VIANNA
(Binti aliyebadilisha maisha ya playboy wa kizungu.
Hii ni simulizi inayomuongelea kijana Chriss. Chriss ni kijana kutoka familia ya kitajiri alikuwa na kila kitu alichotamani.
Alitumia pesa zake kwenye starehe huku alibadili wanawake kama nguo. Tabia ya Chriss hsikuwapendeza wazazi wa Chriss wakaamua kumtafutia mchumba Mercy.
Chriss alianza uhusiano na Mercy lakini hakuweza kuacha tabia yake.
Siku moja Mercy alienda kumfumania Chriss hotelini na kufanya fujo , Chriss anapiga simu polisi Mercy anakuja kukamatwa .
Chriss anamkataa Mercy mbele ya wazazi wake na kuamua kuondoka Afrika kusini na kwenda kuanzisha maisha Tanzania.
Huko anakutana na binti Viana.
Viana alikuwa anafanya kazi mgahawani , anapata oda ya kupeleka chakula kwa Chriss.
Siku moja anakutana na Chriss wanapingana na kusababisha kikapu cha Viana kuanguka. Viana anaongea maneno makali ya kumkashifu na kumnanga Chriss akijua hajui kiswahili , mwisho Chriss anamjibu kwa kiswahili.
Viana anaondoka anafika kwenye nyumba anayopeleja chakula anakutana na Jimmy binamu wa Chriss.
Viana analalamika kazi anayofanya inamchosha na kipato kidogo isitoshe boss wake hawaelewani.
Jimmy anamwambia amkutanushe na binamu yake anakiri kama mfanyakazi.
Kesho yake Viana na Jimmy wanaenda kukutana na Chriss, Viana akashituka kumuona boss ndio yule mzungu aliemuibgelea vibaya.
Chriss anakubali kumpa kazi .
Viana na Jimmy wanapanga mpango wa kubadili mwenendo mzima wa Chriss bila yeye kujua .
Je ni mbinu gani wametumia , na je watafanikiwa?
VIANNA
(binti aliyebadilishwa maisha ya playboy wa kizungu) 1
MTUNZI SMILE SHINE
Ilikuwa majira ya saa kumi na moja jioni, katika nyumba moja mzuri iliyokuwa na madhari nzuri ya kuvutia , binti mrembo mercy alikuwa kakaa nyumbani kwao pamoja na mashoga zake wanne, HAPPY , JULIET, SAUDA NA ZENA. Walikuwa wakipiga story huku wakiwa wanafurahia kwani Mercy alikuwa anawaambia wenzake kuwa hivi karibuni anavakishwa pete na mpenzi wake Chriss. Kijana wa bilionea knight ambae walianzisha uhusiano miezi minne iliyopita kwa kuunganishwa na wazazi wao.
" Kwahiyo kutakuwa na sherehe kubwa ya kuchumbiwa? Aliuliza
Mmoja wa marafiki zake aliuliza.
" Hivi wewe unanionaje, unanichukuliaje kwanza kwa hadhi yangu na Chriss unafikiri tutachumbia kimnya kimnya ? Sherehe ni lazima mama hata kila mtu ajue naenda kuwa mchumba wa Chriss na muda sio mrefu nakuwa mke kabisa.
Rafiki zake waliangaliana huku wengine wakifinyana maana wanamjua vizuri sana Chriss na tabia zake.
Chriss ni kijana wa miaka 25 anatokea kwenye familia inayojuweza mno pia familia yao inajulikana sana kutokana na mali , kampuni, hotel mbili za hadhi ya nyota tano, restaurant alizokuwa anazomiliki baba yake pia baba yake mkubwa alikuwa ni mtu mwenye kujiweza na kumiliki mali nyingi.
Pia Chriss alikuwa ni kijana mtanashati mno alikuwa na kila kitu alichokitaka alikuwa na nyumba ya ndoto yake, magari aliyotaka ya kutembelea pia alipenda mno starehe, alibadili wanawake kadri wawezavyo sababu hakuamini katika mapenzi, alichukuliwa wanawake wote ni wasaliti hakuna mwenye mapenzi ya kweli. aliwahi kupenda lakini mwanamke aliyempenda alimpa kila kitu lakini aliamua kumsaliti na kutembea na mwanaume mwingine kuanzia hapo Chriss aliamua kutokupenda alitumia pesa kupata mwanamke kwaajili ya kustarehe nae na mwisho alimua aliachana na kuendelea na mambo yake mengine. Aliamini pesa ndio kila kitu kwake na inamfanya apate kila anachokitaka.
Mercy akiwa anaendelea kuwapa mashoga zake ratiba ya sherehe yake ya uchumba simu yake iliingiza messege upande wa whatsapp
Mercy hakujali aliendelea kuongea mara zikaingia messege nyingine mbili hapo ndipo alipoamua kuangalia ni nani ametuma messege. Alipofungua alikutana na picha tatu za Chriss akiwa na mwanamke wakiwa kwenye moja ya hotel yao. Na chini iliingia messege nyingine ikisema.
" Wapo chumba no 112.
Mercy alikunja uso wake alibadilika mpaka sura yake ikawa nyekundu.
" Vipi Mercy kwema? Happy aliuliza.
Mercy hakujibu alinyanyuka haraka akaingia chumbani kwake akachukua pochi yake ndogo akatoka tena.
" Mercy unatoka una tuacha hapa?
" Natoka mara moja kama mnaweza kunisubiri sawa na kama hamuwezi tutaonana siku nyingine
" Tunaweza kusindikiza uendako ?
" Hapana .... Alijibu Mercy huku akitoka .
Aliwaacha wenzake wakiangaliana na kuishia kuguna.
" Huyu atakuja kuwa chizi kwaajili ya huyo Chriss .
" Unajuaje kama sababu ya kuwa vile ni Chriss.
" Unajifanya mgeni , ukimuona Mercy yupo kwenye hali ile jua kumechafuka huko shushushu wake wameshampa habari kuhusu Chriss nilimwambia akitaka kumla Bata asimchunguze lakini hasikii.
" Hahahaha... Mmoja wao alicheka.
" Unacheka nini?
" Mercy ananifurahusha sana yani anachanganyikiwa sababu ya mtu alieshindikana hata kwa wazazi wake hivi ni ndoa ndio inatafutwa au ni hizo mali aonekane kuolewa kwenye ukoo wa kitajiri?
" Shoga naona anatafuta vyote ndoa na umaarufu ila mpaka kupata hivyo vyote lazima imghalimu.
Mercy alifika hotelini alipita mapokezi na kutaka kuelekea kwenye lift ili aende chumbani ghafla akashikwa mkono . Aligeuka kumuangalia alimshika mkono huku akunja uso wake.
Alimshika mkono alikuwa muhudumu wa kiume pale hotelini.
" Samahani madam naweza kukusaidia kitu?
" Khaaaaa wewe hebu achia mkono wangu haraka kabla sijakurarua na kucha zangu.
Muhudumu aliangalia hizo kucha za bandia jinsi zilivyokuwa ndefu ilimbidi amuachie tu kwa sababu ya usalama wake.
" Pumbavu unaona una hadhi ya kushika huu mwili wewe kibaraka unajua natumia gharama gani kuhudumia hii ngozi na huu mwili?
" Nisamehe madam. Aliongea yule muhudumu huku akiwa kainamisha kichwa chake chini.
" Mfyuuuuu
Mercy alifyonza kwa hasira alafu akaondoka kwenda kupanda lift.
Muhudumu alirudi mapokezi .
" Sijui kwanini yupo hapa na inavyoonekana anajua hadi chumba alichokuwepo Chriss.
" Sasa wewe unaogopa nini muache akakutana na mke mwenzie.
" Mmmh sijui nini kitatokea huko juu.
" Wewe tulia Chriss kazidi.
Mercy alifika mpaka chumba namba 112 alisimama mbele ya mlango na kugonga kwa nguvu wakati huo Chriss alikuwa akiburudika na mwanamke wake huko ndani hakujali hodi mpaka yule mwanamke akamwambia.
" Baby kuna mtu anagonga.
" Aaaaah achana nae. Alisema Chriss huku akiendelea kuhusu shingo ya yule mwanamke na mlango uliendelea kugongwa kwa fujo mpaka ikawa kero .
" Mpuuzi gani ananifanyia fujo hivi? Aliuliza Chriss huku akinyanyuka kitandani , alienda kuchukua taulo akajifungua kiunoni na kwenda kufungua mlango.
Alipokutana na sura ya mercy alishituka.
" U...umefuata nini hapa?
Aliuliza Chriss kwa kigugumizi.
" Nipishe niingie ndani.
" Ukafanye nini? Aliuliza Chriss kwa kujiamini, Mercy hakujibu alimsukuma kwa nguvu mpaka Chriss akataka kuanguka. Mercy akaingia ndani akamkuta yule mwanamke kakaa kitandani. Kabla Mercy hajaongea chochote walirusha pochi yake , yule mwanamke akijikinga uso wake ili pochi usifikie uso wake.
" Wewe malaya unafanya nini na mchumba wangu?
" Hey wewe acha ujinga , Oya wewe vaa nguo uondoke.
" Unafikiri atatoka hapa kirahisi yani mpaka nije niingie jino au nitoe jicho mtoto wa mtu ndio akili itakaa sawa watajua mwanaume wa mtu anavyouma.
Chriss aliushikilia Mercy asiendelee kuleta fujo yule mwanamke kuona anatetewa alianza kujibu.
" Eti mwanaume wangu ana alama usoni? mvalishe bango shingoni ili tujue mwanaume wa mwenyewe alafu ukiona mwanaume anatafuta wanawake wengine ujue una kasoro unatakiwa ukae ujitathimini.
" Wewe malaya.... Mercy alitaka kurukia kichwa
" Oya fanya utoke nitamuachia akupasue.
" Nipe hela yangu.
" Chukua Wallet kwenye suruali yangu uchukue pesa yako.
Yule dada alienda kuchukua suruali akachukua pesa zote za kwenye Wallet.
" Chriss wewe ni mtu wa aina gani yani una mruhusu achukue hela ona inachukua hela zote.
Chriss hakuonyesha kujali kuhusu pesa.
Yule mwanamke alivyoondoka walibakia wenyewe wakiendelea kurumbana.
" Nini sasa?
" Nini kivipi hivi unavyonifanyua unaona sawa?
" Sikiliza Mercy mimi siwezi kutulia na mwanamke mmoja na kama umeamua kuwa na mimi basi nipe uhuru wa kufanya mambo yangu.
"Yani unamaanisha nikuachie uendelee kunichangamsha na hawa malaya.
" Kama huwezi nenda zako sababu sikukuchagua na sikuwa tayari kuowa ni hao wazazi ndio wanataka .
" Unamaana huna mapenzi na mimi?
" Sikiliza wewe usitake kuchimba mambo ambayo yatatumika moyo wako kubaki kuwa wewe ni mwanamke uliochaguliwa na wazazi wangu na sio.....
Kabla Chriss hajamaliza kuongea alishtushwa kofi shavuni kwake.
Chriss alishika shavu lake huku akimuangalia Mercy kwa hasira.
" Umenipga kofi?
" Na nitakupigia zaidi endapo utaendelea kuongea ujinga wako.
Chriss alimuangalia huku akiwa anafikiria kumpiga lakini aliona hakuna sababu akamwambia.
"Toka mbele yangu kabla sijafanya kitu kibaya kwako.
" Fanya Chriss, fanya kama wewe mwanaume kweli.
Chriss alimuangalia akaniuliza
" Hivi anajiamini nini?
Kwa hasira Mercy alianza kuvunja vunja vitu pale chumbani alipasua mpaka taa.
Chriss alimfukuza lakini haikusaidia ikabidi aite walinzi wamtoe.
Baada ya dakika chache walinzi na wafanyakazi wengine walifika , walinzi walimchukua na kumvuta nje.
" Hebu subiri kwanza. Walinzi wakisimama kumsikiliza Chriss.
" Mpelekeni polisi mfungulieni mashitaka ya kuvamia na kufanya fujo kwenye hotel yangu.
" Chriss unanipeleka polisi?
" Pelekeni hiyo takataka huko.
" Hebu niache ni huko, Chriss, Chriss......
Mercy aliita na kuomba aachiwe hakuna aliemsikiliza walimzoa mzobemzobe wakampandisha kwenye gari na kumpeleka polisi.
VIANNA
(Binti aliyebadilisha maisha ya playboy wa kizungu) 2
MTUNZI SMILE SHINE
Walipotoka Chriss akichukua simu na kumpigia polisi mmoja akieleza kuhusu Mercy .
" Huyo mwanamke mjinga muweke ndani ajifunze adabu.
" " Sawa usijali.
Baada ya masaa mawili kupita wazazi wa mercy walipata habari kuwa binti yao yupo rumande kapelekwa na Chriss .
Wazazi wa Mercy waliwapa taarifa wazazi wa Chriss.
Wazazi wa Chriss walichukizwa sana na hizo taarifa walimpigia simu mtoto wao lakini Chriss hakupokea simu.
" Hivi huyu mtoto anataka kutoa uhai wangu ndipo alidhike , hii ni aibu gani mke wangu?
" Chriss katidhalisha sana yani mchumba wake kumuweka ndani wazazi wenzetu watatufikiriaje?
" Acha kwanza binti atoke polisi tutajua la kufanya.
Baba yake chriss alifanya mpango akamaliza kesi na Mercy akarudi nyumbani kwao.
Chriss alirudi nyumbani kwao akawakuta wazazi wake wanamsubiri wakiwa na hasira.
" Hallow mimi, hallow dady.
" Hebu njoo hapa. Aliongea baba yake kwa ukali na Chriss alisogea walipo wazazi wake.
" Umefanya jambo gani la kutudhalilisha?
" Mama hujui alichofanya Mercy yani amefanya uharibifu mkubwa sana pale hotelini.
" Lakini chanzo, sababu ni wewe hivi kwanini hautaki kubadilika Chriss, yule ni mchumba mke wako mtarajiwa kwanini unamtendea vibaya?
" Inatakiwa twende ukaone msamaha.
" Dady siwezi kuomba msamaha na wala sijali anajisikiaje kwanza mimi sikuwa tayari kuowa nyie ndio mlilazimisha.
" Kwahiyo hatumtaki Mercy?
" Ndio kwa sasa sipo tayari kuowa niachieni nichague mwanamke nitakaeamua kuishi nae alafu swala la kuowa bado sijapanga kuowa wakati huu.
Chriss alikuwa mkali kuhusu swala la kuowa na alimkataa Mercy mbele ya wazazi wake.
Baba yake alikasirishwa sana na maamuzi ya Chriss alitoa tamko moja
" Kama umeamua hivyo na mimi nasema hivi sitaki kukuona nyumbani kwangu unatakiwa kuondoka.
" Sawa baba nitaondoka hata sasa ukitaka.
" Nyamaza Chriss usimjibu baba yako, utaondoka unaenda wapi?
" Mimi ni mwanaume mama nawashukuru mmenipa elimu hiyo ni siraha bora kwangu itanifanya nitafute maisha.
Alijibu Chriss kwa kujiamini kisha akaindoka kuelekea chumbani kwake.
Kesho yake kulikuwa na kikao kati ya familia mbili , familia ya Mercy na familia ya Chriss walikaa ili kuweka sawa maswala ya watoto wao.
Muda huo Chriss hakuwepo na ndio alikuwa akisumbuliwa ili kikao kianze.
" Mama Chriss hebu jaribu tena kumpigia mwanao.
Baba Chriss alimwambiake wake na mama Chriss akafanya hivyo.
Alipiga simu lakini haikuwa inapatikana.
" Bado hapatikani.
Baada ya muda alikuja msichana wa kazi akiwa na karatasi mkononi alimfuata mama Chriss na kumnongoneza kitu kisha akampatia ile karatasi.
Mama Chriss alisoma ile karatasi kisha akampa mume wake.
Baba Chriss alisoma ile karatasi kisha akashusha pumzi na kuegemea kichwa chake kwenye sofa.
" Kuna nini mr William? Aliuliza baba yake Mercy huku kila mtu akionekana kuwa na shauku ya kujua kilichoandikwa kwenye ile karatasi .
" Chriss ameondoka leo asubuhi inaelekea Tanzanian.
Mercy alishituka akamuangalia mama yake , mama yake akamtuliza.
" Vipi kuhusu mpango wa kumuoa binti yangu?
" Hatakaa tena, maisha yake yatakuwa huko .
Mercy kusikia hivyo aliondoka huku akiwa anatokea na machozi ilikuwa aibu kwake sababu alikuwa ametangaza marafiki zake wote na watu wengi walijua atapokewa na Chriss.
Chriss alifika Tanzania na kusimamia jengo kubwa la kibiashara lililokuwa linamilikiwa na baba yake, pia alipangisha apartment na kununua gari safi kwaajili ya matumizi yake.
Kama kawaida yake na tabia ni kama ngozi hakuweza kubadilika alikuwa alinunua wanawake kwaajili ya kumaliza shida zake kimwili.
Siku moja Chriss alikuwa akiangalia haki ya hewa na mazingira ya maeneo aliyokuwa akiishi .
" Kweli Tanzania inavutia nadhani natakiwa kutembelea vituo vyote vya utalii ili nipate kitu nisiishie kusikia bali natakiwa kusimulia kile nilichoshuhudia.
Akiwa bado anatembea huku anatafakari aligongana na binti mmoja ambae alikuwa anatembea haraka kama vile anawahi sehemu na mkononi alikuwa kabeba kikapu. Kile kikapu kilianguka chini , Viana aliziokota haraka na kuangalia vilivyopo ndani kama vipo salama.
Alipoona kila kitu kipo sawa alimuangalia Chriss usoni kwa hasira.
" Am sorry. Alisema Chriss
" Wewe mzungu kwani huoni, sijui unashangaa nini cha maana hapa? Umeshindwa kushangaa huko kwenu unakuja kushangaa hili vumbi la Tanzania au huko ulikuwa unakaa uswahilini basi umefika hapa vingi unashangaa huu mtaa wa kitajiri na hizi lami zilizochaguliwa kila mwaka tunaziona vilaka.
Alisema Viana huku akiwa anamuangalia na alikuwa na uhakika Chriss hajui kiswahili.
Chriss alimuangalia bila kumuongea .
" ile sasa mimacho unanikodolea nini watu tumevurugwa huko alafu tunakuja kukutana na vituko vingine. Hebu nipishege nipite
Bado Chriss alisimama mbele yake na hakujibu alimuangalia tu huku akitoa tabasamu kwa mbali.
" Hiiiii anataka kucheka Muone kama mdoli kasimamishwa dukani, muone mashavu yalivyokuwa mekundu.
Viana alipita pembeni akapiga hatua kutaka kuondoka mara akasikia sauti ikisema.
" Aaaaah unamaana nafanya na mdoli ? Kilikuwa ni kiswahili safi mpaka Viana akageuka kumuangalia.
" Kheeee kumbe unajua kiswahili?
" Tena kiswahili faraja kukushinda wewe.
" Mmmmmh aibu yangu. Lakini sijali wala nini.
Viana aliguna alafu akaondoka na kuelekea kwenye moja ya apartment kupeleka chakula huko alipokelewa na Jimmy .
" Umechelewa sana mpaka alihitaji chakula kaondoka.
" Nisamehe sana si unajua kazini kwangu kuna kazi sema nashindwa tu kuacha sababu sina ramani ila kwa kelele za yule mama pale mgahawani mbona shuhuri ninayo. Alafu nimefika hapo nikakutana na mzungu sijui muarabu nikagingana nae nusu chakula kumwagike ni Mungu tu kaa muda kunistiri ila sitamuacha nimempa maneno yake nikajua hajui kiswahili bwana wewe kumbe mswahili pure. Aliongea Viana wakawa wanacheka.
" Viana una vituko sana . Kuhusu swala la kazi nitaongea na binamu yangu ili uje kufanya kazi hapa ana uhitaji wa msaidizi wa kazi.
" Nitashukuru sana fanya hivyo jimmy mwenzio napitia magumu ujue kwenye hii kazi.
" Usijali leo nitaongea nae mambo yakiwa sawa nitakukutaniaha nae .
" Poa.
Baada ya kuongea Viana aliondoka
Chriss alipotoka kwenye matembezi yake alienda kuoga alipomaliza alienda kupata chakula ambacho lilipelekwa na Viana.
Chriss alikuwa anapenda sawa chakula kutoka kwenye mgahawa anajifanya kazi Viana ila hakuwahi kuonana nae.
" Hiki chakula kitamu sana.
" Hivi kwanini usiajiri mtu wa kuwa anakupikia na kufanya usafi hapa ndani?
" Unamaanisha nitafute house girl?
" Ndio.
" Je ataweza kupika chakula kitamu kama hiki?
" Mpishi ya hicho chakula anatafuta kazi unaonaje kama utamuajiri?
" Si anafanya kazi mgahawani?
" Ana changamoto na boss wake.
" Basi sawa nitahitaji kuonana nae kesho majira ya saa 4 asubuhi .
" Muda huo itakuwepo nyumbani?
" Nitakuwa kazini utaleta huko .
"Sawa.
Baada ya Chriss kukubali kuonana na Viana ili wapange jinsi ya kulipanda. Jimmy alienda kumpigia simu na kumpa habari njema , Viana alifurahi sana pale pale alianza kuandaa nguo ya kuvaa kesho kwaajili ya kukutana na boss mpya.
VIANNA
( Binti aliyebadilisha maisha ya playboy wa kizungu)3
MTUNZI SMILE SHINE
Kesho yake Mida ya saa mbili asubuhi Viana alivalia mavazi yake safi sketi ndefu ya rangi ya ugoro na blauzi nyeupe na kichwani alikuwa kashika nywele zake nzuri za kupendeza . alitoka nyumbani kwao huku akimuomba Mungu aweze kupata kazi , alitoka mapema ili kuwahi miadi , si unajua tena foleni za barabarani zingeweza kuchelewesha na kujikuta anakosa kazi.
Majira ya saa tatu na nusu walikutana na Jimmy, alipanda kwenye gari Jimmy aliwasha gari wakaelekea kazini kwa Chriss.
" Boss wako ni mtu poa eee?
" Sio boss wangu ni binamu yangu, baba yangu na mama yake wamezaliwa baba mmoja mama mmoja.
" Ahaaaa sawa hapo nimekuelewa sasa.
" Ukisema anaitwa nani vile?
" Chriss
" Unaweza kuniambia ni mtu wa aina gani?
" Wa kawaida tu hana mambo mengi ila ukifika usiongee sana.
" Ahaaaa nilitaka kujua hivyo nisije nikaharibu
Walifika kazini kwa Chriss wakaribishwa mpaka ofisini kwake , wakati wanaingia Chriss alikuwa Bize na laptop yake.
Aliponyanyua uso kuwaangalia Viana alishituka kumuona Chriss lakini kwa Chriss ilikuwa kawaida tu hakuonyesha hali yoyote ya mshangao wala kushituka
Viana alimvuta shati Jimmy .
Jimmy waligeuka na kumuuliza
" Vipi?
" Huyu ndio binamu yako? Aliuliza kwa sauti ya chini
" Ndio.
" Mungu wangu hapa kazi sina na kwa mama abby nitakuwa nimelikoroga sijaomba hata ruhusa.
" Kwani vipi?
" Mmmmmh......
Kabla Viana hajaongea wakasikia Chriss akisema
" Karibuni mbona mmesimama huko?
" Mama yangu ndio mwenyewe sauti ni ileile.
" Hebu twende bwana.
Jimmy alimshika mkono wakaenda kukaa kwenye viti , Viana alikuwa anaona aibu kumuangalia Chriss usoni wakati huo Chriss alikuwa kamkazoa macho anamuangalia usoni.
" Chriss huyu ndio yule dada tuliemuongelea jana anaitwa Viana.
" Nimefurahi kukutana na wewe kwa mara nyingine tena miss Viana.
" Kumbe mmeshawahi kukutana?
" Ndio tulikutana japokuwa kukutani kwetu kulikuwa na Shari kidogo ila yamepita.
" Naomba unisamehe boss wangu zile zilikuwa stress za maisha tu . Aliongea Viana kwa upole
" Usijali. Alijibu Chriss huku akiwa na tabasamu usoni kwake.
" Kwahiyo kazi nimepata?
" Ndio kwa sifa alizonipa jimmy kazi umepata ila .....
" Ila nini boss mzungu mwenzio nimekosea na nina uhitaji wa kazi familia yangu unanitegemea na pale jirani yetu kuna bibi mmoja mzee hajiwezi mimi ndio huwa nampa msaada hivyo nakuomba unipe kazi ili niweze kusaidia hawa watu wenye uhitaji na wewe utalipwa na Mungu.....
" Mmmmh utaharibu sasa maneno mengi ya nini? Alisema Jimmy
" Nilikuwa najielezea ili aelewe.
" Sawa nimekuelewa utataka nikulipe mshahara kiasi gani?
" Siwezi kujipangia nakusikiliza wewe boss mzungu.
" Vipi kama tukianza kwanza kwa matazamio baada ya hapo nitakulipa laki tatu.
" Kwakuwa nina shida haina shida Hiyo inatosha sana boss wangu naweza kuanza lini kazi?
" Kesho .
" Mapema sana nitakuwa nimefika .
" Una karibishwa sana.
Walimaliza maongezi alafu Jimmy na Viana wakiondoka.
Wakiwa kwenye gari Viana hakuacha kumsifia Chriss.
" Jamani wazungu wapewe mauwa yao huwa hawana vifua vya kubeba beba Chuku yani ungekuwa ni wewe Jimmy usinge thubutu kunipa kazi . Nawaza sana watu wenye ngozi nyeusi .
" Kwani ulimfanya nini?
" Si ndio yule niliekwambia nilikutana naye nikamchamba na kuishia kumuita mdoli.
" Mmmmh chunga sana huo mdomo utakuponza.
Kesho yake mapema sana Viana alienda kuanza kazi huku akiwa kabeba mabegi yake.
Alimkuta Chriss ndio anajiandaa kwaajili ya kwenda kazini.
" Habari za asubuhi boss mzungu.
Chriss alitabasamu alafu akasema
" Salama, unaweza kuniita Chriss inatosha.
" Pole kama nakosea kukuita boss mzungu , nitatoa hilo jina mzungu nizakukuta tu boss maana kujutia jina lako peke yake nitakuwa nimekukosea heshima
" Chriss inatosha sana.
Jimmy atakueleza kila kitu cha kufanya hapa nyumbani.
" Sawa bo.... Chriss.
Baada ya kumaliza kuongea
Chriss alipiga hatua kulifuata gari lake lilipo na jimmy aliingia ndani akiwa kaongozana na Viana.
Walipofika sebleni Viana alisimama kwanza .
" Hebu subiri kuna kitu nimesahau kumuuliza Chriss.
Alitoka nje akamkuta Chriss ndio anawasha gari.
" Chriss, Chriss.... Aliita Viana huku akiwa anakimbilia gari ,Chriss alisimamisha gari akawa anamsubiri.
" Vipi kuna tatizo.
" Nilisahau kukuuliza jambo muhimu sana.
' jambo gani?
" Unapenda leo nikuandalie chakula gani?
" Mmmh niandalie ugali na dagaa, kuku wa kuoka mwenye viungo usisahau salad.
" Yani kachumbari na mandimu ya kutosha kitoke kitu mchapuko ukiweka mdomoni mpaka mwili wote unapata kusisimua.
" Mchapuko? Ni nini hiyo mchapuko?
" Yani uchachu uchachu kama vile limao, ndimu.
"Ok, Ndio. Alijibu Chriss huku akicheka.
" Usijali ukija utakuta vinakusubiri mezani.
" Sawa asante.
Ok bye mzungu uwe na kazi njema.
Alisema Viana huku akipunga mkono kisha akaingia ndani huku akiwa anakimbia , Chriss alimuangalia huku akicheka na kutingisha kichwa aliona bado Viana ana akili za kitoto.
: VIANNA
( Binti aliyebadilisha maisha ya playboy wa kizungu) 4
MTUNZI SMILE SHINE
" Bye mzungu uwe na kazi njema. Alisema Viana alafu akakimbia kuingia ndani. Chriss alicheka na kutingisha kichwa alimuona bado ana akili za kitoto .
Siku zilienda Viana aliendelea vizuri na kazi yake , Chriss alizidi kufurahia chakula alichoandaliwa na Viana .
Mara kwa mara chriss alikuwa akirudi nyumbani mapema alipata chakula baada ya hapo alienda kujiandaa alivalia vizuri tena nguo za gharama alafu alikuwa anatoka alikuwa anaenda sehemu za starehe na kuchukua wanawake na kwenda kumalizana nao hotelini alafu kesho yake mapema alirudi nyumbani .
Siku moja alirudi Mida ya saa kumi na moja asubuhi alikuta bado Viana amelala, alianza kumuita tangia akiwa mlangoni.
" Viana, Viana.....
Jimmy aliposikia alitoka na kwenda kuangalia imekuwaje Chriss amuite Viana moja kwa moja tena kwa sauti ya juu.
" Kuna shida gani?
" Wewe ndio Viana?
" Mmmh lakini huo uwitaji sio wa kistaarabu hata kidogo ukizingatia sasa hivi bado asubuhi watu bado wamelala.
" Jimmy niache nimechoka sana sitaki kupigishana kelele na wewe mwambie Viana nahitaji supu .
Aliongea Chriss huku akienda chumbani kwake na Jimmy alikuwa akimsindikiza kwa macho .
Wakati akapandisha ngazi alikutana na Viana.
" Ulikuwa unaniita?
" Kumbe umesikia kwanini haukuja mapema?
" Nilikuwa nahisi nipo ndotoni.
" Nenda kwa Jimmy atakupa maelekezo.
Viana alisogea pembeni akampisha apite ndipo nae akashuka chini akamkuta Jimmy kasimama.
" Amekwisha anakunywa pombe sasa anakuja kutuamsha asubuhi.
" Niandalie supu acha nikamuangalie huko chumbani.
" Sawa ila ongea na mzungu wako hapa ni Tanzania sio huko uzunguni kwao anakunywa ovyo ipo siku atakunywa pingu ajiharishie mimibaitashika uharo wa mtu mzima.
Jimmy alienda chumbani kwa Chriss na Viana alienda jikoni kuandaa supu.
Jimmy alifika chumbani kwa Chriss akamkuta kajilaza kitandani alijaribu kumuamsha lakini Chriss alijifanya Kalala fofofo hasikii kabisa.
" Najua unanisikia ila ujeuri tu na ukiendelea na hizi tabia zako za ajabu nitamwambia shangazi pia hautaweza kuishi na mtu hapa ndani Viana ni mfanyakazi wako haina maana umfokee unavyotaka.
Jimmy aliongea ikawa kama vile anaongea mwenyewe mwishowe aliondoka akaenda jikoni kwa Viana .
Alimkuta Viana anapika supu.
" Viana nisamehe mimi kwa kule kilichotokea .
" Usijali nikawaida nimegundua huwa akielewa akili yake inabadilika .
" Sijui ataacha lini hizi tabia zake za ulevi na kubadili wanawake kama vile anabadili nguo.
" Unasemaje jimmy , inamaana huyu mzungu anakitembeza haogopi maradhi? Mwambie ndugu yako hapa sio huko kwao ukimwi nnje nje yani niwakujizolea atarudi kwao Kakunda kama kijiti shauri yake.
" Wewe endelea kupika ikiwa tayari peleka chumbani kwake.
" Na wewe usiache kuongea nae.
Jimmy alitoka jikoni akamuacha Viana anaendelea kupika huku akiendelea kuongea mwenyewe kuhusu Chriss.
" Sikujua kama ni kuruka njia kumbe nae yumo namuonea huruma Chriss kwanza wanawake wa huku watamchuna mpaka ile ngozi yake wacha akifanya mjuaji hii ndio bongo bwana.
Supu ilipokuwa tayari Viana alibeba akaelekea chumbani kwa Chriss , alipofika mlangoni alisimama akagonga.
" Karibu. Alijibu Chriss akiwa kajilaza kitandani.
Viana aliingia na kuweka supu juu ya meza ndogo iliyokuwa karibu na kitanda.
Chriss alinyanyuka kitandani akakaa na kushukuru.
" Asante.
Viana alimuangalia jinsi alivyokuwa kachoka na macho yake kuwa mekundu , alimsikitikia na kutaka kuongea jambo lakini akasita na kupiga hatua ili kutoka pale chumbani , alipokaribia mlangoni akasikia anaitwa alisimama na kumgeukia Chriss .
" Abeee.
" Subiri kidogo.
Viana alisimama kusikiliza .
" Unajua kupika, wewe ni mpishi mzuri na bora sana , hivi imeshawahi kufikiria kufungua mgahawa?
Viana akitabasamu alijua zali linataka kumuangukia aliamini wazungu sio watu wa mchezo kwa kusaidia wapo vizuri na ukizingatia Chriss anatoka kwenye familia yenye pesa sana.
" Hapana sijawahi kufikiria kwa hii hali yangu pangu pa kavu , leo afadhali ya jana nitapata wapi mtaji wa kufungua mgahawa?
" Unatakiwa kufikiria sasa , hujui mambo jinsi yalivyo huko unaweza kupata maisha bora kuliko haya.
Viana alimuangalia huku akiwa amamsoma kama kile anachokiongea anamaanisha au ni akili ya pombe.
Wakati huo Chriss alichukua kijiko akaendelea kunywa supu.
" Mmmh huyu mbona sikuelewi anamaanisha nini kusema hivi au anataka kunifukuza kazi na ndio kwanza nina miezi miwili tu .
Akiwa bado anafikiria akasikia Chriss akisema.
" Haya maisha inayoishi sio yako Viana ni yangu , ipo siku utachoka italazimika kuondoka haijalishi utaondoka kwa kheri au kwa Shari.
Maneno ya Chriss yalimchoma Viana mithili ya mafuta ya moto, hakuwa na nguvu ya kuongea tena alimsogelea mlango akashuka kitasa akafungua mlango na kutoka nje kimnya kimnya.
Akienda kukaa nje kwenye ngazi akiwa anatafakari maneno ya Chriss mara Jimmy alimuona na kumsogelea karibu lakini Viana alikuwa mbali sana kimawazo huku mkono wake ukiwa shavuni.
Jimmy alitoa mkono shavuni kwa Viana
" Unawaza nini mpaka ukae kama mwana mkiwa?
" Nawaza mengi sana sijui hata ya hii kazi ni ipi.
" Kwanini unasema hivyo, Chriss kakuvunjia tena heshima?
" Hapana lakini kuna mambo jaingea yani ni kama vile mtu anayetaka kufa sasa anatoa wasia....
" Unamaana gani kusema hivyo?
" Ameniambia haya sio maisha yangu ni yake ipo siku nitaondoka hivyo natakiwa kujipanga.
Jimmy alicheka alafu akasema
" Kasema hivyo tu?
" Ndio
" Hayo ni maneno ya kawaida alafu ukizingatia yule kalewa.
" Lakini kumbuka walevi huwa wanaongea kweli maana hawana aibu.
VIANNA
( Binti aliyebadilisha maisha ya playboy wa kizungu) 5
MTUNZI SMILE SHINE
Jimmy alimuangalia Viana akahisi hakusikia vizuri kutokana na maneno ya Chriss na ilionekana aliyapa uzito sana.
Jimmy alimshika begani, Viana alimuangalia usoni kisha Jimmy akasema
" Hiyo ni misemo ya watu usiyaoe uzito maneno ya Chriss.
" Kumbuka ugali wangu upo hapa kupata hati sehemu nyingine sio rahisi kama unavyofikiria.
" Najua lakini hutakiwi kujipa wasiwasi kiasi hicho acha Chriss apumzike tutajua alikuwa anamaana gani huwezi jua labda anataka kukufungulia mgahawa.
" Sijui.
Baada ya masaa mawili kupita Chriss alikuwa kashaamka alitoka nje akakaa bustani kupunga upepo huku akiwa na grass ya juice .
Jimmy alimfuata na kuungana nae.
" Vipi upo sawa?
" Nipo sawa.
Jimmy alimuangalia huku akitafakari aanzie wapi kuongea.
" Mbona unaniangalia hivyo?
" Chriss umesahau ahadi yako uliyoniahidi kipindi umefika Tanzania?
Chriss alitulia huku akiwa anamuangalia kisha akasema
" Nakumbuka kila kitu.
" Acha nikumbushe huenda ukawa umesahau.
Kwanza baba yako hakutaka usimamie mali yake yoyote alitaka itafute pesa yako , uchezee pesa ukiyoitafuta mwenyewe kwa jasho lako, lakini mama yako alikumbwa sana kwa baba yako akupe jengo la CROWN usimamie kwa kumuahidi baba yako kuwa utafanya kazi kwa bidii na itaachana na mambo yako ya starehe.
Na wewe iliwaahidi wazazi wako. Pia na mimi kuwa utafanya kazi kwa bidii na kweli ulifanya hivyo lakini sasa naona unajisahau unataka kurudi kulekule.
" Jimmy mimi ni mtu ninaejitambua sio mtoto naelewa nini nafanya tafadhali niache na maisha yangu.
" Sawa lakini hii ni Tanzania watajifunza adabu.
" Hakuna cha ajabu kwangu na hakuna wa kujifunza hiyo adabu wameshindwa wazazi wangu wataweza hawa watanzania ambao hawana wanachojua zaidi ya kutaka pesa tu.
Jimmy alichukizwa na kauli ya Chriss pia Viana alikuwa amebeba sinia la nyama choma anawaelekeza alisikia pia hakupenda ile kauli ya kuwasemea vibaya mabinti wa nchi yao.
Alifika akaweka sinia la nyama mezani alafu akataka kuondoka kisha akasita kidogo akageuka nyuma .
" Jimmy nilikuwa nakuomba mara moja.
Jimmy alinyanyuka akamfuata Viana.
Walienda jikoni na kusimama .
" Eeeh
" Huyu mzungu wako ana kiburi flani kuna jambo nimefukiria linaweza kumfunga adabu na kumfanya abadilike.
" Jambo gani?
Jimmy alikuwa makini kusikiliza mpango wa Viana.
" Kwanini tusifanye mpango tunatafuta mtu wa kuwa nae baada ya hapo amchukulie kila kitu hapo ndipo anashika adabu , yani amchukulie mpaka pale languo kidogo la ndani .
Jimmy alimuangalia Viana anavyoongea kwa umakini alafu akacheka.
" Unefikiria nini mpaka ukawa za hivyo?
" Ni wazo tu limekuja . Akidhalilika mara mbili mara tatu atajifungua kitu.
" Sawa ningependa wazo lako sasa tunafanyaje kumpata mtu wa kuifanya hiyo kazi?
" Hiyo kazi niachie mimi kuna watoto wa Manzese, vita wanaoweza hizo kazi na watazifanyia kwa ufasaha .
" Poa basi kila kitu na kuachia wewe utanipa tu mrejesho, lakini naomba wasije wakamdhuru.
" Hakuna wa kumdhuru ni kumfunza adabu tu.
" Sawa na kuachia wewe.
Baada ya siku mbili kupita nyumbani kwa Chriss kulikuwa na ugeni alikuwa ni Jenipha rafiki yake Viana.
" Shoga yangu umebahatika kupata kazi kwa mzungu sisi wenzio tunasota huko mtaani.
" Usinionee wivu mwenyewe bado sijajipata alafu kuna mpango nataka kupangwa.
" Ni kuhusu pesa ?
" Najua bure huwezi kufanya nitakupa elfu 30 unifanyie kazi moja ndogo tu.
" Kazi gani?
" Huyu boss wangu ni kicheche sana anapenda sana wanawake bila shaka alikiona wewe kwa jinsi ulivyo lazima atakutamani. Nataka umtege aliingia kwenye mitego yako utaenda kulala nae huko itamchukulia kila kitu yani muache mweupe alafu ondoka zako.
" Eheeee alafu baada ya hapo?
" Hivyo vitu nitavifuata kwako.
" Hiyo kazi ni kubwa hailingani na pesa utakayonipa utaniongeza shilingi ngapi?
" Wewe nae unapenda sana hela ukasahau kama unanisaidia mimi rafiki yako.
" Wewe mwenyewe unapenda hela ukute umepewa hela nyingi ukazibania unaona 30 unanitisha hiyo ni pesa ndogo sana.
" Basi nitakupa 50.
" Sawa nipe nusu nianze kazi.
Wakiwa wanaendelea kuongea mara chriss aliingia .
" Hallow.
" Hallow, Chriss huyu ni rafiki yangu anaitwa Jenipha.
" Waoooo she is so beautiful, karibu sana Jenipha.
" Asante . Alijibu Jenipha huku akimuangalia kwa jicho flani lenye ushawishi na tabasamu mwanana usoni mwake. Pia Chriss aliachia tabasamu akajua mtoto anata kujichanganya na mwenyewe habipiwi anapiga.
Viana alivyoona vile alinyanyuka akaelekea jikoni ili kumpa nafasi Jenipha afanye kazi yake kwa uhuru. Jenipha hakutaka kupoteza muda alianza kulegeza macho kuku akimuangalia Chriss usoni.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote