Follow Channel

TAMIKA (Dereva wangu )

book cover og

Utangulizi

TAMIKA (Dereva wangu )

Nimeamini ule msemo wa chuki uzaa upendo wa dhati, upendo ambao bond yake sio rahisi kuvunjika.

Call me Ezra, Kijana wa kitajiri, Kijana ambaye shida siijui, Kijana ambaye napatiwa kila kitu na wazazi wangu na sikuwa nafosiwa kufanya kazi licha ya Kuwa msomi mzuri sana.

Ezra Mimi niliangukia kwenye penzi la Binti Paula, Binti ambaye nilijua sana kumpenda na yeye aliniheshimu sana, nilimpatia Paula kila alichokitaka, lakini Mimi na Paula hatukuweza kufika mbali baada ya Mimi kukutana na Dereva wangu.

JE DEREVA WANGU ANA MAAJABU GANİ TILILIKA NAYO.

TAMIKA (Dereva wangu )
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 01

www.tupohapa.com

ANZA NAYO…….

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

Ni Majila ya jioni, Ndani ya Jumba zuri la kifahari, jumba lenye hadhi ya juu kabisa, Yaani kWa kuangalia tu unajua mmiliki wa hii sehemu ni mtu mzito maana yoooh.

Ndani ya Nyumba hiyo sebuleni, anaonekana Kijana mmoja mtanashati, Mwenye mwili wa mazoezi, Mwenye weusi mzuri kabisa wa king’aa wengine usema rangi ya chocolate si mnajua wenyewe Bwana.

Kwenye sebule hiyo hiyo, anaonekana mubaba mtu mzima akizunguka uku na uku, na mwana mama mtu mzima pia akiwa amekaa pembeni na akionekana Kuwa na hasira sana, na kWa sauti ya ukali mwanamama huyo anazungumza.

“Haya ndio madhara niliyokuwa nikikuambia baba Ezra, huyu Kijana Unamlemaza sasa, Yaani mpaka umri huu unamfanyia kila kitu, mpaka umri huu Ana ata future kwaajili yake, haya sasa Angalia na haya majanga anayoyaleta”

Kijana huyo anamgeukia mwana mama huyo na kumuuliza.

“Future gani unaongelea mama ? I have my dad’s money, kwani ni kitu gani kingine natakiwa kufanya ? “

“Lione kwanza bichwa lake, Yaani unazungumza kama kichwani hakuna kitu hivi, Yaani umri huo mpaka Saa hizi Huna plan ya mke Wala nini, kazi utaki sasa ulisoma kwaajili ya nini, umri huo ata kujiendesha ujui Unakazi ya kubadilisha watu wa kukuendesha tu , nakuambiaje, huyu uliyemfukuza Leo ndo Dereva wa mwisho utaanza kujiendesha Mwenyewe, Sijui utajifunza wapi lakini utaendesha Mwenyewe hakuna Pesa za kuajili Dereva Mpya kila hiitwapo Leo “

Kijana huyo kWa hasira anakasilika na kuondoka mbali kabisa na eneo ilo.

“Umeona sasa Mtoto amechukia?”

Alizungumza mwanaume Yule ambaye ni baba wa huyo Ezra.

“Mtoto gani kwnza unaongelea? Yaani Ezra Anautoto gani jitu linakaribia miaka 31, mwanzo nilikuachia majukumu yote juu ya Ezra lakini sasa inatosha Mimi Kama mama yake nitasimamia kila
Kitu, lazima anyooke kama kaka yake”

Alimaliza mama Yule kisha akaondoka na kumuacha mumewe akimshangaa tu.

SONGA NAYO SASA ………

Niite Ezra , last born wa familia moja ya kiTajiri sana hapa jijini Arusha, Ezra Mimi ni msomi mzuri sana aswa kwenye mambo ya ICT.

Nyumbani kwetu tuna magari ya kutosha lakini Ezra Mimi Sijui ata kukanyaga gia, na hii yote ameyataka baba yangu ambaye hakuwai kunipa nafasi ya kujifunza zaidi amekuwa akiwalipa watu kwaajili ya kuniendesha na kunipeleka kokote ninakotaka.

Baba yangu amenifanya nione Kuwa maisha ni mepesi sana aswaah ukiwa na hela, ata hivyo Baba amefanya hivyo ata kWa kaka yangu lakini kaka yangu ni tofauti na Mimi hivyo aliweza kuchagua maisha yake Ila
Mimi sasa ndio Nipo na baba bega kWa bega.

Ilo unaloona hapo juu ni valangati kati yangu, mama lakini pia na baba, na valangati ili limekuja baada ya mimi kumfukuza kazi Dereva wangu, na nilimfukuza kWa Kuwa tu alikataa kunipeleka sehemu ambayo Mimi nilitaka, ingawa yeye hakuwa Sawa Kiafya.

Nikiwa chumbani kwangu nimekasilika baada ya mama kunifokea, baba yangu akaja chumbani na kunituliza Na Kuaidi kuzungumza na mama ili niweze kupata Dereva mwingine.

Kitu kingine Kuhusu Mimi Bwana, sio mtafutaji Pesa lakini ni mtumiaji mzuri sana 😂🙌 Yaani mimi ni kila siku bata na totozi lakini pia washkaji zangu wa hapa na pale,
Mimi marafiki zangu wote wananiita Tajiri yote kwaajili ya Kuwa spoil kinomanoma.

Week nzima ilipita nikiwa siijapata Dereva wa kuniendesha uku na uku Walahi nilikuwa na hasira sana lakini ndio nitafanyaje usukani kashika mama muda huo ata baba hana kauli.

*********

Ikiwa ni siku ya weekend Yaani ijumaa Majila ya jioni, nilijianda zangu kwajili ya kutoka kwenda kula bata na nililazimika kuita huba maana sina ubavu wa kujiendesha Mwenyewe.

Nilitoka chumbani kwangu chap baada ya Dereva wa huba kuniambia Kuwa ameshafika, Ile nafika tu chumbani, ikakutana na msichana ambaye alivalia Gauni yake kubwa, kWa wa mama wa uswazi uwa wanaita gubeli.

“And who are ??”

Nilimuuliza kWa ukali sana, kwani alikuwa amekaa kwenye kochi langu peke yangu, Yaani hapa sebuleni Nina kochi langu tu ambalo sijawai kuruhusu mtu mwingine kukaa hivyo huyu mgeni ni Kama alijichajichanganya hivi.

“Habari yako “

Mgeni huyo alinisalimia.

“Kabla sijaitikia salama yako
Nyanyuka hapo ulipokaa”


Mdada wa watu Wala hakuwa na
Hiyana, kWa haraka akataka kunayanyuka lakini muda
Huo huo ikasikika sauti ya mama
Yangu.

“Tamika Kaa chini “

Haraka nikamgeukia mama yangu na kumwambia.

“This is my coach mama “

“This is my coach mama, ujawai kujinunulia ata socks ndio uweze kununua kochi, kwanza Kaa chini “

“Me natoka mama “

“Ezra nimesema Kaa chini”

Aaah nisiwe Muongo Mimi mama yangu namuogopa sana sana, mama yetu ni makali sana na ajawai kuunga mkono ujinga wowote ule na kauli yake ni amri sio ombi.

Muda huo huo Dereva wa huba akanipigia simu kwani nilikuwa nilimchelewesha, nilichofanya ni ku cancel kisha nikamtumia Pesa yake kwenye simu.

Baada ya hapo nikatulia na kumsikiliza mama yangu ni kitu gani anataka kuzungumza.

“Huyu ni Tamika lakini pia ni dereva wako Mpya, na sio dereva tu ni mwalimu wako wa kukufundisha kuendesha Kuanzia sasa”

“Mama are you serious? Yaani mimi niendeshwe na mwanamke ? Si kila siku nitakuwa hospital Mimi jamani ??”

Mama akaniangalia kwa muda kisha akaniuliza.

“Mimi naendeshwa na Naani ??”

Hapo kwakweli niliona haya na kuangalia chini maana mama yangu amekuwa akijiendesha Mwenyewe miaka kenda na kurudi.

Mama akamgeukia Tamika
Na kumwambia.

“Tamika, mwanafunzi wako huyo, all the best, kwa sasa Mimi natoka.”

“Siku njema madam “

Alijibu msichana huyo kWa sauti moja nzito Sana, sauti ambayo ata Mimi Sina 😂🙌, sasa Sijui huyu Tamika ndio ladies and gentlemen au laaah 😂.

Baada ya mam kuondoka nikazungumza.

“Kuna sehemu nataka Kuwai nipeleke sasa hivi “

Ila mimi jamani uwiiih napenda Sana kutuma.

“NAKUJA “

Alizungumza Tamika kisha akaendelekea kwenye chumba cha wageni ni wazi Kuwa mama alishamkabizi chumba chake.

Baada ya muda Tamika akarudi akiwa amevalia mavazi ya kızamadı sana, Yaani zile suti za mahaba wa miaka 47 uko 😂.

“Unataka kuongozana na Mimi Ukiwa kwenye mavazi hayo ??”

Nilimuuliza.

“Nafikili safari yako ni muhimu kuliko ilo swali ililoniuliza, can we go now ??”

Hapo kwanza nikashtuka na kutabasamu na kumuuliza.

“Küme unajua na kingereza ?”

Tamika Wala akunijibu zaidi akatoka nje na kwenda kupands kwenye gari yangu na kubaki akinisubilia.

Eeeh Yaani huyu Tamika ni Ana muda mchache hapa Nyumbani lakini ni tayali Ana ratiba na anajua. Kila kitu.

Baada ya muda safari kati yangu na Tamika ikaanza na tukiwa kwenye gari nikamuuliza.

“Hivi ni huu muonekano wako mbaya ndio umekufanya uwe dereva au ? 😂🙌 maana ufai ata Kuwa mama wa Nyumbani”

Tamika Wala akajibu kitu zaidi akasogea mbele na kuangalia sehemu nzuri kisha akageuza gari na kuanza kurudi tulipotoka.

“Uku wapi mwehu ?!”

Nilimuuliza nikiwa nimeshapaniki.

Tamika hakujibu kitu zaidi anaongelea mwendo na baada ya muda tukajukuta tukiwa Nyumbani.

“Wewe ni Chizi au ? Nimekuambia nataka kutoka”

Tamika akaniangalia na kujibu.

“Una Lisaa limoja la kupumzika, baada ya hapo tunaingia uwanjani kwaajili ya mazoezi”

Alijibu Tamika na kuondoka Ndani uku akiniacha nikimshangaa tu.

HUYU TAMIKA NITAKUJA KUMKATA MIGUU.


TAMIKA (Dereva wangu )
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 02

www.tupohapa.com

ANZA NAYO…….

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

Kiukweli nilichukia sana na kuona Kuwa huyu msichana ni ananiletea dharau ya hali ya juu, Yaani Nimekuwa nikiendeshwa na wanaume wa kila aina lakini awajawai kuniletea dharau Kama hii halafu yeye ndio aniletee shida Kama hii huyu mjinga kweli.

KWa mwendo wa haraka nikaingia Ndani na kumkuta Tamika akiwa amekaa kwenye kochi langu, Yaani kochi lile lile ninalolipenda, Yaani kochi ambalo hakuna mtu mwingine Anatumia zaidi yangu.

“Binti kwanza jiinue kwenye hiyo sehemu umekaa, kisha nipeleke ninapotaka kwenda”

Tamika akaniangalia kisha akaangalia Saa yake aliyokuwa amevaa mkononi na kuniambia.

“Zimeshapungua dakika 6 sasa “

Nilijikuta nikichukia zaidi na kumsogelea Karibu na kunyoosha mkono wangu nikitaka kumpigia kibao, woiiiiiih huyu Tamika ni ladies and gentleman me nawaambia, maana sio kwa kunidaka uku, Tamika alidaka mkono wangu na muda huo huo akanigeuza na kuanza kufinya mkono wangu.

“Yalaaaaaaaah”

Nilipiga Kelele kutokana na maumivu makali ambayo Nilitapata kutokana na kifinyo kutoka kwa Tamika.

“Unaniumiza Bwana “

Nilifoka uku nikijitaidi kujitoa mikononi mwake.

Tamika aliniachia kWa kunisukuma na kunifanya nianguke chini kama mzito uku Komwe langu likitangulia chini.

“Uziinizoee”

Alizungumza Tamika kisha akaondoka chumbani kwake.

Katika maisha yangu sijawai kukutana na mwanamke Mwenye nguvu kama huyu, Yaani Tamika uwiiiih alijua kuninyoosha na kuniacha nikijisonya sonya uku akiwa ameshanijengea kauoga Fulani hivi.

Majila ya Saa 1 usiku, Tamika akaja chumbani kwnagu na kunigongea na kwa sauti yake ya ubabe akaniambia.

“Jiandae chap ni muda wa mazoezi “

Nilikaa kimya kWa Muda kisha nikajibu.

“Nimelala “

Tamika akaniuliza.

“Nije kukusaidia kukubembeleza ili ulale vizuri ??”

Eeeh hapo kwanza nikashtuka maana yoooh 😂🙌 sebuleni tu kaninyoosha pasi na kujali Kuwa anaweza akakutwa, uku chumbani si ndio anaweza akanivunja Shingo huyu, kuna muda nashindwa kuamini Kuwa Tamika ni mwanamke kabisa.

“NAKUJA “

Nilijibu kwa sauti ya kisilani uku Nilijvuta pale kitandani Kama Jongoo aliyetolewa miguu.


Baada ya muda nikatoka nje nikiwa nimeshajiandaa kila kitu, na nilijiandaa kutokana na maelezo ambayo nilipatiwa na Tamika.

Baada ya muda Mimi na Tamika tukawasili kwenye Kiwanja kikubwa sana, ambacho kilikuwa ni maalumu kwaajili ya wanaojifunza kuendesha magari.

KWa Mara ya kwanza katika
Maisha yangu nikaanza kufanya kitu pasi na kuambiwa Mara Mbili Mbili, Yaani Tamika alikuwa akiniambia lala chini nalala muda huo huo 😂🙌.

So far so good, Tamika pia ni mwalimu mzuri sana na anaonesha wazi Kuwa anapeenda kile alichokuwa akikifanya, Yaani alikuwa akinifundisha kwa moyo wake wote, na kWa siku huyo niliweza kuokota mambo mawili
Matatu.

“Aaaaah nimechoka sana “

Nilizungumza baada ya kumaliza mazoezi na muda huo nilikuwa nimekaa chini nimenyoosha miguu utazani ni mama mjamzito.

“Kwakuwa ni siku ya kwanza lakini utazoea tu na utapenda kufanya zaidi na zaidi “
Alizungumza Tamika.

Nikamuangalia kwa muda na kumuuliza.

“Kwahiyo wewe ni mwalimu wa waendesha magari au ??”

Tamika akatabasamu na kujibu.

“Mwalimu wa kila kitu”

“Ukiwa Unamaanisha nini ?”

“Wewe elewa Kuwa ni mwalimu wa kila kitu, Ezra inakupasa kuanza Kuwa serious kwenye kila unachokifanya kwa sasa “

Hapo nikaona huyu dada anaanza kuniingilia kwenye mambo yangu, nilichofanya ni kumuomba Twende Nyumbani.

*******

Siku ziliendelea kwenda uku nikiendelea kujifunza kuendesha gari lakini bado Tamika aliniendesha na kunipeleka kila sehemu ambayo nilikuwa nikienda.

Kitu ambacho Tamika alikuwa akinikela ni haya mavazi yake, Yaani mtu tayali ni shapeless 😂 ukichanganya na mavazi yake Basi weeeh anakuwa kama katuni Wala
Ana aiba ya kike huyu msichana.

Ikiwa ni siku ya weekend, siku hiyo Bwana ilikuwa ni siku ya Mimi kukutana na Demu wangu, Yaani siku hii nilikuwa nakula Mzigo wa babe wangu na nilimuomba aje Nyumbani kabisa.

Demu wangu Bwana ni msichana Fulani hivi Ananiheshimu na kunipenda sana hivyo Mara nyingi uwa anafanya vile ambavyo Mimi nataka na ajawai kuniangusha kwakweli.

Mida mida hivi, mpenzi wangu alifika Nyumbani na kumkuta Tamika akiwa Sebuleni kWa heshima akamsalimia.

“Shikamoo babu “

Woiiiiiih nilishindwa kujizuia kucheka nilijikuta nikicheka sana, Yaani Tamika anajiweka hovyo mpaka mtu anajua Kuwa yeye ni mwanaume Tena Yule ambaye umri umeenda sana.

Basi siku hiyo nilijilia vyangu pasi na wasiwasi na Tamika akuleta shida na zaidi akanipatia na Mapumziko kwa siku hiyo hivyo Atukwenda mazoezini.

Siku ziliendelea kusonga na nilianza kumuelewa Tamika kWa kiasi chake, Tamika alikuwa ni muongeaji sana na maongezi yake na ushauri Yaani ni moja kwa moja unajua huyu Ametoka kwenye familia yenye shida sana yaan Pesa Wanatafuta kWa shida sana.

Tamika alihakikisha Kuwa nafanya mazoezi zaidi na kujua kuendesha gari, na kweli baada ya miezi mwili nikawa vizuri kabisa ata Barabarani naingia vizuri kabisa.

KWa msaada wa baba yangu na mama yangu nimafanikiwa kupata leseni mapema sana lakini pia baba yangu akaninunulia gari jipya Jambo ambalo lilimchukiza sana mama yangu.

Majila ya saa 2 usiku nikiwa na familia yangu kwenye meza ya chakula, lakini pia Tamika alikuwa hapo maana ni Mwana familia pia ingawa alikuja kwaajili ya kazi.

Tukiwa tunaendelea kupata chakula, mama akazungumza.

“Leo ni siku ya mwisho ya Tamika Kuwa na sisi hapa “

Nyieeeeh Sijui ni nini lakini nilijikuta nikipaliwa na chakula kwa mshtuko wa hali ya juu.

Haraka Tamika aka…….

NAKUJA MY ZANGU.


TAMIKA (Dereva wangu )
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 03

www.tupohapa.com

ANZA NAYO…….

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

KWa mshtuko wa hali ya juu nikauliza.

“Siku ya mwisho ? Kwamba anaondoka au ??”

Mama na baba yangu walinigeukia na kuniangalia uku wakiwa Kama wamepigwa na butwaa hivi, kWa sauti ya utulivu mama akajibu.

“Anaenda kuendelea na Mishe zake nyingine kwani ameshamaliza majukumu yake ya hapa “

KWa haraka nikauliza.

“Amemeliza kivipi Yaani ??”

“Ezra Una shida gani kwani ? Wewe ujui majukumu ya Tamika kwenye hii Nyumba au! Wacha nikupe shavu mwanangu, tamika alikuwa hapa kukusaidia wewe ili uwe dereva mzuri sana na Mungu ametenda na umekuwa dereva mzuri sana, umekuwa ni zaidi ya dereva mwanangu na leseni yako umeshatoka kWa sasa unaweza kujiendesha Mwenyewe, unauwezo wa kuingia kila barabara mwanangu “

“Lakini ma……”

“Ezra unataka kuzungumza nini ? Usiniambie Kuwa bado unataka kuendeshwa baada ya kila kitu “

“Ndio mama sitaki kuendesha Mwenyewe”

“Hatuna Pesa ya kumlipa KWa sasa “

Kwa haraka nikalopoka.

“Nitakuwa nikimlipa Mwenyewe mama”

Hapo baba yangu alijikuta akipaliwa halafu mama yangu akaangua kicheko.

“Sasa Mnacheka nini ?”

Niliwauliza uku nikiwa najisikia vibaya sana, Yaani nilikuwa natamani ata kulia kwakweli.

“Unamlipa na Pesa gani ??”

Mama aliniuliza.

Uku machozi yakiwa yananilenga Lenga nikazungumza.

“Nitaatafuta kazi, nitafanya kazi naadi nitapambana na nitamlipa Tamika “

Ila Mimi jamani sina ata Mia 😂 ambayo nimewai kutafuta Mwenyewe halafu muda huu Naongelea kumlipa mtu laki 4 kwa mwezi 😂🙌 eeeeeh mambo
Ya pempeee na sasampa yanaenda kuniendesha.

Kwakuwa Nilizungumza vizuri na wazazi wangu wote wakakubali na ata Tamika pia alikubali kubaki.

Mnajua nini my zangu, Sawa Nina uwezo wa kuendesha gari kWa sasa, lakini huyu msichana nataka kumuonesha Kuwa Mwenye Pesa Sio mwenzio, Yaani huyu msichana kipindi ambacho alikuwa analipwa na familia yangu alikuwa ananiendesha sana so kipindi hiki nataka nimuoneshe mimi ni Nani.

********

Siku iliyofuata nilianza kuingia Chaka tu Chaka nikitafuta kazi, sio kwamba nilishindwa kufanya kazi kwenye kampuni ya familia, lakini nilitaka kufanya kazi sehemu nyingine na niwaoneshe wazazi wangu Kuwa naweza pasi na usaidizi wao.

Mungu Mwema sana kwakweli, Ndani ya week Mbili tu niliweza kupata Kazi, Tena kazi nzuri kabisa, kazi ambayo mshahara ni umechangamka, kazi ambayo Pesa yake ninaweza kumlipa Tamika lakini pia kuendesha maisha yangu.

Ikiwa ni Majila ya asubuhi sana, niliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kazini na hiyo ikiwa ni siku yangu ya kwanza.

Baada ya kujiandaa na kila kitu, nikatoka nje kwaajili ya kuondoka.

“Kwahiyo unatarajia utanipeleka kazini na hii gari chafu au ??”

Nilimuuliza Tamika.

“Aaaaah”

Kabla ajamaliza kujibu nikazungumza.

“Una dakika 15 tu hii gari iwe safi”

“Ezra, hii gari unatakiwa ikafanyiwe service Leo ndio maana sijaosha, ikishafanyiwa service tu naosha boss wangu”

“Uwezi kunipeleka kazini siku ya kwanza na gari chafu, safisha haraka na hakikisha Kuwa Nafika ofisini on time “

Tamika wa watu aliganda akiniangalia tu uku akiwa aamini kile anachokiona.

Baada ya muda kila kitu kikawa Sawa Yaani gari ilikuwa tayali na safari ya kwenda kazini Ikaanza..

Eeeeh nilisahau kuwaambia Bwana Mimi ni handsome Bwana, Yaani Nina muonekano ule wa kuombwa mbegu kabisa😂🙌.

Niliingia ofisini utazani mimi ndio boss jamani maana uko kWa kutunisha kifua jamani 😂😂 Yaani Natembea utazani ndio mwekezaji mkubwa wa kampuni.

KWa upande wa dada sasa jamani, walikuwa wakiniangalia sana na wengi walionekana kuvutiwa na Mimi na hiyo ndio ilikuwa furaha yangu, kiufupi mimi napenda kuonekana jamani.

Baada ya muda board nzima ya ofisini ikakutana kwenye chumba cha mkutano na niliweza kutambulishwa.

Baada ya muda kila mtu akarudi kwenye ofisini yake, nikiwa ofisini kwangu naendelea na majukumu yangu, akaingia msichana Fulani hivi ambaye nilitambulishwa Kuwa ni Mshirika mwenzangu na ndio nitakuwa nikisaidiana nae kwenye majukumu yangu.

“Ezra si tunaweza kuanza sasa au ??”

Msichana huyo aliniuliza.

“Ooooh yaaah, hakuna shida kabisa”

KWa utulivu wa hali ya juu akakaa kwenye kiti kilichokuwepo mbele ya meza yangu.

“Ooooh samahani unaitwa Nani vile ?”

Nilimuuliza Msichana huyo maana nilisahau kabisa Jina lake.

“Ooooh naitwa zuwena, Ila niitee Zuuh”

“Sawa “

Basi Mimi na Zuuh tukafanya majukumu yetu na niseme Kuwa. Zuuh ni Binti Mwenye akili sana na anajua majukumu yake, lakini pia anajua nini Anafanya kwenye kazi yake Kiukweli si kupata shida.

Aaaah finally muda wa kwenda Nyumbani ulifika jamani maana yooh nilichoka Kama mbwa mlinzi hivi 🥹 haya mambo ya kazi sijazoea kabisa.

Ile natoka tu nje na Tamika nae akawa Amefika yaani Tamika amefika on time kabisa.

“Aaaaaah nimechoka sana “

Nilizungumza baada ya upanda kwenye gari.

“Pole sana boss “

Alizungumza Tamika uku akijiandaa kuondoa gari.

“Subili kwanza “

Nilimwambia Tamika, kisha nikatoa kichwa changu nje na kuzungumza..

“Zuwena ongozana na Mimi “

Aaah my zangu zuwena nikishangaa ni sehemu gani anaka hivyo ilikuwa rahisi sana kwa mimi kumpa lifti kwani mtaa anaokaa mimi ndio napita.

“Ooooh Ezra Asante sana lakini kWa Sasa Kuna mahali naenda Mara moja”

“Hata zuwena bye”

Mimi na Tamika tukaanza safari ya kwenda Nyumbani sasa, tukiwa njiani nikazungumza.

“Umeona wanawake wenzio anavyovaa ? Tamika badilika na uanze kuvaa Kama wenzio labda unaweza ukawa na muonekano wa kike “

Tamika Wala hakunijibu kitu zaidi aka focus na usukani wake kuelekea Nyumbani.

“Oooooh nilisahau Bwana Ageuza gari kuna sehemu nataka kwenda Mara moja “

Nilimwambia Tamika muda huo alikuwa akijiandaa kuingia za gari Ndani kwani tulishafika Nyumbani, Tamika akaniangalia kisha akaniuliza.

“Nakupeleka wapi ??”

“KWa dizo masuit pale Jina suit zangu nazitaka “

Nilijibu na Tamika akufanya ajizi akageuza gari na safari ya kwenda kwa dizo ma suit yakaanza, Kabala hatujafika mbali nikazungumza.

“Au Basi turudi tu Ndani “

Kiukweli sikuwa na kitu chochote kila zaidi ya kutaka kumkomoa Tamika wa watu mwaya. 🥹

KWa hasira Tamika akashuka kwenye gari na pasi na kuzungumza kitu akaanza kuondoka, nika…….

ITAENDELEA.


TAMIKA (Dereva wangu )
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 04

www.tupohapa.com

ANZA NAYO…….

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

KWa upande wa Tamika akarudi zake Nyumbani akiwa amechukia sana Tena sana, lakini pia kWa upande wangu pia nilichukia mno baada ya Tamika kuniacha barabarani Mwenyewe, kWa haraka nikasogelea usukani na kuendesha Mwenyewe kwaajili ya kurejea Nyumbani.

Nilifika na moja kwa moja nikaenda chumbani kWa Tamika ambapo nilimkuta akipanga nguo zake kwenye begi ni wazi Kuwa alikuwa anataka kuondoka.

“Hivi Tamika unashida gani wewe eeeh, Yaani ulipata wapi nguvu ya kuondoka na kuniacha Mimi pale ??”

Nilimuuliza pale tu nilipoingia chumbani kwake.

Kama kawaida, Tamika sio mtu wa. Kujibizana na mtu alichofanya ni kuniangalia tu kisha akaendelea na kazi yake ya kuweka nguo zake kwenye begi.

“Nazungumza na wewe Tamika “

Hapo Tamika akanigeukia na kuzuungumza.

“Kama hautabadilika kwenye maisha yako Basi mafanikio yako
Yata Kuwa ya shida sana Ezra, Sijui kichwani kwako kuna shida gani lakini chochote kile ulichokuwa nacho kitakukosti, kitu ambacho naweza kukushauri ni kwamba Jaribu kuishi na watu vizuri hii itakusaidia sana Tena sana”

Baada ya hapo Tamika akashika begi lake na kuanza kuondoka kWa jazba nikauliza.

“Unaenda wapi sasa ??”

Tamika akaniangalia kisha akajibu.

“Ooooh nimeacha kazi Ezra, kila la kheri na mfanyakazi wako Mpya “

“Unaondokaje Kama hivyo ata mama ujamuga ? Lakini pia sijakulipa “


“ usijali kuhusu vyote hivyo “

Alijibu Tamika kisha akaondoka zake.

Kiukweli hiki kitendo cha Tamika kutaka kuondoka kilinipiga za usoni kabisa, kwanza sikuwa nimetalajia Kuwa anaweza akachukua maamuzii magumu Kama haya, lakini baada ya yote na visa vyote hivi Walahi Tamika nilikuwa nimemzoea sana 🥹.

Kwa upande wa Tamika akugeuka ata nyuma jamani, moja kWa moja akaondoka.

KWa unyonge wa hali ya juu nikarudi zangu chumbani kwangu.

“Ata hivyo Atarudi tu kuomba kazi maana Nina Uhakika Ana shida sana na kazi”

Nilizungumza kimoyomoyo uku nikijitaidi kujipa moyo na kutaka kuamini Kuwa Tamika lazima arudi Tena pale Nyumbani.

Majila ya usiku nilishindwa kabisa kulala jamani 🥹 Yaani Sijui ilikuwaje lakini Nilitumia usiku mzima kuwaza Tamika, yaaah Nimekuwa nikimsema
Sana, Nimekuwa nikimfanyia visa lakini saaah she’s the best, Tamika anajua jinsi gani ya kuzungumza Na mtu, Tamika Ana utu na utulivu, Tamika ni mwanamke ambaye Ana sifa zote za kike isipokuwa muonekano tu na mavazi yake, Yaani Kama Tamika umjui siku ukikutana nae na jinsi anavyojiweka unaweza kusema Kuwa ni mwanaume Tena ambaye umri umesogea.

*******

Siku iliyofuata Walahi nilichelewa kwenda kazini maana sikuwa Sawa kabisa, Yaani muda wote nilijikuta nikimfikilia tamika.

Nikiwa ofisini kwangu, nilichukua simu yangu na kujikuta nikimpigia Tamika pasi ma kutalajia.

“Hellow “

Nilizungumza baada ya Tamika kupokea simu yangu.

“Unataka nini Ezra ??”

Tamika aliniuliza,

Ukweli ni kwamba nilimpigia simu kwaajili ya Kumuomba msamaha lakini kwakuwa mimi sitakagi kuonekana mmyonge nikajikuta nikizungumza kWa dharau.

“Nimekupigia nikupatie last chance ya kurudi kazini Tamika”

KWa haraka Tamika akanijibu.

“Asante lakini siitaji kazi kwa sasa “

Aaah Walahi nilikasilika sana, kWa sauti ya ukalai nikazungumza.

“Tamika utakuja kujutia me na……”

Kabla sijamaliza Tamika akanikatisha na kuniambia.

“Mwanzo mwisho Leo kunipigia simu Sawa, fanya maisha yako Broh “

Akazungumza Tamika kisha akakata simu, uwiiiih hapa ndio alinichanganya kabisa huyu mwanamke, sikuwai kufikilia kuwa atakuwa mgumu kiasi hiki.

Majila ya jioni mama yangu akiwa jikoni Anamuandalia baba chakula, kWa utulivu nikamfata na kuanza kuzungumza nae.

“Mama Naomba unisaidie kuniombea msamaha kwa Tamika nimemkosea sana “

Kwanza mama alinishangaa sana maana huu utulivu niliouonesha sio wangu kabisa, Yaani sijawai Kuwa na utulivu wa Namna hii, na hii ya kutaka kuomba msamaha ndio kabisa ilimshangaza mama yangu.

Kwa utulivu mama akanigeukia na kuanza kunipima joto langu la mwili kupitia mikono yake..

“Uko Sawa ?”

Mama aliniuliza.

“Yaaah niko Sawa, lakini sio sana mama mpaka pale Tamika atakaponisamehe Mimi “

“Mmmmh Ezra Tangu lini wewe ukaitaji msamaha kwa mtu mwanangu ? Na Kama kweli unaitaji msamaha wa dhati kabisa Basi itakupasa kumuomba msamaha kila mtu, Namaanisha madereva wote ambao wamewai kukuendesha”

“Lakini ma….”

“Hakuna cha lakini mama, Ezra mwanangu maisha ayaendi hivyo Kijana wangu, Nimekuwa nikikuelezea kila siku lakini ukuwai kunielewa kabisa”

“Unaweza kuzuungumza na Tamika mama ??”

Hapo Nilimuuliza mama yangu kWa kumaanisha kabisa, Kiukweli Nimekuwa nikiwakosea watu sana Tena sana lakini huyu Tamika ameniweza kabisa Yaani naona Kama nimefanya dhambi kubwa sana.

“Sawa nitazungumza nae “

Alizungumza mama na hapo nikajisikia afueni.

********

Baada ya siku Tatu kupita, ikiwa ni weekend na ni Majila ya jioni nikiwa nimekaa sebuleni, muda huo huo akaingia Tamika akiwa na mama yangu, woiiiiiih nilijikuta nikifurahi sana na kuna Namna niliona ni Kama naashindwa kuficha furaha yangu hivi, kwa haraka nikamkaribisha.

“Karibu sana Tamika “

“Asante “

Alijibu Tamika akiwa na tabasamu pana sana.

“Ezra peleka mabegi ya Tamika chumbani kwake “

Alizungumza mama na muda huo huo nikafanya hivyo Wala awakiwa na haja ya kuniambia Mara Mbili Mbili.

Nikiwa chumbani kWa Tamika Namuwekea mabegi yake,
Muda huo huo Tamika akaingia na kuniuliza.

“Huu msamaha wako Unamaanisha au ??”

Nikaacha nilichukuwa nafanya na kumgeukia Tamika kisha nikamjibu.

“Chochote ulichosikia kutoka kwangu Basi jua kuwa Namaanisha Tamika, nimeishi na watu mbali mbali lakini wewe kuna kitu special kipo Ndani yako Tamika, am sorry “

Ila nyieeeh huu utulivu Mimi nimeutolea wapi jamani sio kawaida yangu kabisa. 🥹

“Sawa “

Alijibu Tamika kWa kiufupi kabisa, nilimuangalia kWa muda na kumuuliza.

“Nikusaidie kupanga nguo zako kwenye kabati ??”

Tamika akatabasamu na kujibu.

“Utakuwa umenisaidia sana”

Basi nikaanza zangu kumsaidia kuweka nguo zake kwenye kabati, wakati huo Tamika akaingia zake bafuni na baada ya muda nikasikia saauti ya maji yakimiminika ni wazi Kuwa alienda kuoga.

Baada ya muda Tamika akatoka nje akiwa amevalia taulo fupi nyeupe, lakini pia na kichwani mwake alikuwa na nywele Ndefu sana ambazo sikuwai kuziona lakini pia sikuwai kufikilia Kuwa Tamika ndio Ananywele kiasi iko maana Mara nyingi Nimekuwa nikimuona na kofia ambayo ilikuwa ni kuu kuu.

Achana na nywele sasa jamani, njoo uku, uku kwenye vya Kurithi halafu vinazidi, weeeeh Simjui mama Tamika lakini Tamika Amerithi kwa mama yake 😁 hiii sio nyashi jamani, Sijui Tamika alikuwa Anavaa vitu gani kwaajili ya kuficha lakini weeeh ili alilikuwa nalo Tamika ni zigo.

Nikajikuta niki…..::

NAKUJA MY ZANGU TAMIKA KANICHANGANYA.


TAMIKA (Dereva wangu )
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 05

www.tupohapa.com

ANZA NAYO…….

🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺🌺

Nikajikuta nikilopoka.

“Ilo lote lako ??”

Uwiiiiih mimi jamani 😂 si ndio kwanza nimetoka kuomba msamaha Saa hizi naanza kuonesha mambo mengine.

Tamika akaniangalia kiasha akaniuliza.

“Uko Sawa ??”

“Ndio “

Nilijibu haraka haraka uku nikiendelea kupanga nguo zake kwenye kabati, nisiwe muongo kwakweli Tamika alijua kuniachanganya na hii shape yake, Yaani woiiiih sikuwai kutalajia Kuwa ndio ana Mzigo mkubwa Kama huu, lakini pia Nilimchukulia powa sana lakini Tamika ni bonge la pisi Yaani pisi ya kwenda sio kitoto.

Tamika akaachukua mavazi yake na kwenda bafuni kwaajili ya kuvaa kwani Mimi nilikuwa pale.

Baada ya muda Tamika akatoka akiwa amevalia dela kWa Mara ya kwanza tangu namuona Tamika Leo ndio amevaa vizuri na kujiweka vizuri kwani siku zote uwa anajiweka OVYO sana, lakini pia kichwani alibana nywele yake vizuri kabisa.

“Umependeza “

Nilijikuta nikimsifia.

Tamika akacheka na kusema.

“Aaaah we nawe, na ili dela au ??”

“Yaaah si unajua ndio mavazi ya stara kwa sasa “

“Sawa, Ezra unaweza kwenda kuendelea na kazi zako nitaanza ulipoishia”


“Sa Mbona Kama unanifukuza hivi”

Nilizungumza kimoyomoyo uku nikimuangalia usoni mwake ni kaama nilikuwa nataka huruma yake hivi.

Muda huo huo sauti ya mama ikasikika ikiniita kutokea sebuleni, haraka nikatoka nje na kwenda kusikiliza wito wa mama yangu .

“Haya sasa, Tamika uliyemtaka huyo amekuja, lakini nakuambia sasa hivi ukifanya tu fyokooo, namruhusu aondoke Sijui Kama unanisikia”.

“Nakusikia na nakuelewa pia mama yangu, nitamlinda Tamika “

Majibu yangu yalimfaanya mama kushangaa na kuona Kuwa ni kweli Ezra Mimi nimeanza Kuwa mtu wa tofauti.

*******

Siku iliyofuata Kama kawaida niliamka asubuhi na mapema kabisa nikajiandaa na kwenda zangu kazini, siku huyo niliendesha Mwenyewe na Tamika alikuwa amelala chumbani kwake Kana kwamba alikuwa amechoka sana.

İle nafika tu kazini Tamika akaanipigia na nilipopokea tu akaanza kuomba msamaha.

“Boss pole sana aiseeeeh nimejikuta Leo nikilala sana na kupitiliza, Nisamehe sana, nitawai kufika hapo muda wa kukufuata, Na Kama utataka nije ata sasa
Hivi nitakuja Tajiri yangu “


Nilimsikiliza kwa makini sana na sauti yake ya jazba na wasiwasi ilinifanya nimcheke sana mwisho nikamuuliza.

“Unajua kipika ??”

“Nani Mimi ??”

Tamika aliniuliza.

“Hapana Tamika nazungumza na mizimu ya ukoo wako mama, Naomba nisaidie kuiuliza Kama inajua kupika”

“Oooh boss Mimi ni mwanamke Bwana kupika najua”

“Sasa ili nikusamehe, Naomba Leo niangalie chakula kizuri kabisa, Yaani chakula Kitamu, chakula ambacho nikila Mwenyewe tu nikusamehe “

“Sawa boss “

Alijibu Tamika kisha akakata simu.

Majila ya jioni chapu nikarudi Nyumbani uku nikiwa na shauku sana na kula chakula kilichopikwa na Tamika, Sijui Kwanini Nilimwambia afanye kitu Kama iko ikiwa tayali Nyumbani Tuna mfanya kazi kwaajili ya kutupikia na majukumu mengine mengine.

Nilifika Nyumbanina kwenda kuoga mwisho nikarudi zangu sebuleni na Tamika hakuwa mbali akaja na kunitengea chakula utazani anamtengea mume wake wa Ndoa vile.

“Asante sana Tamika”

Nilizungumza baada ya Tamika kumaliza kuniwekea chakula.

“Ungana na Mimi “

Nilimwambia Tamika baada ya kumuona Kuwa anataka kwenda chumbani kwake, kWa utulivu Tamika akajibu.

“Aaaah niko Sawa aiseeeh nimetoka kula musa sio mrefu boss wangu “

“Mmmmh Tamika jamani, huo uongo umeanza lini jamani, jumuika na Mimi jamani “

“Niko Sawa boss “

“Hapo kwenye boss sasa, Naomba nite Ezra Bwana “

“Sawa”

********

Siku ziliendelea kwenda uku Mimi na Tamika tukiwa watu wa Karibu sana Tena sana, Yaani Tamika sikuwa na kila aina ya vibe , kila siku zilivyozidi kwenda ndio nilizudi kuona uzuri wa Tamika ambao amekuwa akiufucha kWa mavazi yake mabaya, lakini pia na kujiweka Kama mwanaume ambaye umri umeenda.

Yaani kumkuta Tamika akiwa sana nywele zake Ndefu ni kazi sana, Mara nyingi Tamika amekuwa ni mtu wa kufunika nywele zake kwenye mzula ambao ilipauka sana.

Siku moja ikiwa ni siku ya weekend, nilitoka zangu mjini na kuchukua vizawadi kwaajili ya Tamika, lakini pia nilimchukualia nguo nzuri sana kwani nilitaka Kwenda nae club kwa siku hiyo.

Majila ya usiku Kama kawaida nikatoka nikiwa na Tamika, Walahi alipendeza sana, mavazi ambayo nilimjumulia yalikuwa on top Yaani, ukiwa kuangalia na shape yake ndio kabisa Yaani niliweza halafu nikaweza tena.

“Kwahiyo Tamika wewe utumii Pombe kabisa ?”

Nilimuuliza Tamika tukiwa kwenye gari.

“Ahşaba Ezra Bwana nimeamka uamini hivi si ndio ? Yaani Mimi na Pombe ni Kama radhi na mbingu atuwezi kushikana kabisa, lakini ikitokea siku nimekunywa nakuomba Kama ni Nina Siri zako Walahi nazizagaza 😂🙌”

“We mjinga kweli Mbona kuzizagaza jamani 😁”

Hizo zilikuwa ni story za hapa na hapa kati yangu na Tamika, yooooh huyu girl ananıza vibe la maana kabisa na kuna muda ni Kama nilianza kumkwepa Demi wangu hivi kwaajili ya kutumia muda mzuri na Tamika.

Hatimaye tulifika club na kulikuwa Bna vibe Kama lote, kila mtu alikuwa bize na vinywaji lakini pia na kunywa na kula, Tamika alionekana Kuwa sio mtu wa starehe ata kidogo, Mara nyingi alikuwa chini akiangalia mambo yanayoenda.

Muda huo huo akaingia mkaka Fulani hivi, huyu kaka jamani yuko hot, muonekano wake ni kila mwanamke Anadata nae, na Kama yuko vizuri sana kila demi anapita Nae na yote hii ni kwakuwa alikuwa nampesa na hapo club alijulikana Kama PEDESHEE.

Siku hiyo pedeshee aliingia akiwa na pisi moja Kali sana, muda huo huo Tamika akanyanyuka kwenye kiti chake na kumsogelea PEDESHEE na kumchezeshea kibao kimoja Matata sana.

Kiukweli nilishtuka sanana haraka nikamuwai na kumuuliza.

“Kuna nini ?”

“Ezra Kaa mbali Tena mbali sana”

Alizungumza Tamika Ka hasira sana kisha akamgeukia pedeshee na kumchezeshea kichwa cha mwana ukome, kila mtu alishangaa ikiwemo mimi.

Kabala sijaingilia kati kwaajili ya kutuliza vulugu Tamika akamuuliza PEDESHEE.

“Hapa ndio marekaji Issah ?”

Kwanza macho yalinitoka Walahi, tangu NAKUJA huyu Issah hakuwai ata kutoka nje ya Mikoa halafu Leo hii anaulizwa hapa ndio Marekani.

KWa sauti ya kejeli PEDESHEE akajibu.

“Mshangazi Kaa mbali na Mimi Sawa huu ni muda wa mabinti “

Weeeeh kitendo cha yeye kumuita Tamika mshangazi kilinikasilisha na nikajikuta Nikiununua ugomvi, woiiiiih Sijui nilipatwa na nini lakini sio kWa hizi ngumi ambazo nilianza kumchezeshea huyu pedeshee.

Tamika akaniwai na kunitoa nje, lakini Tamika hakuwa Sawa kabisa, kitendo cha kutoka nje tu Tamika aakajitupia chini na kuanza kulia, nyie nilimuonea huruma sana Tamika.

Nilimsogelea na kumkumbatia kWa nguvu sana na kumtuliza, Ila mwenzenu hii ni dhambi, Yaani nimemkumbatia mtu kwaajili ya kumuuliza lakini weeeh nikajikuta nikianza kumpapasa Tamika wa wakati 😁🙌, kwakuwa Tamika alikuwa na Machungu sana hivyo hakuweza kuelewa kabisa.

Baada ya muda nikamchukua na kumuweka Ndani ya gari tayali kwaajili ya kuondoka.

Safari Wala haikuwa Ndefu kwakweli, Yaani tuliwai snaa kufika Nyumbani, kwa upande wa Tamika hakuwa Sawa kabisa, kilimsaidia moja kWa moja mpaka chumbani kwake, nilifika na kumlaza kitandani, ile nataka kuondoka tu Tamika akanivuta kWa nguvu sana na nikajikuta nikitua kwenye midoo yake ambayo ilikuwa tayali kWa kiss.

JE NINI KITATOKEA ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO…..


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote