OUR STORY.
Niite Tully ingawa Nyumbani kwetu waliniita tulinagwe, ni Mwenyeji wa mbea Ndani Ndani uko, lakini ikiachana na Tulinagwe niite Tully sitaki shule 😂🙌, Yaani Mimi na shule ni vitu 12 tofauti.
Baada ya Kufeli sana shuleni nikaamua tu kuacha shule na kuoingia mjini kama Mdada wa kazi.
Mambo ya dasilamu sasa 😂🙌 Yaani kila miaka ni mzuri kila miaka anavutia, Ila Mimi macho yangu yakatua kWa huyu Kijana Gee, Kijana ambaye aliuteka moyo wangu maziima mpaka kuna muda nikawa naweza kumbaka 😂.
Hii penda penda na Kutanani ndio ikaniponza🥹 naweza nikasema hapa ndio matatizo yangu yako ANZA Rasmi.
Nikuulize ushawai kuruhusu kuteseka ili tu mtu wako wa Karibu apate amani ? Ushawai kuteseka ili tu mtu wako wa Karibu atimize ndoto zake ?? 🥹, hiii nilifanya mimi na kumfanya mtu afanikiwe lakini baadae kila kitu kiliniyeukia.
Natamani kulia mama watatu Mimi Wema ni Mzigo jamani sio azina Wema unakuwa unakwamisha sana, lakini pia mapenzi yanaharibu maisha.
UNATAKA KUJUA KWANINI MASEMA HIVI TILILIKA NA MIMI….
OUR STORY
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 01
ANZA NAYO.......
"Aaaaaah sasa hapa gari ni ipi na gari zenyewe ziko mapacha "
Ilisikika sauti ya kishamba ya kike, ikiwa ni katikati ya stendi kubwa ya mabus, kelele za uku na uku zilisikika, wapiga debe awakuwa mbali na shughuli zao.
Lakini pia wafanya biashara awakuwa mbali, wauza maji, biscuit na zagazaga walikuwa wakiendelea kupiga kazi, yaani hakuna kupumzika.
Muda huo huo anaonekana msichana akiwa amekumbatia mfuko wake wa shangazi kaja ambao ulikuwa mkubwa mno, msichana wa watu alizunguka uku na uku akishangaa shangaa pasi na kujua nini afanye.
"Sasa hapa naenda wapi jamani, magari haya yote ni ya blue langu ni lipi ? Inakuwaje wanaleta magari mapacha mapacha " msichana huyo alijiuliza uku akisogelea moja ya mabasi ambayo yalikuwa yamepaki kwenye stendi hiyo na watu walikuwa wakipanda.
Msichana huyo alipanda kwenye moja ya basi na kukaa kwenye siti ambayo ilikuwa karibu kabisa na dereva.
"Dada hii ni siti yangu " alizungumza mkaka fulani hivi ambaye alipanda kwenye bus ilo ilo.
"Weeh nawe Toka hapa, kwani kuna jina lako, nioneshe jina lako kama lipo hapa"
"Si jina, umeona tiketi yangu imeandikwa namba mbili "
Hapo ndipo msichana yule alipata akili ya kutoa tiketi yake ambayo alikuwa ameweka ndani ya shangazi kaja lake na kuanza kuiangalia na kukuta kuwa imeandikwa namba 15.
"Eeeh ni 15 kwani namba zenyewe unazionaje ??" Aliuliza msichana yule na kumfanya mkaka huyo kutabasamu.
Bila hiyana wala kinyongo mkaka yule alimsaidia binti kupata siti yake na hapo aliweza kukaa. Baada ya dakika kama 10 hivi alikuja mwanamama mtu mzima na kwenda kwenye siti ambayo alikuwa amekaa msichana yule.
"Samahani binti hii ni nafasi yangu "
"Eeeh, hii ni yangu angalia tiketi yangu imeandikwa 15 na hii ni siti namba 15 " msichana wa watu alijitetea baada ya kujua watu wanakaa kutokana na namba zilizopo kwenye tiketi zao.
"Hawa watu ni wapuuzi sana, wanatoaje siti moja kwa watu wawili " alilalama mama yule kisha akatoka eneo ilo na baada ya muda mfupi akarudi akiwa na konda ambaye alivalia sale ya gari husika.
"Samahani naweza kuona tiketi yako ??" Konda huyo alimuuliza msichana ambaye alikuwa amekaa kwenye siti namba 15.
Baada ya muda na kuangalia angalia konda yule akazungumza.
"Binti umekosea gari, gari yako ni ile pale na ndio inaondoka, fanya haraka "
"Aaah sasa kwanini mnaweka magari mapacha ? Mimi nitawajuaje ? Ndio maana mama anasemaga watu wengi ni wachawi "
"Acha maneno mengi inuka Chapu gari inakuacha"
Kwa haraka na wasiwasi msichana yule aliinuka na kutoka nje ili kuwai gari ambayo alitakiwa kupanda.
Ile anatoka tu gari yake ilianza kuondoka na kumfanya kuanza kuikimbiza uku akipiga kelele, ila huyu msichana ni kama kichaa, alipoona gari inachochea moto alitupa mizigo yake ili kuongeza mwendo wa kukimbiza gari.
"Kuna mtu umemuacha dereva " alizungumza mmoja Kati ya abiria waliokuwamo ndani ya gari ilo.
Hatimaye gari ilisimamishwa na muda msichana yule alifika akiwa anahema juu juu.
"Ungechelewa tungekuacha kweli " alizunguma dereva.
"Aaah nimekuita sana lakini umewasha gari lako na kuondoka, inaamaana ulikuwa haujui kama mimi sijapanda au ??' Alilalamika msichana huyo akiwa ameshika na kiuno kabisa.
"Unapiga domo na mzigo wako uliacha kule utaibiwa wewe " alizungumza mkaka ambaye alivalia sale za wafanyakazi wa bus ilo na alikuwa ameshika shangazi kaja la msichana huyo.
Safari ilionekana kuwa ndefu sana na majila ya saa 12 jioni, gari hiyo iliwasili kwenye stendi kuu ya dar es salaam na watu wakawa wanashuka.
Kila mtu alishuka isipokuwa msichana yule ambaye alikuwa na begi lake la shangazi kaja.
"Mbona ushuki ??" Dereva alimuuliza binti baada ya kumsogelea.
"Mimi naenda Dar "
"Ahahahaah dar ipo tena jamani eeh dar si ndio hii mtoto mzuri " alizungumza dereva huyo uku akinyoosha mkono na kuchezea mashavu ya binti.
Msichana wa watu kwa aibu na kutabasamu akainamia chini, na kuchezea chezea vidole vyake.
Muda huo huo simu ya msichana iliita na ili kuipata simu yake ilimpasa kumwaga vitu vyote ambavyo vilikuwa ndani ya shangazi kaja, jambo ambalo lilimchekesha sana dereva na kujua kweli huyu ni wakuja.
Binti huyo alifanya mawasiliano yake na muda mfupi aliweza kukutana na mwenyeji wake ambaye ni mwanamke, alikuwa sio mtu mzima wala binti lakini umri wake ulicheza kwenye miaka 35 hapa.
SONGA NAYO.....
Anyway, achana na drama za uko juu za kuangaika na magari, niwaambie tu ushamba hauna kabila kudadeki, huyo msichana ni mimi, na ilikuwa ni siku yangu ya kwanza kutoka kijijini kwetu na kuja dar es salaam.
Kwa sasa nina miaka kadhaa tangu nifike jijini na ni mjanja hatari, najua kona zote sijui unaelewa.
Ingawa ni mdada wa kazi za ndani nashukuru Mungu nimekutana na familia ambayo inanipenda na kunijali, awajanifanya kama mfanyakazi bali binti yao.
Familia hiyo ilibarikiwa watoto wawili ambao walikuwa bize sana na masomo yao na mimi nilikuwa hapo kwaajili ya kuwahudumia.
Nikiwa zangu jikoni naandaa chakula cha jioni, niliweza kusikia sauti ya boss wangu ambaye aliniita.
"Tully "
Nilikaa kimya kwa muda kisha nikaenda sebuleni nilipoitwa pasi na kuitika.
"Umekuwa bubu au, nakuita wala huitiki jamani " alilalamika boss wangu wa kike ambaye uwa namuita madam.
"Aaah, yaani nilikuwa sina uhakika kama ndo mimi naitwa, kwahiyo nimekuja gafla gafla kuhakikisha nisije nikaitikia majini bure "
Maneno yangu yalimfanya madam kucheka lakini pia na mkaka mgeni ambaye aliongozana na madam akuacha kucheka.
"Jinga wewe, kwamba umu ndani kuna majini au ? Achana na maneno mengi, kwenye gari yangu kuja mizigo, naomba ingiza ndani"
Alizungumza madam lakini akili yangu na macho yangu yote yalikuwa yakimtazama mkaka huyo ambaye alikuwa mzuri mno, sijui niwaambie nini ili mnielewe lakini huyu mkaka ni mzuri mno.
"Tulinagwe unanisikia ??" Madam aliniuliza baada ya kuona nimeganda.
"Abeh, sorry umesemaje ??"
"Mmmh akili yako leo sijui iko wapi, nimekuambia kachukue mizigo kwenye gari yangu girl una nini leo "
"Oooh akili ilisafiri Samahani " nilijibu na kutoka nje.
"Gerald karibu sana na ujisikie upo nyumbani " madam alimkaribisha mkaka huyo.
Nilienda moja kwa moja kwenye gari na kuanza kutoa mizigo, yalikuwa ni mabegi ya mkaka yule ambaye alikuja na madam.
"Kwamba ameshindwa kubeba mabegi yake mwenyewe au ? Mijitu mingine bhana, dume Zima limeshindwa sasa mimi nabebaje mibegi mizito hivi " nililalamika tena kwa sauti na sio kimoyomoyo.
"Nikusaidie mtoto mzuri ??' Mlinzi aliniuliza.
"We nawe angaika na shughuli zako uko kwani nimekuomba au ??" Nilijikuta nikimfokea.
Niwaambie kitu, huyu mlinzi simpendagi ni mtu ambaye ananitaka kimapenzi lakini sikuwai kuvutiwa nae ata kidogo, sawa hisia uwa zinanisumbua lakini kwa huyu mkaka jamani nimeshindwa kabisa kukubali ombi lake.
"Oooh nilifikili unaitaji msaada wangu, samahani lakini " alijibu mlinzi na kutaka kuondoka.
"Sasa unaenda wapi si unisaidie jamani mkaka mzuri " nilianza kujibebisha maana mabegi yaliiitosheleza ujue.
Kwa msaada wa mlinzi niliweza kuingiza mabegi ndani na moja moja yakapelekwa kwenye chumba cha wageni.
Majila ya saa 2 usiku familia nzima tuliungana kwenye meza ya chakula na kila mtu alikuwa bize na chakula chake.
"Uku tunaendelea kula, nazani niendelee na utambulisho, maana tukimaliza kila mtu atakuwa na shughuli zake "
Alizungumza baba wa familia na sote tulitulia na kumpatia nafasi ya kuzungumza.
"Gerald, hii ni familia yako mpya kwa sasa, naitaji uwe huru, jisikie uko nyumbani sawa, hawa ni wadogo zako, ambao wanasoma boarding schools lakini wamerudi mara moja tu" alizungumza baba kisha akavuta glass ya maji na kunywa kidogo kisha akaendelea.
"Na huyu anaitwa Tulinagwe ni binti yetu wa hiyali ambaye tumeishia nae hapa kwa mikaa kadhaa, so hii ni familia yako yote.
"Baba umeanza vizuri ukaja kuharibu kwenye Tulinagwe " nilidakia.
"Nimeharibu nini sasa ??"
"Kwani si ungesema tu kuwa ni tuli, hii tulinagwe ilikuwa na sababu gani jamani ??" Niliuliza uku nikicheka cheka.
"Acha zako uko, ulikuja hapa kila ukiulizwa unajibu tulinagwe, sasa hivi utaki kulisikia " madam alijibu na familia nzima ikaanza kucheka.
"Aaah jina linashusha bland unajua ".
"Kwa bland gani bwana "
Kwakweli familia hiyo ilinifanya kuwa mtoto wao, nilijisikia amani, na niliajiachia sana, namtania kila mtu na maisha yanasonga kwa Amani na furaha ya hali ya juu.
"Haya jamani achaneni na maneno ya tulinagwe, umu ndani narudia sote ni ndugu, mambo ya kuja kusikia huyu kampenda huyu, huyu kampenda huyu sitaki kuja kuyasikia, jitunzeni ninyi bado wadogo mno " baba alizungumza.
Yaani baba katika speech zake hii ya kukataza mahusiano nahisi ndio point yake kubwa sana, amekuwa akirudia kila siku.
Kauli yake ni kama ilinikatisha tamaa hivi, maana nilianza kumuwazia mbali sana huyu kijana Gerald, muonekano wake tu ulijua kunichanganya sana.
********
Week nzima iliisha na hatimaye Gerald akaanza kwenda Shule na alikuwa ni kidato cha sita, Gerald ni kijana ambaye mtaratibu sana aliweka juhudi zake kwenye masomo.
Ila maisha yako tofauti sana, Gerald akiwa anapambana na masomo, kwa upande wangu nilikuwa na jina la Tully sipendi shule, lakini pia akili yangu ilikuwa inanituma kumtega tu Gerald wa watu.
Mara nyingi Gerald ndio amekuwa mtu wa kwanza kurudi nyumbani, na mara nyingi uwa tunakuwa wenyewe mpaka pale wazazi watakaporudi saa 2 usiku.
Ikiwa ni siku ya jumanne, majila ya saa 4 usiku, nilishindwa kabisa kulala nikajikuta nikitoka chumbani kwangu na kwenda chumbani kwa Gerald.
Niliwaza kugonga malango lakini niliwaza itakuwaje kama wazazi watasikia, nilichofanya ni kufungua mlango na kuingia ndani polepole.
Ile naingia tu uso kwa uso na Gerald ambaye aliganda akinishangaa uku akiwa ameshika peni yake mkononi ni wazi alikuwa akijisomea.
"Mbona ??" Gerald aliniuliza.
"Aaah, nilizani umelala na ukasahau kuzima taa so nikaja kuangalia ili nikuzimie "
"Aaah nawezaje kulala saa hizi, muda bado sana ni muda wa kujisomea"
Nilisogea polepole na kujikuta nikiwa nimeshafika karibu na Gerald, polepole nikakaa juu ya meza yake ya kujisomea Gerald alibaki akinishangaa tu.
"Gerald " nilimuita.
"Unaweza kuniita gee ni sawa maana naona unapata shida sana kutaja jina zima ".
"Aaah kweli wewe msomi umejua kunirahisishia nitakuwa nikikuita gee"
"Ouk" alijibu gee uku akinianglia usoni, kana kwamba ananiambia unaweza kushuka kwenye meza na kuondoka.
"Ila gee unanishangaza sana unapata wapi nguvu ya kusoma kama hivi ? Hivi unajua mimi kwetu walikuwa wananiita Tully sitaki shule ".
"Tully au Tulinagwe??" Aliniuliza Gerald na kwa pamoja tukajikuta tukicheka.
"Ukiniita ilo jina lako nakutoa kolomeo lako " nilizungumza uku nikiweka mikono yangu shingoni mwake. Walahi binti yenu sio kwa kujilengesha uku kwa kijana wa watu.
"Ahahahaha, nakutania tu, wait kwahiyo wewe hujasoma kabisa ?"
"Nimesoma, lakini kichwa changu ni box over box, unajua nimerudia kidato cha pili mara mbili na zote nikafeli "
Kidogo story yangu ilianza kumshawishi Gerald na kufunika daftari zake na kuanza kunisikiliza.
"Aaah kwahiyo ulikuwa ukifeli tu ??"
Kabla sijajibu kitu niliweza kusikia sauti ya madam ikiniitilia, kwa woga na wasiwasi nikasogelea kitufe cha taa na kuzima.
Muda huo huo, madam alisogea kwenye mlango wa Gerald na kuita.
"Gerald "
"Naaam "
"Tully umemuona au yupo uko ??"
Weeh niliogopa sana na kumwambia Gerald adanganye kuwa ajaniona.
"Hapana mama, sijamuona kwani chumbani kwake hayupo ??"
"Hayupo, jamani huyu binti ameenda wapi usiku huu "
Eeeh kina nilamba Mwenzenu, mniombee tu maana nilijikuta nikipata wasiwasi wa hali ya juu.
OUR STORY
MTUNZI: PATRICIA
SEHEMU YA: 02
Niliogopa sana na kutetemeka niliwaza madam atanifikiliaje akijua nipo chumbani kwa Gerald lakini pia Gerald amemdanganya.
"Kwanini utaki ajue kama upo uku ??' Gerald aliniuliza.
"Kaa kimya kwanza"
Baada ya muda nilisikia sauti ya mlango mkubwa wa nje ukifunguliwa ni wazi kuwa madam alienda kuniangalia nje, na hapo nilipata chance ya kutoka chumbani kwa Gerald na moja kwa moja nikakimbilia store.
"Usiku huu atakuwa wapi na simu yake apokei huyu binti jamani " madam alilalamika uku akirudi ndani.
Lakini pia na baba akatoka nje baada ya kuona kuwa ishu iko serious sana.
Nilijipaka paka vumbi la store kisha nikatoka, uku nikiwa na hema sana kuliko kawaida.
"Wewe jamani " madam alishtuka baada ya kuniona.
"Ulikuwa unafanya nini store saa hizi jamani ? " boss kubwa yaani baba aliniuliza kwa mshangao wa hali ya juu.
"Aaah nilikuwa naangalia fyekeo, ili kesho niweze kufyeka yale majani ya uku nyuma naona yanakuwa marefu sana, na kwakuwa nilitaka kufanya kazi hiyo asubuhi ndio maana nikaenda kutafuta fyekeo sasa hivi.
"Achana na hizo kazi, Tully wewe ni mwanamke sawa mama, tunajua ni mchapakazi, lakini kazi za nje kwa sasa utasaidiwa na Gerald kwa siku za weekend sawa " alizunguma madam.
Nyiee hii nyumba inajua nini maana ya utu na nini maana ya upendo, kwa mtu ambaye ajui kama mimi ni mfanyakazi umu ndani anaweza akaja na akajua mimi ni ndugu au ata mtoto wao wa kwanza.
"Anyway nilikuwa nataka kukuambia kuwa kesho, usiandae kifungua kinywa cha familia nzima, itakuwa ni kwaajili yako wewe, Gerald na kaka mlinzi hapo nje, mimi na baba tunaenda semina ya kanisani ambapo tutarudi jumatatu "
"Aaah kwahiyo miwaandalie nguo si ndio ??" Nilimuuliza madam.
"Nimeshaandaa "
*******
Hatimaye ni siku nyingine tena na ni siku ya jumamosi, madam na mumewe walijiandaa na kuondoka, nyumba nzima tulibaki watu watatu tu, nyie upwiru sio kitu kizuri kabisa muda wote nilibaki nikiwaza ni jinsi gani nitajiachia nikiwa na Gerald wangu.
Muda wote huo Gerald alikuwa nje akiendelea na shughuli ya kufyeka majani.
Majila ya mchana niliandaa chakula na kumpelekea kaka mlinzi, baada ya hapo nilipakua chakula changu na cha Gerald kisha nikaenda moja kwa moja chumbani kwake.
"Oooh Tully bhana, usingepata shida ya kuniletea chakula uku ningekuja uko uko "
"Ahaha usijali, najua umechoka mno lakini Pia unaitaji kujisomea si ndio "
"Yaaah kusoma muhimu, si unajua tena darasa la mtihani ili "
"Ni kweli, lakini hayo mambo yako ya kusoma kwangu hapana kwakweli, yaani mimi na kusoma ni maji na mafuta "
"Ahahah, unajua bhana kwa upande wangu elimu ni kila kitu, na sio elimu tu, mimi kuja kuwa mwanasheria mkubwa sana ndio kila kitu, naitaji kusoma na kuwa mwanasheria ambaye kila kona nitazungumziwa "
Alizungumza Gerald akionesha kumaanisha kile anachokizungumza.
Nilimkabizi chakula chake kisha nami nikakaa chini kabisa na kunyoosha miguu yangu ili niweze kula sasa.
"Daaah umenikumbusha mbali, shuleni ndio tulikuwa tunakaa hivyo kwaajili ya kupata chakula " alizungumza Gerald kisha akashuka chini na kukaa kama mimi.
Kuna namna fulani hivi niliona kumbe kumpata Gerald ni kazi rahisi sana sana maana ukijua vitu anapenda tu basi ni rahisi kuwa karibu nae.
Tuliendelea kula, uku story za hapa na pale zikiendelea.
"Unajua Mr John ni mtu mwema sana, baba yangu ana marafiki wengi sana lakini katika wote hao ni yeye tu ndio amenisaidia baada ya mimi kupitia matatizo mengi " alizungumza Gee kwa huzuni .
Niwakumbushe kuwa Gerald ndio Gee.
"Kwani kimetokea nini ??" Nilianza kumdadisi.
"Aaah, miezi 8 nyuma nimepoteza wazazi wangu wote wawili kwa ajali, lakini ndani ya miezi hiyo michache, watu wameweza kuharibu maisha yangu, Tully mimi ni mtoto wa kishua sana, lakini binadamu awana huruma, wamegawana mali za wazazi wangu pasi na kunifikilia, kitu walichoniachia ni mavazi yangu tu, nimeangaika sana, kila mtu ambaye alikuwa na ukaribu na baba amekataa kunisaidia, nashukuru Mungu Mr John amenipokea na kuchukua majukumu juu yangu"
"Tusema umezulumiwa mali baada ya wazazi wako kufariki ??"
"Yaaah, na ndio sababu kuu ambayo inanifanya niende nikasoma uwanasheria ili nipambanie haki yangu uku nikiwa najua nini nafanya"
"Usijali kila kitu kitakuwa sawa, Gee maisha yanatofautiana sana, mimi kwetu ni kijijini ndani ndani uko, utegemezi wetu ni kilimo, ingawa kuna elimu lakini sio sana, mimi ni mtu ambaye shule imenishinda, na baada ya kushindwa shule ndipo nikapata kazi za ndani katika nyumba hii, ni miaka sasa naishi umu ndani, nataka nikirudi kijijini kwetu niwe na pesa ya kutosha ili niweze kumsaidia mama yangu ambaye ameolewa na mwanaume mnyanyasaji"
Story zilikuwa nyingi mno jamani, ila nyie kumbe kutongoza mwanaume ndio kazi hivi, yaani nilibaki nikijiongelesha tu na kumlegezea Gee macho lakini ni kama alikuwa anielewi hivi.
Tulimaliza kula nikanyanyua sahani na kutaka kutoka nje, lakini nilisimama mlangoni na kumuuliza Gee.
"Kwamba ndio unaanza kujisomea muda huu au ??"
"Hapana, nitasoma usiku, saa hizi nipumzishe akili sasa "
"Twende jikoni basi ukanipe kampani "
Gee wa watu hakuwa na hiyana, akavuta ndala zake na kunifata, tulifika jikoni na alikaa pembeni uku mimi nikiendelea na zoezi la kusafisha vyombo.
Baada ya kila kitu, nilitumia mbinu zangu zote na kumfanya Gee kuja chumbani kwangu na mimi, ubaya wa chumbani kwangu, kulikuwa na kitanda, kabati la nguo na dressing table tu na hakukuwa na kiti hivyo Gee ilimpasa kuja kukaa kitandani.
"Siwezi kumkosa mkaka mzuri kama huyu " nilijiongelea kimoyomoyo.
Muda huo akili yangu yote ilikuwa ni kumpata Gee lakini ni kama alikuwa mzembe hivi, ni kama aelewi, hakuonesha kunitamani ata kidogo.
"Ulivyokaa hivyo mgongo hauchoki ??" Nilimuuliza Gee ambaye alikaa lakini akuwa ameegemea sehemu yoyote.
"Aaah usijali mimi ni mwanaume bhana, sema chumba chako ni kizuri sana "
"Asante, mambo ya madam hayo, Gee panda kabisa tu kitandani upate sehemu ya kuegemea "
Nilitumia uwanamke wangu na kumfanya Gee kupanda kabisa kitandani na kupata kuegemea kwenye ukuta.
Nilitumia wakati huo kujisogeza lakini pia kuweka kichwa changu kwenye mapaja yake.
"Unajua umu ndani nilikuwa nikipooza sana pindi wote wanapokuwa hawapo, lakini kwa sasa najisikia amani wewe upo hapa " nilijiongelesha.
"Usijali Tully mimi nitakuwa mtu wako wa karibu sana "
"Hivi kwa hivyo ulivyoama shule, mchumba wako wa shuleni si atakuwa anakumisi sana "
"Ahahah mchumba gani ? Weeh Tully sijui utanicheka sijui utanionaje ila sijawai kuwa na mchumba, baba yangu aliniambia nijiweke mbali na wasichana"
"Mmmh Gee wewe ni muongo jamani "
"Muongo wa nini, sijawai kuwa na mahusiano, ata hivyo nimekuwa nikisoma shule za boys tupu ".
"Eeeh kwahiyo ata mambo ya ta ta ta ujawai ??"
Ila mimi sio kwa haya maswali jamani.
"Sijawai" alijibu Gee na kuangalia chini kwani aliona aibu.
"Hapa napigwa na kitu kizito, mtu gentlemen kama wewe unawezaje kuwa singo halafu ujawai kufanya mambo matamu "
Kauli yangu kidogo ilimshtua Gee ambaye alibaki akiwa amenitolea macho tu.
"Usiniangalie kama hivyo ujue naona aibu mwenzio " nilimwambia Gee uku nikimlegezea macho.
"Mambo matamu unamaanisha nini ??" Aliniuliza.
"Gee acha zako, kwani wewe si umesoma mambo mengi uko eeeh kwenye biology nina uhakika mmesoma acha kunichora ujue "
Story za mapenzi na mahusiano yakashika nafasi yake, nilimpigia kila aina ya story ya mapenzi ili kumfanya mwili wake uchemke tu, maana anakuwaje mzembe kiasi iko.
Na kwa namna moja au nyingine zoezi langu lilianza kufaulu, Gee hana kigugumizi lakini kilianza kumshika, macho yake tu yaliongea kuwa hayuko sawa kwa wakati huo.
Tulinagwe mimi nikaona nafasi ndio hii sasa ni golden chance na sikutaka kuipoteza, nilitoa kichwa changu kwenye miguu yake na kumgeukia vizuri na kumuangalia usoni kwa muda kidogo ambapo yeye alishindwa kuniangalia alibaki akipepesa macho.
"Gee" nilimuita kwa sauti fulani hivi ambapo pia alishindwa kunijibu.
Niliamua kuweka aibu pembeni na kumkiss mdomo mwake, ukitaka kujua alikuwa akitamani kitu iko ni pale alipotulia pasi na kunikataza, lakini baada ya muda akawa anatoa ushirikiano.
Ila bhana, huu mchezo mbona atufundishwagi na tunaweza my zangu Gee aliweza halafu akaweza tena, nikawa najiapia mwenyewe kuwa siwezi kumuacha ata mara moja.
Baada ya lisaa limoja, kila mtu alikuwa amegeukia upande wake akihema juu juu.
Niliona aibu sana kumuangalia Gee, ila shetani huyu anakuongoza kufanya kitu halafu kikifanikiwa anakuacha ubaki peke yako, nilijikuta nikianza kujilaumu kwa jinsi ambavyo nimejilahisisha kwa Gee.
Niliinuka na kwenda bafuni ambapo nilikoga lakini pia niliona aibu kutoka nje kwani Gee alikuwa hapo.
Baada ya kujifikilia sana nikiwa bafuni nikaona liwalo na liwe, nilitoka Na kumkuta Gee akiwa amekaa wima akiangalia mbele tu.
"Kweli ni mambo matamu" alizungumza Gee.
Kauli yake ilinifanya nicheke sana, ila daaah hivi unawezaje kuwa kidato cha sita na haya mambo uyajui jamani.
Basi Gee akanishukuru pale na kuondoka, nilitulia nikijipongeza kuhusiana na jambo langu.
Tangu hapo mimi na Gee tukaanza mahusiano na niseme kuwa Gee ni man and half anajua kujali, anajua jinsi ya kuwa na mwanamke ni wazi kuwa wazazi wake walimfundisha jinsi ya kumuheshimu mwanamke.
Ukiachana na yote mahusiano yetu yalikuwa ya siri sana, ukizingatia mule ndani tuliambiwa sote ni ndugu hivyo hatukuruhusiwa kuwa na mahusiano.
Naweza nikasema kuwa mimi na Gee tuliishi kama mke na mume hivi maana ukiangalia muda mwingi tulikuwa wenyewe na tuliinjoy kama kwamba tumeowana au ni wamiliki wa nyumba hiyo.
Muda ulikimbia na Gee aliweza kufanya mitihani yake, na majibu yaliweza kutoka kuwa amefauru na utaratibu wa chuo ukaanza.
Mimi na Gee tulipanga mengi Sana, hivi mnajua tulipanga mpaka majina ya watoto wetu.
Nikiwa jikoni napika nilianza kujisikia hovyo kizunguzungu kama chote, niliogopa sana, na nilipopata muda wa kutoka nje nilienda kununua kipimo cha mimba na baada ya kupika kitu kimo, hii ni moja ya hasara za kujiachia ikiwa ujajipanga.
OUR STORY
MTUNZI: PATRICIA & RITHA
SEHEMU YA: 03
Niliogopa sana, na nilitamani kuzungumza na gee ili aweze kujua nini kinaendelea, ila sikupata muda kwani ilikuwa ni weekend na familia nzima ilikuwa nyumbani.
Muda wa mchana, baba aliita familia nzima na tukakutana sebuleni na kuanza kuzungumza.
"Aaah, nisiwachoshe sana, hapa nataka kuzungumza na Gerald tu lakini naitaji nyote muwe hapa mkisikiliza na muwe kama mashahidi pale chochote kikutokea"
Nilikuwa na wasiwasi sana, niliwaza au ameshajua kuhusu mahusiano yetu jamani.
"Aaah Gerald mwezi ujao unaanza chuo, mimi uwa sitaki kuongea kwa siri siri naitaji kuongea na wewe wazi wazi, unakoenda uko maisha ni tofauti, ukiwa chuoni ndio unaona kama umefika hivi, kule unajiona wewe ndio mwanaume, nikuambie tu kule nenda ukasome baba sawa ? Sikukatazi mahusiano kwasababu umeshakuwa mtu mzima, ila kuniletea mwanamke mwenye mimba hapa ndio itakuwa mwisho wa mimi kukusaiidia"
Kamoyo kangu kakafanya paaaah, yaani najiandaa kumwambia Gee kuwa nina mimba yake halafu anapewa maneno kama hayo, niliishiwa nguvu ndugu yenu.
Baada ya kumaliza maongezi kila mtu akaendelea na shughuli zake. Majila ya usiku nikiwa chumbani kwangu Gee alikuja akiwa na furaha zake kama zote.
"Aiseeeeh hatimaye ndoto zangu za kwenda chuo zinatimia "
"Yaah Mungu ametenda hongera sana mpenzi wangu "
"Asante, but Tully ni kama hauko sawa mpenzi wangu "
"Amna bhana, niko sawa, ila nawaza utakavyoenda kukutana na wanawake wazuri uko chuoni" niliamua tu kumdanganya.
Gee alinisogelea kisha akaweka kichwa changu kwenye kifua chake na kuzungumza.
"Tully, naomba ujue kuwa nakupenda mno, wewe ndiye mtu ambaye umeniingiza kwenye dunia hii ya mapenzi na nataka safari yangu nimalize nikiwa na wewe sawa mama "
Daaah nilitamani ata kulia, nilikuwa Njia panda, niliwaza kumwambia kuhusu ujauzito lakini niliona kama ni kuchanganya akili yake, ukiachana na kuchanganya akili yake niliwaza pia kumpotezea nafasi ya kusomeshwa.
Kama ujuavyote tena mimba ni kama pembe la ng'ombe kufichika sio rahisi kabisa, hatimaye ujauzito wangu ulifikisha miezi mitatu na lilikuwa likionekana.
Yaani lilionekana mno sijui kwa sababu nilikuwa na tumbo flat maan daaah lilichomoza sana.
Baada ya kujulikana kuwa ni mjamzito, niliwekwa kikaangoni na kuulizwa baba wa mtoto ni nani, nilitamani kumtaja Gee ambaye alionekana kuogopa sana, lakini pia niliogopa kuvunja matamanio yake ya kuwa msomi mkubwa.
"Tully, tulikuamini sana sana, miaka yote umekaa umu ndani lakini leo hii imekuwaje eeh ? Kwamba umeona umeshakuwa tayali kubeba majukumu ya mama ??" Madam aliniuliza kwa huzuni mno.
"Hapana madam" nilijibu uku nikiangalia chini.
"Unalia nini sasa eeh ? Muhusika wa ujauzito huo ni nani ??" Baba alinifokea.
Niliogopa sana, kwa upande wa Gee aliniangalia sana usoni kisha, akawa anasogea mbele ili kujitaja lakini nilimuwai na kusema.
"Ni mkaka wa kule sokoni juu, anaitwa Thomas "
Maneno yangu ni kama yalimfanya Gee ku pause alisimama na kubaki akiwa ametoa Macho.
"Niseme kuwa sina msaada na wewe, haya mambo tulishazungumza, nafikili muda wa wewe kwenda kuanza maisha yako na mwanaume wako umefika, na ukizingatia saa hizi ni mapema sana" Alizungumza baba.
"Lakini mu..." madam alitaka kuzungumza jambo lakini baba akusikiliza zaidi akaniamuru niende kupaki mizigo yangu kwaajili ya kuondoka.
Niliingia chumbani kwangu nikiwa nimechanganyikiwa, niliwaza nitafanyaje, nikiangalia akiba yangu haikuwa kubwa kwani pesa nilikuwa nikituma kwa mama ili aweze kukidhi mahitaji yake na watoto maana mama alikuwa na watoto wadogo wapatao wanne, yaani wadogo zangu walikuwa wamefatana sana.
Nilichukua begi langu na kuanza kupanga nguo, Gee alikuja chumbani kwangu kwa pupa, akanivuta na kunifanya niiinuke kwani nilikuwa nimekaa kitandani.
"Ni nini umeongea pale nje ??" Gee alinifokea.
"Kwani haukuwa umenisikia ??"
"Tully usinijibu kama hivyo, nambie hiyo mimba ni ya nani ??'
"Kwani si nilishamtaja Muhusika pale nje"
"Usinijibu kama hivyo, kwahiyo unataka kusema ulikuwa ukinicheat au ? Tully mbona unanifanya nikuone wa hovyo sana, yaani unataka nikuoneje mimi "
"Nione kama unavyotaka lakini hii mimba sio yako am sorry "
"Usiniambie kama hivyo, sema nini nakuchukia Tully, nakuchukia mno "
Gee alitoka nje kwa hasira lakini pia machozi yalikuwa yakimtililika.
Nilimaliza kupanga nguo zangu na kwenda kuaga, madam aliniangalia kwa upole sana lakini hakuwa na namna mwanaume ndio ameshasema hivyo.
Nilitoka nje nikiwa na huzuni sana, niliumia mno lakini sikuwa na namna, nikiwa nje ya geti kabisa gafla akaja Gee ata sijui umo ndani aliagaje na kuja kunikimbilia mimi.
"Tully, Tully " Gee aliniita mfululizo lakini sikutaka kuitikia zaidi nilisimamisha bodaboda iliyokuwa ikipita chap nikapanda na kuondoka.
Kwakuwa muda ulienda sana niliamua kufikia kwenye nyumba ya wageni ili niweze kutuliza akili, na kujua nini nafanya sasa.
Kwa namna moja au nyingine nilijilaumu mwenyewe, maana nilishindwa kuzuia hisia zangu na kumuingiza Gee mwenye dunia ya mapenzi na kumfanya anipende sana, ukiachana na kunipenda nimembebea na mtoto ikiwa yeye pia anasaidiwa.
Niliamua tu kujiukumu mwenyewe kwaninjilistahili, hivyo niliona ni sawa tu kumuacha Gee atimize ndoto zake kwanza.
********
Siku iliyofuata niliweza kupata gari ya kurudi nyumbani kwetu, yaani kijijini, kwenye gari nilikuwa nina mawazo sana, niliwaza muhitasari wa maisha yangu unaenda kuwaje, niliwaza ile roho mbaya ya baba yangu wa kambo ambaye alikuwa akituchukia waziwazi mimi na mdogo wangu, ambaye sio mtoto wake.
Mungu aliweza kusaidia na hatimaye nikafika kijijini kwetu, katika moja na mbili nilifika nyumbani kabisa, mama alifurahi sana kuniona, alinipokea kwa furaha isiyo kifani si unajua mama ni mama.
Kwa muda ambao nilikuwa nimefika baba sikuwa nimemkuta hivyo nilipata muda wa kuzungumza na mama yangu.
"Tulinagwe mama, ndio umeenda kufanya nini jamani, eeh tazama mambo yenyewe sio mambo, kula yetu ni ya shida sana, baba yako kama unavyomjua anajali sana pombe kuliko chakula"
"Mama huu sio muda wa kunilaumu, nina imani nitajua nini cha kufanya ikiwa kama wewe utakuwa upande wangu"
"Siwezi kukuacha mama sawa, wasiwasi wangu ni baba yenu si mnamjua jamani "
"Usijali mama baba nitaongea nae mimi, najua atanielewa tu "
Majila ya usiku baba yangu wa kambo alirudi nyumbani akiwa amelewa sana, matusi kama yote alilalama na kulalama, na muda wote huo hakuwa anajua kama mimi nimerudi.
********
Ikiwa ni siku nyingine tena niliweza kuamka asubuhi na mapema na kuanza kufanya shughuli za usafi wa pale nyumbani, nikiwa bize nafagia uwanja, baba aliweza kuamka na kunikuta nje nikiwa nafanya usafi.
"Eeeh wewe, unajua jana mama yako alivyosema umerudi sikuwa nimemuamini kabisa " alizungumza baba yangu huyo akiwa na tabasamu pana kabisa.
Niliinuka na kumpatia heshima yake, lakini alishtuka sana baada ya kugundua kuwa mimi ni mjamzito.
"Eeeh umekuja na mkwe nini ??" Baba aliniuliza.
"Aaah hapana baba ni story ndefu lakini kila kitu kitakuwa sawa"
"Kila kitu gani ? Kwamba mwanaume amekutelekeza au ??" Aliuliza baba tena kwa sauti ya juu sana ambayo iliweza kumuamsha mama ambaye alikuwa amelala.
"Aaaah jamani, mbona ni asubuhi sana na mnapigizana kelele " alizungumza mama akitaka baba atulie.
"Napiga kelele sio ? Huyu binti yako amekuja na kitu gani hapa ? Eeeh anawezaje kurudi akiwa katika hali hii ? Mwanaume wake yuko wapi "
"Aaah ndio kwanza asubuhi, tupate kifungua kinywa kisha tutazungumza mume wangu sawa "
"Naona amnielewi nyie watu, iko hivi, kama hii mimba haina baba siwezi kumruhusu huyu binti yako akae hapa, alikataa shule mwenyewe na alienda mjini kwaajili ya kazi kwahiyo huu ndio mshahara au ? Nimekulea wewe, nalea mdogo wako ambaye baba yenu aliniachia, ila siwezi kulea huyo mtoto wako, naenda uku nikirudi nisikukute"
Alizungumza baba kwa hasira sana na hakutaka ata kunisikiliza kwa mwendo wa haraka na ule urefu wake akaondoka.
Nyieeeh nilihisi kuchanganyikiwa nguvu ya kufanya usafi yote iliniisha, kwa mwendo wa polepole na unyonge nilisogea chini ya mti na kujiweka chini maana nilihisi kuishiwa nguvu miguuni.
Mama ni mama jamani, ukiachana na kila kitu alikuwa karibu yangu kwaajili ya kunituliza, na kunipa moyo.
Baba alikuja kurudi majila ya saa 12 jioni, na alirudia akiwa amelewa chakali, aliponiona akaanzisha fujo ambayo haikuwa ya kawaida na kufanya watu kujaa.
Mama alikuwa mbelembele akinitetea lakini hakufua dafu zaidi aliambulia kipigo cha kufa mtu.
"Naona unanichezea wewe, cha kufanya beba watoto zako wote na uwende sitaki kuwaona tena "
Eeeh nimekuja kuleta shida nyumbani, mama na hawa watoto wote tunaenda wapi jamani. Nilijifikilia kwa muda kisha nikasema.
"Baba, haina haja ya kumfukuza mama, Aaaah mimi nitaondoka "
Mama alilia sana lakini hakuwa na chaguo ukiangalia ata Akiondoka na mimi tutaenda kukaa wapi jamani eeh, yaani tutaenda wapi au ndo tuanze kuwatesa tu watato.
Niliingia ndani na kuchukua mabegi yangu, na kuanza kuondoka nikiwa sijui naenda wapi.
Mmoja kati ya wamama, alinichukua na kuniifadhi nyumbani kwake kwani jua lilikuwa lishazama.
"Kesho utaondoka, maana siwezi kukuifadhi siku zote uku nitakuja kupata shida kwa majilani zangu, lakini pia baba yako awezi kunielewa kabisa "
"Sawa shukran sana " nilimshukuru mmama huyo.
*********
Niliweza kustilika kwa usiku mmoja na siku iliyofuata nilishika njia na kuanza kuondoka.
Nilitembea na kuzunguka uku na uku pasi na kujua ni wapi nitaenda, nilitamani kwenda ata kwa rafiki zangu, lakini wengi awakuwepo tena pale kijijini.
Nilizurula mno, na njaa pia haikuwa mbali nami, si mnajua tena mama vijacho na njaa, halafu mambo ya kijijini biashara ya chakula cha kupikwa sio kama mjini.
Hatimaye baada ya kuzurula sana, niliweza kufika kwenye kijiji cha pili, ambapo niliweza kupata ata ndizi za kuchemsha na nikala.
Shida nyingine ambayo niliipata ni ya mtandao, yaani simu yangu ilikuwa kama bosheni hakuna mtandao ambao ulisoma, na ukizingatia ilikuwa ni simu ya kibatani.
Raha ya kijijini bhana, kuna vile vibanda banda vinavyobakigi baada ya wenyewe kuama au kufariki, niliweza kupata ka kibanda ambacho hakikuwa na mwenyewe na kilikuwa kimejitenga sana na makazi ya watu, niliona kuwa kitanifaa sana kwaajili ya kujistili ingawa nilikuwa na wasiwasi itakuwaje wenyewe wakija kunitoa.
*****
Hatimaye nilianza maisha yangu rasmi kwenye kibanda cha watu ambacho sikuwa na imani nacho, maana niliwaza kuwa naweza nikatolewa muda na saa yoyote ile.
Nilikaa kama miezi mitatu hivi, na kitumbo changu kilikuwa zaidi, ilikuwa ni hatari sana, kwani nilikuwa mwenyewe lakini pia sikuwai kuudhulia clinic ata siku moja.
Ukiacha na kila kitu, sikuwa nikila chakula cha kueleweka, yaani ni ndizi, muda mwingine Mahindi kutokana na pesa ambayo nilikuwa nayo na nilikuwa nikiitumia taratibu sana sana.
Ikiwa ni majila ya mchana, nimejilalia zangu kutokana na uchovu wa hali ya juu, niliweza kusikia sauti za watu wakizungumza lakini pia kuzunguka uku na uku, kwa wasiwasi nikatoka nje.
"Eeeh na wewe ni nani ??" Aliniuliza moja kati ya watu hao na alikuwa Ni mkaka ".
"Aaa naitwa Tully"
"Sitaki kujua jina lako, unafanya nini kwenye nyumba ya babu yangu ?"
Eeh yaani siku ambayo nilikuwa nikiiogopa isije ikafika hatimaye imeweza kufika.
"Fungasha kila kilicho chako na uondoke, watu kama nyie amshindwi kusema kuwa ni kiwanja chako "
"Hapana, nimejiifadhi tu kaka angu naomba unistili "
"Nazunguka uku nikirudi nisikukute binti sawa "
Nikaona mambo yasiwe mambo, nilifungasha begi langu na kuingia tena mtaani, nilitembea mno na mwisho niliweza kufika mtoni ambapo nilikaa kwa muda mrefu sana mpaka giza liliponifika.
Giza lilianza kushika nafasi yake, lakini pia miungurumo radi na manyunyu ilikuwa sambamba kabisa.
Niliogopa sana lakini sikuwa na chaguo zaidi ya kutulia tu hapo mtoni, maana nilichoka kutembea na njaa ilikuwa ikiniuma sana.
"Utakaa hapa mpaka saa ngapi ?" Ilikuwa ni sauti ya kike lakini ya kizee.
Kwa wasiwasi niliinuka na kuanza kuangalia sauti ilikuwa ikitokea wapi, na baada ya kuangalia kwa muda niliweza kumuona mtu ambaye aliniuliza na alikuwa ng'ambo ya pili ya mto.
"Mto huu ukifulika sizani kama utaweza kutoka uku na ni hatari sana " bibi huyo aliendelea kuzungumza.
Nikaona huyu huyu ndiye mtu wa kumuomba msaada maana sioni kama naweza kupata msaada mwingine ikiwa giza tayali limeshia nafasi yake.
Kwa mwendo wa taratibu nilianza kusogelea mto ule ili niweze kuvuka na kufikia alipo yule bibi, ila giza ni giza, niliweza kukanyaga jiwe ambalo liliniangusha na kunifanya nitumbukie ndani ya maji nikiwa nimepoteza fahamu kwani niliweza kujigonga kichwani.
OUR STORY
MTUNZI: PATRICIA & RITHA
SEHEMU YA: 04
Nilikuja kuamka siku iliyofuata, na nilikuwa ndani ya kibanda, niliinuka na kuanza kushangaa uku na uku lakini pia jua lilikuwa limeshaanza kuchomoza, na kalikuwa ni kale ka jua ka asuhuhi.
Nilihisi maumivu makali sana ya kichwa, nilijikaza nikainuka na kutoka nje ili niweze kujua niko wapi, nilishtuka na kuogopa baada ya kuona kuwa niko mistuni..
Haukuwa msitu mkubwa sana lakini majani na miti yalileta giza na kuogofya, nilizunguka uku na uku kwa wasiwasi pasi na kuona mtu, sauti ambazo niliweza kuzisikia niza ndege tu.
Niliweza kukaa kwa muda kwa kukadilia naweza kusema labda ni lisaa limoja hivi, ndipo alikuja bibi yule ambaye nilionana nae kule mtoni.
"Hatimaye umeamka " alizungumza bibi huyo.
"Shikamoo bibi " nilimsalimia.
Nilipata wasaa wa kuzungumza na kikongwe huyo, sikuwa na sababu ya kumficha chochote maana kwa muda huo niliitaji msaada wake sana.
"Ilikupasa kumwambia ukweli muhusika wa mimba hii, labda mngepata suluhisho " alizungumza bibi huyo baada ya mimi kumsimulia mkasa wangu wote.
"Nisingeweza bibi, kumwambia ukweli ilikuwa ni kwenda kumuharibia maisha yake "
"Na ukaishia kuharibu maisha yako, unajua bhana nyie vijana mna mambo mengi sana aswaaah uko mjini "
"Ni mitihani ya maisha tu bibi "
"Ni mitihani ya kujitakia"
Bibi huyo alijua kunisema bhana, na kuna namna niliona kama nilikosea sana kutokumwambia Gee ukweli lakini mambo ndio yameshatokea hivyo.
Baada ya maongezi bibi alijitolea kunisaidia na hapo nilianza maisha yangu upya na bibi huyo.
Tuliweza kupanda mboga mboga ambazo zilitusaidia kwenye misosi.
"Lakini bibi kwanini unakaa mwenyewe uku kwenye misiti na sio kule kwenye vijiji?"
"Ni maamuzi ya amani ambayo niliyataka "
"Lakini...."
"Hakuna cha lakini, haya ni maamuzi yangu mimi sawa Tully "
Eeeh nikaona nifyate tu mdomo wangu maana bibi ni kama kapaniki hivi.
*******
Muda uliyoyoma na miezi kukimbia hatimaye, siku ya kujifungua ilifika nyie, kumbe ndio uchungu uko hivi, yaani maumivu ambayo niliyapata nilijikuta nikijiambia kuwa sizai tena.
Nilipata maumvu ambayo hayakuwa ya kawaida, nashukuru bibi alikuwa bega kwa bega na mimi, alihakikisha kuwa najifungua salama.
Nilitumia takribani masaa mawili maana zoezi lilikuwa gumu sana, bibi alikuwa mzoefu sana, lakini mimi pia kwa upande wangu sikuwa nimepata mafunzo kutoka kwa mtu yeyote yule.
Yote kwa yote, niliweza kujipatiwa watoto zangu watatu, ambapo mwanamke alikuwa ni mmoja na wanaume wawili.
Ni jambo la kushangaza lakini kwa uwezo wa Mungu niliweza kujifungua watoto watatu tena kwa njia ya kawaida.
"Eeeh ni nini iki jamani,.eeeh Mungu kwanini mimi jamani eeeh kwanini eeeh " nilijikuta nikianza kulia kwa sauti ya hali ya juu sana.
"Unalia nini badala ya kufurahi kuwa umejifungua salama salimini "
"Bibi napataje furaha mimi eeeh, yaani kwenye mtihani nimeongezewa mtihani, mimi mwenyewe tu nimeshindwa kujisaidia halafu saa hizi napata watoto watatu kweli jamani "
"Hahaha una vituko sana wewe, umenishtua sana na iko kilio chako " alijibu bibi na kuanza kunicheka "
"Aaa kama tutapata watu wanataka kununua watoto nitauza wawili me siwezi kulea watoto watatu "
"Jinga sana wewe "
*******
Upande wa mjini anaonekana Gee akiwa chuoni, na kwa kipindi iki alizoeleka sana pale chuoni kutokana na kuwa mcheshi sana.
Gee alionekana akiwa ameshikilia picha za watu kadhaa na kati ya picha hizo picha ya Tully ilikuwepo.
"Labda uwe umekufa lakini kama upo duniani Tully nitahakikisha unajutia kucheza na maisha yangu" alizungumza Gee kimoyo moyo.
Muda huo huo alionekana msichana fulani hivi, umbo namba nane, ka rangi fulani hivi cha mtume ambacho kilimfanya ainekane mrembo zaidi.
Msichana huyo alisogea mpaka alipo Gee kisha akamziba macho kwa nyuma na kusema.
"Otea ni nani ??"
"MY baby " Gee alijibu uku akitoa mikono ya msichana huyo kwenye uso wake.
"Aah umejuaje kama ni mimi baby " alizungumza msichana huyo na kusogea mbele ya Gee kisha akakaa mapajani mwake.
"Vai bhana, hivi unafikili kwa jinsi ninavyokupenda hivi nitashindwa kukukalili kweli jamani "
"Ooooh jamani, me ndio maana nahisi kuchizika na penzi lako " Alijibu msichana huyo kwa kudeka.
Gee na vai walionekana kuwa ni watu ambao wanapendana sana na mapenzi yao yalikuwa moto moto, mahusiano yao walifanya wazi wazi na kufanya baadhi ya wanafunzi kujua kuwa wao ni wapenzi.
*******
Hatimaye kwa uwezo wa Mungu watoto wangu waliweza kufikisha umri wa miezi sita, na kwa msaada wa bibi huyo niliweza kuwalea watoto wangu vizuri kabisa na waliweza kuwa na afya ya kutosha.
Ikiwa ni majila ya saa4 asubuhi, niliamka na kwenda kuchimba mihogo ili niweze kuandaa kwaajili ya chakula cha mchana, gafla akaja bibi akiwa mbio mbio na alikuwa akihema kwa kasi Sana na alionekana kuwa na wasiwasi wa hali ya juu.
"Bibi kuna nini ??" Nilimuuliza bibi baada ya kumuona kuwa hayuko sawa.
"Chukua watoto wako na muondoke, awa watu watakuja kukudhuru na wewe bure "
"Watu gani tena bibi ?"
"Tully huu sio muda wa maswali, ni muda wa wewe kubebelea watoto wako na kuondoka, nina imani utapata msaada uko mbele, lakini kwa mimi leo sizani kama napona, awa watu siwezi kuwakimbia kabisa "
"Basi tuondoke wote "
"Tully ondoka utakiwi kuonekana ukiwa na mimi "
Niliogopa sana lakini pia niliitaji kujua ni kwanini ananiambia hivyo na hao watu kwanini wanataka kumdhuru.
"Uchawi unaniponza mimi, Tully mjukuu wangu nimekuwa nikitumikia uchawi tangu nikiwa na umri wa miaka 15 baada ya bibi yangu kufariki na kuniachia mimi, sio kazi ambayo nilikuwa nikiipenda lakini cheo ambacho alikuwa nacho bibi yangu ndicho kilinifanya nitumikie kazi hiyo, kuuwa watu kwangu ikawa kawaida, na watu kijijini walinichoka na kutaka kuniua na ndio sababu ya mimi kuja kujitenga uku, lakini kwa sasa mtoto wa mwenyekiti amefariki na wananchi wanafukili ni mimi nahusika, mimi sihusiki lakini najua awawezi kunielewa wameshajua wapi nilipo na sina nguvu ya kuwakimbia kwa sasa"
Mmmh nikaona hapa kweli huu ni msala, niliingia ndani na kubeba watoto wangu, wawili niliwafunga mgongoni ingawa kwa kuwabana sana, na mmoja nikamfunga kwa mbele.
"Bibi unaweza kujikaza na tukakimbia wote "
"Siwezi na nitakuponza "
Kabla sijaendelea kumshawishi bibi, tuliweza kusikia kelele za raia na walikuwa wakisogea kwenye eneo ilo, nilitoka mbio, kwa jinsi ambavyo nilikuw anikikimbia unaweza ukasema kuwa nilikuwa sijabeba kitu mwilini mwangu.
Nilikimbia mno, na nilipohakikisha kuwa niko mbali na watu wale niliweza kutulia chini na kunyonyesha watoto wangu ambao walikuwa wakilia sana.
Niliwanyonyesha watoto wangu nikiwa nalia mno, kuna muda niligundua kuwa nilikuwa nalia sana kuliko hao watoto wangu.
Baada ya kuwaza na kuwazua kwa muda wazo ambalo lilikuja kichwani mwangu ni kimi kwenda kwa mama yangu uku nikijipa moyo kuwa nitapokelewa.
Nilibeba tena watoto wangu na safari ikaanza, nilitembea kwa kuchoka mno, na ukijumlisha na njaa nilihisi kukata tamaa, lakini kila nilipowaangalia watoto wangu nilipata nguvu ya kupambana kwaajili yao.
Majila ya usiku sana niliweza kufika kijijini kwetu, na kulikuwa kimya sana kwani watu walishalala, nilienda nyumbani kwetu na kugonga mlango sana tu pasi na kuitikiwa wala kufunguliwa.
Kwakuwa nyumba yetu ilikuwa na kibanda cha jiko ambacho kilikuwa kwa nje, niliweza kusogea nikaweka mambo vizuri na kulaza watoto wangu ambao walichoka mno, awakuweza ata kulia.
********
Asubuhi niliamka na kutoka nje, ili kujiami pale tu nitakapokutana na baba maana yeye ndiye mtu ambaye niliamini kuwa ataleta shida.
Nilikaa kwa muda mrefu pasi na mtu kutoka nje, na hapo niliamua kusogea na kugonga sana lakini pia kulionesha kuwa na dalili ya kutokuwa na mtu Ata mmoja.
Nilibeba tena watoto wangu na kwenda kwa yule mama ambaye alinisaidia siku ile ambayo baba alinifukuza.
"Eeeh jamani wewe baraka iliyoje watoto watatu jamani " Alizungumza mama huyo baada ya kumaliza salamu.
"Eeeh ndo hivyo mama angu, sasa nilienda pale nyumbani lakini naona kama hakuna mtu hivi, tangu jana usiku"
"Aaah ni miezi minne sasa nyumbani kwenu hakuna mtu anaishi Pale "
"Wameama au ??'
"Kwa taarifa za juu juu baba yako ameenda mjini, lakini mama yako alifariki kipindi kile kile ambacho wewe ulifukizwa "
Nilishtuka sana, yaani mama yangu Anafariki na kuzikwa nikiwa sina taarifa, nililia mno, nilikumbuka macho yake ya huruma aliyokuwa akinitazama siku ile ambayo nilikuwa nikiondoka nyumbani.
"Na vipi kuhusu wadogo zangu ??" Niliuliza ili niweze kupata taarifa kamili.
"Wale wadogo wapo kwa bibi yao mzaa baba, lakini huyu Tusajigwe yupo kwa mwenyekiti maana hakuwa na sehemu ya kwenda "
Kama ni mapito basi haya ya kwangu yamezidi, maumivu ambayo nayapata moyoni mwangu ni makubwa mno.
"Na pale nyumbani anakaa nani sasa ??" Niliendelea kuuliza.
"Eeeh baba yenu aliuza mbona "
Nilichoka ndugu yenu, kwakuwa, hatukuwa na sehemu ya kwenda mama yule aliamua kutustili maana mwanzo alikuwa akimuogopa baba.
Nilikaa nyumbani kwa mama huyo takribani miezi sita uku nikijishughulisha na vibarua vya kulima lima pale kijijini, muonekano wangu ulibadilika mno, nilipauka kuliko kawaida.
Niliweza kuifadhi kiasi cha pesa kwenye kila kazi ambayo nilikuwa nikifanya, na nashukuru Mungu niliweza kupata pesa ambayo niliweza kupanga chumba changu mwenyewe, lakini niliamua kwenda kupanga mjini na niliweza kumchukua mdogo wangu Tusajigwe ambaye nilikuwa nikimuita tusa.
Maisha mapya yakaanza nikiwa mjini jijini mbeya, mitaa fulani hivi ya uswazi, Tusa alinisaidia sana kwenye kutuza watoto kwani nilipoingia mjini niliweza kupata kazi ya kuuza bar.
Nilifanya kazi kwa juhudi sana, na watu walinipenda sana, niliweza kupata vile vi keep change nini, na hapo nilianza kujinunulia ata vinguo vya mtumba ili niweze kuendana na mazingira ambayo nilikuwepo.
Kuna namna Mungu alianza kunimulikia njia zangu, pesa zilianza kuja kwangu na kunifanya nianze kuishi maisha kama ya watu wengine, watoto wangu ata wakaanza kuonekana maana daah walikuwa wamepauka sana.
OUR STORY
MTUNZI: PATRICIA
SEHEMU YA: 05
Nikiwa kazini na ilikuwa ni siku ya weekend, wateja walikuwa kama wote, magari yalikuwa yakutosha mziki mnene.
Siku hiyo kulikuwa Hakuna kupumzika kwakweli, maana niliingia kazini asubuhi na nilitakiwa kutoka saa 10 jioni lakini kutokana na wateja kuwa wengi, boss akanitaka ku double uku akiahidi kuniiongezea pesa na kwakuwa nilikuwa na uhitaji wa pesa nikaamua kubaki.
Majila ya saa 5 nilikuwa nimechoka mno, lakini wateja waliendelea kumiminika na kunifanya nizunguke uku na uku, katika kuhudumia, mmoja kati ya wababa aliweza kunipatia business kadi uku akisisitiza niweze kumtafuta.
Nilichukua kadi na kuifadhi vizuri kisha nikaendelea na kazi zangu, kwa mara ya kwanza tangu nimeanza kufanya kazi hiyo, siku hii ndio nilirudi nyumbani nikiwa na pesa ya kutosha.
Nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana lakini kila nilipoangalia ile pesa, nilibaki nikitabasamu tu.
Asubuhi niliweza kuingia sokoni na kununua zagazaga aswaah ni lishe ya watoto wangu, maana nilitamani sana wawe na afya nzuri na mionekano mizuri.
*******
Siku iliyofuata niliingia kazini na kuendelea na majukumu yangu.
"Shoga angu jana alikuja baba fulani hivi amekuulizia sana " Alizungumza shoga yangu ambaye tulijuana hapo hapo kazini.
"Mbona mbaba shoga angu ??"
"Ndo hivyo ni mbaba, jana alikuwa na watu wake kwenye meza ile ya nyuma ambayo haina taa, mpaka ukawa unasema ile meza wamejua kutumia pesa "
"Aaah kumbe yule, hivi sijakuambia, juzi alinipatia business card yake lakini sijamtafuta, shoga angu mimi na wababa wapi na wapi jamani "
"We jishaue eti wapi na wapi, shoga angu sasa hivi wababa ndio mpango mzima, kwanza wanajua kujali na kuthamini mwanamke, jaribu bahati yako shoga angu, mtu mwenyewe anaonekana pesa ipo "
"Naogopa wababa mie "
shoga angu alijua kunijaza bhana, alionekana kuwa na uzoefu sana na wababa, na kuna muda niliona kama ni sawa tu maana umri pia unaenda tu na sijui nitapata wapi mwanaume wa kueleweka.
********
Upande wa Gee alikuwa alikuwa ameshapata kazi na maisha yake yalikuwa mazuri sana, aliweza kujimudu na alitoka kwenye ile familia ambayo iliamua kumsaidia.
Ndani ya jumba moja kubwa matata kabisa, anaonekana Gee akiwa ndani ya nguo za kulalia, akiwa amekaa kwenye sofa akiangalia movie kwenye TV moja kubwa sana.
Gee aliinuka kochini na kusogelea moja ya picha ambazo alikuwa amening'iniza kwenye ukuta wa pale sebuleni kwake.
"Tully " Gee aliita, kisha akanyoosha mkono wake na kupapasa uso wangu kwenye picha kibwa aliyoitundika.
"Uko hai au umekufa ? Tully kwanini umeniingiza kwenye shimo ambalo nashindwa kutoka, kwanini unanifanya niwachukie wanawake wote, kwanini bado moyo wangu unakufikilia wewe, uko wapi mama " Gee alilalamika kwa kuzungumza na picha yangu
Muda huo huo, alionekana msichaana fulani hivi akiwa kwenye mavazi ya kulalia, alikuwa ni mwanamke ambaye ameumbika sana, alikuwa na nyashi ya kutosha.
Msichana huyo, alikuwa bi tofauti kabisa na msichana ambaye Gee alikuwa akidate nae wakiwa chuoni.
"Baby " ilisikika sauti nyororo kabisa ya msichana huyo ambaye alisimama nyuma ya Gee, lakini pia hakuishia tu kusimama kwani alimkumbatia Gee kwa nyuma.
"Nilipofika nilikuuliza huyu ni nani babe wala ukunijibu " alizungumza msichana huyo kwa kudeka uku akimpapasa papasa Gee.
"Aaah ni sister angu ambaye tumepotezana kwa miaka mingi " alijibu Gee uku akiendelea kukazia macho kwenye picha yangu, kisha akashushia na wine ambayo alikuwa nayo mkononi kwenye glass zile zenye kiuno kirefu au uku kwetu uwa wanaita shingo ya twiga.
********
Upande wangu niliendelea kupiga kazi, kwani ndio kwanza ilikuwa ni saa 4 usiku, baridi ilindelea kunipiga na kunifanya nijikunyate kama kitoto cha mbuzi.
Siku hiyo hakukuwa na wateja wengi, na ata niliweza kukaa chini, wateja wenyewe wa siku hiyo walikuwa wateja uchwara tu, mtu bia moja analamba lamba lisaa lizima ndipo anaagiza nyingine.
Nikiwa nimejikunyata kwenye kiti na kujiinamia chini kutokana na baridi, nikishtuka sana baada ya mtu kuja nyuma yangu na kunifunika kwa blanket zito kabisa la manyoya manyoya.
Kwa jazba niliinuka na kulitupiga blanket lile pembeni.
"Ooooh ni wewe " nilizungumza kwa upole baada ya kumuona mtu ambaye alikuja kunistili kwa blanket.
"Pole naona nimekustua sana "
Mtu huyo alikuwa ni yule baba ambaye siku moja nyuma alinikabizi kadi yake ya mawasiliano na sikuweza kumtafuta.
"Karibu sana Mr deo " nilimkaribisha uku nikimuachia tabasamu pana kabisa.
"Asante, pole naona baridi inakushambulia vilivyo "
"Aaah kawaida, si unajua tena nipo kazini, aaah nikuhudumie nini leo au kama siku zote ??"
"Aaah, kwa leo naomba tu maji ya moto, maana naona leo baridi imeamua kupuliza bhana, hivyo maji yatanitosha kabisa "
Basi niliweka lile blanket pembeni na kwenda kumchukulia maji yake.
Siku hiyo nilizungumza mengi sana na baba huyo ambaye alionesha Nia ya dhati kabisa ya kuitaji kuwa na mimi.
Hakuwa muongo alinieleza kuwa amejaaliwa watoto wanne na wote anaishi nao nyumbani kwake kwani mke wake alishafariki, na kati ya watoto zake wa kiume alikuwa ni mmoja tu.
Baada ya kusikiliza historia yake sikusita kumpa ya kwangu, ingawa kwa upande wa baba wa watoto wangu nilidanganya kwa kusema kuwa nilibakwa na mtu ambaye sikuwa nikimjua.
Na huo ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yangu mapya, kwa namna moja au nyingine, nilihisi aibu sana kuwa na mahusiano ana mtu ambaye anaweza akanizaa.
Kwa upande mwingine niliinjoy sana niwaambie tu mubaba wangu anajua kujali bhana, alinitreat kama mtoto wake, yaani hatumii nguvu nyingi.
Nilianza kupendeza zaidi na kuvutia, ka umbo kangu kazuri kabisa kalikaa mahala pake maana enzi za shida ni kama kalipotea hivi.
Mr deo aliweza sana kwa upande wa watoto wangu, aliwapenda na kuwajali kama watoto wake, alihakikisha kuwa wanapata mahitaji yao muhimu tena kwa wakati kabisa.
Ilifika kipindi nikaacha na kazi kabisa kule bar kwani Mr deo alitaka kunihudumia uku akiahidi kunifungulia biashara ambayo ingeweza kunisaidia mimi na familia yangu.
Ndugu yenu penzi lilijua kunikolea jamani, ilifika kipindi nikikaa pasi na yeye kunipigia nakosa raha nakosa amani nakaa nawaza atakuwa wapi na anafanya nini.
"Nafikili sasa ni muda wa wewe kuja kuishi na mimi Tully au unaonaje ??" Mr deo aliniuliza uku akichezea chezea nywele yangu ya bei kali kabisa ambayo niliisuka.
"Na vipi kuhusu watoto wako ??"
"Aaha awana shida nimezungumza nao na ndio nimeona ni wakati sahihi sasa wa wewe kwenda kukutana nao lakini pia kuanza kuishi nao uku tunaendelea na utaratibu wa mambo ya harusi na kila kitu "
Kwakuwa kipindi iko binti yenu nilikuwa nimeshakolea penzini sikutaka kuuliza mara mbili tatu, nilichofanya ni kukubali tu.
Siku ya kuamisha vitu vyangu iliwadia na mwisho mimi na familia yangu tukaamia nyumbani kwa Mr Deo nikiwa kama mke wake mtalajiwa kwani nilishavikwa Pete ya uchumba.
Picha linaanza kwanza ile tumefika tu nyumbani, nakutana na mkaka pande la mtu, sio kwamba ni Menene hapana, namaanisha kuwa ni mkubwa na umri wake ulionekana kuwa sawa na mimi.
"Frank utasaidiana na Masai pale nje kuingiza vitu vya mama ndani "
Eeh hapo sasa ndio akili inanikaa sawa kuwa huyu ndio mtoto wake wa kiume na ndio mtoto wake wa kwanza.
Nilihisi kuchoka, nachokumbuka aliniambia kuwa wa watoto zake wamepishana mwaka mmoja na nusu, mmoja na nusu, lakini hakuwai kuniambia ni watu wenye umri gani.
Niliona aibu sana, yaani watu wa lika langu ndio wanatakiwa kuniita mimi mama kweli jamani.
Sikuwa na budi, moja kwa moja tukaanza kukabidhiwa chumba, aswa ilikuwa ni chumba cha mdogo wangu Tusajigwe ambacho angetumia na watoto wangu ambao sikuwa nimewapa majina zaidi ya kuwaacha na yale ya Kulwa, doto, shiza.
"Dada kwahiyo huyu wa kiume ni mtoto wake ??" Mdogo wangu tusa aliamua tu kuniuliza maana na yeye alikuwa ni kama aelewi elewi hivi.
"Eeeh ndo hivyo, na sikuwai kufikilia kuwa watoto zake ni wakubwa hivi, kwa jinsi ambavyo alikuwa akiwaelezea haikuwa rahisi mimi kujua.
"Kuwa makini dada angu "
Ila Mungu ni waajabu sana, yaani mimi ni muongeaji sana na vituko vya kutosha, lakini mdogo wangu ambaye baba, mmoja na mama mmoja ni mtu mkimya sana,mtulivu na apendi kuongea ongea kama mimi.
Kwakuwa maji nilishayavulia nguo sikuwa na budi kuyaoga.
Majila ya saa 12 jioni niliingia jikoni kwaajili ya kuandaa chakula cha usiku kwaajili ya familia nzima.
Nikiwa bize naandaa chakula jikoni, gafla waliingia mabinti wawili ambao walionekana kuwa na dharau ya hali ya juu.
"So wewe ndio mke mtalajiwa wa baba " mmoja kati ya mabinti hao aliniuliza.
Kwa mionekano yao, ni kama niliwapita miaka miwili hivi au mitatu.
Niliachana na kukologa mboga yangu nzito kabisa iliyokuwa ikitokota, kisha nikageuka na kuwaangalia kwa muda kisha nikawasalimia.
"Za jioni ??"
"Hatujaziandika, so wewe ndiye mama watatu ? I wonder hao watoto ulipata ukiwa na umri gani ikiwa uko na umri mdogo hivyo " alizungumza mmoja kati ya wasichana hao, uku akisogeza nywele yangu pembeni kwani, nilikuwa nimevalia wigi.
Nilitamani kuwajibu hovyo maana mimi mwenyewe akili yangu ni imevulugwa vilivyo ni vile tu naheshimu kwakuwa ni mgeni lakini pia ni watoto wa mume wangu.
Niliendelea na mapishi yangu uku nikiendelea kusikiliza maneno yao mazito na machafu ambayo walikuwa wakinitupia.
Kwa namna fulani yalikuwa yakiniumiza sana, lakini kwa wakati huo sikuwa na chaguo zaidi ya kukubali kile kitu ambacho kilikuwa kinatokea kwa wakati huo.
Baada ya kumaliza kupika nilitenga mezani kama ilivyo ada kwenye familia nyingi za kitajiri, na niseme kuwa nilichukua utaratibu wa ile familia ambayo nilikuwa nikiifanyia kazi.
Lakini katika familia hii ya Mr deo ilikuwa tofauti sana, hakukuwa na utaratibu wa kukaa mezani pamoja kama familia, yaani kila mtu alipakua chakula chake na kwenda kula chumbani kwake, hii ilinishangaza kwakweli.
"Baby " nilimuita Mr deo kwa sauti nyororo kabisa kwani ilikuwa ni usiku na nilikuwa nimelala juu ya tumbo lake, nisiseme kifua maana alibarikiwa ndambi bhana.
"Nambie mke wangu "
"Aaah samahani kama nitakuwa nakosea, lakini kuna kitu nimekiona leo na nafikili kuwa hakiko sawa kabisa "
"Kitu gani tena mahabuba " alijibu Mr deo akijaribu kuwa romantic.
"Aah huu utaratibu wa chakula hauko sawa, yaani chakula kinatengwa mezani lakini watu wanaenda kula vumbani, na nina imani hakuna ata mmoja ambaye amerudisha chombo chake cha kulia chakula "
"Umeona sasa mke wangu, huu ndo umuhimu wa nyumba kuwa na mama, mimi sijawai kunotes iki kitu ata siku moja, lakini wewe umekuja leo tu umeliona, na niseme sina wasiwasi na wewe na nina uhakika kuwa utalifanyia kazi "
Nilitaka kusema kitu lakini nikaamua kunyamaza tu, niliwaza ni maisha ya aina gani ambayo Mr deo anaishi na watoto wake, nikaamua tu kufyata mdomo wangu.
******
Miezi ilikimbia na maisha yalisonga, ingawa yalikuwa ya shida sana kutokana na vitimbwi na vimbwanga vya kutosha, niliamua kusimama kama mwanamke Imara.
Shida za watoto wa Mr deo azikuwa kwangu tu, bali ata kwa watoto wangu lakini pia kwa mdogo wangu tulinagwe ambaye alikuwa ni binti mtulivu mno.
Nikiwa kwenye bustani kubwa na nzuri sana ambayo ilikuwa ndani ya nyumba hiyo, alikuja frank na pasi na kunisalimia kaanza kubwabwaja.
"Mmmh natamani kujua iko ambacho kimemfanya baba yangu akulete umu ndani na akupatie heshima ya kutosha " alizungumza frank ambaye ni mtoto wa kiume wa Mr deo.
"Frank jaribu kuniheshimu ata mara moja moja, mbona sijawai kukuvunjia heshima au kukudharau kama ambavyo wewe unafanya kwangu "
"Mmmh wewe huyo, Tully unaongelea heshima ikiwa unatembea na mtu ambaye anakuzaa uku anatembea "
"Frank nitolee hizo kelele zako hapa kama mbu mwenye njaa "
"Tully are you talking to me like that ?"
"Naongea na kuvuli chako chenye matege kama mende aliyetandikwa na ndala"
Baada ya kumpa frank majibu kadhaa ya kukalaisha, niliinuka na kuanza kuingia ndani, lakini frank akadaka mkono wangu.
Niliona huyu sasa ananizoea, na niwaambie tu kuwa nilikuwa nikitumia mashoto, na vile alidaka mkono wangu wa kulia, niliutumia vizuri kabisa mkono wangu wa kushoto katika kumtandika kibao cha shavu.
Frank alichukia sana na kunyanyua mkono wake na kutaka kunitandika kibao lakini gafla tuka.......
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote