,” alisema akicheka, “lakini maisha hayakuwa fair, nilihitaji mahali pa kuanzia upya.”
Kila mmoja alikuwa anacheka naye, hasa Liam aliyekuwa mcheshi kuliko wote.
Lakini nilishtuka zaidi pale macho ya Eli yalipomtazama kwa muda mrefu kidogo—kama mtu aliyeguswa. Na moyo wangu ukapiga kwa wasiwasi kwa mara ya kwanza.
Usiku wake, nikiwa chumbani kwa Eli nimelala kitanda kwake, tukiongea chini kwa chini kama wapenzi wa muda mrefu.
“Unamfahamu Lola?” niliuliza kwa sauti ya kawaida.
Alikaa kimya, kisha akasema, “Niliwahi kumwona mara moja, kitambo sana akiwa mdogo. Lakini amekuwa sana…”
Sauti yake ilikuwa na mshangao, lakini haikuwa ile ya kawaida – ilibeba hisia mpya.
Niligeuka upande wa pili wa kitanda kimya kimya. Kwa mara ya kwanza, nilijisikia sio wa pekee tena.
Siku zilizofuata, Lola alianza kuchukua nafasi. Alijua kupika vizuri, aliweza kucheka na kila mtu, na kila alipovaa, macho yote yalikuwa kwake.

Hata Aunt Sandra alianza kumpa nafasi zaidi, hata kumuagiza sehemu mbalimbali, “nenda na Eli mjini, anataka kununua kitu fulani.”
Na siku hiyo iliuma sana.
Nilimsubiri Eli arudi usiku huo akiwa na harufu ya perfume ya kike kwenye shati lake. Alisema walikuwa kwenye duka moja la mavazi, lakini hakuweza kunitizama usoni.
“Lola ni rafiki tu,” alisema kwa haraka, kabla sijauliza.
Lakini nilikuwa nimeshajua. Penzi langu lilikuwa linazama.
Usiku mmoja niliingia jikoni kuchukua maji. Nilimsikia Liam akiongea na mtu kwa simu:
“Kama Eli atachezea moyo wa Talia kwa ajili ya huyo msichana, nitamchukia milele.”
Nilikwama. Liam aliniangalia na kukata simu kwa haraka.
“Talia… samahani, hukupaswa kusikia.”
“Liam,” nilisema kwa sauti ya karibu na kilio, “Eli ananipoteza, siyo?”
Liam alikuja mbele yangu, akanishika mikono. “Kama hakujui thamani yako sasa hivi... basi nitamwonyesha.
Katika ile hali ya kuumia, ghafla nilihisi macho ya Liam yanakazia kwangu, si kama kaka tena, bali kama mwanaume anayetaka nafasi. Alinisogelea taratibu, akaegemea karibu na mimi, pumzi zake zikigusa uso wangu.
“Talia, unastahili upendo wa kweli… na si kuchezewa.”
Je, Liam anaanza kupigania moyo wa Talia? Na Lola je, anajua anachofanya?


TALIA - (FORBIDDEN LOVE)💔❤️‍🩹
SEHEMU: 4

Siku hiyo usiku, nilijilaza kitandani nikiwa nimevaa nightdress yangu ya silk ya pinki, lakini usingizi ulikuwa mbali sana na macho yangu. Kila mara nikijaribu kufumba macho, nilimwona Eli – lakini si Eli niliyemzoea – bali Eli akiwa na Lola.
Wakicheka, wakitazamana, wakigusa migongo yao kwa utani wa kimahaba.
Moyo wangu ulizidi kujaa shaka. Nilijua kitu kilikuwa kinatokea, lakini hofu yangu kubwa ilikuwa ni kuwa Eli hakuniambia chochote.
Siku iliyofuata, Aunt Sandra alikuwa amesafiri kikazi kwa siku mbili. Usiku wake, kila mtu alikuwa busy na mambo yake. Nilikaa sebuleni nikitazama Netflix nikiwa na chupa ya maji ya baridi. Wakati huo Eli akiwa hapokea simu zangu.
Nilimwona Lola akiteremka ngazi akiwa amevaa gauni refu jeupe la kupendeza sana – lakini nene kidogo kwa ajili ya kulala. Alienda jikoni, akachukua glass ya divai, akarudi sebuleni.
“Upo peke yako?” akauliza kwa sauti ya ucheshi.
“Ndio,” nilijibu bila shaka.
“Aaah… thought ningempata Eli hapa. Aliniahidi atanionyesha jinsi ya kucheza ile game yao ya PS5.”
Game? Wapi tena? Lakini hakunijibu chochote.
Dakika chache baadaye, Lola alipotea ghafla. Na muda mfupi baadaye, nilisikia mlango wa chumba cha Eli ukifungwa kwa ndani taratibu.
Machozi yalianza kunitoka sikusogea. Nilikaa pale kwa zaidi ya saa moja nikisikiliza ukimya. Lakini dakika zilikapita na hatimaye… niliamka.
Nikanyata taratibu hadi mlangoni kwa Eli. Sikugonga. Nilisimama tu pale, moyo ukinienda mbio kwa uwoga.
Ndani, nilisikia sauti za kicheko, kisha kimya... halafu sauti za midomo ikiungana, zikifuatwa na mikwaruzo ya kitanda, pumzi za haraka, na milio ya mahaba isiyodhibitiwa.
Nilifumba macho.
Nilitaka kupiga kelele. Nilihisi kama dunia imeanguka juu yangu. Kila kipande cha moyo wangu kilivunjika ghafla – kama kioo kilichodondoka kwenye sakafu ya sakafu ya tiles.
Nilikimbia chumbani kwangu bila kujali chochote. Nilijilaza chini ya blanketi nikilia kwa kimya, nikigugumia maumivu yasiyo na dawa.
Kesho yake, nilimkwepa Eli. Nilimkwepa Lola. Nilimkwepa hata macho yangu mwenyewe kiooni. Lakini mtu mmoja hakuweza kunikwepa.
Liam.
Alinikuta bustanini, nikiwa nimejifunika na kitenge, nikitazama maua.
Aliketi karibu na mimi bila kusema neno kwa dakika kadhaa.
“Walilala pamoja, sio?” niliuliza bila kumuangalia.
Liam alishusha pumzi ndefu. “Talia…”
“Jibu swali langu,” nilakata maneno. “Walilala pamoja?”
“Ndiyo.”
Alisema bila kupinda. Bila kuupaka sukari ukweli. Bila huruma.
Machozi yalinitoka tena, lakini kwa ndani palikuwa pakavu. Nilikuwa nimechoka. Nilihisi mweupe. Mtupu.
“Basi sina cha kutafuta hapa tena, Liam.”
Alinikamata mkono. “Talia… usiondoke kwa hasira. Nitaumia sana.”
“Ulivyokuwa kimya juu ya haya yote, hiyo pia ilikuwa usaliti.”
“Nilikulinda.”
“Ulilinda ukimya.”
Nilinyanyuka. Nilipokuwa nikitoka, Liam aliniita kwa sauti ya chini.
“Talia… nataka ujue kitu kimoja. Huyo rafiki yangu... anaweza kuwa amekupoteza. Lakini mimi... sijawahi kukuacha hata sekunde moja.”
Nilitazama macho yake. Macho yaliyokuwa yamejaa huzuni… na mapenzi ya kweli, lakini kwa wakati huo nikiwa na hasira sana hata nisiwee kumsikiliza.
Usiku huo nilifunga mizigo yangu. Niliandika barua kwa Aunt Sandra. Niliacha kila kitu nyuma – nguo, picha, kumbukumbu.
Nilipanda teksi alfajiri na kuondoka.
Hakuna aliyejua nilikokwenda.
Lakini walijua kitu kimoja:
Walinipoteza.
Itaendelea……. 💔💫


TALIA - (FORBIDDEN LOVE)💔❤️‍🩹
SEHEMU: 5

Nilikimbilia Bagamoyo, mji wa ukimya, historia, na upepo wa bahari. Nilikodisha chumba kidogo cha gesti ya zamani, kilikuwa na kitanda cha mbao na dirisha lililokuwa likilia na upepo wa mchana. Nilihitaji mahali pa kutafakari – na kusahau.
Sikuwa na mpango wa kurudi Dar es Salaam. Nilifuta kila namba. Niliwafungia wote – Eli, Liam, hata Aunt Sandra.
Kwa wiki nzima, nilikula kimya, nilitembea ufukweni, na nilijaribu kuishi kama mtu ambaye moyo wake haujapondwapondwa na mapenzi.
Ndipo siku ya nane, nilipokutana na kijana mmoja.
Nilikuwa kwenye mgahawa mdogo wa kiasili nikinywa juisi ya ukwaju, wakati mwanaume mmoja aliingia – mrefu, mwenye ngozi ya chocolate laini, macho ya kutoeleweka, na sauti nzito iliyoamuru heshima kimya kimya.
“Nisaidie meza moja,” alisema kwa kirafiki kwa mhudumu, kabla hajanigeukia. “Au nikae tu hapa, kama hauna shida.”
Nilitikisa kichwa. “Hakuna shida.”
Alikaa.
“Talia, sio?”
Nikageuka kwa mshangao.
“Unanijua?”
Akatabasamu. “Mimi ni Damian. Kaka yake Lola. Na nimekuwa nikikutafuta.”

Daminia ni mtoto wa Aunt Sandra, yaani kaka yake Eli, ila wakati naingia nyumbani kwa Aunt Sandra yeye alikua masomoni hivyo hatukuwahi kuonana.

Aliamua kujitambulisha kama kaka yake na Lola ili Kufanya nimuone kama mtu wa mbali, asiye sehemu ya familia moja, ili kuruhusu mvuto wa kimapenzi kuanza.
Kwa sekunde kadhaa, nilihisi dunia imejirudia. Nilitaka kusimama na kukimbia. Lakini uso wa Damian haukuwa na kejeli. Hakukuwa na uovu. Kulikuwa na huruma.
“Sikiliza,” alisema kwa utulivu, “najua nimekuja kwa ghafla. Lakini nataka tu kukusikia. Sio kuzungumza sana. Niliona barua yako kwenye meza ya dining ile siku uliyokimbia. Nilienda nyumani kwa bahati tu”
Nilinyamaza.
“Nimekutafuta sio kwa ubaya,” aliendelea. “Sikujua kwanini uliondoka mpaka nilipo ona picha zenu… jinsi mlivyokuwa na furaha pamoja. Lakini macho yako kwenye picha ya mwisho—yalikuwa yamekufa.”
Nilishindwa kujizuia. Machozi yalianza kunilenga tena. Damian alinyamaza, akavua saa yake, akaishika mkononi kana kwamba anaondoa muda.
“Naomba… angalau nikuonyeshe sehemu yenye amani zaidi ya Bagamoyo.”
Jioni hiyo, alinipeleka pwani ya kimya, mbali na wageni. Aliandaa blanketi, kisha akatoa red wine na glasi mbili.
“Najua maisha yamekuumiza, Talia,” alisema kwa sauti ya upole. “Lakini unajua? Kuna wanaume wanaojua jinsi ya kushika moyo wa mwanamke bila kuutuliza kwa maneno tu, bali kwa matendo.”
Alinigeukia.
Na kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu… nilihisi salama.
“Damian…”
“Hm?”
“Usinifanye nikuamini kisha uniumize tena.”
Akasogea, akashika kidevu changu, taratibu. “Sitobomoa. Nitajenga. Ila kama kuna kitu nitataka kubomoa… ni ukuta uliojijengea kuzuia kupendwa tena.”
Akanibusu.
Ilikuwa tofauti.
Busu la mwanamume, si mvulana.
Laini, joto, na lenye uvumilivu wa mtu aliyesubiri muda mrefu. Mikono yake ilikuwa ya heshima, lakini ya kuwasha kwa hisia. Tulilala kwenye blanketi tukitazama nyota juu, vichwa vyetu vikigusana, mikono ikifunga mikono.
Sikujua kama ni mwanzo wa penzi jipya, au utulivu wa muda mfupi… lakini kwa mara ya kwanza, sikumkumbuka Eli.
Lakini maisha yana mchezo wake.
Kesho yake, nikiwa kwenye balcony ya gesti yangu… niliona gari jeupe likipaki mbele.
Kisha mlango ukafunguliwa.
Na Eli alishuka.
🖋️ Je, Eli amekuja kusema nini? Damian atasimama kama mwanaume mpya? Talia amekua na anastahili kuchagua – lakini atamchagua nani?

Itaendelea........


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote