YOUR SPECIAL FOR ME

book cover og

Utangulizi

YOUR SPECIAL ONE
Queen Alice

Paula nibinti ambae alizaliwa katika familia ya kawaida sana ambayo alikuwa namdogoake aliekuwa mdogo walikimbiwa na baba kutokana na changamoto za maisha hivyo ilipelekea kumfanya Paula ashindwe kusoma na kuamua kuihudumia familia yaani mama na mdogoake huku akiwa bado mdogo sana alilazimika kuwa mfanya biashara na sio kusoma tena japo kuwa ilikuwa inamuuma sana lakini atafanyaje ila sikumoja alipokuwa amejawa msongo wa mawazo aliamua kuelekea ufukweni kupoteza mawazo hivyo alikutana na Mr Travis ambae alijikuta anavutiwa sana na binti mdogo tena aliamua kumpa elimu iliaende kufikia ndoto zake alizokuwa nazo kichwani mwake Mr Travis alikuwa ni mwanaume aliekimbiwa na mke baada ya kuwa namaisha ya hali yachini mkewe alipata mwanamme ambae alikuwa anamaisha hivyo alienda huko na kuzaa ndipo Mr Travis aliamua kumpa taraka yake nakuanza kutafuta maisha kwa nguvu hadi anakutana na binti mdogo Paula alikuwa tayari kajipata na nitajiri haswaa ambae aliamua kulea wadogo zake tuu watoto wa ndugu

Karibu kujua kilicho tokea

YOUR SPECIAL FOR ME
Epsd 1.
Mtunzi ALICE
Mwandishi ALICE

Ilikuwa siku ya jumapili moja tulivu sana nilikuwa nimeboreka sana kukaa nyumbani hivyo niliona nitoke tuu mwenyewe nikiwa na tembea tembea pembezoni mwa fukwe za bahari nilitizama maji huku na kule kunamuda nilijisikia ninahisi akili yangu imepata utulivu mzuri tuu niliona nahita kupumzika nilikaa chini kwenye michanga alikuja mkaka mmoja akiwa ananiuliza

"Samahani dada sijui ungehitaji kinywaji?

"Kinywaji beigani kakaangu?

"Ni elf moja na miatano tuu dada karibu nikakuletee?

"Mmh hapana ahsante kaka nadhani siku nyingine nitakuungisha leo siko poa sana hela niliyonayo haitoshi"

"Ok sawa dada"

Kisha yule mkaka aliondoka na kuniacha mwenyewe pale baada ya muda mfupi niliona nisimame nizunguke zunguke huku nikiokota simbi vidogo vidogo nilifanya hivyo nikiwa hapo yule mkaka alienifuata kuniuliza kuhusu vinywaji alinifuata tena akiwa kabeba kinywaji yaani juice akaniambia

"Dada hii ni juice yako nimeambiwa nikuletee"

"Labda utakuwa umekosea sio mimi maana mimi nilikuja mwenyewe broo"

"Hapana nimeambiwa wewe umevaa gauni nyeusi ya kuchanua naweza kukosea umesuka nywele za mkono sio raster bado nakose mweupe eeh dadaangu nioda yako"

"Ok kamuambie huyo aliekuagiza nimemwambia ahsante mungu ambariki ilanipo sawa"

Kisha nilimuambia

"Rudisha hiyo juice"

Yule kaka alifanya kam nilivyo mwambia aliirudisha hiyo juice na baada ya muda nili niliona sasa nirudi nyumbani kwani muda pia umeenda jioni inaanza kuingia nilitoka taratibu nikiwa natembea mwenyewe kwa miguu nilitembea hadi kando kado ya barabara ya rami ili nivuke kusogea kituoni nilifanikiwa kuvuka nikasogea kituoni nikawa nasubili basi ilikuja gari moja aina ya v8 ikasimama na kusha kioo kilishushwa alikuwepo mbaba mmoja ndani alionyesha kwa inshara kwamba niende ila nilishtuka nikawa naogopa nilisimama nikijifanya sio mimi kuna mdada mmoja alipoona hivyo aliamua ajipeleke yeye ila yule mbaba alimuambia

"Sio wewe yuleee alievaa gauni pale"

Nilikuwa bado najifanya sielewi yule mdada alikuja na kuniambie

"Neda dada unaitwa wewe bahati huwa haiji mara mbili hiyo niyako nenda"

Nilianza kutembea taratibu na kusogea kwani watu pale kituoni walikuwa wakinitizama mimi tuu hivyo kwa aibu niliona niende nilipofika nilimsalimia

"Shikamoo"

"Marhabaah! unaelekea wapi mrembo?

"Mimi?

"Ndio wewe"

"Naenda tabata"

"Ok sawa ingia nikusogeze mbele maana mimi naelekea mbezi"

"Ok ahsante ila sitaki nikusumbue ungeenda tuu nitapanda daladala tuu"

"Ingia nitakusogeza sehem salama na rahisi kupata gari usiniogope mimi sio mtu mbaya bwana"

"Ok sawa"

Nilifungua mlango na kuingia kisha yule mbaba aliwasha gari na tukaondoka tukiwa njiani aliniuliza

"Mimi naitwa Mr Travis sijui wewe unaitwa nani binti mrembo?

"Naitwa Paula"

"Ok Paula unajina zuri kama ulivyo mwenyewe mrembo haswaa mmh! Paula unaishi na nani wewe?

"Mimi naishi na mamaangu pamoja na mdogoangu"

"Ok siku moja kama utapenda nialike kwenu nije kumsalimia mamaako au unasemaje"

"Mmh! umsalimie hapana mamaangu mkali sana atanigombeza"

"Kwanini akugombeze jamani"

"Yaani nimpelekee rafiki mwanaume nyumbani tena mkubwa hivyo atanipiga apana siwezi"

"Usijali nakutania ila naomba kuwa rafiki yako"

"Sasa itawezekanaje rafiki mkubwa hivyo eeh?

"Wewe nikubalie utaona itakavyo wezekana"

"Mmh! Sawaaah"

Mr Travis alilazimisha hapo mpaka nilimkubalia urafiki kisha nilikuwa nimefika sehemu ya mimi kushuka mr Travis alisimamisha gari kisha nilikuwa nataka kushuka Mr Travis alinishika mkono na kisha niligeuka kumtizama akaniambia

"Rafiki mbona unashuka bila hata kuniaga sio vizuri hivyo bwana sisi nimarafiki tayari au sio?

Nilibaki kimya huku nikitabasam kisha nilimwambia

"Samahani nilikuwa naharaka kwani muda pia umeenda sana rafiki"

"Ok basi sawa nivizuri kuwahi nyumbani ila ngoja nikupe hii nauli kidogo ili uchukue bajaji uwahi sawa!

Nilimzuia na kumuambia

"Hapana ninayo nauli ahsante usijali "

"Hapana urafiki sio hivyo chukua"

Kisha alitoa kiasi cha pesa akiwa kakikunja kunja na kuniwekea mkononi kisha aliufunga mkono wangu akaniambia

"Naomba namba yako ya simu kabla ujashuka"

Niliona nibora nimpe tu hiyo namba kisha niliagana nae na kushuka kwenyegari



Je nini kitatokea kwa Paula na Mr Travis tafadhari endelea kufuatilia ilikujua zaidi ........
YOUR SPECIAL FOR ME
Epsd 2.
Mtunzi ALICE
Mwandishi ALICE




Niliposhuka niliona gari inayoelekea tabata nikakimbilia na kuingia nilikaa maeneo ya siti ya dirishani nikachungulia kutizama gari ya Mr Travis nje kama tayari nae ameondoka alikuwa anasubili nipate gari kisha aliondoka nikiwa nimetulia gari niliyopanda imeanza safari nilisikia mlio wa msg nikaitoa simu na kuitazama kilikuwa kisim cha Nokia ya tochi kuitizama msg ilikuwa namba ngeni ndio nikaifungua kuisoma imeandikwa "Nakutakia safari njema ukifika nijulishe tafadhari Mr Travis" nilitabasam kisha niliona nimjibu "Ahsante nashukuru" kusha niliisevu namba yake na kuirudisha simu yangu mfukoni kisha kinda alikuja akawa anadai pesa ndio nikachukuwa kipochi nitoe hela ya nauli nafungua hivii naona ninawekundu wekundu mwingi yaani elf kumi kumi ndio nikakumbuka zilikuwa zimeviringishwa vilingishwa nilipoweka kwenye pochi zikajiachia nikaona nichukue hela niliyokuwa nayo mimi elf mbili nikampa konda akakata nauli kisha alinirudishia chenji nikarudishia kwenye pochi nilianza kujiuliza mbona kanipa hela nyingi hivi jamani sasa zanini hizi zote najisemea kimoyo moyo hatimae tulienda tukafika nikashuka na kuanza kuelekea nyumbani nilifika nikaingia ndani nilimkuta mama kakaa anatizama TV nilimsalimia kisha niliekea chumbani nilipofika nilivua nguo nikaelekea bafuni kwanza nilipotoka nikiwa najifuta maji nilichukuwa simu kwanza nikasema ngoja nimjulishe nimesha fika tayari niliandika ujumbe "Nimesha fika nyumbani tayari" kisha niliisendi nakisha niliiweka simu pembeni nikajifuta maji na nilipochukua mafuta nijipake tuu nilisikia msg imeingia nikachukua simu kuifungua msg ilikuwa inatoka kwa Mr Travis nikaisoma aliniandikia "Ok sawa nafurahi kujua upo nyumbani salama oga kula nitakupigia baadae kidogo" nilijiuliza kwani huyu siyupo nyumbani sasa mkewe siatamfuma mimi sitaki matatizo na watu jamani mmh nilikuwa najiongelea kimoyo moyo tuu kisha niliiweka simu huko pembeni nikamalizia kupaka mafuta na kuvaa nguo zangu zakulalia kisha nilielekea jikoni kuchukua chakula kisha nilikaa dining kupata chakula kisha nilipo maliza nilikwenda kwa mama kumuaga naenda kulala kisha niliingia chumbani kwangu nikapanda kitandani ilinilale ilikuwa mida ya saa tano usiku simu yangu ikaita nikaipokea alikuwa Mr Travis

"Hallow"

"Hallow Paula"

"Abeeh"

"Vipi umesha lala tayari?

"Bado ndio nataka kulala"

"Niambie mtoto mzuri natamani kukujua zaidi"

"Mmh kunijua zaidi! Kivipi yani?

"Paula unasoma au?

"Laah! Nilishindwa kuendelea niliishia kidato cha pili kulingana na matatizo yakifamilia lakini kwasasa ninafanya biashara nauza nguo zamtumba ndio naitizama familia kwasasa"

"Wewe Paula ndio unailea familia?

"Ndio kwani huamini mimi ndio mtoto wakwanza ndio baba wa familia?

"Kwani babaako yupo wapi?

"Achatuu babaangu mimi alitukimbia na kwenda kuanzisha familia mpya huko wala hatujali kabisa"

"Pole sana Paula"

"Ahsante na wewe mbona sasahivi hapo unapiga simu mkeo yupo wapi huogopi?

"Laah hapana Paula mimi sina mke aliolewa na kuniacha mimi nikiwa naumwa alijua nitakufa ila sasahivi ndio anataka kurudi kwangu kwakuwa ninamali nyingi mumewe yeye anamaisha ya kawaida sana ndio maana nipo huru nilichukia sana wanawake kwani niliwaona sio waaminifu kabisa kwaajili yake yeye hadi leo hii sijaoa tena"

"Mmh pole Mr Travis na huna hata mtoto?

"Hapana huyo mwanamke alikuwa mjamzito kabla hajanikimbia alipoondoka alienda kuitoa mimba yangu ilikuwa miezi mitatu kabisa yaani achatuu Paula"

"Pole sana jamani kwahiyo hapo kwako upo wewe tu"

"Hapana ninakaa na wadogozangu wawili wakike na wakiume wapo vyumbani kwao wamepumzika sio watoto wadogo wanasoma wakiume yupo chuo na wakike anamalizia kidato cha tano nawasomesha mimi mwenyewe"

"Ok safi jambo zuri mimi pia ningekuwa na kakaangu kama wewe ningefurahi sana kwani ningezifikia ndoto zangu bila wasi wasi"

"Kwani Paula nikitaka kuwa kakaako huto taka"

"Nataka lakini sio kakaangu wakweli kweli wewe sasa utachoka mapema mimi nimtu baki kwako"

"Nani kakuambia hivyo utapenda kurudi shule kwani?

"Ndio nitapanda lakini sitoweza kwani mama na mdogoangu wanataka mahitaji kula na kilakitu siwezi kuchanganya vyote kwa wakati mmoja"

"Nimekuuliza utapenda kurudi shule tuu hayo mengine niachie mimi kama upo tayari niambie"

"Ndio nipo tayari "

"Ok kesho asubuhi jiandae njoo mjini ofisi yangu ilipo sawa"

"Sawa"

"Haya nimefurahi kukufaham kwa kiasi naomba nikuage nipumzike kesho ninakikao asubuhi mapema ofisini kwangu"

"Ok mimi pia nimefurahi kukufahamu haya pumzika sasa usiku mwema"

"Haya nakwako pia"

Kisha alikata simu na kulala mimi pia nililala nilifurahi kusikia nitarudi tena shule japo nilikuwa najiuliza je nitamlipa nini huyu mbaba mimi looh mbona sielewi ngoja nitaenda kwanza nikamsikilize huko ofisini kwake kisha nilipitiwa usingizi nikalala



Unataka kujua nini kilimtokea Paula endelea kufuatilia ......





YOUR SPECIAL FOR ME
Epsd 3



Mtunzi ALICE
Mwandishi ALICE






Nililala usiku huko kisha palipokucha niliamka na kuoga nikajiandaa kwakuwa nilikuwa ninahela kiasi nilipewa na Mr Travis nikaona ninaweza siku ya leo kuiua nisiende kwenye biashara itatusogeza sogeza nikachukua kiasi nikampa mama nikamuambia

"Mama hii hela utanunua mahitaji ya nyumbani ambayo yatatusogeza sogeza siku kadhaa mbele sawa mamaangu?

"Wow mwanangu Ahsante mungu akutangulie kwa kila hitaji lako la moyo likafanikiwe na uwe na baraka kwa kila utakacho kigusa kiwe na manufaa haya mwanangu"

"Hahahaaa sawa mama Ahsante sana haya mimi ninatoka sasa baadae"

"Sawa mwanangu na mguu wako ukawe na baraka uendapo binti yangu"

"Amina mamaa"

Niliondoka huku nikicheka yaani mamaangu nimtu mwenye kunipa furaha muda mwingi anajua napitiaga changamoto nyingi sana na hajawahi kunivunja moyo yeye huwa ananibariki kila siku hivyo nilivyo mpa ile hela alifurahi sana hakika mimi pia napenda kumuona akiwa anafuraha wakati wote hivyo nilielekea barabarani nikapanda daradara hadi postar nikashuka na kuenda kule nimeelekezwa kisha nilipofika hapo getini nikakutana na walinzi nika wasalimia kisha nikawaambia

"Nahitaji kwenda ofisini kwa Mr Travis"

"Ok je unamiadi nae?

"Ndio"

"Unaweza kukaa hapo akaambiwe unaitwa nani?

"Naitwa Paula"

"Ok"

Mlinzi akaenda kumuambia Mr Travis kuwa nimefika akaambiwa anipeleke hadi ofisini kwake hivyo mlinzi alikuja kuniambia twende nikupeleke alimuacha mlinzi mwenzie hapo getini na kunipeleka hadi ofisini kwa Mr Travis niliingia ndani nikamkuta yupo ila alikuwa bize kidogo aliponiona aliacha shughuri akainika na kuja kunikumbatia kisha alimuambia mlinzi

"Ahsante kwakuniletea mgeni wangu"

Kisha mlinzi alitoka na kuludi getini nilimsalimu na kisha akaniuliza

"Ungependa juice soda au maji?

"Ahsante Mr Travis nipo sawa kabisa"

"Hapana bwana ngoja nikuagizishie juice bwana huwezi kuja kwangu utoke hata maji hujanywa sio poa kabida"

"Ok basi sawa"

Kisha alinyanyua simu akapiga na kutoa oda kisha akakata akaanza kunitania

"Binti mrembo niambie Paula"

Nilikuwa nikitabasam tuu muda wote kisha akaniambia

"Paula vipi nyumbani mama yupo poa na ndugu yako?

"Yaah wapo salama nashukuru kwa hilo"

"Ok haya sasa niambie unataka kurudi shule kweli?

"Ndio nataka kurudi kama nitapata wa kunirudisha"

"Ok mimi nipo tayari kukurudisha"

"Unasema kweli Mr Travis?

"Kweli kuanzia sasa katafute shule ungependa kusoma na kisha utanijulisha gharama zote sawa?

"Sawa"

Kisha baada ya hapo nilimuaga ili niondoke kwani niliona yupo bize sana na alikuwa anawatu wengi wanamsubilia alikuwa nimtu mkubwa sana hapo ofisini kwakweli yaani nilikuwa naogopa pia kumbe nimtu mkubwa hivi na mimi ndio kawa rafikiangu sijui imekuwaje kisha Mr Travis aliniambia

"Kwanini unaondoka haraka hivyo kwani unaenda wapi leo?

"Nikitoka hapa niende kutizama biashara yangu wakati nafuatilia na swala la shule"

"Unaonaje leo usiende kwenye biashara yako nitailipia siku yako ya leo nenda chini nisubili hapo nakuja twende sehemu"

Niliinuka nikiogopa ogopa sijui anataka kunipeleka wapi mimi jamani ila dah! Mambo ya misaada haya mmh ngoja tuone nilielekea nje kwenye paking nikakaa nikimsubili Mr Travis aje tuondoke kweli baada ya nusu saa alikuja Mr Travis akafungua mlango wa gari kisha akanifungulia nikaingia akawasha gari tukaanza kuondoka tuliingia hotelini kwanza kisha akashuka na kunifungulia namimi kisha nilishuka nilikuwa naogopa mbona tuko hapa tena tuliingia hadi ndani asikuambie mtu nihotel kubwa ya nyota tano sikutegemea hata siku moja kama nitakuja kukanyaga hapa lakini ndio nimeletwa na sijui nimefuata nini hapo



Je ungependa kujua nini kilichotokea hapo hotelini endelea kufuatilia......


YOUR SPECIAL FOR ME
Epsd 4



Mtunzi ALICE
Mwandishi ALICE





Tulielekea sehemu ambayo ilikuwa imeandaliwa kwaajili yetu tulifika tukakaa na Mr Travis alimuambia muhudumu atuletee menu kisha tulichagua chakula hapi hakika nisidanganye kulinga na maisha ninayoishi mimi na familia yangu sijui lini ningeingia hoteli hiyo tuliyoingia na Mr Travis kwani ni hoteli yenye hadhi ya nyota tano walikuwa wanapishana watu wenye hadhizao tuu na magari yaliyokuwa yamepaki yalikuwa ya thamani ya juu hata kuchagua chakula kwenye hiyo menu sijawahi alinisaidia kuchagua Mr Travis hivyo hadi chakula kililetwa hapo sikuwa naelew kitakuwa cha aina gani menu ilikuwa ya kingereza walituletea chakula kilikuwa kwa mala yakwanza kukionja kilikuwa nikitam sana na kinywaji Mr Travis aliniagizia juice ya matunda hakika ilikuwa tamu sana tulikula hapo nilikuwa kutumia uma na kiau mtihani ila Mr Travis aliniambia

"Paula be free usione aibu ok"

Nilitabasam nakisha nilianza kula kwa kutumia mkono wangu kisha tulipo maliza kula tulitoka hapo na kuingia kwenye gari akaniambia

"Ntaka twende sehemu moja kama patakupendeza utaniambia"

"Sawa"

Niliitikia japo sikuwa najua napekekwa wapi unajua nilimuamini mno Mr Travis kwa muda mfupi japo nilikuwa nawaza huu msaada mbona sijui nitaulipa vipi mimi maana hakuna vitu vyabure sikuhizi tulienda hadi kwenye shule moja huko mjini ilikuwa nishule ya kulipia ninzuri haswaa tuliingia hapo akapaki na kisha tulishuka na kuingia ndani nilikuwa nashangaa hasa kwani ilikuwa nishule haswaa wanafuzi walikuwa wapo bize na kujisomea Mr Travis aliingia hadi ofisini kwa mkuu na kuongea nae mimi aliniacha nje nikimsubilia hapo baada ya muda alipotoka akaniuliza

"Paula je unapaonaje hapa pazuri sio?

"Mmmh ndio pazuri sana Mr Travis lakini patakuwa ghari sana"

"Sio sana ni kawaida nandio panaelimu nzuri kama umepapenda naenda Bank kufanya maripo ili uje uanze kusoma hapa naimani hutaferi ukiwa hapa"

Nilitamani kumkatalia lakini nilishindwa kwani tayari yeye pia alipenda nisome hapo nilikuwa naogopa hizo garama ila nitafanyaje tulitoka hapo hadi Bank Mr Travis alienda kulipia kilakitu kisha nilikabiziwa risiti zamalipo na baada ya hapo tulienda kwenye duka moja lavifaa vya wanafunzi kulikuwa nakilakitu ila Mr Travis aliniambia nichague bag lashule japo niliona yanauzwa garama sana lakini nilishindwa kukataa nilichukua beg na alilipia vitu vidogo vidogo pamoja na viatu kilakitu kisha tulitoka hapo tukaingia kwenye gari ya Mr Travis kisha aliwasha gari tukaondoka nilimuambia huku nikiona aibu

"Mr Travis umenifanyia vitu vikubwa sana sijui nakulipaje ila mungu akinijaalia nikipata kazi nitakulipa nakuahidi hivyo"

"Hahahaaaa hapana Paula sihitaji unilipe kuwa na amani napenda nikusaidie ufikie marengo yako hivyo be free"

"Mmh lakini msaada mkubwa sana Mr Travis nitakulipa japo hata kidogo"

"Paula bwana acha zako kesho uwahi darasani achana na mambo ya kunilipa nielekeze kwenu nikuache nyumbani ili ukaanze maandalizi ya shule kesho"

"Ok sawa"

Nilimuelekeza Mr Travis alinipeleka hadi karibu na nyumbani kabisa nikamuuonyesha kwetu na kisha nilimuomba tusifike kabisa nyumbani kwani naogopa mama asimuone kwakuwa sijamuelezea kuhusu yeye Mr Travis akafanya kama nilivyomuaomba akapaki gari kisha nilimuambia

"Ahsante Mr Travis nimesha fika nashukuru sana nitakukaribisha nyumbani kwetu hivi karibuni naomba nikaongee na mamaangu kuhusu msaada wako"

"Ok nitafurahi kukaribishwa nyumbani kwenu nakufahamiana na mamaako"

"Sawa usijali utafahamiana nae haya nisikucheleweshe"

Mr Travis aliingiza mkoni mfukoni kisha akanifishia mkononi kiasi cha fedha akaniambia

"Haya by"

Nilibaki nikiwa nimetoa macho nikitamani kumuambia hizi hapana lakini Mr Travis alikuwa akitabasam na huku akiendesha gari lake akaondoka niliamua kumpigia simu Mr Travis aliipokea na kuniambia

"Paula usijali najua unachotaka kusema ila usihofu unamahitaji ya nyumbani hapo yanakutegemea na kesho unatakiwa uudhurie darasani hivyo hiyo itakusaidia usiogope nakata simu sasa niwahi ofisini ninakikao jioni by"

Kisha Mr Travis alikata simu hakunipa nafasi kabisa ya kiongea hivyo nilibaki sina tena chakujitetea nilitabasam na huku nikitembea nilifika nyumbani nikaingia ndani nilimsalimia mama kisha nilikaa kwenye kochi mama akaniuliza

"Leo mapema vipi nabegi lanani hilo?

"Nilangu mama"

Kisha nililifungua na kutoa viatu sox pamoja na vitabu vya shule mama alishangaa na kuniuliza

"Unataka kuludi tena shule?

"Ndio mama kuna mtu mmoja nilikutana nae tukapiga story za kifamilia ndio akaniuliza je ungependa kuendelea na masomo yako nikamuambia ndio ila kwa sasa haiwezekani ila yeye akaniambia inawezekana leo aliniambia niende ofisini kwake ndio akanichukua na kwenda kunilipia shule na kuninunulia beg na vitu vyote hivyo kesho kasema natakiwa kuwa darasani mapema mama"

Mama alinitizama muda wote nikiongea kisha akaniuliza

"Vipi kuhusu biashara nani ataihudumia familia sasa Paula eeh mdogoako nani atamsaidia mahitaji yake ya shule sasa yaani wewe umejifikilia wewetu"

Mama alichukia haswa kisha aliondoka na kujifungia chumbani kwake nilienda mpaka mlangoni kwa mama nikigonga na kumuita

"Mama ...mamaaa basi sitaenda tena shule nitakuwa kwenye biadhara kama unavyotaka"

Nilionge huku nikilia japo mama hakujua kama nimeumia sana mimi kwani ndoto zangu nisome nije kuwa mwanasheria lakini ndoto yangu sio chochote kwa mamaangu anajali kuhusu mdogoangu tu sio mimi tena mimi nimekuwa daraja la mafanikio ya mdogoangu ila sina njia mama ndio kataka niliendelea kulia hapo huku nikimuambia

"Mama kuwa na amani sitoenda hiyo shule usihofu tena nitafanya biashara kama utakavyo"




Je Paula atafanyaje sasa mamaake yeye hataki asome natayari kalipiwa ada na kununuliwa baadhi ya vitu unataka kujua endelea kufuatilia..........


YOUR SPECIAL FOR ME
Epsd 5.



Mtunzi ALICE
Mwandishi ALICE






Baada ya muda mama alifungua mlango akanikuta nimekaa sakafuni alinipa mkono na kuniinua kisha akanipeleka hadi sebreni huku akinifuta machozi akanikalisha na kuniambia

"Mwanangu wewe ndio kichwa cha familia wewe ndio baba hapa tunakutegemea sasa wewe ukienda shule maisha siyatasimama mama wewe jitahidi ndotozako ziamishie kwenye biashara sawa kipenzi changu"

Nilikuwa naumia sana huwezi amini nilimuitikia kwa kichwa huku machozi yakinidondoka mfululizo kwani nilikuwa naumia mno kisha nilimuambia

"Naenda kupumzika chumbani mama"

"Sawa nenda upumzike mimi ninaandaa chakula cha jioni kipenzi changu sawa"

"Sawa"

Nikainuka na kwenda chumbani nilipoingia niliubana mlango nikauegemea na mgongo nililia sana yaani nililia mnoo nikiwa nalia simu yangu iliita kuitizama alikuwa Mr Travis sikuipokea kwani nilikuwa sitaki nimuumize kwani kalipia hela yake ada yangu na vitu kaninunulia niliona hatojisiki vizuri kabisa namimi ndio nilikuwa nazidi kupata hasira kwani sijajua nitaongeaa nini kwa Mr Travis baada ya muda nilipanda kitandani nikalala hata Travis aliamua kuacha kupiga maana alipiga mfululizo akaona sipokei nililala kama lisaa na nusu kishaama alikuja na kugonga akiniambia chakula kipo tayari nilimjibu

"Endeleeni mimi bado sina njaa"

"Sawa ila chakula utakikuta mezani hapa"

"Sawa"

Kisha niliendelea kujilaza nilisikia msg ineingia kwenye simu yangu nikaitizama alikuwa Mr Travis aliandika nakaka kujua kama uko poa tuu wala sio mengine au upo na kiboy friend chako najua wewe ni binti mdogo bado ok ukiwa sawa utanijulisha mimi ndio nipo njiani naenda nyumbani nilipomaliza kusoma ile msg nilijibu kifupi tu mimi sina boyfriend kisha nilimtumia na nilipomaliza niliiweka simu yangu ndogo pembeni kabla sijaegesha kichwa iliingia tena msgkutoka kwa Mr Travis akisema nipo maeneo ya ubungo kwenye hotel ya ubungo plaza naoba chukua piki piki njoo niiitizama ile msg kwakuwa nilikuwa nimeboreka niliona nibora niende nilitoka nikachukua ufunguo taratibu hata mama hakujua nilienda nikapanda boda na kuelekea ubungo plaza nilifika nikamuandikia msg nipo njee Mr Travis alitoka na kunishika mkono aliniingiza huko ndani tulielekea sehemu za kwenye maduka ya nguo za wadada nilibaki nikimshangaa tu kwani sikuelewa nimekuja kufanya nini hapo tuliingia kwenye duka moja akamuambia mdada wa dukani

"Mbadilishe kabisa apendeze kisha utanipa garama muda mfupi sawa"

Yule dada alinishika na kuniingiza kwenye kichumba alinivarisha kigauni kitamu hatari kilikuwakifupi na kimetaiti hivi juu kinamikono kama singled na kifuani nilivyo chuchu kozi sasa huku kishep chauchokozi mamaweee acheni tuu nilipendeza akanivarisha na kiatu kirefu nchi tano kichwani alinivarisha kiwigi flani kifupi kitamu na kasimpo mecap nilikuwa watofauti sana usiku huo kisha akaniwekea nguozangu kwenye mfuko na kunipeleka hadi kwa Mr Travis alivyoniona alibaki kaduwaa kwa kunitanzama yaani aliniona niwatofauti sio yule alienizoea alibaki kimya akiwa anashangaa yule dada akamuambie

"Boss unamuonaje hapo vipi?

"Wow!.. nimrembo hivyo Paula"

Nilikuwa nimesimama tuu Mr Travis alinisogelea akaushika mkono wangu na kuniambia

"Ur beautiful" (wewe ni mrembo)

Nilikuwa bado namtizama tuu yaani alionekana Mr Travis kuvurugwa na urembo wangu alinisogelea karibu kabisa na kuniambia

"Ur special for me"(wewe nimaalumu kwaajili yangu)

Kisha aligeuka na kumuomba bill yule dada alilipa na kuuchukua ule mfuko wa nguo zangu nilizokuja nazo nikiwa nimevaa alinishika mkono na kisha tulielekea sehemu moja huko juu kwanza alimpa kijana ule mfuko na kumuambia akaweke kwenye gari lake tulienda hadi kule juu kabisa kunasehemu nzuri ina swimming pool hapo na sehemu ya kukaa watu kwa kulakunywa na kufurahia na marafiki tulikuta kunawatu wapo hapo Travis aliwaambia

"Naomba niwatambulishe mtu wangu wa karibu kabisa anaitwa Paula karibu Paula hawa ni marafiki zangu na wapenzi wao"

Nilishangaa kwani mbona kanilete kwa watu wake wa muhimu kunitambulisha kwanini kwanza hakuniambia kitu ila sikutaka kumuangusha kwani yeye sio mtu mbaya kwangu ananitendeaga wema malazote hivyo niliwapa mkono na kutabasam kama nikweli vile ninaukaribu nae Mr Travis walimsifia sana na kumuambia mpenzi wako mrembo sana yaani wewe nimtu mwenye akili sana kilakitu unachofanyaga kipo pafect hujawahi kukosea hadi kuchagua mwanamke uko pafect hongera kisha nilikaa kwenye kiti nililetewa kinywaji hapo nikamng'oneza Mr Travis

"Huwa situmii kilevi sijawahi kabisa"

"Usijali kunywa reds nilaini nzuri sio chungu upo namimu usiogope ila kunywa taratibu ok"

Nilikubali ilinisimdhalilishe kuonekana mshamba wakati nimeonekana mjanja haswaa nililetewa na kuanza kunywa kwani huwa sio chungu niliipenda sana



Je nini kitatokea kwa Paula unataka kujua kilitokea nini endelea kufuatilia simulizi yetu..........


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote