Ujumbe mmoja tu uliotumwa kwa namba isiyo sahihi...kwangu...na kila kitu kikabadilika.
Hajaniambia jina lake la mwisho, na labda hilo linapaswa kuwa ishara ya hatari elfu moja, lakini nilipokuwa peke yangu katika jiji jipya na nikihangaika kujiweka hai, jumbe zake zilikuwa kama uzi wa matumaini niliokuwa nikiuomba kwa muda mrefu.
Lakini nisingewahi kujibu ule ujumbe kama ningejua kwamba aliyekuwa ananitumia ni Austin Daniels, nyota mkubwa wa mchezo wa mpira hockey na kipenzi cha mashabiki duniani.
Sasa anajaribu kuniteka moyo kabisa. Anasema amenizimia kweli kweli. Anataka nivae namba yake…milele.
Swali ni hili—je, bado ni ile namba isiyo sahihi, au mungu huyu wa uwanjani anaweza kuthibitisha kwamba yeye ndiye mtu sahihi?
Sehemu ya 1
Nilimkazia macho mama huku akiwa amelala ovyo kwenye kochi letu la zamani. Macho yake yalikuwa mazito, mwili wake ukitingishika kidogo kidogo kana kwamba alikuwa ndani ya ndoto isiyoeleweka. Mchanganyiko wa harufu ya bangi, pombe na madawa ya hospitali ulitapakaa ndani ya nyumba yetu ndogo.
“Mrembo wangu… wateja wanakuja,” alininong’oneza kwa sauti ya kuchoka, akiwa hajitambui vizuri. Aliniita "mrembo wangu" kila alipokuwa kwenye hali hiyo, kila mara nikijua hilo halimaanishi chochote kizuri.
Mlango ukagongwa. Sikuwa hata nimemaliza kuhesabu hadi tatu, kijana mmoja mrefu akaingia. Alikuwa na sura ya kutojali, akamwita mama kwa jina la ajabu: “Roxane!”
Mama akageuka kwa shida na kuniambia kwa sauti ya chini lakini ya dharura, “Brigit, nenda chumbani. Usitoke mpaka mteja aondoke.”
Sikusema chochote. Nilinyanyuka na kuelekea chumbani kwangu, nikijua kinachoendelea lakini bado nikijaribu kujifanya sikielewi. Mara zote huwa hivi. Mteja huja. Mlango hufungwa. Mimi hubaki na ukimya.
Lakini siku hiyo… ukimya haukuwa wa kawaida.
Dakika zilipita. Halafu saa nzima. Halafu tena zaidi. Kulikuwa kimya—kimya cha kutisha. Hakukuwa na sauti ya vicheko, wala mlio wa viatu, wala hata mlango ukifunguliwa. Kulikuwa tu na ukimya mzito, ulionikaba koo.
Mwili wangu ukaanza kusononeka. Nilijua kuna jambo. Nilijua. Kwa hofu na wasiwasi, nilifungua mlango kwa tahadhari na kuchungulia nje.
Nilimuona mama. Alikuwa sakafuni, akielea kwenye dimbwi la matapishi ya kijani kibichi. Alikuwa amepoteza fahamu, au pengine… pengine mbaya zaidi.
Nilikimbia kwa kasi. “Mama! Mama, nini shida?”
Alijaribu kufumbua macho. Kwa shida. Kwa maumivu. Kwa mwisho.
“Brigit… mwanangu mrembo…” alijikokota kusema, “…usijewahi kuukabidhi moyo wako kwa mwanaume yoyote yule…”
Alinirudia tena, na tena. Halafu… kimya.
Macho yake yakapoteza uhai. Mwili wake ukawa mzito. Moyo wangu ukavunjika.
Sikuwahi kuelewa kwa nini alisema maneno hayo. Kwa nini hapo. Kwa nini hivyo. Lakini usiku huo, nilijua moja: maisha yangu yalibadilika milele.
Nilibaki pale chini, nikimkumbatia mama aliyenipotea. Nikijiuliza: ni nini maana ya kumpenda mtu, na ni kwa nini moyo wangu ni wa kuhifadhiwa?
Sikuwa na majibu—lakini niliamua kuanza safari ya kuyatafuta. Endelea…
Sehemu ya 2;
Nilikuwa na miaka kumi tu, mdogo sana kuelewa mengi, lakini mateso hayachagui umri. Mama alipofariki, nilihisi kama dunia ilinimeza mzima mzima. Nilikuwa peke yangu—hakuna mjomba, shangazi, wala dada wa karibu. Nilijikuta mikononi mwa serikali, nikipelekwa kwenye nyumba ya kulelea watoto wasio na wazazi.
Lakini nyumba hizo hazikuwahi kuwa “nyumba” kwangu. Kila nilipopita, nilikuwa kama mzigo tu waliolazimika kuubeba. Hawakuwa wanatafuta mtoto wa kulea kwa upendo—walikuwa wanatafuta picha nzuri kwa jamii, au misaada kutoka serikalini. Na mimi, Brigit, sikuwahi kuwa picha nzuri kwao. Nilikuwa ni mdogo lakini Maisha tulioishi na mama na kifo chake kilinikuza haraka. Walinichukia kwa hilo.
Nyumba ya kwanza, walinilazimisha kuosha vyombo kwa saa nne usiku. Ya pili, walikuwa wakinitishia kunirudisha kila nilipokosea. Ya tatu… ya nne… wengine walijifanya kunipenda mwanzoni lakini yote yaliisha baada yam da mfupi tyu hadi kufikia nyumba ya ishirini. Kila mahali nilipofika, niliwaona watu kwa sura zao halisi—nyuso za kinafiki zilizojaa majeraha waliyoyaficha
nyuma ya tabasamu.
Lakini nyumba ya mwisho… nyumba ya Mr. na Mrs. Robert, ilikuwa tofauti kwa njia mbaya zaidi. Hapa, niligeuka mtumwa wa familia. Nilifanya kazi zote: kupika, kufua, kusafisha... na bado waliniita “mgeni wa muda.”
Lakini kilichoniumiza zaidi ni macho ya Mr. Robert. Macho yake hayakuwa ya mzazi, yalikuwa ya simba anayemvizia swala. Kila nilipopita karibu yake, nilihisi mgongo wangu ukikauka kwa hofu. Alikuwa akinikodolea macho bila haya, na mara kadhaa alijifanya kunigusa kwa kisingizio cha “ajali.”
Nilibaki kimya. Nilijua hakuna mtu angeniamini. Nilikuwa na mwezi mmoja tu kufikisha miaka kumi na minane. Mwezi mmoja tu.
Nilianza kazi ya muda katika mgahawa mmoja mdogo baada ya shule. Kila senti niliyoipata, niliiweka kwenye bahasha ya siri, chini ya godoro langu. Nilihesabu siku kama mfungwa anavyohesabu miaka yake ya mwisho gerezani.
Nilikuwa na ndoto moja tu: kuondoka. Kuanzisha maisha yangu, peke yangu. Bila Mr. Robert. Bila macho ya watu wanaoniona kama kitu. Bila nyumba za uongo. Nilihitaji kuwa huru.
Na nilijua—ikiwa nitasalimika mwezi huu mmoja, basi maisha yangu halisi yataanza.
Endelea…
Sehemu ya 3:
Sikujali kazi nyingi za nyumba hii. Nilizifanya zote—kutoka kufua hadi kupiga deki—ilikuwa bora zaidi kuliko kuwa karibu na Mr. Robert. Nilifanya kazi kama mtumwa, lakini angalau kazi zilinipa kisingizio cha kutoonekana. Kisingizio cha kukwepa macho yake, harufu yake, na tabasamu lake lenye sumu.
Lakini leo… leo haikuenda kama nilivyotarajia.
Alirudi mapema. Sikutarajia. Nilikuwa jikoni, nimevaa apron, nikipika chakula cha usiku kwa haraka. Niliposikia mlango ukifunguliwa na hatua nzito zikiingia, moyo wangu ulianza kwenda mbio.
Alisimama mlangoni na kunikodolea macho kama alivyozoea siku hizi. Lakini leo aliamua kusema. Maneno yake yalinikata pumzi.
“Unajua kuwa birthday yako inakaribia, Brigit?” aliniambia kwa sauti ya upole iliyofichwa sumu.
Nikajifanya sijasikia. Nikazidi kuchanganya wali kwenye sufuria. Lakini alisogea karibu zaidi, sauti yake ikawa ya kunong’ona.
“Muda si mrefu unatimiza miaka 18. Na hivi karibuni nimekuwa na hamu ya ‘kukusanya’ vitu. Huwezi amini, Brigit... katika vitu vinavyonivutia siku hizi ni bikra.”
Mikono yangu ilianza kutetemeka. Nilijisikia kana kwamba dunia imesimama. Mapigo ya moyo wangu yakawa ngoma ya vita masikioni mwangu. Nilishindwa hata kushika bakuli la mayai nililokuwa nalo. Lilianguka na kuvunjika chini kwa kishindo cha mshangao.
“Ivi wewe Brigit, si ni bikra?” aliuliza huku mkono wake ukipanda taratibu chini ya mgongo wangu, akinishika kiuno kama simba aliyemkamata swala.
Nilihisi kutapika. Nilihisi uchafu. Nilihisi dunia ikinizunguka. Nilitamani nipotee pale pale jikoni.
Ndipo mke wake akaingia ghafla, akiwa amebeba kikapu cha mboga. Alitazama chini akaona mayai yamevunjika. Macho yake yaliruka juu, yakatua kwangu.
“Una nini wewe? Unanivunjia mayai yangu, Brigit?” alifoka.
Mr. Robert alicheka kwa sauti ya juu kana kwamba hakuna kilichotokea. Akaondoka bila haraka, akimwacha mke wake akinikazia macho. Hakujua chochote. Na wala asingetaka kujua.
Nilipiga magoti na kuanza kusafisha yale mayai yaliyomwagika, machozi yakinitiririka kimya kimya. Ndani yangu nilimwomba Mungu.
“Tafadhali Mungu, niepushe. Tafadhali, hiyo siku ifike haraka. Siku ya kuzaliwa kwangu. Siku nitakayoweza kutoka hapa.”
Usiku huo sikulala. Nilikaa kitandani na nguo zangu zote, nikisikiliza kila kishindo nje ya mlango. Sikuwa na amani. Nilijua kwamba kulala ni kama kujitupa mwenyewe mikononi mwa adui. Nilihesabu siku tena. Siku kumi na moja tu… kumi na moja tu.
Endelea…
Sehemu ya 4:
Ilikuwa saa nane usiku. Nilikuwa nimemaliza masomo yangu ya nyumbani, nikajipumzisha kitandani, nikazima taa. Nilijiambia, “Brigit, siku kumi tu zimebaki. Vumilia.” Nilikuwa nimechoka, lakini bado akili yangu haikukubali kulala mapema. Kitu ndani yangu kilinitahadharisha.
Ndipo nikasikia… sauti. Sauti ya kitasa. Ilikuwa ni kama mtu anahangaika polepole, kwa makini. Nikakaa kitako kimya kimya, nikasikilizia. Nilikuwa nimefunga mlango, lakini kisha—klik! Mlango ukafunguliwa. Kwa namna ulivyofunguliwa kwa urahisi, nilijua… hakuwa mtu mwingine ila Mr. Robert. Lazima alikuwa na funguo ya spea.
Sikuwaza mara mbili. Hofu yangu ikageuka hasira. Nilipiga kelele kwa nguvu zote.
“AAAAH! AAAAAAAAH! JAMANI SAIDIAAAA!”
Hatua zake zilisikika zikikimbia kwa haraka. Alitoroka. Kelele zangu zikaamsha nyumba nzima. Mke wake, Mrs. Robert, alifika kwanza, akiwa amevaa gauni la kulalia, uso wake umejaa usingizi na hasira.
“Unanini wewe Brigit? Kupiga kelele usiku huu wa manane?”
Sekunde chache baadaye, Mr. Robert naye akaingia — akikimbia, akijifanya mwenye wasiwasi.
“Nini kinaendelea hapa?” aliuliza huku akijifanya hajui chochote. Mrs. Robert akaniangalia kwa macho makali.
“Haya tuambie, ni nini mpaka umetufanya tuamke wote?”
Nilimtazama Mr. Robert. Alinisoma haraka. Macho yake yakanipa ujumbe: “Ole wako. Sema ni mimi, nitaimaliza kazi.”
Nikahisi ulimi wangu ukikauka. Saikolojia ya mnyama ilinitawala — kupigana au kukimbia. Na niliamua kujilinda kwa njia pekee niliyoijua.
“Samahani mama... nilikuwa naota ndoto mbaya. Kwenye ndoto mtu alikuwa ananikimbiza... nilishtuka sana. Samahani kwa usumbufu.” Nikasema kwa sauti ya kupasua kimya.
Mrs. Robert alinisogelea akisema kwa hasira,
“Haya basi kesho usiote tena! Unaamsha watu usiku!”
Lakini alipoanza kutoka, akageuka tena.
“Alafu kipindi naamka sikukuona kitandani, Robert… ulikuwa wapi?” Akatabasamu, akasema:
“Nilikuwa jikoni nikanywa maji. Niliposikia kelele tu nikaja moja kwa moja.”
Wakaondoka. Lakini kabla hajafunga mlango, Mr. Robert akageuka na kuniangalia. Macho yake yalinichoma. Yalisema:
“Nitarudi. Na ole wako upige kelele tena.”
Mlango ulipofungwa, nikasikia mapigo ya moyo wangu yakirindima kama ngoma ya vita. Nikajua kwa uhakika mmoja: sitatoboa wiki nyingine hapa.
Sikutaka tena kungoja siku ya kuzaliwa kwangu. Nilikuwa na siku moja. Kesho. Nilijiambia,
“Brigit, ukiamka asubuhi, chukua kila kitu. Chukua ile bahasha ya pesa chini ya godoro. Hii nyumba siyo salama tena. Ukisubiri, utakufa. Na maisha yako yana maana kuliko hofu.”
Kesho ilikuwa mwanzo wa safari mpya. Au mwisho wangu.
Lakini sikuwa tayari kumuacha mr Robert anishike hata kidogo. Endelea…
Seheu ya 5:
Leo ilikuwa Jumamosi, na shule ilikuwa karibu kuisha. Ningeweza kuvumilia hadi mwisho wa mwaka, lakini moyo wangu haukuwa na nguvu ya kusubiri. Nilijua, kwa uhakika, kwamba usiku wa leo lazima iwe mwisho wa safari yangu ya mateso.
Nilikaa darasani kwa huzuni ya kimya, nikisikiliza mwalimu huku akili yangu ikiwa mbali kabisa. Wanafunzi wengine walikuwa wakicheka, wakipanga mipango ya wikendi—lakini mimi, nilikuwa napanga uhuru wangu. Nilijua kabisa, huu ndio ulikuwa mwisho wa maisha ya shule yangu ya kawaida.
Niliamua kukatisha masomo yangu rasmi.
Badala yake, nitatafuta njia ya kusoma kupitia QT, kwani elimu bado ni ndoto yangu, lakini kwa sasa, lazima nipone kwanza.
Nilipofika nyumbani jioni, nilitabasamu kama kawaida. Nikawasalimia kama kawaida. Nikapika kama kawaida. Nikasafisha nyumba yote hadi ikang'aa — mara ya mwisho nikiifanya kwa moyo wa upole. Sauti ya Mr. Robert haikuwa nyumbani kwa muda huo, lakini nilijua ni suala la saa kabla arejee na kuzama usingizini wake mzito.
Nilikwenda chumbani kwangu kimya kimya, nikafungua godoro, nikatoa ile bahasha niliyoihifadhi kwa miezi kadhaa. Pesa zote nilizokuwa nalipwa katika mgahawa zilikuwa humo — na leo walinipa mshahara wangu wa mwisho. Nilijua nisingerudi tena.
Nilishanunua simu ndogo mpya — isiyotambulika, isiyo na jina lao, wala historia. Simu yao niliiacha juu ya meza, iseme kila kitu. Nilijua watajaribu kunisingizia, kusema nimeiba au kukimbia na mali zao — lakini sikuwa na muda wa kujieleza kwa watu kama hao.
Usiku ulifika polepole. Wote walilala, nyumba ilikuwa kimya. Saa ilipofika saa nane usiku, moyo wangu ukawa kama ngoma ya vita. Nilijua, huu ndio wakati.
Nilibeba begi langu — si kubwa, lakini lilijaa ndoto. Nilifungua dirisha la chumba changu, nikatoka kwa utulivu wa paka. Nilipiga hatua polepole kupitia ua wa nyuma, nikapitia msituni, nikiepuka barabara kuu kabisa. Sikutaka hata mtu mmoja kuniona. Sikutaka hata kuacha kivuli.
Dakika zilikuwa kama masaa. Moyo wangu ulikuwa unadunda kama unaweza kunivunjia mbavu. Lakini baada ya karibu saa moja ya kutembea kwa haraka, niliona taa za stand ya mabasi. Machozi yakanitoka bila hata kugusa uso wangu.
Nilifika.
Nilimwendea muuzaji wa tiketi.
“Naomba tiketi moja ya kuelekea Dalas.”
Alinipa tiketi bila kuniuliza swali lolote. Hakuniuliza kama ni mwanafunzi. Hakuniuliza kama nina ruhusa. Aliniangalia kama mtu mzima mwenye maamuzi. Kwa mara ya kwanza, nilihisi kama mtu mzima — mwenye sauti, mwenye uchaguzi.
Nilipanda basi. Nikakaa kiti cha nyuma kabisa. Nikatazama nje, na nilipoona taa za mji zikianza kupotea nyuma, nilishusha pumzi ndefu.
Nilikuwa naondoka. Kwa kweli, naondoka.
Baada ya safari ya saa sita, nilifika Dalas. Nikiwa na begi langu, simu mpya, na bahasha ya pesa — nilianza kutafuta pa kuishi. Nilipata kituo cha watoto yatima kinachohifadhi wasichana wasio na makazi.
Endeleaa…
Sehemu ya 6:
Niliposhuka stand pale Dalas, nilihisi ushindi ndani yangu. Nilihisi kama nimevuka bahari ya mateso na sasa nipo salama—lakini hiyo ilidumu kwa dakika chache tu.
Sikutaka kupanda teksi. Kila shilingi ilihesabika. Kila senti nilikuwa nimeihifadhi kwa miezi mingi, na sasa ilikuwa ndiyo kila kitu nilichonacho maishani. Kwa hivyo, nikaanza kuulizia watu mitaani njia ya kufika kwenye kituo cha watoto yatima. Watoto waliokuwa wakizunguka mitaani walionekana wema, walikubali kunisaidia.
Niliwaamini. Niliwaamini kwa sababu bado nilikuwa na moyo wa mtoto, wa kuamini kila mtu ni mzuri. Na hapo ndipo waliponichomoa – simu yangu mpya na pesa zote nilizoweka mfukoni mwa suruali yangu.
Nilisimama katikati ya mtaa nikitetemeka. Sauti yangu haikutoka. Watu walikuwa wanapita tu, kama siipo. Kama sina maana. Nilikuwa nimebakiza begi langu tu, na pesa chache kwenye soksi — nilikuwa nimezificha kwa tahadhari.
Lakini sasa, sikuweza tena kufika kwenye kile kituo. Sikuwa na maelekezo, simu, wala hata jina la kuomba msaada. Nilianza kutembea—bila lengo, bila mahali. Nilitangatanga mjini siku nzima, nikibeba begi langu kama ndoto isiyofika.
Jioni ilipofika, miguu yangu ilikufa ganzi. Mwili wangu ulikuwa umechoka, moyo wangu ukawa mzito kama mawe. Giza lilipoanza kutanda, nilijikuta nimeingia kwenye park ya jiji. Kulikuwa na benchi moja lililokuwa wazi, nikaketi.
Nikajilaza taratibu, nikalikumbatia begi langu — rafiki yangu wa mwisho. Sikuwa na pesa ya hoteli. Sikuwa na jamaa wa kumpigia. Nilikuwa na Mungu tu, na usingizi unaonivuta.
Nadhani nilianza kusinzia. Lakini ghafla, nikashituka. Giza lilikuwa limetanda kikamilifu. Taa za barabarani zilikuwa zinamulika kwa mbali, zikitoa mwanga wa huzuni. Na mbele yangu… mtu mmoja alikuwa ameketi kwenye benchi, akinichunguza kimya kimya.
Moyo wangu ulianza kupiga mbio. Nikakumbatia begi langu zaidi. Nikajiandaa kukimbia.
“Usijali,” sauti yake ilivunjika kutoka kwenye ukimya.
“Mimi naitwa bill. Hapa ndipo hekalu langu. Lala tu. Nitakulinda.”
Nilimtazama mara mbili. Mavazi yake yalikuwa yamechanika, machafu. Nywele zake zilikuwa zimejaa vumbi na uso wake ulikuwa umechoka kama historia ya mateso. Alionekana kama ombaomba.
Lakini macho yake… hayakuwa ya kuogopesha. Yalikuwa macho ya mtu aliyeumia sana kiasi cha kuelewa maumivu ya mwingine. Na mimi… nilikuwa nimechoka mno kupambana. Nilihitaji tu kupumua.
Nikamwambia kimoyomoyo Mungu:
“Naomba unilinde. Sijui huyu ni nani. Sijui kesho itaniletea nini. Lakini siwezi tena. Lala ni lazima.”
Nikalala kwenye benchi, pembeni ya mgeni. Na kwa mshangao wangu… usiku huo haukuwa wa hatari. Haukuwa wa majeraha. Nililala kwa amani ya ajabu – kwa mara ya kwanza bila kelele ya Mr. Robert, bila hofu ya mlango kufunguliwa usiku.
Sijui huyu bill ni nani. Lakini usiku huo, alikuwa malaika wa barabarani. ?
Endeleaa…
Sehemu ya 7:
Nilipoamka alfajiri, mwanga wa jua ulianza kupenya kwenye majani ya miti ya park. Nilijikuta bado nikiwa nimelalia begi langu, baridi ikiwa imenipenya hadi kwenye mifupa. Nilipofumbua macho, kitu cha kwanza nilichokiona… ilikuwa macho yale yale ya usiku uliopita.
bill
Alikuwa bado ameketi pale, akinichunguza kwa utulivu. Hakuongea. Alionekana kama mtu aliyekuwa kwenye zamu ya kunilinda usiku mzima.
“Habari ya asubuhi,” nilisema kwa sauti ya upole.
Akatabasamu kidogo, akasema,
“Umeamka salama. Nilikuambia utakuwa sawa. Jina langu bado ni bill.” Nikakaa vizuri, nikamshika mkono kwa aibu na kusema,
“Na mimi ni Brigit…”
Tulikaa kimya kwa sekunde chache. Kisha akaniambia kuwa hiyo park ndiyo nyumba yake ya muda mrefu. Benchi lile… lilikuwa ni malazi yake ya kila usiku. Lakini licha ya maisha yake kuwa magumu, bado alikuwa na moyo wa kusaidia.
“Nitakupeleka kwenye kituo cha watoto yatima,” alisema kwa sauti ya uhakika. “Wananifahamu kule. Tuwahi kabla hawajafunga mapokezi.”
Tulitembea pamoja hadi pale kwenye kituo. Kiingilio kilikuwa na geti la chuma lililopakwa rangi ya buluu, na bango lililoandikwa "St. Grace Youth Shelter". Walinzi walituangalia kwa tahadhari, lakini walipomuona bill, walilegea.
Nilipowasiliana na mfanyakazi mmoja, nikasema tu:
‘’bill ndiye aliyenileta hapa.”
Kwa mshangao wangu, hilo jina lilitosha. Walimpigia saluti kimya kimya, wakaniangalia kwa upole, na kuniambia niingie.
John alinigeukia, uso wake ukionesha uzito wa miaka mingi.
“Brigit,” alisema, “Utafika mbali. Naona kitu ndani yako… kitu ambacho dunia haiwezi kukipuuza. Usikate tamaa. Hii ni mwanzo tu. Siku moja utainuka zaidi ya unavyofikiria.”
Nilimkumbatia. Kwa harufu ya mavazi yake, kwa joto la miwani yake ya zamani, nilihisi moyo wake. Na nilijua — huyu si ombaomba wa kawaida. Huyu alikuwa ni malaika aliyevaa ngozi ya shida.
Mwaka mmoja baadaye...
Maisha yangu yalibadilika. Sikusema kuwa yalikuwa rahisi. Lakini yalikuwa ya kwangu.
Niliweza kupata chumba kidogo cha kupanga, katika mtaa wa watu wa hali ya chini — nyumba ya mbao, yenye dari inayovuja wakati wa mvua. Lakini nilikuwa na funguo zangu. Mlango wangu. Uhuru wangu.
Nilikuwa nafanya kazi kama msaidizi wa mapokezi katika kliniki ndogo, kazi niliyoipata kupitia mmoja wa wafanyakazi wa kituo. Na kila jioni, baada ya kazi, nilikuwa nikipitia mgahawa mmoja kwa shift ya part-time. Si kazi kubwa, lakini ilinisaidia kuwalipa kodi na kula.
Mara baada ya kutoka mgahawani, nilirudi nyumbani, nikaoga, nikavaa nguo safi, na kuelekea kwenye community college. Nilikuwa nasoma kwa bidii — si kwa sababu ya alama, bali kwa sababu ya njaa ya maisha bora.
Nilikuwa na ndoto. Na sasa, kwa mara ya kwanza… nilikuwa na njia ya kuifikia.
Nilijua bado niko mwanzo wa safari, lakini nilikumbuka maneno ya bill kila mara:
“Usikate tamaa, Brigit. Hii ni mwanzo tu.”
Endeleaa..
Sehemu ya 8:
Nilipofika kazini leo, mwili wangu ulikuwa umeisha kabisa. Macho yangu yalikuwa mazito, kiuno kilikuwa kinaniuma, na kichwa kilikuwa kama kinapasuka. Kati ya kusimama muda mrefu kwenye mgahawa jana usiku, na masomo hadi saa za usiku wa manane, leo nilihitaji mapumziko — lakini mapumziko si sehemu ya maisha yangu.
Niliketi kwenye dawati la mapokezi, nikafungua daftari la wagonjwa na kuanza kupanga majina. Nilitamani siku ipite haraka nirudi nyumbani, nijilaze hata kwa dakika chache kabla ya shift yangu ya pili.
Ndipo Kevin akaingia — Daktari Kevin.
Alikuwa anatembea kwa tabasamu la kawaida lake la kujifanya mcheshi. Kila mara alikuwa na njia mpya ya kunisumbua — kama ni utani, au maombi ya “kutoka out”, au kujaribu kuingiza maneno ya mapenzi kwa ujanja ujanja.
Leo alikuja na sura ya ukarimu iliyochanganywa na tamaa.
“Brigit,” alisema kwa sauti ya chini, akielekea upande wa dawati langu, “unaonekana umechoka leo. Mbona usijipe muda wa kupumzika kidogo… nami nikutoe hata mara moja tu?”
Nikampigia tabasamu la uvumilivu — la kujizuia nisijibwage kwa hasira.
“Dokta, sina muda. Nikitoka hapa nashika shift nyingine, halafu masomo. Sina nafasi ya 'out',” nilimwambia kwa upole lakini kwa msimamo.
Akatabasamu tena, kwa ule mtindo wake wa kujifanya mwelewa lakini asiyekubali hapana.
“Brigit, leo tu. Leo tu upumzike, na mimi nikuchangamshe,” aliongeza huku macho yake yakizunguka uso wangu kama mtu anayejaribu kuvua tabasamu kwa nguvu.
Nilijiambia kimoyomoyo,
“Wewe umelelewa maisha mazuri, hata usipokuja kazini dunia haiyumbi. Mimi nikiacha kazi leo, najikuta nimerudi park, benchi, baridi…”
Ndipo nikamjibu kwa ukali uliojaa upole:
“Samahani, sina muda wa kupoteza. Sina nafasi kwa mambo ambayo hayaendani na lengo la maisha yangu.”
Alijifanya kucheka, lakini niliona machoni — amekasirika.
“Wewe Brigit, ulivyo mzuri… utakuja kuzeekea kazini. Hutaki hata mara moja kutoka out, kufanya mambo ya kuchangamsha mwili...”
Aliondoka huku akitingisha kichwa, lakini mimi niliinama, nikapumua kwa nguvu. Nikakumbuka maneno ya mama yangu siku ile alipokuwa anakata roho, akiwa kwenye dimbwi la sumu mwilini:
“Mwanangu mrembo… usiwahi kuukabidhi moyo wako kwa mwanaume yoyote yule.”
Nilimaliza shift yangu, nikavaa haraka, nikapita mgahawani kwa zamu yangu ya usiku. Nilifanya kazi kwa bidii, japo moyo ulikuwa umebeba uzito wa maneno ya Kevin na uchovu wa mwili.
Baada ya saa tatu, nilitoka nikiwa nimebeba chochote walichonipa — mabaki kidogo ya chakula. Nikatembea haraka kuelekea chumba changu.
Lakini nilipofika… moyoni mwangu ukatulia kwa sekunde moja.
Baba mwenye nyumba alikuwa amesimama mlangoni kwangu, mikono ikiwa mfukoni, macho yake yakiwa yamekaa kwangu kama mtu aliyekuwa akinivizia.
Nikashika begi langu vizuri. Mapigo ya moyo yakaanza kuongezeka. Nikasogea polepole huku nikiuliza:
“Shikamoo…”
Endelea…
Sehemu ya 9:
Niliposimama mlangoni na kumwona baba mwenye nyumba, nilijilazimisha kuwa na heshima. Uchovu wangu haukuweza kunizuia kumsalimia:
“Shikamoo…”
Niliendelea:
“Samahani… naomba unipishe niingie ndani…”
Lakini hakusogea. Badala yake, alinikamata mkono kwa nguvu. Mikono yake ilikuwa migumu, baridi, ya mtu ambaye anajua anachokifanya.
“Unajua wewe ni mpangaji wangu mpendwa kuliko wote?” alianza kusema huku sauti yake ikiwa ya utulivu wa mtego.
“Hujawahi kuchelewa kodi hata siku moja. Yaani, uko vizuri sana Brigit. Lakini pia nimeona… unateseka sana kuipata hiyo kodi.”
Nilitabasamu kwa nguvu — tabasamu la tahadhari.
“Leo nimekuja kukupa offer… kama unataka, unaweza kutolipa kodi kabisa. Unajua? Unaweza kunilipa… kivingine.”
Nilihisi tumbo langu linajiviringa. Hakukuwa na chakula tumboni, lakini bado nilihisi kama nitatapika. Dunia ilianza kuzunguka taratibu. Mifupa yangu yote ikawa na baridi.
Nikajaribu kujinasua kutoka mikononi mwake, lakini mkono wake ulinishika kwa nguvu kana kwamba anamiliki uhai wangu. Nilitetemeka huku nikijaribu kuingiza funguo mlangoni kwa mikono isiyo thabiti. Nilipofanikiwa kufungua, nilijirusha ndani haraka, nikamgonga mlango kwa nguvu hadi ukafungwa.
Nilianguka kwenye sakafu ya chumba changu, nikaanza kupumua kwa sauti. Mwili wangu uliogopa. Akili yangu ilipambana na mawazo mabaya. Machozi yalitoka bila sauti.
Leo tu, wanaume wawili wamejaribu kunitumia. Leo tu. Kevin asubuhi, mwenye nyumba jioni.
Nilikumbuka tena maneno ya mama:
“Uzuri wako unaweza kuwa laana…”
Nikajiuliza, je, mama alikuwa sahihi? Kila mara mtu aliponiangalia kwa tamaa, kila mara nilipojivika heshima lakini nikapewa dharau… nilihisi kama mwili wangu ulikuwa mzigo, kivuli kinachonitesa.
Baada ya dakika kadhaa, niliposikia amenyamaza na kuondoka, nikatulia kitandani, nikajifunika na blanketi kama kinga dhidi ya dunia.
Ndipo simu yangu ikatetemeka. Vibrate.
Niliitazama kwa mshangao. Sikuwa na marafiki wa kuchat nao. Nani angenitafuta saa hizi?
Nikaichukua taratibu… ujumbe mmoja tu, kutoka namba nisiyoijua: "Nipe nafasi ya pili babe and I'll blow ur mind."
Nilibaki nimeduwaa. Macho yakikodolea maandishi hayo kana kwamba yangebadilika. Leo ilikuwa…
Siku ya Kitaifa ya Kusumbuliwa.
Nilijiuliza — ni Kevin? Baba mwenye nyumba? Mwanaume mwingine nisiyemjua?
Sikutaka hata kujua. Nikaiweka simu chini kwa hasira. Nilijilazimisha kupuuza. Lakini sekunde chache baadaye, nilibadilisha mawazo.
Nikainua simu, nikatandika ujumbe:
“Si katika miaka milioni moja unaweza kunishangaza. Shika hio.” Nikabonyeza send. Bila emoji. Bila huruma. Bila woga.
Kuweka simu chini, nilijisikia vizuri ajabu.
Simu iliita. ‘’Sote wawili tunajua hiyo si kwel’’i, maandishi yalisomeka.
Ni mpuuzi gani mwenye majivuno. Bila shaka, angefikiri yeye ni zawadi ya Mungu
kwa wanawake. Niliweza tu kuwazia Kevin na mwenye nyumba wangu wakituma hizi
endeleaa…
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote