VIP ROOM π
UTANIPENDA ZAIDI YA NINAVYOKUPENDA
Lulu binti anaejiheshimu , kujipenda na mwenye kujituma anapata ajira kwenye kampuni moja ya uandaaji wa filamu huko anakutana na kijana Adrian kijana mtanashati, tajiri ambae yupo kwenye tasnia ya uigizaji kwaajili ni hobby yake na sio kazi anayotegemea. Adrian anapendwa sana na wanawake hapo ndipo anatumia hiyo nafasi kutembea na mabinti warembo kisha anawaachia.
Siku Adrian alipokutana na Lulu macho yakimtoka kwa kuishangaa urembo wake na sauti yake tamu ya kumtoa nyoka langoni, anajaribu kurusha ndoano ili kumpata Lulu lakini Lulu anakataa na kudai anamfahamu sana adriz kuliko anavyojifahamu mwenyewe pia hawezi ku date na mwanaume maarufu.
Siku moja Lulu akiwa club na wenzie walipewa ofa ya bia ,walikuwa sana mpaka ikapelekea wakawa hawajitambui. Kesho yake Lulu anajikuta yupo chumbani VIP ROOM tena akiwa kama alivyozaliwa na hakukuwa na mtu mwingine lakini pembeni anakuta kukuza cha pesa.
Kuna siku Lulu alikuwa anatoka kazini akakuta nyumba yao inapigwa mnada mama na mdogo wake walikuwa wanalia, Lulu hakuwa na lakufanya.
Mara anapigiwa simu na mtu asiyemjua na kumtaka aende peace hotel kwaajili ya kumsaidia.
Lulu anaenda peace hotel anaongozwa tena VIP ROOM huko anakutana na mwanaume aliyevalia nadhifu marashi ya gharama akiwa kasimama akiwa kampa mgongo.
Alikuwa na shauku ya kumjua ni nani lakini kwa bahati mbaya yule mtu alikuwa kavaa maski na sauti yake ilikuwa inachukuwa na kifaa haikuwa sauti yake halisi.
Yule mwanaume anamsaidia kulipa milioni 15 lakini endapo atakubali kulala nae tena.
Kwakuwa Lulu alikuwa anashinda alikubali .
Baada ya mwezi Lulu anajifungua ana ujauzito wa mwanaume asiekufahamu .
Je Lulu atafanya nini ? Na atampataje huyo mwanaume?
VIP ROOM π 1
MTUNZI SMILE SHINE
Adrian ni kijana mashuhuri anayetoka kwenye familia inayojiweza kiuchumi, wazazi wake walimiliki makampuni makubwa pia hotel kubwa , licha ya kuwa anatoka katika familia inayojiweza pia alikuwa ni mtu mashuhuri sana kutokana na kazi yake ya uchezaji wa filamu na uigizaji wa tamthiria.
Adrian alikuwa mchezaji mzuri wa filamu na tamthilia za mapenzi , na zenye maudhui mbalimbali mashabiki wake wengi walikuwa ni wanawake. Kila alipopita walimpokea kwa furaha na wengine walitaka kupiga nae picha nae hakuwa mtu wa kujisifia mbele ya mashabiki zake aliwapa nafasi ya kupiga nao picha pamoja.
Kuna baadhi ya wanawake walikuwa wakimtafuta na kumtaka kimapenzi lakini licha ya kuwa anapendwa sana na wanawake wa kila aina lakini yeye alikuwa anavutiwa na aina ya wanawake warembo. Wanaojipenda , wenye maumbo na sura nzuri . Kwakuwa alikuwa anamaliza haja zake hivyo hakuwahi kufikiria kuwa na mwanamke mmoja walitulia nae wala kuowa. Familia yake ilimsihi sana aowe mpaka kufikia hatua ya kumtafutia wachumba , Adrian hakuwa anakataa aliwakubali na kuwashawishi akishalala nao aliachana nao wazazi wake walichokaa wakaamua kumuacha mpaka atakapoamua yeye kutulia na mwanamke mmoja.
Upande wa pili kulikuwa na dada mmoja mrembo anaitwa Lulu ana miaka 25 ni binti mchachalikaji anaejituma hachagui kazi ya kufanya mladi iwe halali na inayomuingizia kipato kwajili ya kunisaidia familia yake yani mama na mdogo wake Anayeitwa ruby.
Kwa wakati huo Lulu alikuwa kajushikiza kwenye saloon ya rafiki yake .
Siku moja akiwa ananauka mteja kuna mama mmoja alikuwa kakaa pembeni anamuangalia.
"Lulu naona inajitahidi sana kwenye maswala ya urembo unaonaje kama utapata nafasi kwenye kampuni moja ya uandaaji wa filamu uwe kwaajili ya kuwaandaa wachezaji wa , filamu na tamthilia?
" Nitashukuru sana kama itanisaidia kupata hiyo kazi .
" Basi nikakupatia namba yangu kesho tuonane nikakupeleke kwa wahusika wakuu.
" Sawa mama.
Lulu alimpatia namba zake za simu nae akachukua za yule mwanamke.
Kesho mapema sana Lulu akijiandaa akaenda kukutana na yule mwanamke wakaenda mpaka kwenye kampuni ya HARISI entertainment . Huko alikutana na wahusika na kwa bahati nzuri alipata nafasi ya kazi na kuambiwa anatakiwa kuanza kazi kesho mapema.
Kuku alishukuru na kufurahi sana kupata kazi kwenye maarufu kama ile na ulipaji wao ulikuwa mzuri.
Siku iliyofuata wakiwa wanajiandaa kwaajili ya kushoot Adrian alikuwa kwenye chumba cha kubadili nguo akisubiri kuhudumiwa, alipoona muda unaenda aliuliza
" Hey jamani huyo mtu wa kuja kuniandaa yupo wapi?
" Tulia kidogo anakuja muda sio mrefu.
" Nimechoka kusubiri.
" Yeye ni mgeni bado hajajua ratiba zinaendaje.
" Kwahiyo ni mpya kwenye hii kampuni?
" Ndio Maria ameondoka hafanyi kazi hapa.
" Mna nichosha mnajua nina mambo mengi sana yakufanya.
" Tunajua tunaomba uvumilivu kidogo.
Waliongea upole kwasababu wanajua Adrian hakuwepo pale kwaajili ya njaa bali ni hobby yake ya uigizaji.
Lulu alikuwa anakimbia huku akiwa kabeba mkoba wake akawa anaelekea chumba alichokuwa Adrian, alimkuta Adrian akiwa kasimama dirishani anaangalia nje.
" Habari, samahani kwa kuchelewa. Alisalimia Lulu huku akiwa anaweka vitu vyake mezani.
Sauti nyororo ya Lulu ilipenya vyema kwenye masikio ya aAdrian na kumfanya ageuke haraka kumuangalia mwanamke mwenye sauti nyororo iliyo msisimua.
Adrian hakuitikiwa ile salamu alipiga hatua ndogo mpaka alipo Lulu, wakati huo Lulu alikuwa anatoa vitu vyake kutoka kwenye pochi yake na kuviweka mezani kwaajili ya kuanza kazi. Adrian alisimama akawa anamuangalia na Lulu hakumuangalia aliendelea na kazi yake kwa kuwa alikuwa amechelewa na alikuwa akisubiri wa yeye tu.
" Samahani unaweza kukaa kwenye kiti? Lulu alimwambia lakini
Adrian hakukaa aliendelea kumuangalia usoni kama vile anashangaa kitu. Ilibidi Lulu amuangalie usoni alipogundua ni msanii maarufu aliachia aliachia tabasamu lake mwanana na kusema.
" Samahani naomba ukae unasumbuliwa wewe huko nje.
" Sura yako na sauti yako ni mgeni masikioni mwangu wewe ni nani ?
" Ni mfanyakazi mpya wa hapa naitwa Lulu.
" Waoooo sio utani kweli wewe ni Lulu aliekuwa jina hakukosea kabisa akilenga mulemule, nimefurahi kukufahamu , naitwa.....
" Hakuna asiekufahamu mr aAdrian naomba tuokoe muda tafadhali.
Adrian aliachia tabasamu kisha akakaa kwenye kiti lakini macho yake yote yalikuwa kwa Lulu ,lakini Lulu hakujali hata kidogo alikuwa anafanya kazi yake kwa makini sana maana alijua akiharibu kibarua chake kitaota nyasi.
Alipomaliza kumuweka sawa maeneo ya usoni alimuomba asimame ili amvalishe nguo alivyotakiwa kuvaa. Kabla ya kumvalisha alichukua kitambaa na kumfuta kifuani.
" Vipi haujavutiwa na kifua cha mwanaume? Adrian aliuliza.
Lulu alimuangalia usoni akajua Adrian anataka kuanza ujinga wake na alikuwa anajua taarifa zake za kuwavuruga watoto wa kike na kuwaacha kwa jeuri.
" Nimeona vifua vingi vyenye mvuto hiki chako ni chakawaida sana .
Adrian alishusha pumzi na kuachia tabasamu alafu akanyanyuka mikono yake na kuzisogeza nywele ndefu za Lulu kwa pembeni.
" Lulu hakushituka aliendelea kumuhudumia huku akijisemea
" Wewe jichetue uwezavyo lakini mimi ni habari nyingine sitetereshwi na vishindo vyako.
Lulu alimaliza kumuandaa alipomaliza alimuangalia usoni alafu akamwambia.
" Nadhani kazi yangu imekamilika unaweza kwenda sasa.
" Asante sana mrembo nimefurahishwa na huduma yako unanifaa. Alisema Adrian huku akimsogelea na kutaka kukutanisha midomo yake na ya Lulu lakini Lulu aliwahi kunyanyua mkono na kuusogeza pembeni uso wa Adrian kisha akaenda kuchukua vifaa vyake na kutoka nje.
Adrian alimuangalia huku akitabasamu na kujisemea
" Ni mrembo sana ana sifa za mwanamke ninaemuhutaji lakini Inaonekana ni kasumbufu sana lakini nitafanya niwezavyo kufanikisha ninachokitaka kutoka kwake mimi ndio Adrian bwana.
Lalalalala......
Adrian alitoka ndani ya kile chumba huku akiimba na kwenda kuendelea kushoot. Wakati huo Lulu alikuwa kakaa pembeni akiwaangalia endapo itatokea kuna marekebisho aende kurekebisha
Adrian alikuwa akiingiza walipoambiwa watulie kwanza alihitaji kuwekwa sawa na mtu wa kumuhudumia alikuwa ni Lulu.
Kuna wakati Lulu alichokaa maana alikuwa yupo sawa lakini ilikuwa ni usumbufu tu.
" Hata sijui unataka nikurekebishe vipi wakati upo vizuri tu .
" Lulu ni vizuri ukafanya kazi yako maana hii ndio kazi inayokupa ugali na usisahau kuwa upo hapa kwaajili ya kuniangalia mimi , alafu naweza nikakulipa zaidi kama utani hudumia vizuri.
" Haina haja ya wewe kunilipa maana alieniajiri ndio anatakiwa kubeba jukumu la kunilipa.
Adrian alimuangalia Lulu usoni . Lakini Lulu alikuwa bize na kazi yake.
" Upo tofauti sana na wengine nimeipenda hiyo na unanivutia zaidi kwa jinsi unavyojiamini.
Lulu alimuangalia usoni alafu akatabasamu
" Hapo ndio unatakiwa kujua kuwa kuna mifupa mingine hata fisi hawezi kuivunja. Kazi njema mr Adrian.
Alisema Lulu alafu akaondoka na Adrian alimuangalia mpaka aliposhituliwa kwaajili ya kwenda kuendelea kushoot.
Siku moja wakiwa kwenye jumba la mazoezi Lulu alikuwa kasimama sehemu huku akiwa kaegemeza chuma mara adrian alimfuata .
" Baada ya kutoka hapa unaenda wapi?
" Mimi bado nipo hapa sina mpango wa kuondoka sasa hivi.
" Basi vizuri tunaweza tukakaa pamoja.
Lulu alimkazia macho usoni.
" Vipi mbona unaniangalia hivyo?
" Na kushangaa , unajua bado sijapata jibu kuwa unashindwa gani na mimi maana unanifuatilia sana .
" Sasa kwanini nikufuatilie?
" Jibu unalo wewe.
" Napenda kuwa karibu na wewe kwasababu kuna baadhi ya mambo nimevutiwa nayo kutoka kwako lakini kikubwa zaidi ambacho kimenivutia na sijawahi kukutana na binti mwenye tabia kama yako ni hicho Kibiti chako kina nipa hamasa ya kutaka kukujua zaidi, unajua inafikia wakati nashindwa hata kupata usingizi kwaajili ya kutafakari wewe.
VIP ROOM π 2
MTUNZI SMILE SHINE
Lulu alimuangalia adrian kisha akaanza kucheka.
" Unacheka nini sasa?
" Huoni kama unachekesha? Sikuwa hata na mpango wa kucheka hivi ila maneno yako yamekuwa kichekesho kwangu.
" Sio mbaya kama nimekuwa kichekesho mbele ya mwanamke mrembo kama wewe.
" Ngoja nikwambie kitu Adrian kwangu inapoteza muda tu kwasababu mimi siwezi kuwa na wewe kwanza Watu wanaondoka itakuwa vizuri na wewe ukaenda .
" Vipi wewe kuhusu kuondoka?
" Nimekuambia bado nipo.
" Basi hata mimi sina haraka nitakuwa hapa na wewe mpaka utakapoamua kuondoka.
" Kwani huna kazi nyingine za kufanya?
" Hazina umuhimu kama nikiwa hapa na wewe.
Lulu alimuangalia kwa dharau alafu akachukua pochi yake na kuiweka begani kisha akaondoka.
Adrian alimuangalia huku aling'ata midomo yake ya chini.
" Hakuna mwanamke alie wahi kunikataa Lulu utaingia kwenye njia zangu bila wewe kujua.
Siku moja usiku adrian alitoka alienda club huko alikutana na wenzie wakawa wamekaa sehemu wanapata vinywaji huku wakisindikizwa na muziki na story za hapa na pale.
" Niliwaambia hapa mjini hakuna club ya kijana kama hii kwanza angalia kuna watoto wakali na kila siku pisi mpya zinakuja hapa ushindwe nyie vidume.
Alex aliwaambia wakina Adrian.
" Ni kweli imechangamka lakini watoto wa kiswahili wamejaa kwa hadhi yangu haifai . Alisema Adrian.
" Hapa ndio penyewe sasa sio kule kwa kuku wa kizungu kila siku jaribu na wakienyeji uone radha yake.
Katika kuangalia huku na kule akiangalia wadada warembo si Adrian akamuona Lulu akiwa na wenzie wawili wamekaa sehemu wanapata vinywaji, adrian aliachia tabasamu kisha akanyanyuka na kuchukua grass yake na kwenda kuungana na wakina Lulu.
" Habari warembo.
Adrian alisalimua .
" Waoooo Adrian siamini kukuona mahali hapa mimi ni shabiki yako mkubwa. Naylah rafiki yake lulu alimwambia adrian huku akiwa haamini , Adri aliachia tabasamu kisha akasema
" Asante. Adrian alishukuru alafu akamgeukia Lulu.
" Lulu kumbe huwa unakuja sehemu kama hizi?
" Ni kawaida yangu kujasehemu kama hizi kwaajili ya kulifresh Mind na kufurahi na marafiki kama unapotuona hapa.
" Safi nimefurahi kukuona. Tunaweza kwenda kucheza kidogo?
" Hapana .
Adrian alimsogelea karibu na sikio na kumuongoza.
" Usinifanye hivyo mbele ya wenzako jaribu kunipa heshima kidogo. Adrian alipomaliza kuongea aliushika mkono wa Lulu , Lulu alisimama kwa lazima kitendo cha kusimama adrian alipingisha mkono wake kiunoni kwa lulu na kumvutia sehemu ya wazi wakaanza kucheza.
" Cheza basi .
" Kwanini unanilazimisha kufanya vitu ambavyo sipendi?
" Pole kama hupendi lakini mimi nafurahia sana kuwa karibu na wewe naomba unipe nafasi niwe mpangaji kwenye moyo wako.
Lulu akicheka kwa dharau
" Hilo sahau siwezi kuwa na uhusiano na mtu maarufu kama wewe , siwezi kuweka moyo wangu rehani.
" Umaarufu hauzuii mimi kukupenda , nakupenda sana Lulu .
Lulu alimsukuma kisha akaondoka na kumuacha adrian alimuangalia
Kama vile alikuwa anampigia mahesabu.
" Lulu sijawahi kusota kwaajili ya kumfuatilia mwanamke nitakupata kwa gharama zozote zile.
Lulu alirudi kukaa na wenzake na Adrian alienda kukaa VIP na rafiki zake wakaendelea kunywa champagne na wenzake lakini macho yake yalikuwa kwa Lulu alimuangalia alivyokuwa anacheka na kuongea na wenzake huku wakiendelea kunywa.
Baada ya muda Adrian alimfuata muhudumu mmoja.
" Unawaona wale mabinti watatu pale?
" Ndio.
" Kawaongezee vinywaji , wanywe vinywaji wanavyotaka bili ni juu yangu.
" Sawa boss.
Lulu na wenzie waliendelea kufurahia walinyanyuka na kucheza mara muhudumu alifika kwenye meza yao akiwa na vinywaji kama walivyokuwa wanakunywa.
" Hivi vinywaji nani kaagiza? Naylah aliuliza
" Kuna mtu amesema niwaletee na mkihitaji zaidi mseme bili ni juu yake.
" Atakuwa ni huyu super stars asiejielewa.
Alisema Lulu
" Unamaanisha Adrian?
" Ndio.
" Sasa kuna shida gani tunywe leo tumepata ofa kutoka kwa mtu maarufu.
Waliendelea kunywa kadri wawezavyo mara Lulu alianza kulewa alianza kuchangamka alinyanyuka na kwenda kucheza .
Baada ya kucheza sana alianza kunisikia vibaya akaekejea chooni huko alitapika sana mpaka akaishia nguvu alijikokita mpaka nje ya choo akakaa chini mara alimuona yule muhudumu amesimama pembeni yake.
" Naweza kukusaidia?
" Sawa.
Muhudumu akimsaidia kunyanyuka wakatoka nje mara kuna gari ilifika yule muhudumu akampandisha.
" Mnanipeleka wapi? Aliuliza Lulu kwa sauti ya kilevi
" Unaenda sehemu salama usijali.
Ile gari iliondoka mpaka kwenye hoteli moja kubwa maarufu hapo jijini Peace hotel.
Walipofika Alichukuliwa na kuingizwa ndani ya lift wakati huo hakuwa na kalegea hajitambui akapelekwa moja kwa moja kwenye chumba maalumu akalazwa hapo . Baada ya kulazwa kitandani alisogea mwana ile mmoja akakaa pembeni yake na kupapasa uso wa Lulu huku akimuangalia kwa matamanio.
Kuanzia hapo Lulu hakuwa anaejitambua .
Alishituka asubuhi akajikuta yupo sehemu ambayo haijui, kilikuwa ni chumba kikubwa na kizuri sana ,alikuwa kafunikwa vizuri na duvet nyeupe.
" Nimefikaje hapa? Alijiuliza huku akiendelea kukagua ndani ya kile chumba, alipotaka kunyanyuka akajikuta hana nguo hata moja alikuwa kama alivyozaliwa
" Mungu wangu nimefanya nini mimi?
Alijaribu kuvuta kumbukumbu akakumbuka jana usiku alikuwa na mwanaume lakini hakujua huyo mwanaume alikuwa ni nani.
Alinyanyuka pale kitandani akaenda bafuni kuoga alipomaliza alirudi chumbani alipoanhalia kwenye meza alikuta kiasi cha pesa .
" Inamaana huyu mtu ananifanyia hivi na malipo yangu ni haya ?
Lulu alionekana kuumia sana kulala na mtu ambae hakumjua lakini hakuwa na jinsi aliamua kuondoka . Alipotoka pale ndani alifunga mlango, alipoangalia mlangoni aligundua haukuwa na namba uliandikwa VIP ROOM.
VIP ROOM π 3
MTUNZI SMILE SHINE
Lulu alirudi nyumbani kwao akiwa hana furaha, alipoingia ndani hakukutwa mtu alipitiliza chumbani kwake akajilaza kitandani huku akiwa anaangalia juu akawa anatafakari kilichotokea jana usiku huenda akatambua mtu aliye lala nae jana usiku.
Baada ya kufikiria sana na kukosa majibu alikumbuka kuwa jana alikuwa na marafiki zake akaamua kumpigia simu Caroline.
" Hallow. Aliongea Caroline kama mtu ambae katoka usingizini.
" Mbona umelala mpaka muda huu?
"Mmmh jana tulikuwa sana nahisi uchovu sana.
" Kuna kitu nataka kukuuliza
" Uliza
" Jana niliandika na mwanaume gani pale club?
" Mwanaume? Kwani uliondoka na mwanaume?
" Naomba unijibu badala ya kuniuliza maswali.
" Mimi sijui kila mtu aliondoka mwenyewe pale.
"Sawa.
Alijibu Lulu alafu akakata simu.
" Kila mtu alikuwa hajitambui. Au adrian atakuwa anahusika na hili? Lakini mbona aliondoka mapema?
Kuku aliendelea kuumiza kichwa lakini hakupata jibu .
" Acha nifanye kama ajali sipaswi kufikiria hili swala litaniumiza kichwa .
Lulu aliachana na hayo mawazo akapanda kitandani ili alale mara mama yake akaingia.
" Lulu umelala wapi?
" Shikamoo mama...
" Nakuuliza umelala wapi sijajaa hapa ndani kusalimiana.
" Nilikuwa kazini tulikuwa tuna shoot.
" Ulimpa nani taarifa kama itaingia kazini usiku au ndio unajiona umekuwa unamaamuzi ya kufanya chochote?
" Nisamehe mama nilipitiwa.
" Lulu wewe bado upo kwenye himaya yangu unatakiwa kufuata sheria za hapa ndani sijui tunaelewana?
" Ndio mama nimekuelewa.
" Hiyo tabia ikome kabisa.
Mama yake Lulu aliondoka huku akiendelea kufoka.
Kesho yake Lulu akiwa kazini akiandaa waigizaji Adrian walikuwa akimuangalia sana Lulu na hakutaka kuandaliwa na mtu mwingine zaidi ya Lulu na Lulu hakuwa anataka kumuandaa kwa siku .
" Adrian mbona umesimama muda unaenda tunatakiwa to shoot muda huu.
" Namsubiri Lulu yeye ndio ananipatia.
Lulu alimuangalia kisha akaendelea kumuandaa mtu ambae alikuwa anamalizia.
" Lulu fanya chapu kidogo na kusubiri hapa .
Kwakuwa amesajiliwa kwa kazi hiyo na anayetaka ni star mkubwa Lulu aliamua kukubali kumhudumia.
" Njoo ukae.
Adrian alienda kukaa Lulu akawa anaendelea na kazi yake.
" Lulu naomba tuzungumze baada ya kumaliza kushoot.
" Unataka tuzungumze kitu gani?
" Unajua nini nataka kutoka kwako lakini sijui kwanini unanifanyia nipe nafasi nipende kama mimi ninavyokupenda.
" Hilo sahau siwezi kuwa na wewe hata kwa bahati mbaya nimeshakwambia mimi na watu maarufu siendani nao kabisa.
" Achana na umaarufu wangu angalia ni kiasi gani nakupenda.
" Sitaki kupendwa na wewe.
" Sawa lakini tambua ipo siku itakuja kwangu na utanipenda zaidi ya ninivyokuoenda mimi.
Kuku aliachia tabasamu huku akiendelea kumuweka sawa.
" Nadhani nimeshamaliza unaweza kwenda kuendelea na kazi nakutakiwa kila la heri.
" Asante mpenzi. Alijibu Adrian huku akiwa anataka kumbusu , Lulu akawahi kuzuia na kiganja cha mkono wake.
"Haya maneno uliloniambia mara ya mwisho itakuja kuniambia tena tukiwa chumbani kwetu.
Alisema Adrian kisha akaondoka.
Siku zilizidi kwenda siku moja Lulu alikuwa anatoka kazini akakuta nyumbani kwao vitu vinatolewa nje nyumba mama na mdogo wake Ruby walikuwa wamesimama pembeni huku wakiwa wanalia, Lulu aliwafuata .
" Mama nini kinaendelea mbona vitu vyetu vinatolewa nje?
" Tunatakiwa tuondoke nyumba inatakiwa kuuzwa si unakumbuka tulichukulia mkopo .
Lulu alitishiwa nguvu akakaa chini akawa anaangalia jinsi vitu vinavyotolewa nje. Akiwa haelewi nini cha kufanya simu yake iliita aliekuwa anapiga hakumjua namba ilikuwa ngeni.
Baada ya simu kuita mara kadhaa aliamua kupokea
" Hallow
" Najua una matatizo na unahitaji msaada je naweza kukusaidia?
Lulu kusikia hivyo alikaa vizuri.
" Kwanza wewe ni nani na imekuwaje nina matatizo?
" Kama una hitaji msaada wangu ili nyumba yenu isipigwe mnada basi njoo peace hotel sasa hivi.
" Lakini muda hauruhusu hawa watu wanatoa kila kitu.
" Kwahiyo ukiendelea kukaa hapo utanusuru nyumba isiuzwe?
Lulu alimnyanaza.
" Unakuja au Hauji?
" Sawa nakuja.
Lulu alibeba pochi yake akaondoka mpaka peace hotel alipofika alipiga ile namba .
" Hallow nimeshafika nipo hapa nje.
" Njoo mapokezi kuna muhudumu atakuleta nilipo.
" Sawa. Lulu alikata simu kisha akaenda mpaka mapokezi ile amefika tu kuna muhudumu alifika .
" Habari
" Salama
" Sijui naongea na miss Lulu?
" Ndio
" Ok nifuate.
Yule muhudumu alitangulia na Lulu akawa anamfuta nyuma. Walipanda lift mpaka ghorofa ya nne, walishuka kwenye lift na kuongozana mpaka kwenye mlango wa chumba kimoja , hicho chumba hakikuwa kigeni machoni kwa kilikuwa ni chumba kile kile cha VIP. Yule muhudumu alifungua mlango Lulu akawa bado kasimama nje huku akiwa anamchungulia kwa mbali.
VIP ROOM π 4
MTUNZI SMILE SHINE
Lulu aliogopa kuingia pake ndani hasa akikumbuka tukio lililotokea nyuma
" Karibu miss Lulu ingia. Yule muhudumu alimkaribisha
Lulu alipiga hatua ndogo ndogo kuingia ndani ya kile chumba , aliingia huku anaangaza macho chumba kilikuwa ni kile kile alichokikuta Kalala siku chache zilizopita
Alipoanhalia upande wa dirishani alimuona mwanaume kasimama mbele ya dirisha akiwa kavalia suti yake safi ya gharama huku akiwa kuwapa mgongo anaangalia nje
" Boss miss Lulu yupo hapa.
" Sawa unaweza kutupisha.
Ilikuwa ni sauti nzito ya yule mwanaume.
Baada ya muhudumu kuondoka na kufunga mlango ndipo yule mwanaume aligeuka kumuangalia Lulu lakini uso wake ulikuwa umefunikwa na maski.
" Karibu ukae Lulu.
" Kabla ya kukaa unaweza kuniambia wewe ni nani au unaweza kutoa hicho kinyago usoni kwako?
" Hivyo vyote unavyotaka sio muhimu kwa leo Lulu. Kilicho muhimu kwa sasa ni wewe kuokoa nyumba yenu isipigwe mnada
" Sawa ulikuwa unasemaje?
Yule mwanaume alimsogelea Lulu kisha akasema
" Tunaweza kufanya kile tulichokifanya mara ya kwanza alafu nikulipe million 15 za kukomboa nyumba yenu?
Lulu alimuangalia huku akiwa kakunja uso na kumuuliza
"Kwani lazima tufanye hivyo ndio unisaidie?
" Mmmh maamuzi unayo wewe kama hutaki unaweza kwenda na ukikubali sasa hivi nampiga simu moja tu kwa meneja wa bank kila kitu kinarudi ndani na nyumba inabaki kuwa yenu.
Lulu alifikiria hawana uwezo wa kulipa hiyo pesa na ukizingatia maisha yao yote wanategemea kwenye ile nyumba kutokana na kodi ya wapangaji wao wawili wakiweza kulipa ada ya Ruby akaona bora akubali kuliko kuona wanaenda kudhalilika na hakuwahi kutamani kuishi nyumba za kupanga kutokana na kero za wenye nyumba wengine sio wastaarabu.
" Sawa ila nataka uthibitisho kuwa nyumba itabaki kuwa yetu.
Yule mwanaume alichukua simu na kupiga sehemu akasema waache kutoa viombo deni limeshalipwa.
Baada ya kuongea alikata simu na kusema
" Done
Lulu alishangaa inakuwaje kauli yake moja waachiwe nyumba yao.
'" ina maana hapo umeshamaliza kutoa maagizo na nyumba itarudi kuwa yetu?
" Ndio .
" Siamini.
" Nipigie mtu yoyote wa nyumbani kwenu muulize.
Lulu huku akichukua simu yake na kumpigia mama yake.
" Hallow mama....
" Lulu uko wapi nakutafuta ili tirudushe vitu ndani inasemekana deni letu limelipwa sijui ni mtu gani huyo aliguswa na mimi mjane ..... Lulu hakutaka kuendelea kusikiliza maneno ya mama yake alikata simu.
aligeuka kumuangalia yule mwanaume.
Mama yake alipiga tena simu.
" Mbona umenikatia simu?
" Nipo mbali kidogo nitakuja badae.
" Huko mbali ni wapi wewe mtoto?
"Nikija tutaongea mama
Lulu alikata simu na kushukuru
" Asante.
Sasa ilifika zamu yake kutimiza kile walichokubaliana alisogea kitandani na kuvua nguo zake yule mwanaume alisogea kitandani wakamalizana huku yule mwanaume akiwa na maski yake usoni.
Baada ya kumaliza Lulu akienda bafuni kuoga alipomaliza alivaa nguo zake na kutaka kuondoka.
" Asante sana Lulu kwakuwa umenifurahisha zaidi ya nilivyotegemea basi chukua na hiki kiasi cha pesa .
Lulu alichukua zile pesa akaondoka .
Hatimae siku , mwezi uliopita huku Lulu akiendelea kufanya kazi zake .
Siku zilivyokuwa zinaenda Lulu alishituka kwani mwezi huo hakuingia kwenye siku zake kama inavyokuwa alafu alihusi tofauti kubwa kwenye mwili wake .
" Inawezekana nikawa nimembeba ujauzito?
Hapana ilikuwa mara moja tu na kwa mahesabu yangu haikuwa siku ya hatari.
Kuna muda alijipa moyo kuwa yupo salama , alikaa akijizizamia mpaka mwezi mwingine ukaisha nao ulipita bila kuona hapo ndipo alipoamua kwenda kununua kipimo akapima ujauzito. Wakati anapima alionekana kuwa na wasiwasi sana aliomba MUNGU isije ikawa mimba .
Baada ya dakika kadhaa aliangalia kipimo kilichokuwa kimechora mistari miwili iliyokolea
" Mungu wangu mimekwesha nitakueleza nini mama Lulu.
Aliongea Lulu huku akiwa kaweka mikono kichwani.
VIP ROOM π 5
MTUNZI SMILE SHINE
Lulu alijikuta anaishia nguvu akakaa chini na kuhema kwa nguvu.
" Hivi kwanini sikuwa na akili ya kutumia kinga. Sasa nina mimba itakuwaje kama yule jamaa atakuwa na maradhi mengine? Mimi nitakuwa mgeni wa nani na maisha yangu yenyewe ya kubangaiza alafu leo nina mimba ya mwanaume ambae simjui jina wala sura yake.
Lulu alijilaumu sana kwa uzembe aliofanya . Alichukua kike kipimo cha mimba na kukiweka vizuri kwenye moja ya mikoba yake.
Zilipita siku tatu Lulu alikuwa bado anajifikitia afanye nini juu ya ule ujauzito kuna muda aliwaza atoe lakini kuna nafsi ulimwambia aache kiumbe alichobeba hakuna hatia ni dhambi kuuwa.
Baada ya kufikiria afanye nini lipata wazo ampigie yule mwanaume ambae hakuwahi kujua hata jina lake. Alichukua simu na kujaribu kupiga simu lakini haikuwa inapatikana.
Hakujali sana alijua hapatikani kwa muda ule ataendelea kumtafuta badae.
Kila siku alikuwa anamtafuta lakini hakumpata . Aliwaza kurudi hotelini akamuulizie yule muhudumu aliyempeleka chumbani bahati siku ile alisoma jina lake kwenye shati aliyokuwa kavaa alikuwa anaitwa Winnie
" Ngoja nikamtafute winnie lazima atakuwa anajua yule mwanaume ni nani.
Kesho yake Lulu alipotoka kwenye shuhuri yake ya kuwafanyia make up wasanii aliomba ruhusa kwaajili ya kuondoka . Wakati anaondoka Adrian alimfuata.
" Mbona kama unaondoka unaelekea wapi?
" Wewe mwanaume mbona unanifuatilia sana unataka kujua nini kwenye haya maisha yangu?
" Kwani hujui nataka nini kwako?
" Nimechoshwa na ilo swali lako la kipuuzi .
Safari hii Lulu alionekana kuwa na hasira adrian alimuacha aondoke , Adrian aliiangalia pembeni aliona kuna wasichana wanamcheka alipiga hatua kuwafuata alipofika mbele yao alishika kiuno.
" Mnanicheka si ndio?
" Achana na yule msichana mwenye msimamo kwanza haendani na wewe hebu tuangalie sisi pisi kali watoto wa mjini tuna umaarufu kama wewe , sisi ndio tunaendana na wewe chagua mmoja kati yetu.
Adrian aliwaangalia wote watatu juu mpaka chini kisha akacheka kidogo.
" Katika nyinyi sijaona wakuwa nae maana nyie wote nimesha wapitia na wala hamna maajabu kwasababu kila mwanaume mwenye pesa kashawapitia , katika maisha yangu siwezi kuowa wala kuishi na mwanamke maarufu kwasababu nawajua tabia zenu, alafu
Yule ndio msichana mitakaekuwa nae mimi na ndio mwanamke mwenye hadhi ya kuwa mwanamke wa mtu sio nyie viruka njia ambao mnafanya mili yenu biashara.
Adrian alimaliza kuongea akaondoka.
" Jamani huyu kaka anajisikia laiti ningekuwa najua ana tabia hii wala nisingekubali kulala nae. Alisema mmoja kati ya wale mabinti.
" Hivi kumbe ni kweli ulilala nae?
" Ndio ila ni mara moja tu na tulipo toka chumbani mazoea yakaisha hapo alinichunia nikaona haina haja ya kujipendekeza.
" Hata mimi ilikuwa hivyo hivyo .
" Mimi nililala nae mara mbili ndio akaniacha.
Wote wakajikuta wanacheka .
" Ila anajua kuhonga nilisema nikiwa nae kwa miezi sita nanunua kiwanja.
" Huyo hana shida na pesa familia yake ina pesa sana na kwenye hii fani ya uigizaji yupo kwasababu ni kipaji chake.
Lulu alienda mpaka peace hotel, alifika mapokezi akamuuliza winnie.
" Samahani nilikuwa namuuliza dada mmoja anaitwa winnie.
" Winnie sijui kama yupo hebu kaae pale usubiri kidogo .
Alisema yule dada wa mapokezi , kuku alimpisha akaendelea kuhudumia wateja wengine waliokuwa wanahitaji vyumba .
Lulu alienda kukaa kwenye viti vilivyopo mapokezi akawa anasubiri.
Alikaa kama dakika tano hivi akamuona winnie anapita akiwa kuongozana na mwenzie, Lulu alinyanyuka na kumuita.
" Winnie.
Winnie alisimama akamuangalia , Lulu alisogea alipo na kumsalimia.
" Mambo.
" Safi , habari yako.
" Salama, sijui unanikumbuka?
Lulu aliuliza baada ya kuona winnie anamuangalia sana huku akijaribu kuvuta kumbukumbu.
" Sura yako sio mgeni ila sijui niliwahi kukuona wapi.
" Nilijua tu hunikumbuki. Naitwa Lulu kuna siku nilikuja hapa hotelini kwenu ukanichukua na kunipeleka chumba kimoja cha VIP.
" VIP ROOM? Aliuliza winnie huku akijaribu kukumbuka.
" Ndio.
Baada ya dakika chache winnie alikumbuka .
" Oooh nimeshakumbuka miss Lulu .
" Samahani kuna jambo nilitaka kujuuliza.
" Uliza tu.
" Hivi yule mwanaume aliekuwa ndani ya kile chumba unamfahamu? Ni nani? Anaitwa nani?
Winnie alimuangalia usoni , alishindwa kujibu maswali ya Lulu lakini
Winnie alionekana kumfahamu yule mtu lakini alisita kusema chochote kumuhusu
" Kwanini unaniuliza kwani wewe hujui?
" Simfahamu .
"Mmmmh yule mtu ni mteja wetu hapa lakini sijawahi kuiona sura yake na wala silijui jina lake.
" Mmmh hujui chochote kumuhusu yeye?
" Ninachojua ni mtu mwenye pesa sana na huwa akija hapa anakuja kwa mambo yake na kuondoka.
" Kwahiyo kile ndio chumba chake special?
" Samahani miss Lulu sheria na utaratibu wa hapa hauniruhusu kutia taarifa za mteja.
" Sawa , pole kwa kukusumbua.
" Usijali .
" Kwaheri.
" Karibu tena.
Lulu aliondoka huku winnie alikuwa anamshinikiza kwa macho huku akitingisha kichwa kama vile anamsikitikia.
" Masikini binti wa watu atakuwa kapatwa na tatizo.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote