UNKNOWN BABY MAMA 1
Mhudumu wa hotel, aliyelala na bwana harusi kwenye chumba cha honeymoon
HUSQER BALTAZAR
Ilikuwa ni saa tisa mchana, wakati ambapo meneja wa royal hotel aliponifatya na kunambia kuwa niandae chumba maalumu kwa ajili ya maharusi, nikauliza niadae chumba cha aina gani, akanambia vip, na kwakuwa ni chumba cha maharusi kuna mapambo nikaenda kuyachukua kisha nikaenda kwenye chumba namba 112 ambacho kilikuwa mahususi kwa sababu ya fungate ya maharusi ambao waliqweka odaa siku hio…
Nilianza kuandaa chumba pekee yangu, nikatengeneza maneno ambayo yalikuwa na majina ya bwana na bibi harusi, kulikuwa na neno paulina na jina lingine lilikuwa paul, na kulikuwa na bango kubwa likiwa limeandikwa mr and mrs paul, nikayapanga yote kwa uweledi mkubwa na nikajua kabisa bwana harusi anaitwa paul na mke wake anaitwa paulina….
Basi nikaendelea na kazi yangu na kuweka ile mishumaa kitandani kwa ajili yua kuonge amvuto, na kubadilisha taa na kuweka taa yenye giza kidogo, nilimwaga mauwa kwa mpangilio maalumu kwenye chumba chote, kisha nikaopulizia na manukato flani hivi, kiasi kwamba mtu akija huko chumban hajuti na hatamani kutoka kutokana na mandhari kali na harufu ya kusisismua, kisha nikaweka wine mezani, na ma apple ambayo yalikuwa ni moja ya mapambo na offer ambazo huwa tunawapa wateja wetu wakikodi chumba kwa ajili ya fungate…
Nikiwa namalizia kuandaa mazingira ili nitoke nikasikia mlango umefunguliwa, akaingia mwanaume flani Yule super white, alafu mrefu na ana ndevu flani hivi za kichokozi, alikuwa amevaa suti na ananukia vizur, ukimuona unaweza kudhani ni mtu ambae ameenda kwenye mkutano wa maana au ni bwana harusi, alikuwa kama kalewa vile…
Nilipomuona nikataka kutoka, ila ile nampita tu, akanishika mkono kisha nikahsngaa anaanza kunibusu, nilishangaa sana anaanza vipi kunibusu na wakati hanijui, nikaanza kupurukushana nae, maana nilihisi kama yeye ametangulia basi mke wake anaweza kuwa nyuma yake, ila alikuwa na nguvu sana, kiasi kwamba sikuwa naweza kabisa kumkabili huyu kijana, ingawa alikuwa kama kalewa Ila alikuwa na nguvu sana, akanibeba kwa nguvu mpaka kitandani ….
Alikuwa anaonekana kama kalewa ila anilifanyia maandalizi flani hivi kabambe mpaka nikatamani asiache, ingawa nilishawah kuwa na mahusiano mara kadhaa na nimeshwah kulala na wanaume mara kadha aila sijawah kukutana na mwanaume fundi kama huyu, kwa sababu aliniandaa mpaka nikapata bao la kwanza na nilipolipata alikuwa anaonekana kama anafurahia sana lile bao, akaanza kucheka kisha akazama chumvini bila kujali uchafu wala hakuona kinyaa, alikuwa kama mtoto ambae alikuwa analilia pipi kwa masaa kadhaa na mtu anatokea anampa namna ambavyo alikuwa anafurahia sana kuzama, kuanzia nazaliwa naapa kuwa sijawah kukutana na fundi kiasi hichi, baada ya ,maandalizi kabambe nililegea sana, ila alipotulia ndio kama nilipata nguvu, na kuanza kujiuliza nilikuwa nafanya nini, nikataka kuondoka ila Yule mwanaume hakuniruyhusu kabisa niondoke, akanishika na kunitupa kitandani na kuniingilia kwa nguvu….
Baada ya kumaliza, akalala fofofo, kana kwamba alikuwa anasubiria amalize hamu zake ndio alale, na kwa namna ambavyo alilala alikuwa anaonekana kabisa hakuwa amelala ule mlalo wa kawaida, maana alipata usingizi ndani ya dakika moja na kuanza kukoroma wakati huo huo, nilimshangaa sana ila sikuwa na la kufanya maana nilisikia aibu sana, maana nilipelekwa pale kwaajili ya kuandaa chumba cha fungate, ila badala yake nikajiongezea na kazi za ziada ya kulala na bwana harusi….
Nikatoka haraka haraka maana sikutaka mtu yoyote Yule anikute pale ndani, maana hata meneja wangu angejua ni lazima angenifukuza kazi, na kama mwanamke wa huyo bwana harusi akinikuta anaweza kuniletea fedheha, ila nilikuwa nashangaa, kwanini mpaka muda ule mimi naondoka licha ya purukushani zote zilizotokea bado bibi harusi hakuwa amefika?...
Niliwaza sana ila niliona kama lile jambo halinihusu kabisa, na lile swala la kulala na bwana harusi lilikuwa linaniwazisha sana, maana nilijiona kama najiuza tena najiuza bure kabisa, maana nimeliwa na hata mia sijapewa….
Na kingine nilikuwa na elimu ndogo sana ya maswala ya uzazi, hivyo hata swala la kutafuta dawa za kuzuia mimba sikuwa na wazo nalo kabisa…
Siku hio nilikuwa nina zamu ya usiku, hivyo nikakaa pale mpaka kunapambazuka ila nilikuwa hapo nikiwa na mawazo mno, nilikuwa natafakari kwanini Yule mwanaume alinitaka kimwili na je mke wake alikuwa wapi wakati ule mpaka mimi nalala nae, na je alikuwa labda ananipenda akachukulia hio kama nafasi, na kama ananipenda mbona sijawah kumuona wala kumsikia, maswali yote hayo ambayo nilikuwa najiuliza hakuna swali hata moja ambalo nilikuwa nina jibu nalo la moja kwa moja….
Basi kulipambazuka, nikaamka mapema sana kuendelea na majukum yangu, nilifnya kazi zangu haraka haraka sana, maana nilikuwa nataka kuonana na yule mwanaume, hivyo nilikuwa nakivizia kile chumba sana, maana nilikuwa nataka kumuona Yule mwanaume atafanya nini baada ya kuniona…
Kweli mpaka namaliza kufanya usafi hawakuwa wametoka…
Mara nikamuona muhudumu mmoja wa maswala ya chakula anaenda kupeleka chakula kwenye kile chumba, nimkamuomba nimsaidie, hakukataa maana ni kawaida kwenye hotel ambayo nafanya kazi kusaidizana majukumu, nikaenda kugonga mlango nikitegemea kuwa nitamuona Yule mwanaume, ila badala yake alikuja mwanamke kufun gua mlango na alikuwa amevaa kama kahaba vile nilishangaa maana yeye ni mke wa mtu, na vipi kama angeleta yule kijana wa kiume chakula ingwakuwaje?...
Yule mwanamke alipokea chakula na kusema asante, kisha akaingia na chakula ndani, nilikuwa nashauku sana ya kumuona Yule mwanaume ila nakuja kuwaona wanatoka pamoja kwenye majira ya saa nne asubuhi, na walikuwa wamebeba kila kitu chao kwa wakati huo, kana kwamba walikuwa wanaondoka, wakawa wanataka msaidizi wa kuwasaidia mizigo yao nikaenda mimi haraka haraka kuangalia kama Yule mwanaume ananikumbuka au laa…
Ila hata aliponiona alikuwa anaonekana kama hakuwa ananifahamu kabisa, alikuwa na mke mzuri sana, mwanamke ambae anakila sifa za kuitwa mrembo, kiukweli walikuwa wameendana sana, sasa nikabaki najiuliza maswali ni kwanini alinitaka mimi kimwili na wakati alikuwa ameoa na kwanini mke wake hakuwepo mpaka ana maliza jambo lake…
Maswali yangu hayakupata majibu, nikawasaidia mizigo yao mpaka kwenye gari na kwenda kuendelea na majukumu yangu kama kawaida, siku zilienda na nikaanza kusahau kama nililala na bwana harusi wa watu kwenye siku ya harusi yao, na maisha yangu yakawa yanaendelea kama kawaida…
Sasa miezi kama miwili ikapita nikashangaa sioni siku zangu, maana mzunguko wangu ni wasiku 30. Kwa hio kila tarehe thelathin au tarehe moja ni lazima nione siku zangu, sasa nashangaa mpaka mwezi wa pili ukakata sijaona siku zangu, nikaanza kupatwa na wasiwasi mkubwa sana, na kuanza kuwaza kuwa huenda nilikuwa na mimba, nikaona nisijiulize maswali mengi bali niende hospital kuangalia afya yangu na kama kweli nina mimba au laa…
Kweli nimefika hospital nikapimwa na kugundulika kuwa nilikuwa na mimba ya miezi miwili….
Maskini chichi mimi sijui hata nilie na nani, maana hatab kuyakabili maisha yangu mwenyewe sikuwa naweza, nakuja kujikutan natakiwa kuyamudu na maisha ya mwanangu ambae sijui hata kama kuna uwezekano wa baba yake kumtambua maana ni dhahiri kuwa hajui hata kama alishawahi kulala na mimi…
ITAENDELEA…
UN KNOWN BABY MAMA 2
Mhudumu wa hoteli alielala na bwana harusi kwenye chumba cha honeymoon
HUSQER BALTAZAR
Kwa majina naitwa chitolwa butinge, ila watu wamezoea kuniita chichi kwa kifupi, nimezaliwa mkoani mara, ila nilizaliwa kwenye mazingira magumu kidogo, m,aana kuanzia Napata akili sijawah kumjua baba wala mama yangu, na nilikuwa nalelelewa na mama yangu mdogo ambae nae alifariki nilipokuwa nina miaka kumi na sita, na hapo ndipo njilipoamua kuja dar, maana mkoani mara sikuwa na msaada…
Maisha ya dar kwangu yalikuwa magumu sana, kwa sababu sikuwa na ndugu wala jamaa, hivyo wakati nafika nilifikia kulala stand tu, na kuokota makopo maana ndio kazi pekee ambayo nilikuwa naimudu, mpaka siku moja nikiwa katika harakati zangu kuna mwana mama alidondosha hela nyingi sana, na kwakuwa sikuwahi kuwa na hulka ya uwizi, nikamkimbizia Yule mama pesa zake…
Yule mama hakuamini maana alionekana kama alikuwa hata yeye hajui kama kadondosha, kuna baadhi ya watu walinilaumu na kunambia kuwa nitakufa maskini, ila Yule mama aliniangalia na kunambia ataniudia, kweli alinirudia baada ya kama wiki moja kupita, akaniuliza historia yangu, nikamuambia kila kitu, basi akanipangishia nyumba na kunipeleka nisomee hotel management, kisha akaenda yeye mwenyewe kunitafutia kazi kwenye ile hotel ambayo nafanya kazi mpaka leo…
Ila Yule mama kwa sasa hayupo Tanzania, maana hakuwa mtanzania, alirudi nyumbani kwao, ila angalau alinitengenezea maisha kwa kiasi flani…
Sikuwahi kuwa na mahusiano hapo kabla ila nilishawah kuingiliwa kwa nguvu wakati naishi stand na usichana wangu ulitoka hapo, hivyo hata siku ambayo nilikutana kimwili na bwana harusi sikuwa bikra, huenda ndio maana mambo yalikuwa mepesi…
Sasa kwa aina ya maisha ambayo naishi, sina ndugu wala msaada wowote ule, alafu nakuja kuambiwa kuwa nina ujauzito, nilihisi kuchoka, maana sikuwa nina uhakika kama hata nikigundulika kama nina ujauzito nitaweza kuendelea na kazi, na mshahara wenyewe ulikuwa laki tatu tu, ila angalau ulikuwa unanitosha, ila nilikuwa nina wasiwasi mkubwa sana kuhusu mimba yangu…
Kuna wakati nmilikuwa nawaza kuitoa, ila nafsi nyingine ikawa inaniambia kuwa niache ujinga, maana sina ndugu wala jamaa, hivyo huenda mwanangu ndio atakuja kuwa ndugu na huenda ndio ukawa mwanzo wa kuanzisha familia yangu…
Hivyo maamuzi yangu ya mwisho yakawa nikulea mimba na kujifungua salama, hivyo nikajipa nguvu na kujiambia kuwa naweza, na Mwenyezi Mungu anasababu ya kutaka mimi nipate mimba, huenda huyu mtoto ndio akaja kuwa Baraka kwenye maisha yangu na akawa mwangaza wa kweli kwangu…
Basi nikawa naendelea na kazi zangu, ila sikutaka mtu yoyote Yule ajue kuw anina ujauzito na namshukuru mungu sana kuwa mimba haikunisumbua kabisa, ila pia nikawa najaribu kufuatilia taarifa za Yule bwana harusi ambae kama sikosei alikuwa anaitwa paul, kama naweza kumpata na huenda akanisaidia majukumu, ila haikuwa rahisi kabisa kumpata maana sikuwa najua anaishi wapi au hata anafanya kazi wapi, na kuhusu kina paul wapo wengi sana jijini dar es salamu….
Siku zikaenda na kama mnavyojua mimba ni kama mnazi uliopandwa uwani, hata uufiche vipi ukikua tu ni lazima utaonekana, ndivyo hivyo hivyo kwa mimba yangu, nilificha ila ilipofikisha miei saba ikaonekana, na nikatambulika kabisa kuwa nina ujauzito, na haikuwa tatizo kwenye kazi yangu, maana kunai le likizo ya uzazi, nilikuwa naogopa tu bure, lakini hakuna kitu ambacho kilienda vibaya, kweli miezi tisa ikafika na siku moja nikiwa natoka kazini kabla hata sijafika nyumbani nikaanza kusikia maumivu makali sana kwenye nyonga, nikaenda nyumbani haraka haraka na kubeba vitu vya msingi maana nilishajipanga kisha nikakimbian hospital…
Namshjukuru mungu maana kitendo cha mimi kufika hospital nikajifungua hapo hapo…’
Nilijifungua mtoto wa kiume, alikuwa mzuri huyo, maana mimi nilikuwa mweusi, ila baba yake alikuwa mweupe, hivyo alifanana na baba yake kila kitu, kuanzia sura nywele, macho na kila kitu, nilizaa katoto kazuri sana nikaamua kukaita mwita maana ndio majina ya kikwetu hayo…
Lakin baadae nikawaza kumbadilisha jina, maana kwa wakati ule sikuwa mara nilikuwa dar es salamu jiji la gharama hivyo nikaona nimtafutie mwanangu angalau jina la kizungu kidogo nikaona nimuite Jordan…
Ndio ni Jordan paul maana angalau nilikuwa najua jina la baba yake, na baada ya kujifungua nikaenda kuomba likizo ya uzazi ya miezi mitatu na nikapewa na baada ya hapo nikaanza kujilea, na baadhi ya majiran wakaanza kunisaidia uzazi, mpaka miezi mitatu ikaisha mwanangu alikuwa ameshachangamka sana…
Basi sikutaka hata kumtafuta dada wa kazi bali nilikuwa nampeleka mtoto day care, na kwakuwa kazini walikuwa wanajua kuwa nina mtoto na sina wa kumuachia basi wakaniweka kwenye zamu ya mchana tu, maana nisingeweza kulala kazini na wakati nina mtoto mdogo…
Basi maisha yangu yakawa yanaendelea kwenda, na mwanangu akawa anaendelea kukuwa, kwa kadri alivyokuwa anakuwa ndivyo sura ya baba yake ikazidi kuja, kwa maana hata kama ikitokea siku tukakutana na huyo paul mwenyewe na nikamuambia kuwa Yule mtoto ni wake basi hawezi kubisha hata iweje, maana alikuwa amefanana nae sana…
Ila shida ya mwanangu alikuwa mtundu sana, alikuwa anaumia kila siku, na hapo alikuwa na miaka miwili tu, nilipambana nae maana ndio mwanangu tena siwezi kumtupa…
Siku zilienda na hatimae miaka ikakata na Jordan wangu akaanza shule, ingawa sikuwa napesa ila nilitaka asome shule nzuri, huenda hata elimu yake itakuja kunisaidia mimi siku moja, nilianza kumpeleka shule akiwa na miaka mitatu, hivyo alipokuwa na miaka mitano alianza darasa la kwanza na sasa anamiaka sita alikuwa darasa la pili….
Alikuwa ni mtoto mwenye akili sana ila utundu ndio lilikuwa tatizo lake kubwa, ila kutokana na kwamba alikuwa anafanya vizuri sana shuleni kuna namna walimu walikuwa wanapambana sana kumuelewa na kumuweka sawa…
Nikiwa bado napambana kwa ajili ya maisha yangu na mwanangu, meneja wa hotel akabadilishwa na hapo ndipo maisha yangu yuakabadilika kabisa, kwa sababu alitaka kuleta mapinduzi na kubadilisha mpaka wafanya kazi, na baadhi ya watu ambao walitakiwa kupunguzwa mimi nilikuwa mmoja wapo…
Nilihisi kuchanganyikiwa nilipopata hizi taarifa, maana ile kazi ndio ambayo nilikuwa naitegemea kwa ajili ya kuendesha maisha yangu na mwanangu, sasa kama ndio nafukuzwa kazi maisha yangu yatawezekana vipi tena…
Kwa unyonge wa hali ya juu nilirudi nyumbani, na ada ilikuwa inaisha miezi miwili mbele, hivyo moja kwa moja mtoto wangu ataachishwa shule na kodi yangu ilikuwa inaisha mwezi huo, yaan ukisikia kifo cha nyani miti yote inateleza basi ndicho ambacho kilinikuta mimi, na huyu meneja mpya alikuwa na roho mbaya, kwa sababu hata nilipojaribu kudai stahiki zangu hakunipa hata mia, na sio mimi tu hata wafanyakazi wengine ambao walipunguzwa kazini kama mimi….
Lilikuwa pigo kubwa sana kwangu, nilikuwa na viakiba viliishia kwenye kula tu, na kama mnavyojua usikuwa wa deni hauchelewi kukucha ndivyo hivyo hivyo hata siku ya mimi kulipa kodi haikuchelewa kufika, nikatakiwa nilipe kodi kwneye nyumba ya watu, na yule mama alikuwa mshari na hataki kulaziwa kodi hata iweje, hivyo nikamuomba sana akanambia nipambane ila mwezi ukiisha basi nitakuta vitu vyangu vyote nje….
Nilikuwa napambana huku na kule kutafuta kazi hata kama ya kusafisha tu majumba ya watu ila sikupata, nikaanza kuokota makopo, ili walau mwanangu ale, kuhusu ada mwenyezi mungu atajua atakavyonisaidia kwenye kesho yangu…
Siku moja nikiwa zangu kwenye harakati zangu za kutafuta rizki nikapigiwa simu shuleni kwa mwanangu kuwa kuna tatizo, nikamkuta mtoto wangu amepigana na walipokuwa wanapigana akarushiwa jiwe hivyo akawa amechimbika, na shule ikajaribu kumpa huduma ya kwanza, sasa kuna muda akawa anataka kwenda uwani, kutokana na kutokwa kwingi na damu, na lishe yetu ilikuwa duni sana mwanangu alianguka na kutenguka mguu…
ITAENDELEA…..
UN KNOWN BABY MAMA 3
Muhudumu wa hoteli alitembea na bwana harusi kwenye chumba cha honeymoon
HUSQER BALTAZAR..
Nilipofika shule nilihisi kuchanganyikiwa, nikamchukua mwanangu na kumkimbiza kwenye hospital kwa ajili ya matibabu, na hapo mfukuni nilikuwa nina elfu mbili tu, ambayo ndio nilitakiwa kula siku hio na mwanangu..
Kufika wakaanza kumpa huduma ya kwanza maana alienda na nguo za shule, na baada ya hapo wakaniambia nikafanye malipo, na mguu wake umepata hitilafu kidogo kwa maana kuna mifupa imetenguka anatakiwa kunyooshwa hivyo nikawa natakiwa kulipa laki na themanini kwneye kila kitu…
Nilihisi kuishiwa nguvu, kwa sababu hata nauli ya kurudi nyumbani sikuwa nayo, alafu nakuja kuambiwa kuwa natakiwa kulipa laki na themanini kwa ajili ya matibabu….
Nilitoka nje ya ile hospital na kwenda kukaa nyuma ya lile jengo na kuanza kulia, sikuwa na chakufanya zaidi ya kutoa machozi tu, kwa sababu ningefanya nini na sina hata ndugu wala jamaa wa kumkopa na hata nikipata mtu wa kumkopa nitamlipa nini na sikuwa na kazi ya kufanya…
Nililia sana bila mategemeo na kiukweli nilikuwa nimekata tamaa sana, sikuwa najua natakiwa kufanya nini kabisa kwa wakati ule…
Nikiwa kwneye hali ya majonzi mara nikahisi kuna mtu amenishika bega, hapo nimeshalia mpaka kichwa kinaniuma, niliinua uso wangu taratibu na kumuangalia ni nani huyo ambae alikuwa amenishika, ila nilipotazama vizuri sikuamini macho yangu, alikuwa ndio Yule bwana harusi ambae nimezaa nae bila yeye mwenyewe kujua…
“ nimekuona muda mrefu sana umekaa hapa unalia shida ni nini? Akauliza…
Sijui ilikuwaje ila angalau nikaanza kujisikia vizuri, kwa kumuona bwana paul ni kama niliona mwangaza na nuru mpya kwenye maisha yangu, sikujua hata natakiwa kumjibu nini, maana akili yangu ikawa inaniambia kuwa natakiwa kumuambia kuwa mwanae anaumwa na sina pesa ya kumlipia, ila akili nyingine ikawa inaniambia kuwa nisimwambie maana hanikumbuki huenda nikazua taharuki…
Nikiwa natafakari cha kusema akaniuliza tena “ vipi dada naweza kukusaidia?...
“ ndio ndio, naomba unisaidie maana nahisi kupagawa hapa, kama hautajali naomba ukamuone mtoto wangu, nilijikuta naropoka maana niliamin huenda akimuona Jordan wangu kuna nafsi itamuingia yeye kama baba na huenda akamsaidia mtoto…
“ sawa twende nikamuone , akajibu mpaka sikutegemea kama angeweza kujibu kirahisi namna ile…
Basi tukatoka pamoja na kwenda mpaka kwenye chumba ambacho alilala Jordan, paul alipomuona mwanangu alishtuka sana kisha akaniangalia kwa sekunde kadhaa na kusema “ wewe ni mtu wa wapi?...
“ mimi ni mkurya nikajibu…
“ hapana hawez kuwa damu yetu maana kwetu hakuna wakurya, ila embu nambie baba wa huyu mtoto ni nani?...
“ nilitaman kumuambia ni yeye ila sikujua hata naweza kumuelewesha vipi mpaka anielewe, nikaangalia chini tu kisha nikasema “ ni story ndefu sana, ila naomba umsaidie mwanangu maana sina hata mia ya kumlipia huyu mtoto, ndio maana nahisi kuchanganyikiwa…
Nilihisi atakataa ila alikuwa mwepesi sana tofauti na nilivyofikiria, akamlipia mwanangu matibabu, na akaniachia kama elfu hamsini akanambia kuwa itanisaidia mpaka mtoto atakapo ruhusiwa, na akaniomba na namba ya simu, sikutegemea kama ningepata msaaada kwenye wakati ambao nilikuwa nimeshakata tamaa kama kipindi kile…
Siku rudi nyumban maana sikuwa nataka kukutana na kelele za mwenye nyumba wangu,m aana yule mama anajua kudai kiasi kwamba kama kungekuwa na mashindano ya kduai basi yeye angeshika namba moja…
Hali ya Jordan wangu haikuwa mbaya kabisa, na baada ya siku tatu afya yake ikatengamaa ndio ikabidi nimuulize kwanini alikuwa anapigana shule…
“ mama Yule iyan alikuwa ananiita mimi ni chokoraa na mama yangu ni kichaa ndio maana anaokota makopo, nikawa namuambia mama yangu sio kichaa anatafuta hela akawa ananicheka na wenzake na kunambia mama yangu kichaa nikampiga…
Sikujua kama nilitakiwa kujisikia vizuri au vibaya, maana ni kweli mwanangu kanitetea ila kuna namna nilikuwa nina uhakika namna yangu ya kujitafutia kipato ilikuwa inamuumiza hata yeye ila ni kama hakuwa anataka kuniumiza…
Tukiwa tumekaa pale mara paul akaja, Jordan alipomuona akamuangalia mno kisha akasema “ wewe ni nani? Mbona kama umefanana na mimi…
Nilishangaa sana maana alikuwa ni mtoto mdogo amejuaje maswala ya kufanana tena…
“ hata mimi sijui ni kwanini tumefanana huenda mimi nikawa malaika wako, hivyo naomba usinichukie, akasema paul hapo hajui hata kama mimi najua jina lake…
“unaweza ukawa malaika wangu mimi na mama yangu, maana sitaki kumuona tena mama yangu anateseka, akasema Jordan na kwa namna ambavyo alikuwa anaonge, alikuwa anaongea kwa sauti ya umakini nay a kumaanisha kuwa kama mtu anataka kumlinda yeye basi anatakiwa kunilinda na mimi..
“ nimependa namna unavyo mpenda mama yako, bila shaka wewe ni kijana mzuri sana, akasema paul na wakati huo huo akaja muuguzi na kutuomba tukae nje, kweli mimi na paul wote tukatoka ila wakati wote nilikuwa kimya…
“ sijui ni kwanini ila nafsi na moyo wangu umejikuta umempenda huyu mtoto sana, kuna muda namuona kabisa kama mwanangu, akasema paul …
Nikatabasamu tu na kusema asante kwa msaada wako, hakika laity ungekuwa baba wa mwanangu basi mwanangu angekuw na baba bora zaidi duniani…
Tukiwa tunaongea pale Yule muuguzi akatoka, kisha akatuambvia kuwa tunaweza kuruhusiwa siku hio, nikaingia ndani na kuchukua mambo yetu ya msingi na baada ya hapo nikatoka na mwanangu, hapo paul amelipa kila kitu…
Tukataka zetu tukachukue bajaji ya kutupeleka nyumbani ila paul akasisitiza sana kuwa anaomba atupeleke yeye kwa sababu alikuwa na gari…
Sikuweza kukataa, basi tukaenda kupanda kwenye gari lake, na safari ya kwenda huko nilipokuwa naishi na mwanangu ikaanza…
Tulifika mpaka nyumbani na paul akawa anaonekana kama anataka kukijua mpaka chumba nilichokuwa naishi, ila tulipofika alishtuka na mimi pia nilishtuka kwa sababu vitu vyangu vyote vilitolewa nje na nyumba ikafungwa na mbaya zaidi vilinyeshewa na mvua, hivyo kuna namna baadhi ya vitu vilianza kuharibika…
Paul akaniangalia kisha akanambia “ nafsi yangu inanituma nikusaidie, naomba uangalie kama kuna kitu cha msingi kisha tuondoke…
Nikaenda kuangalia angalia nikawa natafuta picha ya marehemu mama yangu mdogo, na baadhi ya kumbukumbu zangu na vyeti vyangu maana angalau havikuloa, kisha nikamfata paul…
“ nashkuru sana kwa kunisaidia mpaka hapa tulipofika, ila sijui hata naenda kuishi wapi na naenda kuwa mgeni wa nani…
“ mnaenda kuishi kwangu, panda kwenye gari, akasema paul…
Nilitoa macho kama gorong’ondo, maana najua paul ni mume wa mtu alafu anakuja kunambia nikaishi kwake, mke wake akimuona mwanangu si atajua nimezaa na mume wake na vipi maisha yangu yatakuwaje, nikaanza kuwaza bila kuwa na majibu yoyote yale….
ITAENDELEA……
UKNOWN BABY MAMA 4
Muhudumu wa hoteli alielala na bwana harusi kwenye chumba cha honeymoon
HUSQER BALTAZAR
“ oww samahan naitwa paul, na najua kijana mzuri anaitwa Jordan wewe unaitwa nani? Maana sioni busara kukuita wewe kila wakati, akasema paul…
“ chichi, mimi naitwa chichi, nikasema kwa sauti ya kusita sita…
“ mbona kama hautaki kwenda kuishi kwangu, usijal nina nyumba kubwa na vyumba vya uwani, hivyo utakaa na mwanao kwenye vyumba vya uwani, na mambo mengine tutayafuatilia taratibu, akasema
“ umeona? Nikajifanya nauliza kana kwamba sijui…
“ ndio nimeoa miaka sita sasa ila bado sijabahatika kupata mtoto, hivyo Jordan hatakuwa na mtu wa kucheza nae, ila hilo sio tatizo, akasema…
“ na vipi kuhusu mke wako, labda akituona, nikauliza kwa sauti ya wasiwasi…
Akacheka kidogo kisha akasema ‘ mke wangu!, mke wangu mimi hana shida, nan i mtu ambae yupo busy na kazi sana, na mara nyingi anasafiri safari tu, hivyo pale nyumbani huwa kuna mwana mama mmoja mtu mzima sana ndio anatiusaidia saidia kazi za nyumbani, ila mke wangu anaweza kukaa hata miezi mitatu bila kuja nyumbani, hivyo usiwe na shaka nae, na namjua ni mzungu sio mtu wa kufuatilia mambo madogo madogo hivyo twende tu usijali, na nakuhakikishia usalama wako na wa mwanao, akasema…
Sikuweza kubisha maana hata kama nikikataa nitaishi wapi, na sikuwa na hela wala pa kwenda hivyo nikajubali na kwenda kupanda kwenye gari pamoja na mwanangu na safari ikaanza…
Aliendesha gari kwa karibu lisaa lizima, kama mnavyojua foleni za jiji la dar es salam na hizo foleni ndizo ambazo zilituchelewesha kufika huko osterbay ambapo alikuwa anaishi paul na mke wake…
Tulipofika akamchukua Jordan na kwenda nae kwenye nyumba kubwa na mimi nikaelekezwa chumba cha uwani, nilidhani kitakuwa kama banda ila kilikuwa chumba kikubwa na kina hadi choo ndani, basi cha kwanza nikaingia bafuni kuoaga, maana toka nimeenda hospital sijawah kuoga, na vile maji yalikuw yanatoka ya moto, hivyo nikaoga kwa karibu nusu saa, nakuja kutoka nikakuta gauni kitandani pamoja na mafuta, sijui hata alinunua saa ngapi nguo, ila sikutaka kujiumiza kichwa kwa maswali ambayo siwezi kupata majibu, kisha nikasikia sms inaingia ilikuwa inasema “ ukimaliza kuvaa njoo kwenye nyumba kubwa chakula tayari…
Basi kweli nilivaa gauni na lilinikaa vizuri kana kwamba alikuwa anajua saizi yangu, kisha nikaanza kuelekea kwenye hio nyumba kubwa…
Nikakuta mwanangu anakula zake kuku, yaan paul amemuwekea kuku mzima mwanangu, na walikuwa wanapiga story kana kwamba walikuwa wanajuana, ama kweli damu ni nzito kuliko maji, na nikakuta pia mwanangu ameogeshwa na kavaa vizuri tu, na hizo nguo alizo vaa hazikuwa hata nguo zake ila zilimkaa vyema sana, nikashangaa paul amenunua nguo saa ngapi ila sikutaka kuhoji, na kwenda kukaa pembeni ya mwanangu…
“ nani amekuogesha? Ikabidi nimuulize mwanangu…
“ baba, akasema , kiukweli nilitoa macho sana, kisha nikamuuliza NINI!....
“ nimemuambia aniite baba tu, kwa sababu anasema hamjui baba yake, ila sioni kama kuna tatizo la yeye kuniita baba, ila kama wewe kama mama haujapendezwa unaweza kumuambia aache kuniita baba, akasema paul…
“ amna ni sawa ni sawa, hakuna tatizo lolote, nikaanza kusema kwa kujing’ata ng’ata…
Basi tukakaa pale tukala na paul alikuwa anaonekana kumzingatia sana mwanangu, mpaka nilikuwa najikuta nina amani, na hapo hakuwa anajua kama ni mtoto wake ila ndio hivyo damu ni dam utu…
Tumemaliza kula paul akaomba alale na Jordan ila sikutaka, maana huwa simuamin mtu kwa mwanangu, na alipoona nimekataa ila hata hakunilazimisha akasema tu sawa, kisha sisi hao tukaenda zetu kulala kwenye hio nyumba ya nje…
Basi nikaanza kumpigia story mwanangu mpaka akalala, ila mimi sikuwa na usingizi kabisa, nikasema nitoke nje, maana hakukuwa usiku sana, ilikuwa kama saa nne kasoro tu, na inaonekana watu wote wa pale walishalala, maana kuna mlinzi na mfanya usafi, labda kama mlinzi hajalala, ila kulikuwa kimya sana, nikawa natembea tembea bustanini, nikamuona paul amejiinamia kama analia vile…
Niliogopa sana kwanini analia tena usiku, taratibu nikamsogelea na kumuuliza shida nini, aliponiona alishtuka sana kisha akauliza kwa sauti ya ukali kidogo na kusema “ umefata nini huku nje saa hizi…
Nikamuangalia kisha nikamsogelea na kumkumbatia kisha nikamuambia “ ni sawa lia, najua una maumivu na kama kulia ndio njia ya kutoa maumivu yako lia mpaka utakapotosheka, na mimi nitakuwa hapa kwa ajili yako, aiseee alilia kana kwamba kafiwa, na kazi pekee ambayo nilikuwa naifanya ni kumgonga gonga mgongoni na kumpa maneno ya kumtia nguvu, alilia kwa karibu nusu saaa kisha akasema “ asante sana chichi kwa kuja kwneye maisha yangu…
Nilimuangalia na kusema “ asante pia na wewe maana umekuwa na moyo wa kipekee sana kwangu na mwanangu, vipi kuhusu mke wako umeshaongea nae? Nikamuuliza…
Akaniangalia kisha akacheka na kusema “ unaweza ukaniona kama nina mali, na laity ungemuona mke wangu ungehisi nina bahati sana kwa kupata mke mzuri, ila ukweli ni kwamba usije ukathubutu kutamani maisha ya mtu, maana ndoa hizi zina siri kubwa sana, kuna muda natamani niachane na hizi mali na nikatafute maisha yangu, kisha nimtafute mwanamke ambae ataniheshimu na kunisikiliza, na kunipa amani kama mke wake, ila nashindwa maana kuna mipaka mingi sana ninayo kwenye maisha yangu, ila ukweli ni kuwa chichi mimi nimeoa machoni kwa watu tu, ila kwa undani sipo kwneye ndoa bali nipo kwenye biashara yenye kivuli cha ndoa…
“ una maanisha nini, mbona sikuelewi? Nikamuuliza…
“ tutaongea siku nyingine, nashkuru sana kwa muda wako mamaa, naomba ukapumzike maana nina uhakika utakuwa umechoka…
“ sawa paul usiku mwema na ulale salama, nikasema kisha nikawa naondoka zangu nikashangaa navutwa kisha paul akanikumbatia kwa nguvu bila kusema kitu chochote kile, kwa namna ambavyo alikuwa amenikumbatia alikuwa kana kwamba anataka mioyo yetu ikutane, na akawa anahema kwa nguvu kana kwamba mtu aliekuwa anakimbizwa, na akawa amenikumbatia kwa dakika kadhaa kisha akasema “ wewe ndio mtu wa kwanza kunitakia usiku mwema maaa, naomba ulale salama pia, na uwe salama wewe pamoja na Jordan wangu kisha akaanza kuondoka yeye na kuniacha mimi na maswali mengi na nikawa namuangalia namna anavyoondoka, maana sikuwa namuelewa, kwa sababu alikuwa na muonekano mzuri na alikuwa na pesa, sasa inakuwaje mtu kama yeye awe na maisha ya upweke kiasi kile, ila sikutaka kuhoji maana kila mtu anayajua zaidi maisha yake, na mimi maisha yake hayanihusu, hivyo nikaenda zangu kulala….
Niliamka mapema sana, kisha nikaingia kwenye nyumba kubwa na kuanza kuandaa chai, maana hata kama ndio nimepewa hifadhi natakiwa kujipendekeza kwa bosi ili niweze kupewa siku nyingi zaidi za kuishi, nikapika zangu chapatti na supu hapo, na yule mama akawa ananilekeza vitu vilipo, hivyo mimi nikawa napika tu, kisha nikaenda kutenga mezani, sasa wakati huo paul anatoka anaenda kazini, nikamsalimia kisha nikamuambia “ samahani chai tayari, kama hautajali naomba ule kwanza ndio uende kazini…
Nikashangaa amesimama kisha akaniangalia kwa mshangao kwa sekunde kadhaa kisha akatabasamu, na kuelekea mezani, nilishangaa kwa nini alikuwa ameniangalia kwa mshtuko namna ile…
ITAENDELEA….
UNKNOWN BABY MAMA 5
Muhudumu wa hotel alie lala na bwana harusi kwenye chumba cha honeymoon
HUSQER BALTAZAR
Basi akanywa chai, ila wakati wote ambao anakunywa chai alikuwa ananiangalia sana huku anatabasamu, mpaka nikashangaa huyu vipi…
Amemaliza kunywa chai akasimama kisha akasema “ asante sana chichi..
“ karibu sana, nikajibu akatabasamu kisha akanifata na kunikumbatia kisha akanibusu kwenye paji la uso kisha akaniachia na kwenda zake kazini…
Basi mimi sikuwa na wazo lolote lile kuhusu yeye, nikawa nasaidia saidia kazi maana sikuwa na kazi za kufanya, kwenye majira ya saa sita mchana nikasikia simu yangu inaita, na aliekuwa anapiga simu alikuwa ni paul…
“ mama nimekaa kazini nasikia njaa sana, unaweza kunipikia chakula cha mchana nakuja kula…
“ sawa hamna shida, naomba nambie unataka kula nini? Ikabidi nianze kukupikia nikasema…
“ pika chochote kile unachotaka , nakuja baada ya nusu saa, akasema kisha akakata simu…
Nikaenda kumfata Yule mama ambae alikuwa anahusika na maswala ya mapishi pamoja na usagfi na kumuambia kuwa “ boss amesema anarudi kula mchana, huwa anapenda kula nini?...
“ makubwa!, leo anakuja kula mchana, embu nambie kuna nini kati yenu, akaniuliza…
“ hakuna chochote kile ambacho kinaendelea kati yetu, na kwanini unasema hivyo? Ikabidi niulize…
“amna pika ugali na samaki na mboga za majani ndio huwa anapenda, na kuna samaki jana usiku niliwakaanga unaweza kwenda kuwapasha upike kama ni mchuzi au uangalie namna ya kufanya, akasema Yule mwana mama alikuwa anaitwa rozi, kisha akatoka akaniacha jikoni…
Nikapika mchuzi wa samaki wa nazi na kamchicha flani hivi, kisha nikawa nasonga ugali, na nilipika chakula kingi kidogo ili mwanangu, mimi mwenyewe na Yule mwana mama pamoja na mlinzi wote wale, nikiwa ndio naanza kusonga ugali nikasikia geti linafunguliwa nikajua moja kwa moja paul anarudi nyumbani, basi kwlei alikuwa ni yeye, akaingia ndani na kupitiliza mpaka jikoni akanikuta nasonga ugali…
Akanisalimia kisha akatabasamu na kuniambia kuwa “ sikutegemea kama utanipikia asante sana chichi..
“ usijali boss, ungeenda kukaa kwenye meza ya chakula na kuja kukuletea muda sio mrefu, nikamuambia akatabasamu kisha akaanza kuja nilipo, nikajua ananifata mimi, ila alikuja na kufungua fridge kisha akatoa maji ya baridi akaanza kunywa, ila akasimama pale pale kwenye fridge akawa ananiangalia sana mpaka nikawa naona aibu…
“ kwanini unaniangalia kiasi chote hicho? Ikabudi na mimi niulize,….
“ kwani kuna tatizo? Akauliza…
“ hapana ila nilidhani kama unatakiwa ukae ukumbini usubiri chakula, uwe hata unaangalia angalia tv wakati tunaandaa chakula, nikajibu…
Akatabasamu kisha akasema huku akiwa anaondoka kuwa “ na vipi kama wewe ndio luninga yangu, ila nikawa kama sijamsikia vizur nikabidi niulize unaongea na mimi? Akageuka akaniangalia kisha akanikonyeza na kwenda kukaa zake ukumbini…
Basi nikashangaa kwanini ananikonyeza ila nikajua ni tamaa za wanaume tu pengine, basi nikaandaa chakula kisha nikaenda kumtengea, na mimi nikaondoka zangu ,maana nilitaka kumuacha ale pekee yake…
“ unaenda wapi chichi? Akaniuliza..
“ nimeona nikuache ule naenda kucheza na mwanangu Jordan naona kama ni mpweke huko nje anapocheza pekee yake, nikasema…
“ aaaa huu ni muda wa kula, naomba umlete na Jordan tuje kula pamoja, yaan umepika wewe alafu unataka mimi nile pekee yangu unaona ni sawa kweli? Akauliza na mimi sikutaka hata kumjibu maana sikuwa najua hata natakiwa kumjibu nini, na kimya kimya nikaenda kumleta Jordan kwaa jili ya kula pamoja, na paul akataka Jordan akae pembeni yake…
Akaanza kumlisha sasa mpaka akasahau kuwa anatakiwa kula yeye, alikuwa anamuonesha mwanangu mapenzi ya dhati ambayo baba alikuwa anatakiwa kukuonesha mwanae, mpaka nikawa najisikia vizuri, kuna muda nikawa hata natamani kumuambia ukweli kuwa huyo ni mwanao ila ndio hivyo nikawa naogopa nitaanza vipi kumuambia maana sikutaka kujieleza vyovyote vile kwa ambalo lilitokea miaka kadhaa nyuma maana anaonekana kama hakumbuki kitu…
Basi amemaliza kumlisha mtoto akaanza kula nay eye, amemaliza akamuambia mtoto akacheze na mimi nikaw anaondoa vyombo, nikasikia paul anauliza “ umeshawah kuwaza kuwa na familia chichi, kwa maana ya kuwa na mume na mtoto?...
“ ndio nimeshawah kuwaza na mwanamke yoyote Yule ni lazima awaze hivyo, maana hakuna mwanamke ambae anataka kuwa msungo, wanawake wote tunataka kuolewa na tuzae na tuwe na familia ambazo zinafuraha na amani, nikajibu…
Paul akaangalia chini kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ hivyo ndivyo ambavyo najisikia kila nikiwa na wewe pamoja na Jordan, najua nimeoa tena ndoa ya kanisani kabisa, ila nahisi kama wewe na jordan ndio familia yangu, maana Napata amani sana nikiwa na wewe sijui kwanini…
“ labla kwa sababu mke wako kasafiri, huenda labda unahisi upweke, nikajibu, ila nilikuwa najibu tu maana sikutaka kuanza kumtamani mume wa mtu, ingawa kweli hata na mimi kuna muda ananiangalia kwa namna flani hivi mpaka nahisi kama kamwili changu kanasisimka sana, ila kila wakati nilikuwa nayapuuza hayo mawazo, maana najua amefunga ndoa na natamani niendee kumuheshimu kama mume wa mtu, maana kwanza sikuwa na pakwenda, hivyo niliamin kama nikileta ujinga wa aina yoyote ile huenda nikafukuzwa…
Basi maisha yakawa yanaendelea kama kawaida, ila paul akawa anawah kurudi nyumban na alikuwa na kama weekend hakuwa anatoka kabisa, kwa sababu alikuwa anataka kukaa na sisi nyumban, na sikuona tatizo na Jordan alikuwa anampenda sana, na alikuwa anamsisitizia mar azote kuwa anatakiwa amuite baba, na akamrudisha Jordan shule ila alimuhamisha, maana kule ambapo alikuwa anasoma kulikuwa mbali sana na tulipokuwa tunaishi na akamlipia ada ya mwaka mzima…
Hapo tumekaa na paul miezi mitatu sijawah kumsikia paul akimzungumzia mke wake hata kwa bahat mbaya, sijui ni kwa sababu gani alikuwa anafanya hivyo, ila siku moja nilikuwa nambembeleza mtoto alale, maana huwa nina kawaida ya kumsimulia mwanangu simulizi mbali mbali ambazo ndio zilikuwa kama zinabembeleza usingizi wake, nikiwa nimekaa na mtoto mara nikashangaa nasikia sms inagia kwenye simu yangu, nikabid niangalie simyu, maana sio kawaida mimi kutumiwa sms hasa hasa usiku…
Alikuwa ni paul, alikuwa ameandika kuwa “ mtoto akishalala naomba utoke nje nina maongezi kidogo na wewe…
“ sikutaka kubisha kabisa kuhusu kuzungumza nae, basi kwakuwa mtoto alikuwa ameshalala nikatoka na nikamkuta pemben ya mlango kana kwamba alikuwa anasubiri nitoke nje…
Basi tukaanza kuongozana mpaka bustanini, na tulivyofika akanambia “ chichi mke wangu anarudi kesho, ila sijui ni kwanini sikuwa nataman arudi hata kidogo…
“ kwanini unasema hivyo na wakati ni mke wako, na ni muda sasa hamjaonana, mimi huwa najua kama haujaonana na mwanamke wako kwa muda mrefu basi unakuwa na hamu nae sana?ikabidi na mimi niulize….
Paul akaniangalia kisha akasema “ nilijua wanawake wote duniani ni pasua kichwa mpaka nilipokutana na wewe chichi…
“ umemaanisha nini, kusema hivyo? Ikabidi niulize, nikashangaa paul amenisogelea kisha tukawa ile zero distance, nikaanza kusikia pumzi zake, kisha akaanza kunikiss, na ukizingatia mimi sijafanyaga muda wote huo, toka nilipofanya nae ndio kabisa nikawa nimeshindwa kujidhibiti na kujikuta natoa ushirikiano wa kutosha kwenye hilo busU ambalo alitupa na wote tulionekana kuwa na msisimko wa hali ya juu…
ITAENDELEA….
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote