ZENDAYA (tamu ya boss) hii ni story inayo muhusu binti Zendaya binti ambe amepitia changamoto ya kunyanyaswa na familia yake kwasababu ya kuto kuwa na elimu kwani alishindwa kuendelea na shule na hii ni baada ya kufeli mara kadhaa.
Jambo ambalo lilimfanya akaishi maisha ya tabu sana , na ukiachana na kunyanya paliwa kisa elimu pia alikuwa na mwonekano tofauti na ndugu /dada zake , ambao walikuwa na mwonekano mzuri sana .
Maisha ya binti huyo yalikuwa na misuko suko mingi lakini Mungu alibadilisha yote na kumuinua juu na hii ni baada ya kukutana na kijana wa kuitwa Liam , ilikuwaje na nini kilitokea ungana nami katika kisa hiki kitamu na chenye kusisimua😊
ZENDAYA (TAMU YA BOSS)
SEHEMU YA 01
MTUNZI RITHA STORIES
SONGA NAYO.............
Maisha bhna acheni yaitwe maisha tu ila yananyoosha vibaya mnoo,mtu unapanga mipango yako vizuri tu ila inavyo kuja kuvurugika hutaelewa nini kimetokea 😕
Zendaya mie kila siku nilikuwa naota nikiwa mkubwa nitakuwa boss lady, mwanamke mwenye pesa zangu mjini , eeh vitu kama IST nilikuwa naziona kama gari za kuendea sokoni😔
Na sio kama nilikuwa na hela au labda nimetokea familia yenye pesa sana walaa, ila ilikuwa ndoto yangu kuwa siku nikiwa mkubwa nitaishi maisha ya bata sana 😕
Hatmae nimekuwa mfuga bata 😅aaah maisha haya basi tu ila fresh bado napumua nitapata hata kibanda changu cha udongo na maisha yataenda tu🥺
ZENDAYA ndo jina halisi nililopewa na wazazi wangu, me binti mdogo kiumri ila mshangazi kimwili yaani miaka yangu na mwili wangu vinapishana pakubwa sana 😆
Sijui ndo ile wanasema watoto wa elfu mbili wana wahi kuzeeka au ni mimi tu ila iko hivyo mwili na umri haviendani kabisa 🥺, kuhusu elimu nimeishia darasa la saba.
Ilikuwaje nikaishia darasa la saba nikwamba sikuwa na akili darasani kitu kilicho nipelekea kufeli mara mbili mwisho nikaona shule sio vitu zangu na kuamua kiacha kabisa.😔
Kitu ambacho kimetumika kama fimbo ya kunichapia, ndugu zangu na wazazi huninyanyapaa na kunitumikisha kisa sina elimu wala ujuzi wowote 😔
Wamenifanya nione maisha machungu na kujiona sifai wala kustahili kusimama mbele zao 🥺,zarau ,matusi ya bila sababu yamekuwa sehemu ya maisha yangu😔
Huku kila nifanyalo kuonekana ujinga wala hakuna anaeniona na kunithamini💔.
Ukiachana na kutokuwa na elimu ,kitu kingine ambacho kilifanya nikanyanyapaliwa ni rangi yangu,jamani mimi ni meusi haswa na sio ule sijui chocolate sijui mpauko weusi ule wenyewe.
Na kwenye familia yetu mimi peke yangu ndo nilikuwa mweusi wengine wote walikua na rangi zao nzuri huku wakipendezeshwa na sura pamoja na shep nzuri.
Kila mara nilipo waangalia ndugu zangu niliona kama Mungu amekosea kuniumba ,maana sikuona kitu kizuri kwenye mwili wangu. 😔
Mara kadhaa nilihisi kuchomwa na mkuki wa moto pale ambapo nilimsikia baba akisema kuwa mimi sio mtoto wake, maana sijanana nae wala ndugu yake yeyote.
Huku mama akinituhumu kumfanya mumewe amuhisi kuwa ametoka nje ya ndoa , kiufupi maisha yangu yalikuwa kama kuzimu inayo ishi .💔
Nakumbuka siku moja ,ilikuwa mida ya jioni nilitoka na kwenda kulisha mifungo porini,(maana nyumbani kwetu mbali na ukulima pia tunafunga ng'ombe ,mbizi na bata)
Hivyo mara nyingi huwa ninakwenda kuwachunga /kuwalisha mifungo , na sio salama kwa mtoto wakike kama mimi kuingia maporini na kuchunga.
Lakini kwasababu ya namna nilivyo kuwa nikiishi na familia yangu ilinifanya nikafanya kazi zote hizo bila kubisha.
Basi siku hiyo nilipeleka mifugo porini kama kawaida, kufika nikaiacha ile majani kwa uhuru hivyo nikakaa zangu chini ya mti.
Kwa bahati mbaya wakati nimekaa huku nikiwa nimeegemea mti nikapitiwa na usingizi mzito ambapo nilikuja kushtuka baada ya kusikia nikiamshwa kwa sauti kubwa.
Nilikurupuka na kumuangalia mtu anae niamsha , alikuwa kijana kwa haraka haraka ni alikuwa na zaidi ya miaka 25,sura yake ilikuwa ngeni machoni mwangu.
Nilimeza mate kwa hofu na kugeuka kuangalia mifugo yangu kama ipo salama nikaona iko mbali kidogo na pale , taratibu nikageuza sura yangu na kumuangalia yule kijana .
Kwa sauti yenye hasira akaniuliza "umekuja kulisha mifugo yako kwenye shamba langu ina maana huoni sehemu zenye majani?"
Kusikia vile nilitoa macho nikainuka na kutaka kukimbia akanishika na kunirudisha chini nakunambia " Unataka kwenda wapi, yaani unafikili unaweza kunikimbia?"
"Hapana kaka sikukimbii ila nilikuwa nakimbilia mifugo "
"Oooh baada ya kusikia wame haribu ndo unajifanya kushtuka , halafu wewe utakuwa mtoto wa Amosi si ndio"
Aliniuliza nikatikisa kichwa kuashilia ndio ni mimi, ajabu alicheka na kusema .
"Hatimae nimepata njia ya kumnyoosha huyu mpuuzi, baba anajifanya ananguvu sana na ndo maana umepata nguvu ya kulala ile hali unajua kuna mazao ya watu."
"Hapana kaka nisamehe sana nilipitiwa tu nisamehe sana "🥺🙏
Niliongea huku nikitamani kukimbia ili niwazuie wasizidi kusogea kwenye mashamba ya watu ,lakini kijana huyo hakunipa nafasi.
Bila kutarajia alinishika mkono kwa nguvu na kunivutia kwake na kunambia ...............
ITAENDELEA
ZENDAYA (TAMU YA BOSS)
SEHEMU YA 02
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO...............
"Msipo adhibiwa hamtaiacha hii tabia sasa leo utakuwa mfano kwa wenzako wote "
Aliongea na kunichota mtama nikaanguka chini kama mzigo ,bila huruma alianza kunichania nguo zangu na kuniingilia kinguvu.
Nililia na kupiga kelele lakini kelele zangu ziliishia ndani kwani mwenzake ambae alifika mara tu alipotaka kunifanyia kitu hicho alinifumba mdomo😫💔, maumivu niliyosikia yalikuwa makali kiasi kisicho elezeka.
Alimaliza na kumpisha mwenzake nae akafanya vile vile walaipotosheka wakaniacha nikiwa siwezi hata kuinuka💔, damu ilinitoka nyingi huku nguvu ya kuinuka hata kuongea ikinikosa.
Machozi yalinitoka nikabaki nimelala chini bila msaada wowote, hazikupita dakika mbili nikazima na sikujua nini kiliendelea zaidi nilikuja kuamka na kujikuta nimelala kitandani.
Nilifungua macho taratibu kuangalia ni wapi nipo nikagundua niko nyumbani, tukio la ukatili nilililo fanyiwa likajirudia kichwani na kujikuta napiga ukelele mkali sana.
Mama alikuja mbio akafika na kusema "Bora umeamka, embu nambie huyo mtu aliekufanyia hivi ni nani kabla baba yako hajaua watu huko nje .
Maana ng'ombe wawili na mbuzi mmoja hawapo "
Mama alivyo ongea hivyo nilimuangalia usoni bila kupepesa macho, kweli nimebakwa halafu haulizi najisikiaje au kunikumbatia kama mzazi na kunipa pole.
Badala yake anauliza ni nani ili wajue ni namna gani wata wapata ng'ombe wao, hili liliniuma mnoo yaani nimekuwa nikiona nakatiliwa ila si kwa ukubwa huu.
Mama baada ya kuona namuangalia bila kuongea kitu akaniuza " wewe si ninaongea nae wewe au umetolewa na masikio ,nakuuliza unamfahamu huyo mtu? "
Bila kuongea neno nilitikisa kichwa kuashilia hapana na kurudi kujilaza huku machozi yakichuruzika mashavuni, mama kwa hasira akasema.
"Acha ujinga wewe utashindwa kumjua ina maana unipofushwa macho"
Kabla hata jajibu mlango ulifunguliwa akaingia baba akiwa amefura kwa hasira na kusema " wewe tuntufe huyo mpuuzi alieondoka na mifugo yangu ni nani?"
"Ba baba simfahamu"
"Humfahamu na ilikuwaje mifugo ikachukuliwa ?"
Nilimuangalia baba na kurudi kumuangalia mama moyoni nikamuuliza Mungu hivi una uhakika hawa ni wazazi kweli?, ina kuwaje nimefanyiwa kitendo cha kinyama namna hii.
Lakini hawajali badala yake wanawaza mifugo yao, ina maana ng'ombe na mbuzi wana thamani sana kuliko mimi ?🥺
Kwa sauti ya chini iliyojaa uoga na maumivu nilimueleza baba kilicho tokea ,aloooh naomba niwaite hawa wazee wachawi maana hakuna mzazi mwenye roho kama yao.
Baba hakujali kama siko sawa hakujali kama nilikuwa binti mdogo ambae sikuwahi kumjua mwanaume , zaidi alinishushia kipigo kitakatifu.
Na kunambia kama asipo pata mifugo yake niwe na hakika ataniua , nililia na kilio changu hakikuwa kwenye kubakwa ila kilikuwa ni maumivu ya kuona chuki ya wazazi wangu kwangu.
Niliumia kuliko kawaida, na naweza kusema katika siku hii waliua kitu kinachoitwa upendo ndani yangu.
Niliwachukia na kuwaona wanyama walio katika umbo la binadamu, maana ndio nilikosea kulala ile hali niko malishoni lakini haikuwa kusudi langu.
Na kile kilicho nikuta kilipaswa kuwaumiza kama wazazi ajabu halikuonena wala hakugusa mioyo yao 💔😫
Bila huruma walinigeuzia migongo na kuniacha nikihangaika bila msaada wowote.
Siku iliisha nikiwa na maumivu sana ,kesho yake asubuhi msako wa kuwatafuta wale vijana uliendelea tena kwa kasi sana.
Sijui kama walifanikiwa kuwakamata au kufika nyumbani kwao ila baada kama wiki hivi m/kiti alikuja nyumbani akiwa na ng'ombe pamoja na mbuzi walio kuwa wamechukiliwa.
Kidogo nikapata nafuu maana kila siku baba alikuwa ananiambia Ole wangu wasipatikane ,hivyo kupatikana kwa mifugo hiyo kulikuwa afadhali kwangu.
Lakini haukuwa mwisho kwani taarifa za mimi kubakwa zilisambaa kijiji kizima ,kila mahali nilipopita nilinyoshewa kidole.
Huku baadhi ya watu wakini cheka na kunizomea, na mchumba niliekuwa nae baada ya Sakata hilo alinitema kwa maneno machafu.
Niliumia ,niliona aibu nilijisikia vibaya na kujiona sifai kuishi katika dunia lakini mara kwa mara nilisikia sauti ndani yangu ikinambia.
(Wewe ni shujaa , utashinda zaidi ya kushinda, ) sauti hii ilinipa tumaini japo sikuuona ushujaa ndani yangu ila neno moja ambalo nilijua maadamu napumua basi nitashinda.😊
ITAENDELEA
ZENDAYA (TAMU YA BOSS)
SEHEMU YA 03
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO..................
Basi watu waliongea mwisho wakaacha na maisha yakaendelea , ikipita miaka miwili maisha yakiwa magumu sana kwangu .
Nakumbuka niliwaza sana nikaona ni heri niondoke nyumbani ili nikajipambanie , bila kuchelewa nikasubiri baba na mama wakiwa seblen nikaenda na kuomba kuongea.
Nilipewa ruhusa ya kuongea ,kwa heshima nikapiga magoti na kusema " Baba na mama naomba ruhusa niondoke niende mjini nikatafute maisha"
Nilivyo sema hivyo ,baba alivua miwani yake na kuweka gazeti alilokuwa anasoma pembeni na kuniuliza " umesemaje ?"
"Ni mesema naomba ruhusa niendee mjini nikatafute maisha "
"Ukatafute maisha mjini! Kwani hayo maisha auliyaacha huko kwamba ndo unataka ukayatafute ?"
Nilitukisa kichwa kuashilia hapana baba anakinuliza tena " Sasa unatakaje kwenda mjini kwa kigezo cha kwenda kutafuta maisha .
Una elimu gani au una nini cha maana ambacho ukifika mjini kitakupa hayo maishs unayotaka ?"
Nioivyo ulizwa hivyo nilikaa kimya kwa mda kisha nikamjibu" nitaenda kufanya kazi baba "
"Kazi gani ?"
"Yoyote tu ilimradi nipate riziki"
"Umeanza kuwa tahira sasa, hivi unazani kwa hizo akili zako kama za paka mtoto zinaweza kukufanya ukaishi mjini?
Au mjini unapaona kama shamba la bibi yako, wewe huko wanaishi watu waliosoma watu wenye ujuzi wao na sio ma zumbukuku kama wewe.
Mtu huna mbele wala nyuma ,eti unaleta tumbo lako kama furushi la magimbi eti naomba niede mjini pumbavu kabisa"
Baba aliongea na kuinuka kwa hasira akiniacha bado nimepiga magoti, mama alikuwa kimya tu ananiangalia .
Kwa huzuni niliinuka nikitaka kurudi jikoni mama akaniita nakusema"we cheusi unaenda wapi, embu kalisha limwili lako hapo"
Masikini nilirudi na kukaa ,mama akaniangalia na kunambia " kwa hiyo umekaa ukafikilia na kuona umekua na unaweza kwenda kuanza maisha yako?"
Mama aliongea sikuwa na jibu la kumpa zaidi ya kukaa kimya huku nikiangalia chini ,akauliza tena"wewe Tuntufe nakuuliza umeona umekua?"
"Hapana mama niliona naweza kwenda tu"
"Uliona unaweza kwenda, hivi huko mjini unafikili wanakaa matahira kama wewe? Mtu hata shule ilikushinda ndo utaweza kuishi mjini.
Au unataka uende ukafe na njaa ,maana kwa jinsi ulivyo sidhani kama utapata hata msaada kwa watu ,maana utakuwa unaonekana kama litoto la mchawi.
Embu toa miguu yako kama fito, lione lilivyo nenepeana utafikili nguruwe pori, nyonyonyo 🤧uende na hapa nyumbani nani alike nani aangalie mifugo ?"
Alingea na kunisindikiza na sonyo kali, nikainuka na kwenda chumbani kwangu nikakaa chini na kulia 😔
Swala la mimi kutaka kwenda mjini liliwafikia ndugu zangu kila mmoja akaongea lake ,kaka yangu mkubwa akasema ni bora nikajifunze kushona .
Kisha nifunguliwe sehemu yangu nianze kazi walau niwe napata mia mia zangu, lakini mama akapinga na kudai hiyo hela ya kunipeleka kujifunza kushona .
Mara mia ikaninua pumba za ng'ombe au walipwe vijana wa kulima , lakini sio kunipa mimi nisie na akili 😔
Sikuwa na neno la kuongea zaidi ya kuwa msikilizaji huku nikikaa mwenyewe nalia nikichoka nafuta machozi na kuendelea na maisha.
Jambo hilo lilipita nakumbuka baada ya kama mwezi hivi ,dada yangu ambae alikuwa akiishi mwanza mjini akaja nyumbani.
Jamani katika ndugu zangu wote huyu ndo dada ninaempenda kuliko wote, hivyo baada ya kusikia anakuja nilifurahi sana na kuanda chakula kizuri kwa ajili .
Na ulipofika mda wa kwenda kumpokea nikaoga na kutaka kuongozana na mama lakini alinizuia madai nibaki nalinda nyumba.😔
Sinaga kauli ya hapana mbele yao hivyo ikanilazimu kubaki, wao wakaenda ambapo hawakukaa sana wakawa wamerudi huku wameongoza na dada.
Kwa furaha ya hali ya juu nilitoka ndani mbio kwenda kumpokea nikataka kumkumbatia ,nyie nilisukumwa kama vile nilikuwa na ugomvi nae.😥
Dada kwa dharau akajikung'uta huku akijinusa na kusema " ndo upumbavu gani sasa huu ,unataka kuninukisha uchafu wako😖 toto unanuka kama beberu.
Hivi una ogaga kweli au unalala banda moja na ng'ombe maana sio kwa hiyo harufu na naona kila siku unazidi kuwa mweusi .
Soon utaitwa mchawi wa kijiji maana sio kwa mwonekano huo toto la jana ila mwili wa juzi embu nipite mie"😓😓
Masikini nilisogea pembeni akapita huku akiwa amenikunji uso kama kaona kitu cha kumtia kinyaa😥😥, mama aliniangalia na kunambia .
"Umesimama hapo kama msukule embu beba mabegi peleka chumbani haraka sana ,kisha mpakulie mwanangu chakula ale ashibe"
Mama alivyo sema hivyo dada akamjibu" aaah mama hapana asishike mabegi yangu kwa hivyo alivyo hakosi kunguni au chawa.
Aaah hii shida sana mtu unakuwaje kama nguruwe lakini eeeh lione sura yake ilivyo na mishavu embu kaniwekee chakula huko.
Kwanza acha nitaweka mwenyewe maana naweza kushindwa kula hata hicho chakula chenyewe"😏
Aliongea na kuchukua mizigo yake akapeleka mwenyewe chumbani kwake, kwa huzuni nilijiangalia nikasema moyoni.
"Mbona nimeoga vizuri nimepaka mafuta na kubadilisha nguo safi sasa wanasemaje nanuka" 😥😖
Nilionhea kwa sana huku machozi yakinilenga lenga ,nikajinusa sikuwa nikinuka zaidi ya kunukia mafuta yangu ya Asheri🥲haya ndo yalikuwa mafuta mama yangu.
ITAENDELEA
ZENDAYA (TAMU YA BOSS)
SEHEMU YA 04
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO...................
Mtoto wawatu sikuwa na chakufanya nikajisogeza na kukaa pembeni kama mkiwa 🥲, dada aliweka vitu vyake vizuri akaja wakapakua chakula na kula.
Mimi niko pembeni tu maana niliwambiwa chakula ni cha mgeni na wao wakubwa hivyo mimi cheusi mangara nikatulizwa pembeni☹️
Sikuona shida maana hivi ndivyo inavyokuwaga pale ndugu zangu wanapikuja , unapika chakula lakini hauli hadi wao wamalize 🥺
Sasa hapo kwenye kumaliza omba mungu wakuachie hata mchuzi ,maana kuna mda wanakula chote unaambiwa ingia jikoni kapike chaka kwako😕
Cha kwako unapika nini ugari na msusa wa bila mafuta ,na kwakua maziwa niya kumwaga utakunywa na maziwa ila shobo shobo utabaki unazisikia kwenye bomba☹️
Nilizoea maana hayo ndo yalikuwa maisha yangu, maisha ya kuishi kitumwa ndani ya nyumba ya baba yangu😫, na inauma usisikie nasema nimezoea basi ukajua siiumii.
Ndugu hii inauma mnoo ,yaani unaishi kwenu ukijua wazi mama na baba hawanipendi aloooh maumivu yake sio mepesi.
Mara mia usipendwe na dada au kaka walau haiumi sana ila wazazi na unaoneshwa kabisa kwamba hatukupendi , omba sana isikukute utalia kila leo .
Na me niseme ,kama mtu ange niuliza Zendaya hivi leo mtu akija na kukwambia chagua kubaki kuishi na familia yako au ondoke ukaishi msituni .
Wallah ninge chagua kuishi msituni na wanyama ,walau hawa ukiishi nao vyema hawata kudhuru ila hii familia yangu hapana kila mara nasema .
Itakuwa ni moja ya familia za kichawi ambazo zilisalia duniani maana sio kwa roho mbaya hizi 😕eeh hivi utanieleza nini nikuelewe kwamba mama mazazi alieingia leba akazaa kwa uchungu anaweza kuishi na mtoto wake hivi.
Eeh nina bakwa halii au kuonesha kuhuzunika kama mama na sio mama tu basi kama mwanamke hakuna ,halafu huyu mtu ndo nisimame na kumchagua no.
Haitakaa itokee maisha buku, na nina sema siku ikitokea wakaambiwa ueni watoto wenu na kwambia nitafutiliwa mbali katika uso wa dunia hii.
Tena bila hata kuwaza na mimi nahisi nitakuwa niliokotwa maana siamini kama nilizaliwa katika familia hii ,na kama kweli nimezaliwa hapa.
Basi sina bahati na watu hawa au kama kuna nguvu yoyote ya giza iliyo tupiwa juu yangu ee! Hiyo nguvu itakuwa konki maana hii ni kali .
Na unaweza kuona au kuhisi ni maigizo au story tu my friend watu tunapita mahali pagumu mnoo, we shukuru Mungu una watu wanaokupenda ila kwangu mimi acha ninywe kikombe changu.😓
Basi bwana ,dada angu alikaa pale nyumbani kwa siku tatu siku ya nne asubuhi niliamshwa na kuambiwa kuna ugeni utakuja mchana .
Hivyo natakiwa kuweka mazingira safi pamoja na kupika chakula , kama kawaida kijakazi mie nikafanya yote na nilivyo maliza nikaingia bafuni mie na kuoga.
Baada ya hapo nikaamua kuondoka kabla sijaambiwa nitoke kwa maneno mazito nikaja haribu siku yangu bure, japo sikwenda mbali na nyumbani.
Maana naweza kuhitajika kwenye kutoa vyombo au kufuta miguu ya wageni ,eeh hizo ndo kazi pakee ambazo naweza kupewa kulingana na vile ninavyo onekana kwao.🥲
Basi bwana nilienda nje ya nyumbani kabisa na kukaa kwenye kinjia cha kuelekea nyumbani ili tu niwaone hao wageni ni kina nani!.
Haukupita mda mrefu nikaona magari mawili yakija usawa wa kwetu, niliinuka na kusogea pembeni dada asije kuniona nimesimama njiani kushangaa wageni wake ikawa kesi.
Magari yale yalinipita na kwenda nyumbani ,walipofika wakasimama na kushuka wanaume wanne kwa haraka haraka nikajua dada tayari anaenda kuolewa.
Na nikweli watu wale walikuja kwaajili yake ,na familia iliwapokea kwa mikono miwili, wakala na kunywa kisha wakaongea kilicho waleta na walipimaliza wakaondoka.
Bila kuchelewa nikarudi nyumbani nikiwa nafuraha sana ,moja kwa moja nikaenda kumpongeza dada yangu.
Leo alikuwa na mood nzuri hakunigombeza ndo kwanza alifurahi na kunishukuru kuwa nimepika chakula kitamu sana ,wageni wake wamekipenda na kumsifia mnoo.
Sinaga choyo bonge mie nikamwambia hongera kisha nikatoka ili niende nikaoshe vyombo kisha nile magaki kama ilivyo kawaida yangu.
Lakini nikasimama na hii ni baada ya mama kusema "mh Mungu amejua kunibariki watoto wazuri mnao nipa heshima na furaha.
Natamani wote mgekuwa hivi ila nimezaa na mwisho nikatoa kondo😏"
Nilimuangalia mama na kuamua kuondoka bila kusema kitu, sas ningesema nini ndo nishaitwa kondo kondo linaongeaga no so acha nitulize utungunya wangu.
Basi nilifanya shughuli zote pale ,siku ikaenda kesho yake asubuhi na mapema dada akaondoka na safari hii hakukaa sana mjini akarudi tena .
Ambapo alirudi kwaajili ya kutolewa mahali na ilipokwishwa kutolewa taratibu za ndoa zikafuatwa ndoa ikafungwa na kuwa mke wa mtu rasmi.
Maisha yalienda na alipo jifungua nikaambiwa na mama kuwa niende nikamsaidie kazi pamoja na kumlea mtoto wake ,maana hawezi akaajili mtu na mimi ndugu yake nipo.
Jambo hilo nililipokea kwa moyo mmoja tena mweupe maana nilimpenda sana dada yangu huyu, hivyo kitendo cha kuambiwa kwenda kuishi nae.
Kwangu ni furaha na neema kuu😊, jamani nilijiandaa vizuri nikabebeshwa na zawadi kede kede kisha niakenda stend kupanda bus.
(Mh laiti kama ningejua maisha nitakayo enda kuishi huko ,bora ninge baki nyumbani tu😮💨)
Story ndo kwaaanza inaanza tukutane sehemu ijayo
ZENDAYA (TAMU YA BOSS)
SEHEMU YA 05
MTUNZI RITHA STORIES
https://www.tupohapa.com
SONGA NAYO.............
Bwana weee nilisafiri na baada ya masaa kadhaa nikaingia jijini mwanza hapo nimetokea wapi mbeya.
Kufika nikapokelewa na dada mwenyewe, na kumbuka kitu cha kwanza mara baada ya kunipokea alinambia " chukua zawadi ulizo kuja nazo kuhusu nguo achana nazo."
Sikumuelewa nikamuuliza " samahani una maanisha nguo niziache ama?"
"Eeeh unataka uende nazo wapi taka taka hizo ,we beba zawazi hayo manguo yako yaache hapo"
"Lakini dada nitaachaje nguo hapa na huko nitaenda kuvaa nini?"
"Ee wewe usinichoshe nakwambia yaache kuhusu za kuvaa huko nitajua mwenyewe "
Sikutaka kubishana nae nikamsikiliza nakuacha nguo zangu stend ,bila kupoteza mda tukachukua usafiri hadi nyumbani ,kufika nikakuta mumewe yupo sebleni.
Kwa heshima nikamsalimia akaitikia kisha nikapelekwa chumba nitakacho kuwa nikitumia na kuambiwa.
"Unakiona hiki chumba ?"
"Ndio nakuona dada"
"Nikisafi au kichafu?"
"Kisafi"
"Okay, sasa fanya upumbavu wako woote ila sitaki kuona chumba hiki kikiwa kichafu sijui unanielewa?"
"Ndio dada nakuelewa"
"Haya hiyo ilikuwa moja ,mbili umemuona shemeji yako ,dada katika vitu unavyotakiwa kuviogopa na kukaa navyo mbali ni mume wangu.
Yaani nisije nikakuona unakaa karibu yake au unaleta mazoea ya kijinga, we fanya kazi zako ukimaliza kaa chumbani ila ukijifanya chizi ukaenda kunyume changu.
Wallah nakuzika mzima mzima sijui unanielewa ?"
"Ndio dada nakusikiliza "
"Haya masharti ya humu ndani yako mengi nitakwambia baadae saizi oga ukapike chakula mda unaenda"
Niliitikia sawa akaondoka ,nikaingia bafuni na kuoga nilivyo maliza nikatoka na kukuta ameniwekea nguo kitandani .
Nilichukua ile nguo nikaiangalia na kubaki nashangaa ,jamani ulikuwa mgauni mkubwaa balaa, yaani ile nguo jinsi ilivyo nikivaa na mwili wangu huu nakuwa kama nimetundikwa.
Kinyonge nilivaa nikajiangalia jinsi ilivyo nikaa mwilini nikajisemea ,( nimekuwa kama midoli inayokwa kwenye mashamba ya mipunga ili kufukuza ndege☹️)
Ukweli sikupenda ila ndo sikuwa na jinsi maana hata kama ningesema nikatae nitavaa nini ile hali sina nguo hata moja 🥺ko lililopo ni kuvaa tu 😕
Basi nilitoka nikaenda sebleni ambapo walikuwa wamekaa huku wakiangalia TV nikamuuliza dada "nimemaliza kuoga ,ulisema nikimaliza nikapike mh nipike nini na jiko liko wapi?"
Kabla dada hajajibu mumewe(shemeji) akasema "kupika ,hapana bwana pumzika umetoka safari unahitaji kupumzika sawa"
Dada alimuangalia mumewe na kumjibu" akapumzike ili iweje kwamba hiyo safari aliyotoka imemchosha kiasi cha kumfanya asiwezi kupika ?"
"Hapana mke wangu muache apumzike bhna yaani afike na kuanza kazi ,sikia Zena naomba nikuite hivyo ,we nenda kapumzie shemeji yangu sawa!"
Niitikia ndio kwa kutikisa kichwa huku nikimuangalia dada aliekuwa ananiangalia kwa jicho kali sana , kwa uoga wa hali ya juu niligeuka na kuondoka huku kila mara niligeuka kumuangalia dada.
Sikufika mbali dada akamwambia mumewe "Derrick katika vitu ambavyo sitahitaji kuingiliwa basi ni hivi, naomba maswala yangu na mdogo wangu uyaache.
Habari za mimi na sema hivi na wewe unasema vile staki, simama kwenye mambo yako na niache na mambo yangu "
"Aa mke wangu hapo unakosea, mwenzio ndo kafika mda huu na ametokea mbali halafu unataka kumpa jukumu la kupika wakati wewe upo na umekaa tu.
Na ndio nakubali sitakuingilia katika mambo yenu ila popote nitakapo ona au nitakapo takiwa kuongea nitaongea,kingine mununue nguo ndugu yako.
Kama hela hauna sema nikupe maana hatuwezi kukaa na mtu anavaa nguo kama msaidizi wa joker "
Dada alijibu sawa mimi nikaingia chumbani na kujilaza, pamoja na kuchoka ila sikupata hata usingizi ,maana akili ilikuwa mbali sana .
Niliwaza hii ni siku ya kwanza kuwa hapa lakini tayari nimeshaanza kuoneshwa rangi tofauti tofauti nitatoboa kweli?
Niliendelea kuwaza na kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu,taratibu mda ulienda usiku ukaingia na saa ya kupata chakula cha usiku ikafika.
Niliitwa nikainuka na kwenda nikijua kuwa tutakaa pamoja ,ajabu kufika akanambia "chakula chako kiko jikoni huko ndiko utakuwa unakaa na kupata chakula"
Niliitikia sawa nakugeuka ili niende shemeji akanisimamisha na kumwambia dada" Mke wangu kwanini unamtaka mwenzako akale jikoni si akae pamoja na sisi "
"Derrick! Nimeshasema staki uingilie kwenye mambo yangu, we unataka akae hapa ili iweje kwani akikaa huko chakula hakipandi?"
"Shida sio chakula kupanda shida ni kwanini akale jikoni na sisi tule mezan?"
"Kwasababu staki kwani shida iko wapi, wewe embu toka mbele yetu "
Bila kuongea neno nilichanganya miguu na kuingi jikoni nikimuacha shemeji anamuangalia dada kwa jicho la hasira sana .
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote